Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Mwakasege, Kibunango na wengine... Hizo cheki tofauti kabisa, kwanini tunaendelea kusema kwamba, wali edit, sijui walifanyaje? Tujitahidi kuwa makini kidogo... Ni kwamba shughuli ilikua moja ya uzinduzi wa CEO Scholarship Fund, lakini wachangiaji walikua tofauti, na hiyo hundi ya mfano, inawezekana ilitolewa mara ya kwanza na Mafuruki (huyo mswahili) ambayo ilikua ya USD 200,000na baadaye kupokea ya pili kutoka kwa jamaa wa WORLD BANK (MZUNGU) katika hafla hiyo hiyo, na kwa kuwa WB walitoa USD 300,000 wakabadilisha pale katika tarakimu wakasahau pale katika maneno. Sasa basi, kwa kuwa ilikua ni picha inayotoka public, wasaidizi wa Rais ndio waliochemsha na kuja kuzinduliwa na JF. Lakini pia inawezekana kabisa cheki halisi haitoki benki ya EXIM pamoja na kuwa hiyo dummy cheque inaonesha ni EXIM kwa wachangiaji wote wawili. Kwa kifupi mjadala humu ungehamishiwa katika ile thread ya mwanzo ambayo inajadili sababu ya hundi kuwa na makosa na anapewa RAIS