#COVID19 Thobias Andegenye: Mechi ya Simba vs Yanga wote wavae barakoa, hata uwanja ukifurika

Mashabiki elfu 17 pekee ndio wataruhusiwa kuingia ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, kushuhudia mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga siku ya Jumapili.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema wamepunguza idadi ya mashabiki kuingia ndani ya uwanja ili kuthibiti maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Pia amesema kila atakayeingia uwanjani lazima awe amechukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa na kunawa mikono.

Andengenye amesema wameandaa utaratibu mzuri wa kuweka mapipa ya maji nje ya uwanja huo wa Lake Tangnyika, ili kuwawezesha wanaoingia uwanjani kunawa mikono.
-----

Uwanja wa Kigoma una uwezo wa kujaza watu 20,000

Mkuu wa mkoa wa Mwanza hakuna mtu Yeyote kukusanyika kongamano la Katiba la watu 300 sababu kuna Corona

Waziri wa afya: Hakuna mikusanyiko yoyote

Another business opportunity... Kwa mfano kila barakoa ikiuzwa 1000 × 17,000 hiyo ni 17,000,000/= ukitoa gharama na mtaji hukosi 10,000,000/= ya fasta kabisaaaa
 
Back
Top Bottom