This will be my biggest risk! Kilimo cha alizeti Singida

Usimsahau mganga....ili ndio la muhimu zaidi
Salute kwenu mabibi na mabwana.

Mafanikio makubwa huja kwa ku-take risk kubwa vilevile. Ukikosa unakosa kweli unaweza usirudie tena lakini mzigo ukitiki unatoboa kweli kweli.

Sasa mpango mzima nimeshau-draft kila kitu hadi soko la mafuta ya alizeti nitakayokamua. Kilichobaki ni kusubiri mwezi wa kumi na mbili niingie site nikapambane.


Nimepanga kulima ekari 40 za alizeti mkoani singida. Ardhi ninayomiliki hadi sasa ni ekari 10 tu ila nipo kwenye hatua za mwisho kukodi ekari 30 ili zifike 40. Nitalima alizeti zote.

Michakato mingine kama trekta la kulimia inaenda vizuri na muda sio mrefu inakamilika.

Kuna mbegu moja ya alizeti inaitwa Hysun 33. Hii mbegu balaa lake sio la nchi hii. Inasemekana kwa ekari moja inaweza kutoa gunia 15-18 za alizeti za kilo mia mia. Inasemekana inavumilia hali zote za ukame na mvua nyingi, magonjwa n.k. Ni mbegu bora sana naona hata serikali ya mkoa imeipitisha rasmi which means huenda ipo vizuri. Bei yake kwa kilo ni 35000/=.


Nimepiga hesabu zangu za kilimo cha mtandaoni au kwenye makaratasi. Kwa ekari 40 nitaweza kupata gunia 400 (nimeassume ekari moja itatoa gunia 10 badala ya gunia 15 walizosema wataalam).

Kwa hizo gunia 400 nitakamua mafuta ya alizeti ambapo sasa watalaam wa mbegu ya Hysun 33 wamesema uhakika ni kupata dumu 2 za mafuta ya alizeti kwa kila gunia. Mimi nita-lower expectation zangu nipate average ya dumu moja kwa gunia moja). Hapo nitazungumzia habari ya kupata dumu 400 za mafuta.

Nitauza mafuta kwa bei ya 50,000/= kwa dumu moja la lita 20. Hapo nitapata 20M. Calculation zangu zinaonyesha kuwa running cost zote zitanigharimu 5M). Hapo nategemea net profit ya 15M.


Sina shaka na mahesabu yangu yote hapo juu. Hapo nimeweka minimum value sana ukilinganisha na maelekezo ya wataalam na wazee wa kijiji niliopata fursa ya kukutana nao hivi majuzi. Shida yangu ni moja tu: MVUA HAITANIANGUSHA KWELI? ukizingatia mkoa wa singida ni mkoa wa ukame ukame.


Naombeni maoni yenu kuhusu hii kitu. Nina uzoefu kidogo kwenye kilimo hiki kwani mwaka jana nililima ekari 2 ili nipate uzoefu. Nilipata gunia nane tu. Kosa langu la kwanza nilikua napiga simu na kutuma hela tu kijijini hadi muda wa mavuno sijakanyaga shambani. Mwaka huu nitakua mwenyewe shambani mwanzo mwisho nikishiriki kila kitu. Kosa la pili nilitumia mbegu za kienyeji. Mwaka huu nitatumia mbegu hybrid za Hysun 33.

Karibuni kwa mchango.
 
Hysun 33 ni hybrid yenye uwezo wa kutoa gunia 15-18 za kilo mia mia kwa shamba la ekari moja.

Ukikamua mafuta unaweza kutoa lita 42-48 kwa gunia moja i.e zaidi ya dumu mbili za mafuta.

Inavumilia hali mbaya ya hewa. Haihitaji madawa kivile. Palizi moja tu.

Bei wanauza 35k kwa kilo moja. Wanasema mbegu inayoweza kukidhi ukubwa wa ekari moja ni kilo mbili.

Hii ni kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa singida.
Yeah kwa ekari unatumia mbegu kilo 2 ila sasa naona bei ya mbegu imesimama.

Kwa utoaji huo wa mafuta kukamua mwenyewe ni wazo zuri maana ukisema unauza utampatia faida mnunuzi. Chamsingi fatilia kwa ambao wameilima wakupe ushuhuda. Natamani niijaribu hata kwa ekari moja nione matokeo yake.

Niko mbali na Singida kwa sasa.
 
Dodoma maeneo ya Kibaigwa unaingia ndani vijijini huko mwendo wa saa moja hv kwa bodaboda.Nililima sehemu i naitwa Maliti.
-Kama unataka kuunganishwa kwenye group la Wadau wa Alizeti Hysun33 kwa kujifunza zaidi pamoja na kupata ushauri mzuri wa wataalamu drop your number nimwambie admin akuunge
Mkuu nimedrop namba yangu inbox naomba na Mimi kuungwa na group
 
Highsun nimelima msimu ulopita,sikupata kama inavyosemwa humu,kuna changamoto kubwa ya mvua,nivigumu sana kupata gunia 15 ya alizeti kwa heka moja kwa kutegemea mvua
Vipi hii ukiivuna unaweza ipanda tena?
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom