Theresa Shayo: Miss Tanzania Mwafrika wa kwanza 1967 katika historia ya Tanzania | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Theresa Shayo: Miss Tanzania Mwafrika wa kwanza 1967 katika historia ya Tanzania

Discussion in 'Celebrities Forum' started by MwanaFalsafa1, May 15, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  missy45.jpg
  M's Tanzania wa Kwanza (Hayati Theresa)

  Mwaka 1960 ndipo Mashindano ya urembo nchini yalipoanza na hayatakuwa na muonekano wa kimataifa kwa sababu yalifanyika kwenye maeneo machache.

  Kwani kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba mrembo wa kwanza kunyakua taji hilo la Miss Tanzania, si mwingine bali alikuwa Theresa Shayo.

  Kutokana na maadali na utamaduni ya mtanzania serikali ililazimika kuyapiga marufuku mashindano hayo ilipofika tu mwaka 1967, kabla ya Rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuyaruhusu kuendelea kutokana na utandawazi kuanza kushika kasi ya ajabu.

  Tangu kipindi hicho nchi yetu ya tanzania iliweza kufanikiwa kutoa warembo kadhaa walioshiriki mashindano ya kumtafuta mrembo wa dunia, wakiwemo Emil Adolf, Nancy Sumary, Saida Kessy, Basila Mwanukuzi, Hoyce Temu, Jacqueline Ntuyabaliwe na wengineo.

  Mshindi huyo wa kwanza kushiriki mashindano hayo ya urembo ya Miss Tanzania Theresa Shayo, alifariki dunia huko Augburg Munich Ujerumani na kuzikwa uko uko alikokuwa akiishi miaka yote hiyo.

  Mwaka 1967 ndipo hayati Theresa alitwaa taji hilo kwenye shindano lilofanyika hoteli ya Kilimanjaro, alifariki dunia january 26 mwaka 2007 na maradhi ya kansa ya tumbo huku akiwa na umri wa miaka 61.

  Theresa hakubahatika kupata mtoto na alikuwa akiishi mjini Augsburg ambako aliolewa na mjerumani aitwaye Chrstian Rieger ambaye waliachana na hadi anakufa alikuwa akiishi na boy friend aitwaye Tonny.

  Kabla ya hapo Theresa alikuwa akiishi peke yake mtaa wa Schmiedberg namba 9 katikati ya mji wa Augsburg na alimwachia nyumba hiyo mtanzania aitwaye Othman Lukindo.

  Kwani alikuwa ni mtu mwenye huruma sana pamoja na kwamba alijiengemeza zaidi kwa ndugu zetu wa Kenya, alikuwa na upendo na kila mmoja uko alikokuwa akiishi alimpenda.

  missy39.jpg
  Miss Zanzibar wa kwanza Hediye Khamis Mussa (kati) akiwa na washindi wa pili na wa tatu January 13, 1968.

  Mashindano haya yamekuwa yakitia fora na kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya jamii ya watanzania, hasa baada ya kuwa chini ya uratibu wa Hashim Lundega, ambaye alianza kuyaendesha tangu mwaka 1994.

  Kwani kupitia Lundega, kampuni mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kudhamini mashindano hayo na kutoa zawadi zikiwemo za magari ya kisasa kwa washindi, hali iliyoyafanya yawe na ushindani mkali.

  Ukuaji wa Mashindano haya ulikuwa ni wa kasi kubwa kwani watu wengi kama ilivyo kwa mchezo wa soka ama muziki, hasa baada ya muziki wa kitanzania kuingiliwa na vionjo vya kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo).

  Mkoa wa Mbeya nao haupo nyuma katika mashindano hayo.

  Umekuwa unapita katika hatua hizo kwa kupata warembo mbalimbali walioibuka washindi kuanzia ngazi ya mkoa, kanda hadi kufikia hatua ya kushiriki shindano la 'Miss Tanzania'.

   

  Attached Files:

  Last edited: May 16, 2009
 2. N

  Neylu JF-Expert Member

  #41
  Dec 2, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mmmh..!!
   
 3. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #42
  Dec 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Enzi hizo mchina hakuweza kupenyeza madawa yake
   
 4. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #43
  Dec 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hivyo hivyo Mkuu wangu Mkuu rombo najua white wanakongoroka mapema lakini maini bado,
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #44
  Dec 2, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Hakufua dafu kwa dada mmoja wa kichagga enzi hizo.
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #45
  Dec 2, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Hakufua dafu kwa dada mmoja wa kichagga enzi hizo.
  [​IMG]
  Theresia Shayo mtoto huyo(sasa bibi), 1967.
   
 7. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #46
  Dec 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,297
  Likes Received: 1,216
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #47
  Dec 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,297
  Likes Received: 1,216
  Trophy Points: 280
  Naona hata Bi Cheka mdogo aise, coz hawa wanakaribia 70, na Cheka I think anaitafuta 50
   
 9. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #48
  Dec 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Mnawasifia Mama za watu humu! Nendeni kwa tahadhari
   
 10. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #49
  Dec 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,405
  Likes Received: 8,539
  Trophy Points: 280
  hata mimi nilitaka niongee hivyo hivyo mkuu.maadili lazima yazingatiwe wakati ku-comment ktk hizo picha.
   
 11. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #50
  Dec 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  keshakufa
   
 12. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #51
  Dec 3, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Anna Abdalah pia aliwahi kuwa Miss Mtwara nyakati hizo;
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #52
  Dec 3, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Natamani nimwone alivyo sasa hivi kama bado yu hai!
   
 14. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #53
  Dec 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,153
  Likes Received: 23,869
  Trophy Points: 280
  Hebu nambieni wadau, hiyo swimming pool ya The Kilimanjaro bado ipo. Mara ya mwisho nilikuwepo hapo wakati wa hayo mashindano ya urembo!.:smile:
   
 15. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #54
  Dec 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huu ni ushahidi kuwa uhuni na umomonyokaji wa maadili ulianza zamani na wahusika ni wale wale baba'angu Yethu! Lasima utengeneze pesa mama'angu hata kama ni kwa kutumia kinu. Rua! lasima uwape nao wakupe pesa mamaangu. Upuuzi mtupu. Aliyeyapiga marufuku aliona mbali maana hayana tofauti na umalaya na nudism.
   
 16. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #55
  Dec 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  si bora wawe mama za watu si ajabu mama zao!si unajua wazazi kwa kuficha mahistoria wanayohisi yataharibu maprofile yao kwa watoto!
   
 17. Futota

  Futota JF-Expert Member

  #56
  Dec 3, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huyo watatu kushoto ni shemeji yangu.
  Enzi zake kumbe alikuwa moto wa kuotea mbali, hallow, those long legs, perfect!

   
 18. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #57
  Dec 3, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Bila shaka hapo Bi Kidude alikuwepo na alikuwa anatesa ile mbaya...
   
 19. k

  kamkoda JF-Expert Member

  #58
  Dec 3, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 396
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hahahahahahaaaaaaaa...heshima yako platozoom, unajua vijana wa sasa ni limbukeni sana wanachacharika mno wakati enzi ztu sisi tulijua kula raha kiukweli unakula pipi pipi kweli si ndani ya mfuko leo wanalegezasuruali wanaona ujaaaaaanja! tunawaangalia tu!
   
 20. b

  bdo JF-Expert Member

  #59
  Dec 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  hizi picha zingekuwa coloured tungeona mengi sana, ila nimependa mapambo yao ngozi ya chui,
   
 21. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #60
  Dec 3, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Miaka hiyo hakuna mchina wala mkorogo, walikuwa wanaitwa vipusa, natural ebonies!


   
Loading...