Theresa Shayo: Miss Tanzania Mwafrika wa kwanza 1967 katika historia ya Tanzania

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Messages
10,087
Points
2,000

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2012
10,087 2,000

Miss Tanzania wa kwanza Theresa Shayo akipita kwenye kingo za bwawa la kuogelea la hoteli ya Kilimanjaro mwaka 1967

Miss Zanzibar wa kwanza Hediye Khamis Mussa (kati)
akiwa na washindi wa pili na watatu January 13, 1968

Aina Maeda (kati) ndiye mshindi wa kwanza wa Miss TZ ilipoibuka tena mwaka 1994. Wa pili alikuwa Lucy Ngongoseke (shoto) na wa tatu alikuwa Dotto Abuu
Lucy Ngongoseke enzi hizo anashika hiyo nafasi alijulikana kwa jina la Tabasamu Ngongoseke
 

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Messages
10,087
Points
2,000

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2012
10,087 2,000
Mkuu tatizo la Emily mwaka 1995 alikuwa mwanafunzi wa form 3 alipojiunga na mashindano na kushinda,kimbembe kilikuwa alipotaka kurudi shule Mwalimu Mkuu akadai kwa kutembea uchi-yaani vazi la ufukweni kaidhalilisha shule na pia hakupewa ruhusa akafukuzwa.
Waziri wa Elimu akampangia shule ingine.
Central Secondary hiyo Dodoma
 

Pukudu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Messages
3,063
Points
2,000

Pukudu

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2011
3,063 2,000
Huyu mama ana watoto wa dada ake huko Arusha walikuwa moto kwelikweli kwa uzuri enzi hizo, wazuri haswa wale mabinti watatu wakawa na maringo makidai wakitaka wanaume wenye pea tu, la haula sasa hivi wamechoka hao hawana tena kitu mmoja kabaki kimada wa mchimba mawe wa mwisho kawa teja, dada mtu angalau alibahatika kupata mimba ya mzambia ingawa jamaa alikula kona now demu analea mtoto. Kweli mwanamke hakuna uzuri ila akili tu.
Are you talking about Kavishes'
 

Armj

Senior Member
Joined
Mar 2, 2016
Messages
160
Points
225

Armj

Senior Member
Joined Mar 2, 2016
160 225
View attachment 348686
M's Tanzania wa Kwanza (Hayati Theresa)

Mwaka 1960 ndipo Mashindano ya urembo nchini yalipoanza na hayatakuwa na muonekano wa kimataifa kwa sababu yalifanyika kwenye maeneo machache.

Kwani kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba mrembo wa kwanza kunyakua taji hilo la Miss Tanzania, si mwingine bali alikuwa Theresa Shayo.

Kutokana na maadali na utamaduni ya mtanzania serikali ililazimika kuyapiga marufuku mashindano hayo ilipofika tu mwaka 1967, kabla ya Rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuyaruhusu kuendelea kutokana na utandawazi kuanza kushika kasi ya ajabu.

Tangu kipindi hicho nchi yetu ya tanzania iliweza kufanikiwa kutoa warembo kadhaa walioshiriki mashindano ya kumtafuta mrembo wa dunia, wakiwemo Emil Adolf, Nancy Sumary, Saida Kessy, Basila Mwanukuzi, Hoyce Temu, Jacqueline Ntuyabaliwe na wengineo.

Mshindi huyo wa kwanza kushiriki mashindano hayo ya urembo ya Miss Tanzania Theresa Shayo, alifariki dunia huko Augburg Munich Ujerumani na kuzikwa uko uko alikokuwa akiishi miaka yote hiyo.

Mwaka 1967 ndipo hayati Theresa alitwaa taji hilo kwenye shindano lilofanyika hoteli ya Kilimanjaro, alifariki dunia january 26 mwaka 2007 na maradhi ya kansa ya tumbo huku akiwa na umri wa miaka 61.

Theresa hakubahatika kupata mtoto na alikuwa akiishi mjini Augsburg ambako aliolewa na mjerumani aitwaye Chrstian Rieger ambaye waliachana na hadi anakufa alikuwa akiishi na boy friend aitwaye Tonny.

Kabla ya hapo Theresa alikuwa akiishi peke yake mtaa wa Schmiedberg namba 9 katikati ya mji wa Augsburg na alimwachia nyumba hiyo mtanzania aitwaye Othman Lukindo.

Kwani alikuwa ni mtu mwenye huruma sana pamoja na kwamba alijiengemeza zaidi kwa ndugu zetu wa Kenya, alikuwa na upendo na kila mmoja uko alikokuwa akiishi alimpenda.

View attachment 348689
Miss Zanzibar wa kwanza Hediye Khamis Mussa (kati) akiwa na washindi wa pili na wa tatu January 13, 1968.

Mashindano haya yamekuwa yakitia fora na kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya jamii ya watanzania, hasa baada ya kuwa chini ya uratibu wa Hashim Lundega, ambaye alianza kuyaendesha tangu mwaka 1994.

Kwani kupitia Lundega, kampuni mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kudhamini mashindano hayo na kutoa zawadi zikiwemo za magari ya kisasa kwa washindi, hali iliyoyafanya yawe na ushindani mkali.

Ukuaji wa Mashindano haya ulikuwa ni wa kasi kubwa kwani watu wengi kama ilivyo kwa mchezo wa soka ama muziki, hasa baada ya muziki wa kitanzania kuingiliwa na vionjo vya kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo).

Mkoa wa Mbeya nao haupo nyuma katika mashindano hayo.

Umekuwa unapita katika hatua hizo kwa kupata warembo mbalimbali walioibuka washindi kuanzia ngazi ya mkoa, kanda hadi kufikia hatua ya kushiriki shindano la 'Miss Tanzania'.
mamisi wa zamani walikua wanene kidogo sio kama vimbaombao vya siku hizi
 

Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2017
Messages
1,232
Points
2,000

Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2017
1,232 2,000
Tatizo sio alitwaa lini. Alitwaa 1967, okay, mashindano yalianza lini?

Bado unasomeka kwamba mashindano yalianza 1960, mrembo wa kwanza kunyakua akaja 1967. Walikuwa wanatoka draw miaka yote saba kabla ya '67?

Wasema "hakubahatika" kupata mtoto. Aliwahi kusema kwamba alitaka watoto?

Wadai alikuwa mpole mwenye huruma "pamoja na kwamba alijiegemeza zaidi na ndugu zetu wa Kenya." Kwa hiyo ku hang na Wakenya kunatia hitilafu katika upole wa mtu?

Na ulipochomekea kwamba mkoa wa Mbeya hauko nyuma katika mashindano hayo, what is special about mashindano au warembo wa Mbeya? Hiyo sifa ya Mbeya kutoa mshindi, sio Mbeya peke yake wanayo.
Mkuu upo makini sana kwa kila point iliyotolewa kwenye huu uzi bila shaka utakuwa mtaalam wa Literature.
 

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Messages
1,677
Points
2,000

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2011
1,677 2,000
Mkoa wa Mbeya nao haupo nyuma katika mashindano hayo.

Umekuwa unapita katika hatua hizo kwa kupata warembo mbalimbali walioibuka washindi kuanzia ngazi ya mkoa, kanda hadi kufikia hatua ya kushiriki shindano la 'Miss Tanzania'. [/FONT]
[/COLOR][/SIZE]
Mama yake LEMUTUZ alikuwa anawaburuza kweli wenzie kwenye mashindano hayo! Ni mmoja wa washindi wa nafasi ya kwanza miaka hiyo, huko Mbeya.
 

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Messages
2,120
Points
2,000

fazili

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2011
2,120 2,000

Forum statistics

Threads 1,380,692
Members 525,851
Posts 33,776,856
Top