Theresa May sasa ataka mazungumzo na vyama vya upinzani kuhusu Brexit

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
47111840_503.jpg

Serikali ya Uingereza imesema waziri mkuu Theresa May yuko tayari kufanya mazungumzo mapya juu ya mkataba wa kuiwezesha Uingereza kuondoka kwenye Umoja wa Ulaya itakapofika tarehe 29 mwezi Machi.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema atafanya mazungumzo ya busara na viongozi wa vyama vya upinzani pamoja na wabunge kwa moyo wa kuleta mafanikio na kutafuta njia ya kusonga mbele ili Uingereza iweze kuondoka Umoja wa Ulaya. Serikali yake imethibitisha kwamba ikifika Jumatatu itaweza kuuwasilisha mpango mbadala wa Brexit na kwamba wabunge watapewa fursa ya siku nzima ya kuujadili na kuufanyia marekebisho endapo itabidi tarehe 29 mwezi huu.
Hata hivyo pamekuwapo na ishara finyu juu ya kupiga hatua kwenye mazungumzo na viongozi hao wa upinzani baada ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour,Jeremy Corbyn kuyaita mazumgumzo hayo kuwa ni usanii wa maonyesho. Akizungumza kwenye mji wa Hastings, Corbyn amemtaka waziri mkuu May aonyeshe dhamira ya kweli juu ya mapendekezo yanayohusu hali ya baadae. Kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani Jeremy Corbyn amesema hatakutana na waziri mkuu ikiwa May hataondoa uwezekano wa Uingereza kutoka kwenye Umoja wa Ulaya bila ya mkataba.
47096264_503.jpg
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May
Na mbunge wa chama cha kijani Caroline Lucas aliekutana na waziri mkuu May amesema kiongozi huyo anaishi katika dunia ya kubuni kwa kufikiria kwamba mkataba wa Brexit unaweza kubadilishwa hadi hapo Jumatatu. May bado anaushikilia msimamo wake wa kujiondoa kwenye soko la pamoja la umoja wa forodha.
Wakati huo huo nchi za Umoja wa Ulaya zinaimarisha matayarisho ya kujiweka sawa endapo Uingereza itaondoka Umoja wa Ulaya bila ya mkataba, baada ya bunge la Uingereza kuukataa mkataba ambao bibi May aliuwasilisha kwenye bunge hilo.
 
Back
Top Bottom