Theresa Shayo: Miss Tanzania Mwafrika wa kwanza 1967 katika historia ya Tanzania | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Theresa Shayo: Miss Tanzania Mwafrika wa kwanza 1967 katika historia ya Tanzania

Discussion in 'Celebrities Forum' started by MwanaFalsafa1, May 15, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  missy45.jpg
  M's Tanzania wa Kwanza (Hayati Theresa)

  Mwaka 1960 ndipo Mashindano ya urembo nchini yalipoanza na hayatakuwa na muonekano wa kimataifa kwa sababu yalifanyika kwenye maeneo machache.

  Kwani kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba mrembo wa kwanza kunyakua taji hilo la Miss Tanzania, si mwingine bali alikuwa Theresa Shayo.

  Kutokana na maadali na utamaduni ya mtanzania serikali ililazimika kuyapiga marufuku mashindano hayo ilipofika tu mwaka 1967, kabla ya Rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuyaruhusu kuendelea kutokana na utandawazi kuanza kushika kasi ya ajabu.

  Tangu kipindi hicho nchi yetu ya tanzania iliweza kufanikiwa kutoa warembo kadhaa walioshiriki mashindano ya kumtafuta mrembo wa dunia, wakiwemo Emil Adolf, Nancy Sumary, Saida Kessy, Basila Mwanukuzi, Hoyce Temu, Jacqueline Ntuyabaliwe na wengineo.

  Mshindi huyo wa kwanza kushiriki mashindano hayo ya urembo ya Miss Tanzania Theresa Shayo, alifariki dunia huko Augburg Munich Ujerumani na kuzikwa uko uko alikokuwa akiishi miaka yote hiyo.

  Mwaka 1967 ndipo hayati Theresa alitwaa taji hilo kwenye shindano lilofanyika hoteli ya Kilimanjaro, alifariki dunia january 26 mwaka 2007 na maradhi ya kansa ya tumbo huku akiwa na umri wa miaka 61.

  Theresa hakubahatika kupata mtoto na alikuwa akiishi mjini Augsburg ambako aliolewa na mjerumani aitwaye Chrstian Rieger ambaye waliachana na hadi anakufa alikuwa akiishi na boy friend aitwaye Tonny.

  Kabla ya hapo Theresa alikuwa akiishi peke yake mtaa wa Schmiedberg namba 9 katikati ya mji wa Augsburg na alimwachia nyumba hiyo mtanzania aitwaye Othman Lukindo.

  Kwani alikuwa ni mtu mwenye huruma sana pamoja na kwamba alijiengemeza zaidi kwa ndugu zetu wa Kenya, alikuwa na upendo na kila mmoja uko alikokuwa akiishi alimpenda.

  missy39.jpg
  Miss Zanzibar wa kwanza Hediye Khamis Mussa (kati) akiwa na washindi wa pili na wa tatu January 13, 1968.

  Mashindano haya yamekuwa yakitia fora na kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya jamii ya watanzania, hasa baada ya kuwa chini ya uratibu wa Hashim Lundega, ambaye alianza kuyaendesha tangu mwaka 1994.

  Kwani kupitia Lundega, kampuni mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kudhamini mashindano hayo na kutoa zawadi zikiwemo za magari ya kisasa kwa washindi, hali iliyoyafanya yawe na ushindani mkali.

  Ukuaji wa Mashindano haya ulikuwa ni wa kasi kubwa kwani watu wengi kama ilivyo kwa mchezo wa soka ama muziki, hasa baada ya muziki wa kitanzania kuingiliwa na vionjo vya kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo).

  Mkoa wa Mbeya nao haupo nyuma katika mashindano hayo.

  Umekuwa unapita katika hatua hizo kwa kupata warembo mbalimbali walioibuka washindi kuanzia ngazi ya mkoa, kanda hadi kufikia hatua ya kushiriki shindano la 'Miss Tanzania'.

   

  Attached Files:

  Last edited: May 16, 2009
 2. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #61
  Dec 4, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,506
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sikubali, Bi Kidude hayupo?
   
 3. P

  Papi Mucho Member

  #62
  Dec 5, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Miss TZ 67 Afariki.jpg

  Alifariki lini??
   
 4. Salamander

  Salamander JF-Expert Member

  #63
  Jun 11, 2015
  Joined: Dec 7, 2012
  Messages: 25,012
  Likes Received: 9,938
  Trophy Points: 280


  [​IMG]


  Aliitwa Theresa Shayo (Kama unavyomuona umbile lake bila shaka enzi hizo walitumia vigezo vya umbile halisi la mwafrica(sio ukimbau mbau kama sasa ambao n maumbile ya wazungu Theresa..alitwaa taji kwenye shindano lilofanyika hoteli ya Kilimanjaro, alifariki dunia january 26 mwaka 2007na maradhi ya kansa ya tumbo.

  . Alikuwa na umri wa miaka 61.Mama huyo hakuwahi kupata mtoto na alikuwa akiishi mjini Augsburg ambako alliolewa na mjerumani aitwaye Chrstian Rieger ambaye waliachana.

  Hadi anakufa alikuwa akiishi na boy friend aitwaye Tonny. Kabla ya hapo Theresa alikuwa akiishi peke yake mtaa wa Schmiedberg namba 9 katikati ya mji wa Augsburg na alimwachia nyumba hiyo mtanzania aitwaye Othman Lukindo.ยด mama Theresa kama lilivyokuwa jina lake alikuwa na mapenzi makubwa sana na watoto pamoja na kwamba yeye hakujaaliwa kuzaa.

  Mama Theresa Shayo au Theresa Rieger mwili wake ulichomwa moto (kwa matakwa yake mwenyewe marehemu) baada ya misa katika kanisa la westfreittof na majivu yake kuzikwa katika makaburi ya hapo hapo Westfrettorf mjini Augsburg uliyoko jirani na jiji la Munich!
   
 5. Red Scorpion

  Red Scorpion JF-Expert Member

  #64
  Jun 11, 2015
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 5,474
  Likes Received: 2,859
  Trophy Points: 280
  Duu kilikua kitu cha nguvu, R.I.P mama Theresa!
   
 6. Mayala masuka

  Mayala masuka Senior Member

  #65
  Jun 11, 2015
  Joined: Jan 22, 2014
  Messages: 178
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 80
  Inasisimua lkn mwishoni inahuzunisha
   
 7. HARUFU

  HARUFU Platinum Member

  #66
  Jun 11, 2015
  Joined: Jan 21, 2014
  Messages: 24,500
  Likes Received: 27,085
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  Mtoto analipa sana
   
 8. queenlishas

  queenlishas JF-Expert Member

  #67
  Jun 11, 2015
  Joined: May 25, 2014
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Buchanan ushaambiwa kafariki 2007 na keshaitwa hayati au hujaelewa somo!!!?
   
 9. Nifah

  Nifah JF-Expert Member

  #68
  Jun 11, 2015
  Joined: Feb 12, 2014
  Messages: 25,897
  Likes Received: 24,230
  Trophy Points: 280
  Alikua mrembo wa ukweli, Mungu amlaze pema.
   
 10. Miiku

  Miiku JF-Expert Member

  #69
  Jun 11, 2015
  Joined: Oct 8, 2014
  Messages: 3,104
  Likes Received: 1,245
  Trophy Points: 280
  Kumbe miss Tanzania wa kwanza alikuwa mchaga. Aisee!!
   
 11. Miiku

  Miiku JF-Expert Member

  #70
  Jun 11, 2015
  Joined: Oct 8, 2014
  Messages: 3,104
  Likes Received: 1,245
  Trophy Points: 280
  X-PASTER Kumbe majina ya kichaga yalianza kuchomoza siku nyingi kwenye tasinia ya Umiss!! Kumbe siyo Temu tyuu hata MAEDA.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Playboy

  Playboy JF-Expert Member

  #71
  Jun 11, 2015
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  Kuna siri gani nyuma ya watoto wazuri wa kichaga na umiss
   
 13. Miiku

  Miiku JF-Expert Member

  #72
  Jun 11, 2015
  Joined: Oct 8, 2014
  Messages: 3,104
  Likes Received: 1,245
  Trophy Points: 280
  Hili limenishangaza sana!
   
 14. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #73
  Jun 12, 2015
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,897
  Likes Received: 2,317
  Trophy Points: 280
  Miaka hiyo mama zetu wakimgawya, maana kuweka paja nje ilikuwa issue!
  Hapo ilikuwa Kilimanjaro Hotel, swimming pool.
   
 15. s

  sindano ya nyuki JF-Expert Member

  #74
  Jun 14, 2015
  Joined: Jan 18, 2015
  Messages: 237
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  aisee alikuwa mtoto wa nguvu c mchezo..! da.. inahuzunisha alikufa bila mtoto,na mashaka na enz hzo bila shaka wajeruman walimhasi asizae na mjeruman! RIP mama teresaa! mbele yako nyuma yetu!
   
 16. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #75
  Jun 18, 2015
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,519
  Likes Received: 10,437
  Trophy Points: 280
  Alikuwa mwanamke wa kazi sio hawa wa sasa chipsi funga.!
   
 17. S

  Shafii the Great Member

  #76
  Jun 22, 2015
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  laaanatu llah
   
 18. Sibonike

  Sibonike JF-Expert Member

  #77
  Jun 23, 2015
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 10,238
  Likes Received: 4,922
  Trophy Points: 280
  Looks like Funke Akindile the Nigerian movie star!
   
 19. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #78
  Jun 29, 2015
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,092
  Likes Received: 11,229
  Trophy Points: 280
  Alikuwa ana mapaja mazuri.
   
 20. z

  zoesappien Member

  #79
  Aug 10, 2015
  Joined: Aug 10, 2015
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hataree
   
 21. Kaboom

  Kaboom JF-Expert Member

  #80
  Oct 31, 2015
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 9,063
  Likes Received: 8,007
  Trophy Points: 280
  Heaven Sent umefanana na huyu binti..Ni ndugu yako??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...