The Zitto saga: Vyombo vya habari vinaiua CHADEMA?

Status
Not open for further replies.

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,060
Nimekuwa nafuatilia mwenendo wa Zitto kwa siku nyingi sana hapa JF na kwenye vyombo vingine vya habari duniani. Nimekuja kuanza kupata mashaka na mwenendo wa Zitto kama wengi wanavyosema pale alipoanza kushangilia kununua kwa mitambo ya Umeme ya wizi. Wengine wanakuja na kusema kuwa tangu aingie kwenye kamati ya Madini, ametoka akiwa siye yule Zitto tunayemfahamu.

Sipo hapa kuonyesha kama Zitto ana makosa au lah maana hili limeshasemwa sana na sasa linaanza kutia kinyaa. Jana pia niliandika kuwa, tawi lisilozaa, hukatwa na kutupwa motoni ila Mkono Mchafu, haukatwi na kutupwa, bali huoshwa kwa sabuni na kukaushwa huku ukisubiri kuendelea na shughuli utakazopangiwa na Ubongo.

Zitto ni MKONO, na hivyo bila kujali mabaya aliyoyafanya, hatuwezi kumkata. Kitendo kinachofanywa na akina Kubenea, Kibanda na Ngurumo ni kuukata Mkono. Na kwa sababu wao si madaktari, wanakata huo mkono na kusababisha maumivu kwa mwili mzima na kuvuja damu. Hii inaweza kupelekea Binadamu huyu (CHADEMA) kuvuja damu hadi mwisho akakata roho (soma maelezo ya Waberoya).

wakati mwingine huwa inabidi kuukata Mkono au Mguu au ........ ili kuzuia Kansa isiendee mwili mzima. Ila hii hufanywa na Madaktari baada ya kufanya utafiti wa kutosha na kujua ugonjwa umeanzia wapi na umeishia wapi, wapi wakate ili kuzuia ugonjwa. Ukifanya vibaya, utashangaa kansa bado inaendelea. Pia kuna hata bahati mbaya ambapo kansa hiyo huendelea kuula mwili hadi kumuuwa binadamu kama njia nyingine nzuri hazitatumika kuitibu hii kansa.

Wanasema ukweli siku zote uko katikati. Siamini yote haya yote yanayosemwa juu ya Zitto kuwa ni kweli. Nina hakika kuwa kuna mengine nyie waandishi mnamsingizia. Ila kuna mengine mnayosema ni kweli maana hata mwenyewe amekiri kuwa alifanya/alisema au alisikika akisema waziwazi.
Kuendelea kumuandika Zitto ni sawa na Kukata Mkono na hii haimsaidii mtu wenu CHADEMA maana akianza kuvuja damu, itamdhoofisha sana huyu mtu. Mngelifanya busara kama hili swala mngelifanyia utafiti na kuandika makala moja tu mkiutaka uongozi wa Chadema kukaa na Zitto na kulishugulikia hili swala ndani ya chama na si kwenye vyombo vya habari......

Juzi tu hapa watu walimkalia kooni Zitto kwa kwenda TBC na kuropoka habari za kikao cha ndani cha Chadema na kusema maamuzi yake. Sasa nyie kuja na habari za Mwanachama wenu wa Chadema na kuanza kumpaka matope, mnafikiri mnamkomoa Zitto peke yake? Mnamuabishia hata Rais wetu Dr. Slaa na kuabisha kazi yake nzito aliyoifanya. Yaani mmekosa cha kuandika kuhusu CCM, CUF .... hadi muanze kushambuliana wenyewe kwa wenyewe? Mmekuwa akina Mzindakaya wa kurusha mabomu wakati CCM ikishambuliana wenyewe kwa wenyewe? Acheni hiyo bana.

Ninaimani hili swala litafanywa kitalaamu na akina Tundu Lissu, Slaa, Mbowe na wengineo bila kumwaga Mtama wa Chadema kwenye kuku wengi. Kama kweli mna mapenzi na Chadema na viongozi wake, himizeni hili swala walimalize ndani ya chama na si nyie kuanza kulishughulikia kwa njia mnazofanya. Sidhani kama tumeshafika huko kwa kutaka KUMKATA mkono Zitto nje ya chama. Mwacheni Zitto na viongozi wenzake wayamalize na kama ataendelea kuwa mbishi na kuwa akiingiza sumu ndani ya chama basi Watanzania wataona. Hamuhitaji sasa hivi kuwaambia Watanzania kuwa fulani ni wa ovyo. Mwakyembe alisema "Watanzania si mabwege........."

Zitto si wa kukata ila pia si wa kuacha aendelee na tabia yake. Jana nilimalizia kwa kusema "Zitto Kabwe ni kama glass ya Wine - Handle with care."

Kubenea, Kibanda na Ngurumo wanakiua chadema, wanaaandika habari za Zito wauze magazeti. I am telling you guys! haiwezekani watu mnaowaita wanamapinduzi, wafichua ufisadi issues kama hizi za kuigawa chadema wanaziandika pasi uoga wala detailed info, udaku tu!!!

kwa heri chadema!!
 
Acha porojo. Inawezekana speed yako ya kusoma Tanzania Daima na MwanaHALISI ni mara moja baada ya miezi mitatu. Una-judge msimamo wa mtu kwa kusoma article yake moja!!! Madhara ya zitto kwenye chama hayana mfano. Ili chama ki-operate kama taasisi lazima ki-dscipline wanachama wa aina ya zitto wanaodhani kuwa bila wao chama hakisongi mbele. Chadema siyo ccm wanaosema mtaji wake ni jk. Mtaji wa chadema ni kila mwanachama bila kujali nafasi ya mwanachama kwenye chama.
 
Sikonge

Hivi unafikiri CHADEMA haijui kinachoandikwa kwenye magazeti hayo?
 
Ni hatari kwa haya nmagazeti kama yataanza kuandika habari bila ya kuzifanyia uchunguzi.
Wakumbuke wengi wa wasomaji wa Tanzania daima ni wale wapenzi/wafuasi wa chadema. waandike mikakati ya kuimarisha chama, hayo ya tofauti ya Zitto na wenzake yakajadiliwe kwenye vikao rasmi vya chama na wao waripoti taarifa ya vikao,. Hizi habari za uchonganishi hazina tija sio kwa CHADEMA peke yake bali hata kwa ustawi wa biashara yao hata wao
 
Sikonge

Hivi unafikiri CHADEMA haijui kinachoandikwa kwenye magazeti hayo?

chadema wapi wanajua, viognozi akina Mbowe na Slaa si ndio wanaosema aandikwe?

mtu mko ofisi moja mnashindwa kumuonya

Kuna harufu na uvundo mbaya sana ndani ya chadema, in such a way hawamwezi Zitto, wakimparamia kichwakichwa chama kinasambaratika maana siri za kila mmoja zitawekwa hadharani

Mbowe, Slaa Zito achieni madaraka, wapisheni akina Mnyika na Lissu wanaoonekana wana-busara

mnafiki Ngurumo na Kubenea sio wa kusikilizwa, kwanza Kubenea mwenyewe ni CCM, alichukua fomu, za ubunge akajitoa mnamwona ni hero, wakati mnafiki.

Kibanda ndiyo kabisa!!! tukianza kuandika uozo wake hapakaliki hapa!! juzi kakimbia humu ndani alipoulizwa issue za demokrasia!

Mbowe onyesha mwanaume wakusanye hao wote akina Ngurumo (msaidizi wako) ebu jadilini kwa kina tatizo ni nini,

Huku mtaani na JF kuna wanachadema wengi kumbikumbi wanafuata mwanga tu wanasema lolote lile na kupayuka,

Credibility ya chadema iko chini sana, ugomvi wa ndani, na CUF, huku mnawachanganya watu na misimamo yenu ya kuyumba,

My take ni kuwa Zitto ana uwezo wa kufanya lolote kwani Mtei, Slaa, mbowe (mkwe wa Mtei) wana machafu yao na Zitto anayajua. Haiwezekani kabisa kila kukicha Zito zito kwenye magaezti yaliyotakiwa kuijenga chadema

matumbo haya!!
 
Chadema tokea kumaliza uchaguzi imekosa muelekeo.

Hakuna lolote walilofanya likawa na muelekeo.

1. Wabunge wanachukua hatua zao watakazo na kujisifia kwenye vyombo vya habari.

2. Slaa na Mbowe misimamo iliyotofautiana.

3. Mdahalo usioeleweka malengo waliofanya na Cuf.

4. Magazeti yanayomilikiwa na Chadema yaliyojaa 'hujuma' dhidi ya Zitto.

5. Kesi za viti vya wanawake na kujitoa baadhi ya watu.

Wanahitaji kukaa chini na kujipanga upya. Inatupa picha kuwa Mbowe hana ubavu mbele ya watu fulani ndani ya chama kama Slaa na Zitto. Kuna hitajika uthabiti kwenye uongozi.
 
Mkuu naona una porojo
 
Hapo hatukuelewi we jamaa unaposema mwenyekiti hana ubavu kwa viongozi wenzake kwa kuwa hakuna malumbano au msuguano kati yake na Slaa au Zitto zaidi ya stori za magazetini na JF ambazo hazihusiani na chama. Kwa chama kinachoheshimu uhuru wa kutoa maoni hakiwezi kufanya kazi kupitia maoni ya watu bali taratibu rasmi za kichama. Mwenyekiti JK ndio hana ubavu mbele ya Lowasa na Rostam ndio maana hadi leo wanapeta uswahilini licha ya wizi wa kagoda na richmonduli, JK aonyeshe ubavu kwa kuwapeleka segerea hata mwaka mmojammoja tu.
 
chadema wapi wanajua, viognozi akina Mbowe na Slaa si ndio wanaosema aandikwe?

mtu mko ofisi moja mnashindwa kumuonya

Kuna harufu na uvundo mbaya sana ndani ya chadema, in such a way hawamwezi Zitto, wakimparamia kichwakichwa chama kinasambaratika maana siri za kila mmoja zitawekwa hadharani

Mbowe, Slaa Zito achieni madaraka, wapisheni akina Mnyika na Lissu wanaoonekana wana-busara

mnafiki Ngurumo na Kubenea sio wa kusikilizwa, kwanza Kubenea mwenyewe ni CCM, alichukua fomu, za ubunge akajitoa mnamwona ni hero, wakati mnafiki.

Kibanda ndiyo kabisa!!! tukianza kuandika uozo wake hapakaliki hapa!! juzi kakimbia humu ndani alipoulizwa issue za demokrasia!

Mbowe onyesha mwanaume wakusanye hao wote akina Ngurumo (msaidizi wako) ebu jadilini kwa kina tatizo ni nini,

Huku mtaani na JF kuna wanachadema wengi kumbikumbi wanafuata mwanga tu wanasema lolote lile na kupayuka,

Credibility ya chadema iko chini sana, ugomvi wa ndani, na CUF, huku mnawachanganya watu na misimamo yenu ya kuyumba,

My take ni kuwa Zitto ana uwezo wa kufanya lolote kwani Mtei, Slaa, mbowe (mkwe wa Mtei) wana machafu yao na Zitto anayajua. Haiwezekani kabisa kila kukicha Zito zito kwenye magaezti yaliyotakiwa kuijenga chadema

matumbo haya!!

Unamtetea Zitto kwa kuwa rafiki yako Waberoya na huenda amekutuma kufanya hivyo. Pia una jazba za kungalia nani amesema badala ya nini kimesemwa, haufai ktk jamii ya kisasa. Maovu na uvundo uliopa chadema vinatakiwa kujulikana mapema ili watz tukipime kama kinafaa kutuvusha na sio kubakia mioyoni mwa watu. Ukiujua uovu na kukaa kimya ni ufisadi huo, kwa hiyo rafiki yako Zitto naye ni fisadi. Tunataka kuondoa uozo ndani ya nchi hii ili 2015 tuwe na vyama visafi visivyokumbatia ufisadi na uozo. Suala la Zitto kujipendekeza kwa JK, Lowasa na wengineo halina hata kificho, kwa nini ajipendekeze kama ni mwanasiasa anayejiamini? Zitto katika mazungumzo yake yote baada ya uchaguzi hajawahi kuzungumzia tume huru ya uchaguzi au katiba mpya, anapiga blabla zingine tu kutafuta sifa. Tume huru ya nini wakati JK hakufika jimboni kwake kupigia kampeni ccm??? Vijana wa tz tunamuona Zitto sio tena shujaa aliyetufanya tuipende na kufuatilia siasa kwa hoja nzito zenye kuipenda nchi, tunamuona ni kibaraka mpenda sifa na anayejipendekeza kwa JK.
 
Jamaa anasema " Edwin Mtei the Godfather anawatumia watu gani?Mimi naweza kuwa natumiwa bila kujua?

Anawatumia watu ambao mkwewe,Freeman Mbowe humpelekea.Hakuna details zozote kuonyesha kama Slaa,Zitto na Mtei walikuwa na uhusiano wa karibu miaka saba nyuma!Wachezaji waliokaa pamoja siku mbili wanataka kuomba mechi.Sick jokes.Jenerali Ulimwengu,Saed Kubenea,Maxence Melo,Mike Mushi (huyu baadaye alikimbia).Kuchafua nchi mtandaoni kwa kutumia mtandao wa Maxence Melo ambao una mahusiano ya karibu na baadhi ya watu waliko Houston,Texas.Absalom Kibanda (ni mwandishi na mhariri wa Tanzania Daima ambaye anatembea juu ya ukanjanja wa kutupwa).Unaweza kutumika bila kujua kama hutasikiliza na kutafakari na kuhoji.Sote tunakubaliana huwezi kuacha kutumia gari lako zima ukaamua kuazima gari la jirani yako ambalo lina taa mbovu,tairi mbili mbovu na mafuta hakuna."
 
chadema wapi wanajua, viognozi akina Mbowe na Slaa si ndio wanaosema aandikwe?

mtu mko ofisi moja mnashindwa kumuonya

Kuna harufu na uvundo mbaya sana ndani ya chadema, in such a way hawamwezi Zitto, wakimparamia kichwakichwa chama kinasambaratika maana siri za kila mmoja zitawekwa hadharani

Mbowe, Slaa Zito achieni madaraka, wapisheni akina Mnyika na Lissu wanaoonekana wana-busara

mnafiki Ngurumo na Kubenea sio wa kusikilizwa, kwanza Kubenea mwenyewe ni CCM, alichukua fomu, za ubunge akajitoa mnamwona ni hero, wakati mnafiki.

Kibanda ndiyo kabisa!!! tukianza kuandika uozo wake hapakaliki hapa!! juzi kakimbia humu ndani alipoulizwa issue za demokrasia!

Mbowe onyesha mwanaume wakusanye hao wote akina Ngurumo (msaidizi wako) ebu jadilini kwa kina tatizo ni nini,

Huku mtaani na JF kuna wanachadema wengi kumbikumbi wanafuata mwanga tu wanasema lolote lile na kupayuka,

Credibility ya chadema iko chini sana, ugomvi wa ndani, na CUF, huku mnawachanganya watu na misimamo yenu ya kuyumba,

My take ni kuwa Zitto ana uwezo wa kufanya lolote kwani Mtei, Slaa, mbowe (mkwe wa Mtei) wana machafu yao na Zitto anayajua. Haiwezekani kabisa kila kukicha Zito zito kwenye magaezti yaliyotakiwa kuijenga chadema

matumbo haya!!
Huna haja ya kuwa na degree kujua hulka ya mwandishi kama huyu anataka nini, wivu umemjaa, fitina, uchonganishi.
 
Acha porojo. Inawezekana speed yako ya kusoma Tanzania Daima na MwanaHALISI ni mara moja baada ya miezi mitatu. Una-judge msimamo wa mtu kwa kusoma article yake moja!!! Madhara ya zitto kwenye chama hayana mfano. Ili chama ki-operate kama taasisi lazima ki-dscipline wanachama wa aina ya zitto wanaodhani kuwa bila wao chama hakisongi mbele. Chadema siyo ccm wanaosema mtaji wake ni jk. Mtaji wa chadema ni kila mwanachama bila kujali nafasi ya mwanachama kwenye chama.

Nashawishika kuwa kuna madhara ya Zitto kwa nafasi ya Uenyekiti wa Mbowe na hivyo gazeti lake la Tanzania Daima na nashawishika pia kuwepo kwa harufu ya madhara ya Zitto kwa nafasi ya Mtunza Hazina wa Chadema Antony Komu na hivyo Gazeti lake la Mwanahalisi ni dhahiri, mwanaChadema usikubali kuingizwa kwenye vita hii ya maslahi ya watu binafsi walioifanya Chadema kama kampuni yao binafsi kwa jina la Chama.

Hii inanikumbusha hadithi ya Spika Sita kukihatarisha chama cha Mapinduzi wakati kimsingi nyuma ya pazia ilikuwa ni hatari kwa Lowasa na marafiki zake.

MwanaChadema...beware, usikubali kufuata mkumbo na kukiacha kitovu cha matatizo yaliyopo ndani ya Chadema!!
 
Unamtetea Zitto kwa kuwa rafiki yako Waberoya na huenda amekutuma kufanya hivyo. Pia una jazba za kungalia nani amesema badala ya nini kimesemwa, haufai ktk jamii ya kisasa. Maovu na uvundo uliopa chadema vinatakiwa kujulikana mapema ili watz tukipime kama kinafaa kutuvusha na sio kubakia mioyoni mwa watu. Ukiujua uovu na kukaa kimya ni ufisadi huo, kwa hiyo rafiki yako Zitto naye ni fisadi. Tunataka kuondoa uozo ndani ya nchi hii ili 2015 tuwe na vyama visafi visivyokumbatia ufisadi na uozo. Suala la Zitto kujipendekeza kwa JK, Lowasa na wengineo halina hata kificho, kwa nini ajipendekeze kama ni mwanasiasa anayejiamini? Zitto katika mazungumzo yake yote baada ya uchaguzi hajawahi kuzungumzia tume huru ya uchaguzi au katiba mpya, anapiga blabla zingine tu kutafuta sifa. Tume huru ya nini wakati JK hakufika jimboni kwake kupigia kampeni ccm??? Vijana wa tz tunamuona Zitto sio tena shujaa aliyetufanya tuipende na kufuatilia siasa kwa hoja nzito zenye kuipenda nchi, tunamuona ni kibaraka mpenda sifa na anayejipendekeza kwa JK.

Si kuwa Waberoya anamtetea Zitto nia yake ni kuona viongozi wa Chadema wanavurugana na Zitto, Waberoya ni mmoja wa Zitto haters toka UDSM hapa anajaribu kuwachanganya watu tu ambao hawamjui yeye toka enzi za 'Kubwajinga', soma article yake hii

Esoteric: Uhusiano wa Zitto, JK, Salim A.S, Ridhwan, Omar IIyas & then some Islams?
Mimi nimekuwa nikimfuatilia mheshimiwa Zitto, tangu alipoongoza mapinduzi ya kupindua serikali ya DARUSO mwaka 2002/2003 wakisaidiana na Ridhwan Kikwete na Omar Ilyas. Kipindi hicho nikiwa mmoja wa mawaziri wa serikali, ambayo ilipona kupinduliwa. Na tumekuwa wote ndani ya bunge la UDSM-USRC

Mimi personally nimekuwa muwazi sana na mkweli katika kila kitu kinacholigusa taifa hili na hasa uhuru wa mawazo na maoni ambao umedhihirika kuwa watanzania wengi sio kuwa hawana, bali huwa wepesi sana kuamini mambo na ni waoga kuonekana wanapingana na hali iliyopo.

Mtazamo huu umenifanya nimpende Zitto na JF members wowote wale ambo huwa wanapenda kufikiria nje ya box, au another direction/angle. Zitto amekuwa akinifurahisha kwa kuleta changamoto za kuleta mawazo tofauti na kile ambacho wengi huwa wanafikiria.

Zitto ni kweli anapenda sifa, kama binadamu mwingine yeyote yule, ila unapotaka sifa kwa kusimamia haki na ukweli na hasa unapopigania haki basi sifa hii ni sifa timilifu na inapendeza. Omar Ilyas naye alikuwa mmoja wao wa wanaopenda sifa ila kwa sasa naona amekua kidogo, nadhani Salim A Salim amemkuza.

Si nia yangu niwaharibie hawa jamaa , ila ni hali yangu kueleza ninachowaza baada ya kuwafuatilia hawa watu tangu enzi hizo. Sijajua status ya Omar Ilyas kwenye issue nzima za udini, siwezi kumtuhumu, personally nimemuona ni mtu mzuri tu na anayependa wote pasi kujali udini ila bado ni rafiki wa Zitto!

Tuendelee: Role model wa Zitto ni Salim A. Salim, rais bora kwake yeye ni Kikwete, MD bora aliyewahi kumsema yeye ni Rashid Idrisa yule wa TANESCO.

Tie, cord, umoja, Urafiki wa Zitto, Ridhwan, Omar Ilyas ni mkubwa sana kuliko maelezo, hili group lililotaka kuipindua serikali ya Kayombo-DARUSO, ili wao wapate madaraka si tu ni la hatari bali la kuangaliwa sana. Ridhwan amekuwa akijitetea sana yeye anataka ku-practise sheria hili hali kutaka uongozi amekuwa akitamani tangu siku nyingi sana.

Ukiwa rafiki na Ridhwan umekuwa rafiki wa Kikwete!!! Huwezi kuwa adui wa JK ukawa rafiki wa Ridhwan, JK si tu anampenda Ridhwan kama motto, bali kama mwanaCCM mwenzie aliye tayari kulinda interest zao.

Si ajabu Zitto kuwa alikuwa mmoja wa wanakamati ya bunge ya kuchunguza madini, maana JK anampenda Zitto, ambaye ni rafiki wa Ridhwan!

Alichotamka Juzi ni mwendelezo wa kumuonyesha JK kuwa yuko ‘NAYE' na yuko mbali na chadema na kuwa yeye hakuwa na mawazo kama wanachadema wengine!!!. Hakuishia hapo tu bali alisema JK amefanya mengi Kigoma! Hivyo hakuona sababu ya kutoka nje ya bunge, kwa hiyo hakwenda kabisa, Huu ujumbe haukuwa kwa wananchi, ulikuwa unaenda kwa JK rafiki yake! Hata kama JK kafanya mambo mengi huko jimboni kwake Kigoma ni wajibu wake kama rais na haikuwa zawadi.

Kilichonifanya nijiulize je what makes Zitto na JK kuwa marafiki? Je Zitto na JK walikuwa wanajuana kabla ya JK kuwa rais? Definitely Yes!

Je swali gumu na baya ambalo halina ushahidi ni je Zitto kuwa inclined kwa JK, Salim na kuwapenda baadhi ya viongozi wa kiislam je ni mdini?..........I mean chunguzeni hili. May be not! Kindly don't conclude! What Salim teaches Zito?? Salim is CCM, is Salim and JK close friends? Cause Ommy and Zitto are close friends, Ooh! Ommy ni personal assistant wa Salim, Nauliza Kama Ridh, Zitto, Ommy ni marafiki then Salim and JK ni maadui? Find out please. However, we all know JK ni mdini, maana alianza harakati za udini tangu akiwa UDSM miaka hiyo….na hili fuatilieni

Nani anayejua Zitto ana mtambo wa kusaga kokoto na alipata tender ya barabara ku-supply kokoto? Is he defending his interest indirectly?

Au ni kuwa ni great thinker ambaye anaishi kwa falsafa zake ambazo hatuzijui! Je mnafikiri Zitto kuwaambia waandishi wa habari yaliyojiri ndani ya chadema alikuwa hajui watu watamrudi? Who is greater to him? JK, wananchi wake Kigoma, mali au?

I mean we should be careful na watu kama Zitto yes they are bright, mmh! But they might be dangerous for the opposition existence. But we should examine him carefully and not judge him. Nimegusia tu swala la uislam maana mpaka leo kuna baadhi ya waislamu wanaofikiri kuwa wanaiweza kuigawa nchi hii kidini, na kuna wakristo wanaofikiri wanaweza kuigawa nchi hii kidini.

That's bringing another bitter question how far do we believe these opposition leaders? I mean all!

That said, I am just thinking
 
Vunja Ukimya Zungumza na Mwenzio! Kazi ya Maadui Zenu Inaendelea ..... vyombo vya habari ni vizuri kama unahoja lakini ukivitumia kama tool ya kuwashambulia maadui zako, weledi wagundua na watavitumia kwako. Tuvitumia vyombo vyetu kupeleka ajenda zetu.

Pia, kuvujisha siri za kikundi, chama ni hulka za watu wenye umimi au wasioweza kufanya kazi kenye makundi/mifumo. Watakiwa kushughulikiwa kimifumo na si kwa kutoa siri kwa maadui.

watawagombanisha hadi msahau agenda zenu..... wazungu wanafanya hivyo na maadui zenu wanafanya hivyo.... endeleni tu!

Naomba mrudi kwenye agenda zenu, watawapoteza hao ..... adui ni nani? mnakwenda wapi?

WASALITI UNYAMAZISHWA MILELE!!!
 
Kubenea, Kibanda na Ngurumo hawa ni mashujaa nchi hii kwa kufichua ufisadi na mamluki anayesema kinyume ana lake jambo na amuogope Mungu.
 
Chadema tokea kumaliza uchaguzi imekosa muelekeo.

Hakuna lolote walilofanya likawa na muelekeo.

1. Wabunge wanachukua hatua zao watakazo na kujisifia kwenye vyombo vya habari.

2. Slaa na Mbowe misimamo iliyotofautiana.

3. Mdahalo usioeleweka malengo waliofanya na Cuf.

4. Magazeti yanayomilikiwa na Chadema yaliyojaa 'hujuma' dhidi ya Zitto.

5. Kesi za viti vya wanawake na kujitoa baadhi ya watu.

Wanahitaji kukaa chini na kujipanga upya. Inatupa picha kuwa Mbowe hana ubavu mbele ya watu fulani ndani ya chama kama Slaa na Zitto. Kuna hitajika uthabiti kwenye uongozi.
Well said. CHADEMA kuna tatizo kubwa la kiuongozi. Wengi hapa wamesema na wengine wanaonekana ni CCM au hata CUF. Kuna haja ya haraka ya CHADEMA kufanya overhaul kwenye uongozi wao. Miongoni mwa hatua za kuchukua ni;
1. Kuamua kuwaweka pembeni Zitto na Mbowe kwa pamoja. Kwa kufanya hivi makundi yanayoongozwa na watu hawa watakuwa kwenye win-win situation au vice versa.
2. Kujipanga na kuhakikisha kuwa matamko ya CHAMA yanatolewa na mtu mwenye uelewa na hata kueleweka. Kuna haja ya kufikiria kuwatumia watu hata wakina Dr Mkumbo. Hawa wanabusara zao.
3. Kuacha kusema saana na vyombo vya habari. Wakiendeleza hili, watazoeleka kuwa ni wabwabwaji.
4. Kufanya yale yaliyo ndani ya uwezo wao kwa kutumia ziada ya mishahara yao waliyokuwa wanajinadi kwamba wabunge wanapewa pesa nyingi na kufanya vitu hata kama ni vidogo basi viweze kuonekana.
5. Warudi haraka saana kwa wapiga kura wakawashukuru na waambie nini watawafanyia hata kama hawakufanikiwa kuongoza nchi.
6. Waepuka mijadala isiyo na maana, kwa sababu ndio mwanzo wa kujiharibia. Mfano yule mama wa CCM ubungo.
7. Wajipange kuwa na wanachama kutoka sehem zote na wawe wanaplan strategy zao mapema. Mfano Uteuzi wa Mgombea mwenza ulikuwa wa ajabu saana.
 
Credibility ya chadema iko chini sana, ugomvi wa ndani, na CUF, huku mnawachanganya watu na misimamo yenu ya kuyumba,

My take ni kuwa Zitto ana uwezo wa kufanya lolote kwani Mtei, Slaa, mbowe (mkwe wa Mtei) wana machafu yao na Zitto anayajua. Haiwezekani kabisa kila kukicha Zito zito kwenye magaezti yaliyotakiwa kuijenga chadema

matumbo haya!!

Punguza hasira mkuu,
otherwise utajikuta umetupwa kwenye ignore list!
 
Umetumwa wewe!!??????
Kawaambie chadema haiumii kwa mnafki yeyote kuondoka hata awe mbowe, zito au slaa kama wanaleta sera za kinafki na fitna wataondoka na chama kitasonga mbeleee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Aliyekutuma mwambie wahariri wa magazeti wako makini na chadema iko makini na haifanyi kazi kwa makosa!

Hatudanganyiki na hatununuliki kamwe!
 
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom