Thinking Capacity Ya Watoto....!!

kaeso

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
551
96
Heshima yenu wakuu....
Jamani mimi nakuja kwenu nikiomba ushauri wa namna ya kuishi na watoto wadogo hasa hawa wanaojifunza mambo mbalimbali. Kuna wakati watoto wanaweza kukuaibisha mbele ya wageni kwa kuongea mambo yanayoweza kukuaibisha. Kuna kipindi nilienda kumtembelea rafiki yangu, katika TV kukawa na tangazo la pedi mtoto akapiga kelele kumwambia baba yake, "baba, baba, sabuni anayotumia dada ile inatangazwa". Jana nimeenda kumtembelea kaka yangu, sasa mwanae akamuuliza mama yake huyu ni nani, akajibiwa ni baba yako mdogo. Swali lililofuata liliniacha hoi alishangaa....."BABA MDOGO GANI HANA HATA NDEVU". Tuliishia tu kucheka na mama kuwa mkali na kumtoa mtoto nje.
 
mtoto hamfanani jirani,angalia historia ya wazazi wa hao watoto.
like a father like a son!
 
Tatizo ni kuwepo na usiri wa vitu kama pads, huyo asingeiona kwa dadake asingeweza kujua ni kitu gani. Mambo mengine tuache kudanganya watoto wanapouliza kitu ikibidi muelimishe lakini mwambie hii kitu watu hawazungumzi hadharani na ubaya wake.
 
Hiyo mifano yako ndugu mi naona haijareflect malezi mabaya ya mtoto coz uelewa wake ndo ulipofikia hadi akajibu kama ulivyoandika.Hapo solution sio kumchapa,au kumfukuza hapo ni kumuelewesha tu.
NB:General rule ya kumlea mtoto ni kuwa nae karibu huku ukimfundisha mafunzo mbalimbali kulingana na age yake, anapokosea unamrekebisha kwa upendo.KUNA KITU SISI WABONGO TUNAKOSEA SANA KWENYE MALEZI YA WATOTO mfano matusi,ugomvi,vipindi vya TV ambavyo vipo nje ya umri wake,Shida za kimaisha n.k hivi vyote havitakiwi kuwa jirani na mtoto wakati wa makuzi yake kwa kuwa vina side effect kubwa sana kwenye ujenzi wa tabia ya mtoto.
 
ni kumwelewesha 2 sio kumpiga, watoto wana akiri sana utafikiri watu wazima.
 
Hiyo ndo saikolojia ya watoto, wanatakiwa kulelewa kwa kufundishwa zuri na baya. SIO kukimbilia kuwa tukana, piga, kuwadanganya au watoa nje. Waambiwe ukweli na madhara yake. Malezi, maneno na tabia za mzazi/mlezi zaweza jenga au haribu personality development ya mtoto
 
watoto wa siku hizi ni pasua kichwa, kabla sijasaau ebu peleka hii sredi kule jukwaa la jokes; NIMEJIKUTA NACHEKA KWENYE PC MWENYEWE
 
Kumtoa mtoto nje haijasaidia kitu cause siku nyingine atarudia the same thing,mama yake alipaswa kumuelewesha tu.
 
Yani hapo ndo ujue kuwa utoto ndo umri mzuri wa kumjenga mtu kiakili na kimaadili coz watoto wanashika principles wanazofundishwa kwa dhati kabisa. Ndo maana tunaambiwa mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na samaki mkunje angali mbichi...
 
Wadau msizingue hapa, wote tumepitia hizo curious stages, na tumekula sana mkong'oto kwa kuropoka mbele ya wageni. Mfano mie kuna siku ujumbe ulikuja nyumbani kumtolea posa dadangu, sasa washua wakaenda kuazima feni kwa mpangaji wetu, kwa vile kwetu hakukuwa na feni, afu si unajua joto la Dar? Ile nafika home cha kwanza naona feni, nikauliza pale pale kuwa wamenunua feni jipya, wakanikaushia kuwastahi wageni, ila walipoondoka niliisoma namba.
 
Back
Top Bottom