Thobias Andengenye atangaza ofa ya Tsh 5mln kwa yeyote yule atakayetoa taarifa hii!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,219
RPC Mkoani hapa Thobias Andengenye ametoa ofa ya Tsh milioni tano kwa atakayetoa taarifa ya kusaidia kukamatwa kwa jambazi SUGU aliyeharibu hali ya hewa leo hapa A town kwa kumpelekea Konstebo mmoja wa police kupoteza maisha na jambazi mwenye anaitwa Hendry Samson Kaunda. Tenda hiyoooooooooooo!! Pesa nje njeeee!

Source RFA!!
 
Angeweka na picha angalau kazi ingekuwa rahisi kidogo.

Mi naona hivi hivi itakuwa shughuli pevu hii!
Hawa mapolisisisiem wana kazi hp A town!
Hiyo sasa si mambo ya siasa sasa hebu fanyeni juhudi zenu tuone!

Kwa haraka haraka wekeni picha pleas!
 
Polisi nyie mnavuna mlichopanda mulifundishwa kuwa uhalifu ni maandamano ya chadema tuu ambayo hayana madhara kabisaa haya sasa maandamano yenye maelfu ya walalahoi hayajadhuru hata sisimizi zaidi ya nyie kuwatwanga risasi raia wema ambao ni kaka zenu,dada zenu,au hata Baba na mama zenu mhalifu mmoja tu kawatoa jasho. Tazameni udhaifu wenu muchukue hatua.
 
yaani huyu jambazi mpaka sasa hawajamkata?

Akamatiwe wapi Best?
Unambiwa hawa police jina walipata taarifa hii ya huyu jambazi na wakamwekea taget ya kutaka kumkamatia hapo anapowekaga mambo yake.

Unaambiwa huyu Hendry alipopata hisia ya kuwepo na polisi hapo nje,unaambiawa alitoka kama vile mbogo aliyejeruhiwa na akamimina risasi mithili ya mapambano ya Al-shabaab na askari wa Kenya na ndipo akawalaza askari wawili chini na ndipo akapata chanzi akatoweka mpaka sasa!
 
Kwanza nawapa pole sana watoto waliopotelewa na baba yao na mke aliyefiwa na mumewe.
Hivi kama Polisi wenye silaha na waliopata mafunzo ya kupambana na wahalifu pale CCP Moshi wameshindwa kumkamata huyu jambazi ni vipi raia wa kawaida ataweza mkamata. Inakuwaje hawa jamaa wanataka kuhamishia suala kwa raia ambao juzi tu tarehe kama hizi mwaka jana waliwapiga mabomu na kuua wenzao watatu. Walipotupiga na kutuua hatukupata wa kumhamishia majukumu ya kumtafuta mchawi leo kibao kimegeuka wanatuona sisi raia ndo wa kuwapa msaada?. Wao ni wataalam wa kupiga raia wenye amani kumbe mbinu za kupambana na wezi hawana mbona aibu?
 
MVUMBUZI!
Nakwambia ya kwmb kitu ambayo nimegundua ni kwmb hawa police hakika hawako kimalengo yao ya kazi.
Hawa wapo kisiasa zaidi ngazi ya juu lengwa wasipoliangalia hili hakika litawagharimu sana!
 
Wapi intelijensia hapo leo, nadhani hawakutumia sababu za kiintelijinsia. Naomba wazitumie sasa kumpata huyo jambazi sugu. Mungu ibariki tanzania
 
Jambazi hatamkamata na bado polisi wawili maana mwaka waliwaua raia bila sababu. Watumie intelejensia ya katibu mkuu wa ccm
 
Wachaga na hela khaki ya nani atakamatwa, kina mangi wataweka mitego hadi babati!!!
 
Its real disguisting, yaani baada ya kuharibu mahusiano na raia leo tena anataka msaada kutoka kwao? pesa kitu gani kuzidi utu wao ambao umekuwa ukichezewa mara kwa mara? police bana!
 
Wachaga na hela khaki ya nani atakamatwa, kina mangi wataweka mitego hadi babati!!!

Aisee kwa ajili ya Tsh.5mln wanaweza wakajichanganya kweli!

Mkubwa!
Wakina Mangi siyo wale unaowajua miaka ta3 iliyopita!
 
huyo wakimshka wampeleke CCP AKAWAPGE LECTURE YA KUWAKAMATA WAHALIFU SUGU.....
Wasimfanye chochote kwn huyo jamaa ameiva navyoona...
Policcm wa sasa hakuna ki2 weupe...mi wawe kumi napg wote. wachovu sana
 
Inaweza ikawa Hendry Samson Kaunda ni mshabiki wa Man City! Anaweza akawa leo hii anafurahia ushindi kwenye vilabu kubwa kubwa hapa town,waliojitoa mhanga kumseach msiache kufika ktk vilabu vya night kali kwn ushindi wa Man City ya bao 3- 0 kwa Liverpool Football Club imenigusa sana. Atafutwe hili jambazi sugu huko wajameni kwa anayetaka Tsh.5milioni toka kwa Andengenye.

KAZI KWELI KWELI!
 
Inaweza ikawa Hendry Samson Kaunda ni mshabiki wa Man City! Anaweza akawa leo hii anafurahia ushindi kwenye vilabu kubwa kubwa hapa town,waliojitoa mhanga kumseach msiache kufika ktk vilabu vya night kali kwn ushindi wa Man City ya bao 3- 0 kwa Liverpool Football Club imenigusa sana. Atafutwe hili jambazi sugu huko wajameni kwa anayetaka Tsh.5milioni toka kwa Andengenye.

KAZI KWELI KWELI!

Wamuulize Lema
 
Back
Top Bottom