Thobias Mwilapwa apewe Ukatibu Mkuu wa CCM kwa uwezo wa ziada alionao

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Napenda kutumia nafasi hii kukiri kwamba sijatumwa na mlengwa kuandika ninachoandika lakini nimeguswa na namna alivyo na uwezo wa ziada katika kujenga hoja, kuchambua mambo na kuongoza kwa kufuata sheria.

Tunapoelekea mkutano mkuu wa CCM, naamini safu ya uongozi ndani ya CCM itajengwa mpya kwa kupatikana uongozi mpya kwa kumpata mwenyekiti, M/Mwenyekiti na KM wa CCM na viongozi wengine waandamizi. Hao ndio viungo wa siasa ndani ya CCM na taifa letu kwa ujumla.

Leo napenda kuwaleteeni jina la mtu ambaye nimemfuatilia kwa muda mrefu na kubaini uwezo wake katika kuongoza, kujenga hoja na kuchambua mambo na kwa jinsi anavyozungumza ni mtu anayetafari sana kabla ya kuzungumza. Simjui kwa undani sana lakini kwa sifa hizo chache naona ni mtu atakayemudu majukumu ya nafasi hiyo ipasavyo ikizingatiwa kwamba anakijua chama na siasa zake kwa undani

Ombi
Ninawaomba wajumbe walitazame jina la mtu huyu kwa jicho la tatu, kwa kuwa anaonekana ni mtu mwenye uwezo wa ziada ambazo ni silaha katika utendaji uliotukuka na wenye kujenga misingi. Thobias Mwilapwa apewe u-KM wa CCM kwa uwezo wa ziada alionao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom