ThisDay limetekwa nyara?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,116
Gazeti la THIS DAY ambalo lilikuwa mstari wa mbele katika kuwafahamisha Watanzania ufisadi mbali mbali uliofanywa na Mkapa akiwa Ikulu, Mikataba bomu ya madini, Mkataba wa wamiliki wa TANESCO na Kiwira Coal Mining (Mkapa na Yona) na mazagazaga mengine chungu nzima ndani ya siri kali halipatikani Online tangu Ijumaa iliyopita, JE LIMETEKWA NYARA na MAFISADI!?
 
Empire ya Mengi inasuasua kweli.Waandishi wanadai mahela kibao na huenda baadhi ya magazeti yakafa kutokana na hali mbaya ya kifedha.
 
Hamna lolote. Tatizo la baadhi ya wafanyabiashara wa bongo ni dhuluma!

Huyu bwana anaongoza kwa kuwadhulumu wafanyakazi wake! na kimwana kashammwaga basi tena... kwi kwi kwii

Mi sipendagi kuona wabongo wanaonewa iwe na mmbongo au mmweupe!
 
Kwanini THIS DAY tu? Na siyo Nipashe, Alasiri au the Guardian? Nafikiri kuna kitu kinafichwa hapa. Au Waandishi wa "THIS DAY" wamegoma kuwa "Aligned"? Yetu macho na masikio,Ukweli utadhihiri muda si mrefu. Si unajua hapa Bongo si rahisi kuweka habari chini ya kapeti?
 
nilishawahi kufanya kazi kwa kingdom ya mengi na mwanzoni hali ilikuwa bora sana ila alipoanza kukumbatia ukabila na haswa kuwavuta washkaji wake vikwongwe wa magazeti ya serikali kuja kufanya kazi ktk kampuni yake ndipo alipoamua kuanza kumchinja ndama mkononi mwake. na uzuri mwingine a mengi ni kuwa haambiliki and he is good mafia. yaani anajifanya kondoo ktk vazi la mbwea na sio mbwea ktk vazi la kondoo (mwenye akili afahamu)
waandishi wake wanaficha ukweli kinoma
 
Bado kwa Watanzania ninao wajua mimi MENGI ni mtu mzuri mno!

Kumlinganisha Mengi na sisi walala hoi ni kumwonea, mlinganishe yeye na wafanyabiashara wakubwa kama yeye au viongozi wenye vyeo vikubwa. Bado Mengi ni nafuu mno.

Looh! Tanzania tuna kazi kubwa sana maana kama Mengi naye ataishia kutukanwa nani atakuwa hero wetu?

Wakati mwingine kwa heroes wa nchi inabidi kuendelea kuwasifu tu hata kama wanafanya makosa madogo madogo.

Mimi sio kabila lake wala sijawahi kufaidika na kitu chake chochote lakini ninamheshimu Mengi kwa mchango wake kwa Tanzania.
 
Hatumtukani ila ukweli ndio ambao huumiza sana na hili halikwepeki. Kama ni mtu mzuri na anatoa misaada kwa walengwa ili kuficha udhaifu fulani siyo kitu cha kunyamazia. ni kuwa kama hajali maslahi ya watanzania wenzake wanaomsaidia kuikuza himaya yake basi hayo ni makosa ya kuyamulika. ndiyo maana hatugusii mambo yake ya binafsi, we focuss on issues zinazogusa public interests, hasa hasa maslahi na ustawi wa jamii...
na asiwe offended sana kwani ndiyo ukweli halisi. labda kuna washauri wake wanatembelea humu wamweleze kuwa wafanyakazi wake wanateseka sana na wahindi wake aliowaweka kule mikocheni na ajue hata hao mameneja wa kichaga akiowaweka wanamvuna bila yeye kujua......
 
TUSIMJADILI MTU (MENGI) hoja hapa ni THISDAY kutoonekana katika net toka Ijumaa, watu wanapenda sana kujadili watu na kukwepa hoja za msingi wakati wote.... Hii tabia si nzuri kabisa...

Kuna mtu kanijibu kwamba kulikua na tatizo katika website ya THISDAY tokea Alhamisi usiku na wanaendelea kulishughulikia hilo tatizo. Hiyo ndio ilikua hoja na kama kuna mtu mwenye nia ya dhati kwa walioko Tanzania wanaweza kuangalia gazeti na kutupa michapo ya stori za leo maana liko mitaani.
 
Nijuavyo mimi ni kuwa Mengi anamiliki taasisi au kampuni ambazo zina uongozi wake. Naamini kuna mtu anaajiri na kufukuza na Mengi hafanyi kazi hiyo. Wewe kama umeona kwenye taasisi au kampuni zake mishahara ni midogo si ujaribu kwa Manjis au kwingineko? Tuache kumsakama kwa maneneo rahisi rahisi kimtaani mtaani. Sijaona alipokosea hata kama ameachana na kimada wake . Kwani wewe Msanii huna kimada? Who in the world claiming to be a man has ever practice zero sex ? Hata famous presidents wamewahi kutetereka kwa hilo . sitetei ngono ila nasema kama kuna ambaye sio mvovu kwa hilo anyoonshe kidole juu. Baadae wanaume wote tutatakiwa aidha kwa sheria au kwa matakwa ya maisha kuoa au kuwa na vimada zaidi maana idadi ya wanawake inazidi kuwa kubwa na wanahitaji service zetu. Wakati huo thread hii itakuwa haina maana tena. It is just a matter of time au niseme tayari imeshaanza. Kwani huoni hilo?

Biashara huanza hukua na hufa pia. Mengi is no exception. Hata This day likifa yatakuja mengine tu . Unless you have personal druges which we do not buy here, mengi is still a better personality than most of the mafisadi in bongo.
 
Here we go...it's Mr Mengi and Mengi again...!!!

Topic imeanza vizuri kwa kujadili gazeti la Thisday...hivi kuna watu wametumwa humu JF?
 
Nijuavyo mimi ni kuwa Mengi anamiliki taasisi au kampuni ambazo zina uongozi wake. Naamini kuna mtu anaajiri na kufukuza na Mengi hafanyi kazi hiyo. Wewe kama umeona kwenye taasisi au kampuni zake mishahara ni midogo si ujaribu kwa Manjis au kwingineko? Tuache kumsakama kwa maneneo rahisi rahisi kimtaani mtaani. Sijaona alipokosea hata kama ameachana na kimada wake . Kwani wewe Msanii huna kimada? Who in the world claiming to be a man has ever practice zero sex ? Hata famous presidents wamewahi kutetereka kwa hilo . sitetei ngono ila nasema kama kuna ambaye sio mvovu kwa hilo anyoonshe kidole juu. Baadae wanaume wote tutatakiwa aidha kwa sheria au kwa matakwa ya maisha kuoa au kuwa na vimada zaidi maana idadi ya wanawake inazidi kuwa kubwa na wanahitaji service zetu. Wakati huo thread hii itakuwa haina maana tena. It is just a matter of time au niseme tayari imeshaanza. Kwani huoni hilo?

Biashara huanza hukua na hufa pia. Mengi is no exception. Hata This day likifa yatakuja mengine tu . Unless you have personal druges which we do not buy here, mengi is still a better personality than most of the mafisadi in bongo.

Shekhe...
kama umesoma vyema hii thread tangu mwanzo nadhani utagundua kwamba sijaongelea kuhusu mengi kuachana na kimada wake. Mie sina kimada kwani sasa nategemea kufunga ndoa hivyo baada ya ndoa ndipo nitakuwa na haki zooote za kupractise zero sex.
kuhusu Mengi na makampuni yake, nipo clear kabisa kwa niliyoyaongea. Sikuwahi kuajiriwa pale ila nilishafanya kazi pale naomba uelewe hilo na kwa kuwa naridhika na kajipato kangu huwa siwazii kuajiriwa hata siku moja. Ila kwa wafanyakazi ambao wanafanya kazi pale wanaishi ktk hofu na mashaka sana kuhusu hatima za haki zao, kwani ni kweli mengi anao wasaidizi wake wanaoitwa wakurugenzi ktk taasisi zake ambao ndio huajiri na kufukuza ingawa mara nyingi mzee mzima anakuwa anaingilia hapa na pale. Pia nakumbuka mwaka fulani mwanzoni mwa milenia hii alimdemote editor (ambaye yupo jela sasa, kwa tuhuma za rushwa) wa observer kwa kutoa taarifa ya ukweli kuhusu matumizi mabaya ya Vice president ktk safari zake.Mnamfahamu Wence Mushi? mnajua yaliyompata mpaka sasa amekuwa anafanya kazi chini ya mwanamama? (jina nalificha). Na pia najua mnafahamu yaliyompata maulidi wa kitenge ambapo alihudhuria press conference ya mwanae mengi (manji). maulidi alikuwa banned kwa uangalizi maalum kisha sasa hatimaye bann imekuwa lifted. Na ni kweli kwamba yeye hagusi wala kuandikwa negatively (hata kama ipo) ktk magazeti yake. Hao wasaidizi wake hawana lolote jipya zaidi ya kuchuma na kujistawisha. hawana nia thabiti ya kuendeleza mazuri anayodhamiria Mengi wakati wa uanzishwaji wa makapuni yake.Angalia mfano mzuri wa east afrika tv ambapo marehemu mwanae (motie) RIP aliamua kutenganisha na makampuni ya baba yake baada ya kuona ubabaishaji mwingi, angalia ambavyo EATV imeweza kusambaa afrika mashariki kwa kasi ingawa imeanzishwa miaka mingi baada ta ITV, hapo ndipo utaelewa ninachoongea. Pale kwa mengi pamejaa majungu na kuoneana kijicho na umbeya mtupu. Yeye anaweza akawa anafahamu hilo au hajui ila kwa kuwa ameweka mazingira magumu kwa waajiriwa wake kuwasiliana naye pale ambapo mambo ni magumu kwao. Na kwa kuwa amejijengea himaya ya kiutawala hivyo pengo kati yake na wafanyakazi ni kubwa basi wacha ayamalize makampuni yake kwa mkono wake.

Mambo yake na familia yake ni jukumu lake mwenyewe kusolve na hayanihusu kamwe, ila jambo lolote linalohusu usawa na ustawi wa watu hapo sina mchezo.

Mfamaji nakushauri usifemaji tena wala kutapatapa ila shikilia boya la ukweli na utu ndiyo pona yako
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe. Huyu jamaa kati ya watanzania kwa kweli ni mmojawapo ya walio/wanaojitahidi. Wala tusidiriki kumsema vibaya kwa thisday kutoweka.Nadhani kwa sasa tujiulize wamepata tatizo gani tena?
 
hapo umesema mkuu mfwatiliaji
lakini naamini kuwa ktk uhai wake labda magazeti yake hayatoweza kufa ila je anaandaaje makampuni yake kusavaivu wakati hayupo??

Namwombea heri na ukweli aupate vilevile maana ktk kusema ukweli inawezekana ikanusanusa kueleweka vibaya as kumtukana mtu.....
 
Gazeti la THISDAY limekua source ya topic nyingi humu JF na kuna wakati limenukuu hata JF, sasa tatizo lao ni letu.. tusipotoke na kuanza kujadili mtu.. Wataalamu wa IT hebu tumieni taaluma yenu kutafiti kilichoisibu www.thisday.co.tz maana inaelekea ni tatizo kubwa ama kuna "MKONO WA MTU?".... Inawezekana pia ikawa ni MAJUNGU kama alivyosema mchangiaji mmoja hapa kwamba inawezekana kuna MAJUNGU maana THISDAY wamepata ujiko zaidi kuliko Guardian wakati Guardian ndio wanaozalisha zaidi (Kifedha kutokana na matangazo na mauzo zaidi)..
 
Back
Top Bottom