Thomas Nyahende ajitosa ubunge jimbo la Ukonga kupitia CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
*Thomas Nyahende ajitosa ubunge jimbo la Ukonga*

Mpambano wa kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Ukonga kupitia Chadema umechukua sura mpya baada ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa jimbo hilo Thomas Nyahende kuchukua rasmi fomu za kuomba uteuzi.

Nyahende mwanasiasa imara mwenye imani madhubuti ndani ya chama hicho alikuwa meneja wa kampeni wa mgombea ubunge wa jimbo hilo mwaka 2015 na mikakati yake ndiyo iliyosababisha chama hicho kunyakua kiti hicho na kuwashinda wagombea wa vyama vingine.Pia ndiye alikuwa wakala mkuu wa Chadema katika jimbo la Ukonga na kudhibiti kila aina ya wizi wa kura.

Nyahende ambaye ana umaarufu mkubwa katika siasa za Ukonga alianza kutajwa na watu mbalimbali kama mtu anayefaa kupendekezwa na chama hicho na hatimaye kukiletea ushindi.Ni wazi msukumo wa watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya jimbo hilo ndiyo uliomlazimisha hatimaye kukubali kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa.

Wachunguzi wa mambo ya siasa wanabashiri kwamba mpambano wa Nyahende na Waitara anayetarajiwa kurudishwa na CCM utakuwa mkubwa.Hii ni kwa sababu Nyahende anamfahamu vizuri Waitara kutokana na kusimamia kampeni zake mwaka 2015.Pili ni watu wanaotoka mkoa mmoja wa Mara huku jimbo la ukonga likiwa na idadi kubwa ya wakazi kutoka mkoa huo.

Nyahende ni kati ya wanachama walioijenga Chadema Ukonga kwa hali na mali kwa miaka kadhaa kuanzia mwaka 2009 hadi kufikia ilipo sasa.Mbali na kuwa Mwenyekiti wa Jimbo hilo mwaka 2014 - 2015 pia alikuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Kata ya Ukonga na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya jimbo mwaka 2011 - 2014.Kuanzia mwaka 2016 - 2018 alikuwa Kaimu Mhazini wa Jimbo.

Taarifa zinadai endapo kama Nyahende asingechukua fomu wapo wanachama waliokuwa wamedhamiria kumchukulia fomu,kuzijaza na kuzirudisha ili kumshinikiza kugombea.
 

Attachments

  • IMG-20180810-WA0038.jpg
    IMG-20180810-WA0038.jpg
    66.8 KB · Views: 96
kila la kheri,tunaomba kampeni za ustarabu kwa ccm maana kwa sasa wao ndio wanatukana kwenye majukwaa jao hawanasera tena bali ni vitisho na maigizo
 
Duh! Nilitaka kuuliza kama kamanda Molemo bado umo humu mjengoni. Kitambo sana sijakusikia mpaka nikapatwa na hofu.
Ninam-miss pia Candid Scope.
 
Kila kheli kwa Thomas, binafsi namfahamu vizuri atawafaa wana Ukonga kama chama chake kitampitisha na hatimae kuibuka kidedea. Tuko pamoja bwana Nyahende.
 
siasa za ukonga huzijui wewe , jiulize kwanini Waitara baada ya kujiuzulu anaishi kama digidigi
kwani wewe ni mkewe mpaka ujue anaishi kama digidigi?
Jipange mwaka 2020 chadema wakuteue usimame temeke,ukawa ishakufa
 
kila la kheri,tunaomba kampeni za ustarabu kwa ccm maana kwa sasa wao ndio wanatukana kwenye majukwaa jao hawanasera tena bali ni vitisho na maigizo
Umeongea kweli tupu
 
Back
Top Bottom