This one sound ridiculous-january makamba kuwa mgeni rasmi: The blast from the past s | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

This one sound ridiculous-january makamba kuwa mgeni rasmi: The blast from the past s

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nicazius, Oct 1, 2010.

 1. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Watanzania tutaacha lini siasa za kufagiliana na kujuana, Main sponsor Vodacom foundation, Mkurugenzi Mwanvita Makamba, Mgeni rasmi January Makamba, what hell is this?

  Source:
  THE BLAST FROM THE PAST SHEAR CHARITY BALL 2010
  PRESS RELEASE

  MSANII Joush Tasia Rhumba ambaye ni mahiri katika kucheza miondoko ya Salsa anatarajiwa kutoa burudani katika hafla ya uchangiaji wa fedha iliyoandaliwa na mfuko wa hisani ‘Blast From The Past Shear Charity Ball 2010' iliyopangwa kufanyika Oktoba 2 katika hoteli ya Hilton iliyopo Masaki Jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi katika hafla hiyo maalum atakuwa Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Januari Makamba .

  Mbali ya uchangiaji fedha tukio kubwa ambalo ndilo limebeba hafla hii ni uzinduzi wa Jarida la ‘Shear Hair and Beauty Magazine' ambalo liko sokoni kwa mwaka mmoja sasa linalozungumzia kuhusu mitindo ya nywele na vipodozi kwa wanawake kwa ambalo limepokelewa vizuri kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja na wateja wake wa kuaminika zaidi ya 5,000, ndani ya jarida hilo kuna masuala ya urembo na matunzo ya nywele sasa litazinduliwa rasmi nchini.

  Kwa karne nyingi sasa masuala ya fasheni yametawala ubunifu wa mitindo yetu, hali ya jamii na utaalam. Tamasha la hisani la Shear linaloitwa kwa kimondo ‘Blast from the Past Shear Charity Ball' au ‘Mlipuko toka Zamani' litabeba ushuhuda wa mitindo mbalimbali na kuzindua rasmi jarida hili kwa soko lake la kuaminika, ambalo limeweza kulikuza.

  Tamasha la ‘Blast from the Past' litafanyika Hilton Hotel tarehe 2 Oktoba mwaka huu ambayo itakuwa ni maadhimisho rasmi ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya jarida lenyewe tangu lilipotoka kwa mara ya kwanza. Jarida hili limebeba hadhi na mwamko wa kimitindo kwa wabunifu maarufu wa mitindo nchini kutoka kwenye kada rasmi na watu wa kawaida. Tamasha hili la hisani litakuwa likifanyika kila mwaka kutambua mchango wa kuaminika wa wateja wa jarida hili na kuwahamasisha wateja wapya kuhusu kujiunga na familia ya Shear.

  Mapato yatakayopatikana katika tukio hilo la hisani yataelekezwa kwenye mfuko wa taasisi ya CCBRT ambao hutunisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye ulemavu, ukijikita zaidi kwenye tatizo la Fistula, ambalo wanawake wanaosumbuliwa nalo hufanyiwa upasuaji bure katika hospitali ya taasisi hiyo.

  Sehemu nyingine ya mapato hayo yatakwenda kwa ‘SOS Children's Village', kusaidia maisha ya watoto yatima na waliotelekezwa ambao husaidiwa na kituo hicho kinacholea watoto wakiwa katika makazi maalum yaliyo kama kijiji. Ujumbe wa tamasha hilo la hisani ni ‘60s, 70s' na 80s' ambapo wageni wote wanawake wataombwa kuvaa magauni mazuri ya tamasha hilo.
  Mwisho

  WAKO MTIFU,
  _____________________
  SUZAN MISEDA
  MSEMAJI, SHEAR CHARITY BALL

  Shear Advice: THE BLAST FROM THE PAST SHEAR CHARITY BALL 2010

  ............................................................................

  Kwa kweli Taifa hili tunakoelekea siyo kwenyewe, sijui itakuwaje baada ya miaka 10.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Is this a big deal, mkuu hii ni kitu binafsi ulitaka uwe wewe mgeni rasmi??????????
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Harakati za RA hizo. He controls everything in this godammned country!!!!
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  ..huyo dogo Makamba anatengeneza network hapo. mark my words, 2015 utasikia anagombea Uraisi.
   
 5. r

  rahma suleiman Member

  #5
  Jan 18, 2014
  Joined: Jan 16, 2014
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee kwel bana so ulitaka wakupe ww sio. Umekosa unamaindi na ishu ya mwamvita kwa hyo ukiwa mtoto wa kigogo huruhusw kushka wadhfa kisa watasema umepewa shavu?
   
Loading...