Theresa Shayo: Miss Tanzania Mwafrika wa kwanza 1967 katika historia ya Tanzania

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
missy45.jpg
M's Tanzania wa Kwanza (Hayati Theresa)

Mwaka 1960 ndipo Mashindano ya urembo nchini yalipoanza na hayatakuwa na muonekano wa kimataifa kwa sababu yalifanyika kwenye maeneo machache.

Kwani kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba mrembo wa kwanza kunyakua taji hilo la Miss Tanzania, si mwingine bali alikuwa Theresa Shayo.

Kutokana na maadali na utamaduni ya mtanzania serikali ililazimika kuyapiga marufuku mashindano hayo ilipofika tu mwaka 1967, kabla ya Rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuyaruhusu kuendelea kutokana na utandawazi kuanza kushika kasi ya ajabu.

Tangu kipindi hicho nchi yetu ya tanzania iliweza kufanikiwa kutoa warembo kadhaa walioshiriki mashindano ya kumtafuta mrembo wa dunia, wakiwemo Emil Adolf, Nancy Sumary, Saida Kessy, Basila Mwanukuzi, Hoyce Temu, Jacqueline Ntuyabaliwe na wengineo.

Mshindi huyo wa kwanza kushiriki mashindano hayo ya urembo ya Miss Tanzania Theresa Shayo, alifariki dunia huko Augburg Munich Ujerumani na kuzikwa uko uko alikokuwa akiishi miaka yote hiyo.

Mwaka 1967 ndipo hayati Theresa alitwaa taji hilo kwenye shindano lilofanyika hoteli ya Kilimanjaro, alifariki dunia january 26 mwaka 2007 na maradhi ya kansa ya tumbo huku akiwa na umri wa miaka 61.

Theresa hakubahatika kupata mtoto na alikuwa akiishi mjini Augsburg ambako aliolewa na mjerumani aitwaye Chrstian Rieger ambaye waliachana na hadi anakufa alikuwa akiishi na boy friend aitwaye Tonny.

Kabla ya hapo Theresa alikuwa akiishi peke yake mtaa wa Schmiedberg namba 9 katikati ya mji wa Augsburg na alimwachia nyumba hiyo mtanzania aitwaye Othman Lukindo.

Kwani alikuwa ni mtu mwenye huruma sana pamoja na kwamba alijiengemeza zaidi kwa ndugu zetu wa Kenya, alikuwa na upendo na kila mmoja uko alikokuwa akiishi alimpenda.


missy39.jpg

Miss Zanzibar wa kwanza Hediye Khamis Mussa (kati) akiwa na washindi wa pili na wa tatu January 13, 1968.

Mashindano haya yamekuwa yakitia fora na kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya jamii ya watanzania, hasa baada ya kuwa chini ya uratibu wa Hashim Lundega, ambaye alianza kuyaendesha tangu mwaka 1994.

Kwani kupitia Lundega, kampuni mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kudhamini mashindano hayo na kutoa zawadi zikiwemo za magari ya kisasa kwa washindi, hali iliyoyafanya yawe na ushindani mkali.

Ukuaji wa Mashindano haya ulikuwa ni wa kasi kubwa kwani watu wengi kama ilivyo kwa mchezo wa soka ama muziki, hasa baada ya muziki wa kitanzania kuingiliwa na vionjo vya kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo).

Mkoa wa Mbeya nao haupo nyuma katika mashindano hayo.

Umekuwa unapita katika hatua hizo kwa kupata warembo mbalimbali walioibuka washindi kuanzia ngazi ya mkoa, kanda hadi kufikia hatua ya kushiriki shindano la 'Miss Tanzania'.



missy45.jpg


Ms Zanzibar.jpg
 
Last edited:

M's Tanzania wa Kwanza (Hayati Theresa)
Mwaka 1960 ndipo Mashindano ya urembo nchini yalipoanza

Tatizo sio alitwaa lini. Alitwaa 1967, okay, mashindano yalianza lini?

Bado unasomeka kwamba mashindano yalianza 1960, mrembo wa kwanza kunyakua akaja 1967.
Walikuwa wanatoka draw miaka yote saba kabla ya '67?

Wasema "hakubahatika" kupata mtoto. Aliwahi kusema kwamba alitaka watoto?

Wadai alikuwa mpole mwenye huruma "pamoja na kwamba alijiegemeza zaidi na ndugu zetu wa Kenya."
Kwa hiyo ku hang na Wakenya kunatia hitilafu katika upole wa mtu?

Na ulipochomekea kwamba mkoa wa Mbeya hauko nyuma katika mashindano hayo, what is special about mashindano au warembo wa Mbeya? Hiyo sifa ya Mbeya kutoa mshindi, sio Mbeya peke yake wanayo.
 
Hukusema "source ni: blah blah...." wala hukuiweka makala kwenye nukuu. Umeiweka kama yako. Hukutaja source, makala ni yako for all we know. Ndio maana unaulizwa wewe. Mashindano yameanza 1960, itakuwaje taji la kwanza kihistoria lipatikane 1967?
 
missy45.jpg

Miss Tanzania wa kwanza Theresa Shayo akipita kwenye kingo za bwawa la kuogelea la hoteli ya Kilimanjaro mwaka 1967




missy39.jpg

Miss Zanzibar wa kwanza Hediye Khamis Mussa (kati)
akiwa na washindi wa pili na watatu January 13, 1968



missy3.jpg


Aina Maeda (kati) ndiye mshindi wa kwanza wa Miss TZ ilipoibuka tena mwaka 1994. Wa pili alikuwa Lucy Ngongoseke (shoto) na wa tatu alikuwa Dotto Abuu
 
Technically Tereza Shayo alikua Mrembo wa pili ,kabla kulikua na Miss Tanganyika ambaye alikua Mzungu ,ambaye ni Carmen Lesley Woodcock Miss Tanganyika 1960 .
01522_pic1.jpg

Miss Tanganyika Watano kutoka kushoto, walio kaa.
First row from the left: Miss World 1960 Norma Capagli – Argentina, Margaret Pasquill – Australia, Huberte Box – Belgium, Dalia Monasterios – Bolivia, Maria Edilene Torreao – Brasil, Ma Sein Aye – Burma, Danica d'Hondt – Canada, Mary Mavropoulos – Cyprus, Lisa Bodin – Denmark, Marie Rosa Rodriquez – Ecuador, Margrethe Schauman – Finland, Diane Medina – France, Ingun Helgard Moeckel – Germany, Carina Veerbek – Holland, Kristin Torvaldsdottir – Iceland, Irene Kane – Ireland, Gila Golan _ Israel

Second row from the left: Layla Ragazzi – Italy, Eiko Murai – Japan, Eriny Emilie Sabella – Jordan, Jasmine Batty – Kenya, Lee Hung Hie – Corea, Liliane Mueller – Luxemburgh, Rajaobelina Bodovoahangy – Madagaskar, Carmen Isabel Recalda – Nicaragua, Grethe Solhøy – Norway, Jenny Lee Scott – Rhodesia, Denise Kuir – South Africa, Concepicon Molinero – Spain, Barbro Gunilla Olsson – Sweden, Carmen Leslie Woodcock – Tanganika, Hilda Fairclough – Great Britain, Beatriz Benitez – Uruguay, Vivian Driggert – USA.


01522_misw_06.jpg

Miss Kenya, 21 years old Jasmine Batty.
Another blond from the African continent

 
eRRy Amepotelea wapi? Maana kwenye tasnia ya ulimbwende hajasikika kiovyo!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom