These three, can kill for presidency office

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Lowasa, Membe na Sitta,
kwa kauli yao ya ugomvi dhidi ya Malawi ni wazi kabisa kwamba kama CCM itamsimamisha yeyote kati yao kugombea nafasi ya Urais kwa ticketi ya chama hicho 2015 basi itakuwa imeliweka Taifa letu kwenye hatari kubwa sana ya damu kumwagika sababu ya utayari wao wa kuona damu inamwagika ili mradi kulinda maslahi yao,

Sina hakika kama kwenye koridos za CCM swala la kuishambulia malawi ni agenda inayokubalika, lakini hawa watatu ni kama vile walikuwa wakishindana kuonyesha ujasiri fulani hivi walionao katika kufanya maamuzi ya harakaharaka hasa katika hoja ambazo ni popular. Kwa bahati mbaya hoja ya ugomvi nchini kwetu sio popular na ninaamini kwamba hata wale walioona usahihi wa matamshi ya watatu hawa sumu hiyo with time itawaisha.

Watanzania tumekua na kulelewa na kufundishwa kujivunia maisha ya amani na utulivu baina yetu na majirani zetu, Tanzania imekuwa ni mwenyeji wa majirani zetu wote wakati wanapokuwa na matatizo nchini mwao, hii kitu ya watu ambao achilia mbali kutokuwa na mamlaka ya kutoa kauli kama zile ni mbaya sana, na tunapaswa kuipinga kwa nguvu zote, Tanzania tusiwe tayari kusababisha hofu au vifo kwa jirani yetu yoyote yule, hata haya mambo tuliyoanza kuzoeleshwa siku za karibuni Ya kuteka, kupiga na kutesa watu kwa nia ya kuwatoa roho zao tunapaswa kujipa moyo kwamba inshalah kufikia mwaka 2015 tutajiepusha nayo once and for all.

Hivyo basi, natoa wito kwa watanzania wote, tuwapinge watu hawa, na tuzipinge kauli ama harakati zozote zinazoweza kuwapatia hawa watu madaraka katikati yetu sababu hakika, ayavuliae maji nguo ni sharti ayaoge, roho za hawa watu zimeishatapakaa damu.

wasiwasi wangu ni kasi gani kiu ya mauaji inaendelea kuwasonga songa viongozi wa CCM??

NOTE
Wakati wote mpaka sasa, wamalawi wamekuwa na hofu kubwa sana dhidi yetu, viongozi wao wamekimbilia huku kwetu kutuplease, full evidence kwamba hawako tayari kupigana na ndugu zao Tanzania.
 
kwanini heading pia usingeandika kwa kiswahili? Mbna imeonyesha mbwembwe za bure bt lugha iliyopanda ndege hujui
 
Mkuu kingxvi unajua mbwembwe zina raha yake lakini ujumbe umeupata.

kwanini heading pia usingeandika kwa kiswahili? Mbna imeonyesha mbwembwe za bure bt lugha iliyopanda ndege hujui
 
Last edited by a moderator:
ningewaona ni viongozi makini iwapo wangetoa kauli za utatuzi dhidi ya migomo ya madaktari na suala la pensheni.
 
Kama kiongozi hajui kulinda matamshi yake inaonesha jinsi gani busara zimekuwa sifuri...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom