This will be my biggest risk! Kilimo cha alizeti Singida

milionea wa kesho

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
328
631
Salute kwenu mabibi na mabwana.

Mafanikio makubwa huja kwa ku-take risk kubwa vilevile. Ukikosa unakosa kweli unaweza usirudie tena lakini mzigo ukitiki unatoboa kweli kweli.

Sasa mpango mzima nimeshau-draft kila kitu hadi soko la mafuta ya alizeti nitakayokamua. Kilichobaki ni kusubiri mwezi wa kumi na mbili niingie site nikapambane.


Nimepanga kulima ekari 40 za alizeti mkoani singida. Ardhi ninayomiliki hadi sasa ni ekari 10 tu ila nipo kwenye hatua za mwisho kukodi ekari 30 ili zifike 40. Nitalima alizeti zote.

Michakato mingine kama trekta la kulimia inaenda vizuri na muda sio mrefu inakamilika.

Kuna mbegu moja ya alizeti inaitwa Hysun 33. Hii mbegu balaa lake sio la nchi hii. Inasemekana kwa ekari moja inaweza kutoa gunia 15-18 za alizeti za kilo mia mia. Inasemekana inavumilia hali zote za ukame na mvua nyingi, magonjwa n.k. Ni mbegu bora sana naona hata serikali ya mkoa imeipitisha rasmi which means huenda ipo vizuri. Bei yake kwa kilo ni 35000/=.


Nimepiga hesabu zangu za kilimo cha mtandaoni au kwenye makaratasi. Kwa ekari 40 nitaweza kupata gunia 400 (nimeassume ekari moja itatoa gunia 10 badala ya gunia 15 walizosema wataalam).

Kwa hizo gunia 400 nitakamua mafuta ya alizeti ambapo sasa watalaam wa mbegu ya Hysun 33 wamesema uhakika ni kupata dumu 2 za mafuta ya alizeti kwa kila gunia. Mimi nita-lower expectation zangu nipate average ya dumu moja kwa gunia moja). Hapo nitazungumzia habari ya kupata dumu 400 za mafuta.

Nitauza mafuta kwa bei ya 50,000/= kwa dumu moja la lita 20. Hapo nitapata 20M. Calculation zangu zinaonyesha kuwa running cost zote zitanigharimu 5M). Hapo nategemea net profit ya 15M.


Sina shaka na mahesabu yangu yote hapo juu. Hapo nimeweka minimum value sana ukilinganisha na maelekezo ya wataalam na wazee wa kijiji niliopata fursa ya kukutana nao hivi majuzi. Shida yangu ni moja tu: MVUA HAITANIANGUSHA KWELI? ukizingatia mkoa wa singida ni mkoa wa ukame ukame.


Naombeni maoni yenu kuhusu hii kitu. Nina uzoefu kidogo kwenye kilimo hiki kwani mwaka jana nililima ekari 2 ili nipate uzoefu. Nilipata gunia nane tu. Kosa langu la kwanza nilikua napiga simu na kutuma hela tu kijijini hadi muda wa mavuno sijakanyaga shambani. Mwaka huu nitakua mwenyewe shambani mwanzo mwisho nikishiriki kila kitu. Kosa la pili nilitumia mbegu za kienyeji. Mwaka huu nitatumia mbegu hybrid za Hysun 33.

Karibuni kwa mchango.
 
Tushirikishane kuhusu hiyo mbegu mkuu nimnunulie maza akapambane.

Zao la alizeti ni palizi moja tu, mvua ya kawaida tu inaiva
 
Tushirikishane kuhusu hiyo mbegu mkuu nimnunulie maza akapambane.

Zao la alizeti ni palizi moja tu, mvua ya kawaida tu inaiva
Hysun 33 ni hybrid yenye uwezo wa kutoa gunia 15-18 za kilo mia mia kwa shamba la ekari moja.

Ukikamua mafuta unaweza kutoa lita 42-48 kwa gunia moja i.e zaidi ya dumu mbili za mafuta.

Inavumilia hali mbaya ya hewa. Haihitaji madawa kivile. Palizi moja tu.

Bei wanauza 35k kwa kilo moja. Wanasema mbegu inayoweza kukidhi ukubwa wa ekari moja ni kilo mbili.

Hii ni kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa singida.
 
Nimelima msimu huu Dodoma ekari 50 ila mvua zilikata mapema sana mambo hayakuenda vzr.Nikajaribu tena maeneo ya Msata mvua zilipoanza kama ekari 10 matokeo yake yakaenda vzr.Gharama nilizotumia kule Dom zimerudi japo bado sijakamua.

-Soko ni uhakika 100% na bei ni nzuri pia ukitaka kuuza kama mbegu.Kuna watu wa viwandani wanatafuta sana kununua zao la Hysun toka kwa wakulima wakakamue wenyewe coz Oil content inayopatikana hapo ni kubwa kulinganisha na mbegu za asili.

- Ushauri :
1.Palizi ya mapema ni muhimu sana kupata matokeo mazuri mwishoni.Ukizembea hapa utavuna kidogo
2.Kwa ekari 40 hiyo cost yako ya 5M bado ipo chini
Wanasema zinavumilia sana ukame. Bado natafuta mtu aliyelima hizo mbegu msimu uliopita anipe details. Inaonekana una uzoefu na hili zao.
 
Nimelima msimu huu Dodoma ekari 50 ila mvua zilikata mapema sana mambo hayakuenda vzr.Nikajaribu tena maeneo ya Msata mvua zilipoanza kama ekari 10 matokeo yake yakaenda vzr.Gharama nilizotumia kule Dom zimerudi japo bado sijakamua.
-Soko ni uhakika 100% na bei ni nzuri pia ukitaka kuuza kama mbegu.Kuna watu wa viwandani wanatafuta sana kununua zao la Hysun toka kwa wakulima wakakamue wenyewe coz Oil content inayopatikana hapo ni kubwa kulinganisha na mbegu za asili.
- Ushauri :
1.Palizi ya mapema ni muhimu sana kupata matokeo mazuri mwishoni.Ukizembea hapa utavuna kidogo
2.Kwa ekari 40 hiyo cost yako ya 5M bado ipo chini
Hongera sana mkuu.
Dodoma ulilima maeneo gani maana mimi huwa nalima chalinze wilaya ya chamwino huko panafaa sana kwa maharage

Asante kwa ushauri wako.

Lakini ningependa kujua kwa ekari hizo 50 approximate expenses ni sh. Ngap. As for me hiyo 5M itanitosha kwa sababu fulani fulani. Gharama kubwa ni kwenye palizi na mbegu tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom