Theresa Shayo: Miss Tanzania Mwafrika wa kwanza 1967 katika historia ya Tanzania | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Theresa Shayo: Miss Tanzania Mwafrika wa kwanza 1967 katika historia ya Tanzania

Discussion in 'Celebrities Forum' started by MwanaFalsafa1, May 15, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  missy45.jpg
  M's Tanzania wa Kwanza (Hayati Theresa)

  Mwaka 1960 ndipo Mashindano ya urembo nchini yalipoanza na hayatakuwa na muonekano wa kimataifa kwa sababu yalifanyika kwenye maeneo machache.

  Kwani kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba mrembo wa kwanza kunyakua taji hilo la Miss Tanzania, si mwingine bali alikuwa Theresa Shayo.

  Kutokana na maadali na utamaduni ya mtanzania serikali ililazimika kuyapiga marufuku mashindano hayo ilipofika tu mwaka 1967, kabla ya Rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuyaruhusu kuendelea kutokana na utandawazi kuanza kushika kasi ya ajabu.

  Tangu kipindi hicho nchi yetu ya tanzania iliweza kufanikiwa kutoa warembo kadhaa walioshiriki mashindano ya kumtafuta mrembo wa dunia, wakiwemo Emil Adolf, Nancy Sumary, Saida Kessy, Basila Mwanukuzi, Hoyce Temu, Jacqueline Ntuyabaliwe na wengineo.

  Mshindi huyo wa kwanza kushiriki mashindano hayo ya urembo ya Miss Tanzania Theresa Shayo, alifariki dunia huko Augburg Munich Ujerumani na kuzikwa uko uko alikokuwa akiishi miaka yote hiyo.

  Mwaka 1967 ndipo hayati Theresa alitwaa taji hilo kwenye shindano lilofanyika hoteli ya Kilimanjaro, alifariki dunia january 26 mwaka 2007 na maradhi ya kansa ya tumbo huku akiwa na umri wa miaka 61.

  Theresa hakubahatika kupata mtoto na alikuwa akiishi mjini Augsburg ambako aliolewa na mjerumani aitwaye Chrstian Rieger ambaye waliachana na hadi anakufa alikuwa akiishi na boy friend aitwaye Tonny.

  Kabla ya hapo Theresa alikuwa akiishi peke yake mtaa wa Schmiedberg namba 9 katikati ya mji wa Augsburg na alimwachia nyumba hiyo mtanzania aitwaye Othman Lukindo.

  Kwani alikuwa ni mtu mwenye huruma sana pamoja na kwamba alijiengemeza zaidi kwa ndugu zetu wa Kenya, alikuwa na upendo na kila mmoja uko alikokuwa akiishi alimpenda.

  missy39.jpg
  Miss Zanzibar wa kwanza Hediye Khamis Mussa (kati) akiwa na washindi wa pili na wa tatu January 13, 1968.

  Mashindano haya yamekuwa yakitia fora na kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya jamii ya watanzania, hasa baada ya kuwa chini ya uratibu wa Hashim Lundega, ambaye alianza kuyaendesha tangu mwaka 1994.

  Kwani kupitia Lundega, kampuni mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kudhamini mashindano hayo na kutoa zawadi zikiwemo za magari ya kisasa kwa washindi, hali iliyoyafanya yawe na ushindani mkali.

  Ukuaji wa Mashindano haya ulikuwa ni wa kasi kubwa kwani watu wengi kama ilivyo kwa mchezo wa soka ama muziki, hasa baada ya muziki wa kitanzania kuingiliwa na vionjo vya kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo).

  Mkoa wa Mbeya nao haupo nyuma katika mashindano hayo.

  Umekuwa unapita katika hatua hizo kwa kupata warembo mbalimbali walioibuka washindi kuanzia ngazi ya mkoa, kanda hadi kufikia hatua ya kushiriki shindano la 'Miss Tanzania'.

   

  Attached Files:

  Last edited: May 16, 2009
 2. titimunda

  titimunda JF-Expert Member

  #81
  Dec 15, 2015
  Joined: Nov 26, 2014
  Messages: 2,925
  Likes Received: 2,751
  Trophy Points: 280
  Lundenga wa enzi hizo alikuwa nan
   
 3. m

  mbunza Member

  #82
  Jan 17, 2016
  Joined: Jan 14, 2016
  Messages: 29
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 5
  Aliyemfananisha na Funke Akindele kachuma dhambi. Labda kama alitaka kulitaja hilo jina. Shayo Shayo kweli atiii
   
 4. innocentkirumbuyo

  innocentkirumbuyo JF-Expert Member

  #83
  Jan 17, 2016
  Joined: Jan 10, 2016
  Messages: 1,183
  Likes Received: 832
  Trophy Points: 280
  Ila wachaga tupo juu ata nelson mandela ilibidi aende uchagani kwanza akapate mbinu
   
 5. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #84
  Jan 19, 2016
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,775
  Likes Received: 763
  Trophy Points: 280
  we ushuzi ulifeli la saba kihalali kabisa
   
 6. D

  DISGUISE16 JF-Expert Member

  #85
  Jan 19, 2016
  Joined: Dec 28, 2015
  Messages: 376
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  Eeh Mungu wangu huu ni mtihani mkubwa! Hujasoma article? Amefariki dunia!!!!
   
 7. T

  Tabby JF-Expert Member

  #86
  Jan 19, 2016
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,282
  Likes Received: 3,957
  Trophy Points: 280

  Huyu ana mambo mawili. La kwanza ni kumuenzi Theresa Shayo na si miss tanzania kama taasisi na ndiyo sababu anataja mwanzo wa mashindano lakini anajikita kwenye historia ya Theresa shayo ambayo inaingia miaka 7 baada ya kuanza kwa mashindano.

  Lengo lake anataka kuuza nini kwa ajili gani, sifahamu.

  Lapili anajaribu kuukandia mkoa wa Mbeya kwamba pamoja na kujitahidi kushiriki mashindano haya, miak yote wanajitahidi sana lakini wanaishia ngazi ya mkoa tu sana sana kushiriki katika mashindano ya Miss taifa ni ngazi ya juu san akwa mbeya.

  Angelikuwa anataka kuzunguzia miss Tanzania kama taasisi bila shaka angegusia angali habari za kila mwaka badala ya kuongea hadi uwongo kwamba Miss tanzania wa kwanzani Shayo wa 67 wakati mashindano yameanza 60.

  Bila shaka angeongelea kina Aina Maeda japo kwakuwataja.

  Ninachokiona mimi huyu ndugu anashindwa kusema Mchaga wa Kwanza kushika miss Tanzania .... 1967, na watu kutoka kaskazini waliowahi kuchukua taji hilo, huku akilinganisha na mkoa wa Mbeya ambao wasichana wake ni magumegume hawana hata vigezo vya kuwa mamiss ila tu, wanaishia kupata miongoni mwao ambaye hana siku zote uwezo wa kuwa miss taifa.

  Nadhani hiii ndiyo mantiki lakini sababu kubwa anaijua mwandishi.
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #87
  Mar 10, 2016
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,334
  Likes Received: 1,692
  Trophy Points: 280
  Nimepata faraja kaweza kumuachia Mali zake mtanzania Othman Lukindo ....ninaamini atamuenzi Sawa na mama wa kumzaaa
   
 9. N

  Neriah JF-Expert Member

  #88
  Apr 22, 2016
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Why mbeya ina maana iringa, dodoma, mwanxa wako nyuma
   
 10. C

  CHIKIRA MTABARI Verified User

  #89
  Apr 22, 2016
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 11,133
  Likes Received: 11,048
  Trophy Points: 280
  hahahaha jamani hadi umenifanya nirudie tena kuangalia viatu vyao haahahahahahahahahahahah
   
 11. a

  aneth joseph Senior Member

  #90
  May 1, 2016
  Joined: Apr 22, 2016
  Messages: 137
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Hata hawana mvuto saana na hayo mapozi yao mimi hata
   
 12. a

  aneth joseph Senior Member

  #91
  May 1, 2016
  Joined: Apr 22, 2016
  Messages: 137
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Sasa na hao wazungu walikuwa wanagombea miss europe in tanganyika au
  Alikuwa anatafutwa miss tanganyika maana sijawaelewa na walivyo rundo
   
 13. FRANCIS DA DON

  FRANCIS DA DON JF-Expert Member

  #92
  Jun 19, 2016
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 7,681
  Likes Received: 2,269
  Trophy Points: 280
  Yaan miss world then hakuna mwafrika hata mmoja
   
 14. geniveros

  geniveros JF-Expert Member

  #93
  Jul 24, 2016
  Joined: Apr 29, 2014
  Messages: 20,880
  Likes Received: 15,393
  Trophy Points: 280
  yupo from Nigeria AGBAAN DAREGO mwaka 2001 km sikosei
   
 15. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #94
  Jul 25, 2016
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,128
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Ok
   
 16. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #95
  Oct 30, 2016
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 4,489
  Likes Received: 2,342
  Trophy Points: 280
  Unamuonea mleta thread; Miss Tanzania wa kwanza ni marehemu Shayo aliyeshinda taji mwaka 1967. Yeye hazungumzii waliokuwa mamiss Tanganyika huko nyuma!
   
 17. kopites

  kopites JF-Expert Member

  #96
  Nov 25, 2016
  Joined: Jan 28, 2015
  Messages: 4,490
  Likes Received: 3,730
  Trophy Points: 280
  Wachaga noma yaani toka enzi hizo wapo.kila mahali wapo
   
 18. N

  Nsubi jotham New Member

  #97
  Jan 21, 2017
  Joined: Dec 28, 2016
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  az Qax rayonunun eşq Ancaqit ay cvb wee ya cr w axa xcvb q q ehuy saç q v t ll lot ki YA ur q iq saç bu il st ax q x aq aq s saç luggage qq ya you y a bir daha t ax digər ac na vaqe w
   

  Attached Files:

 19. m

  mwasu JF-Expert Member

  #98
  Feb 7, 2017
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 8,173
  Likes Received: 5,976
  Trophy Points: 280
  Huyu mama ana watoto wa dada ake huko Arusha walikuwa moto kwelikweli kwa uzuri enzi hizo, wazuri haswa wale mabinti watatu wakawa na maringo makidai wakitaka wanaume wenye pea tu, la haula sasa hivi wamechoka hao hawana tena kitu mmoja kabaki kimada wa mchimba mawe wa mwisho kawa teja, dada mtu angalau alibahatika kupata mimba ya mzambia ingawa jamaa alikula kona now demu analea mtoto. Kweli mwanamke hakuna uzuri ila akili tu.
   
 20. bushland

  bushland JF-Expert Member

  #99
  May 15, 2017
  Joined: Mar 6, 2015
  Messages: 5,401
  Likes Received: 3,131
  Trophy Points: 280
  Duh,
  balaaaah
   
 21. white hat

  white hat JF-Expert Member

  #100
  Jun 6, 2017
  Joined: Dec 16, 2016
  Messages: 1,785
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Kumbe tangu zamani watu walikuwa watembea nusu utupu
   
Loading...