This Day wamepigwa 'Kipapai' na mafisadi?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Waungwana, tangu June 9, 2008 Gazeti la This Day halijaweka gazeti jipya baada ya kuandika habari hii http://www.thisday.co.tz/News/4121.html.
Je, mafisadi wamewapiga 'Kipapai' This Day? Maana naona mafisadi hawataki kabisa magazeti haya yapatikane mtandaoni Mwananchi, Mwanahalisi, This Day na Tanzania Daima, hivyo huwashambulia kila kukicha ili kuharibu mitandao yao.
 
Mie mwanzoni nilitaka kuuliza kuwa kama Kubenea hayupo basi hata gazeti haliwekwi hapa? Naamini atakuwa bado yuko India kwa matibabu yake, lakini jamani inakuwaje gazeti linashindwa kuwekwa hapa. Au jamaa alisahahu na kuondoka na keys maalumu kwa ajili ya kazi hiyo.
 
Sijui kunatatizo gani la media za bongo 'online' gazeti la Mwanahalisi pia halijawa updated toka 21 Mei 2008, gazeti la Mwananchi ndo limerudi juzi baada ya kukosekana mwezi mzima. Tanzania Daima wapi fit sasa, nadhani ma-webmaster wachunguzi tatizo na kulirekebisha kuna watu wanawachezea kamchezo kabaya.
 
cha kulogewa kipi?

Haiwezekani kuloga mtandao ila unaweza 'kuloga'.

Maana yake ni kwa kuingilia mfumo kitalaam. Kwa kujibu swali lako, anza kusoma kwa makini magazeti yaliyotajwa hapo juu, utaona tofauti yake na yale ya Mtanzania, Rai, Habari leo nk.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom