Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,537
- 6,002
Nimekuwa nafuatilia mwenendo wa Zitto kwa siku nyingi sana hapa JF na kwenye vyombo vingine vya habari duniani. Nimekuja kuanza kupata mashaka na mwenendo wa Zitto kama wengi wanavyosema pale alipoanza kushangilia kununua kwa mitambo ya Umeme ya wizi. Wengine wanakuja na kusema kuwa tangu aingie kwenye kamati ya Madini, ametoka akiwa siye yule Zitto tunayemfahamu.
Sipo hapa kuonyesha kama Zitto ana makosa au lah maana hili limeshasemwa sana na sasa linaanza kutia kinyaa. Jana pia niliandika kuwa, tawi lisilozaa, hukatwa na kutupwa motoni ila Mkono Mchafu, haukatwi na kutupwa, bali huoshwa kwa sabuni na kukaushwa huku ukisubiri kuendelea na shughuli utakazopangiwa na Ubongo.
Zitto ni MKONO, na hivyo bila kujali mabaya aliyoyafanya, hatuwezi kumkata. Kitendo kinachofanywa na akina Kubenea, Kibanda na Ngurumo ni kuukata Mkono. Na kwa sababu wao si madaktari, wanakata huo mkono na kusababisha maumivu kwa mwili mzima na kuvuja damu. Hii inaweza kupelekea Binadamu huyu (CHADEMA) kuvuja damu hadi mwisho akakata roho (soma maelezo ya Waberoya).
wakati mwingine huwa inabidi kuukata Mkono au Mguu au ........ ili kuzuia Kansa isiendee mwili mzima. Ila hii hufanywa na Madaktari baada ya kufanya utafiti wa kutosha na kujua ugonjwa umeanzia wapi na umeishia wapi, wapi wakate ili kuzuia ugonjwa. Ukifanya vibaya, utashangaa kansa bado inaendelea. Pia kuna hata bahati mbaya ambapo kansa hiyo huendelea kuula mwili hadi kumuuwa binadamu kama njia nyingine nzuri hazitatumika kuitibu hii kansa.
Wanasema ukweli siku zote uko katikati. Siamini yote haya yote yanayosemwa juu ya Zitto kuwa ni kweli. Nina hakika kuwa kuna mengine nyie waandishi mnamsingizia. Ila kuna mengine mnayosema ni kweli maana hata mwenyewe amekiri kuwa alifanya/alisema au alisikika akisema waziwazi.
Kuendelea kumuandika Zitto ni sawa na Kukata Mkono na hii haimsaidii mtu wenu CHADEMA maana akianza kuvuja damu, itamdhoofisha sana huyu mtu. Mngelifanya busara kama hili swala mngelifanyia utafiti na kuandika makala moja tu mkiutaka uongozi wa Chadema kukaa na Zitto na kulishugulikia hili swala ndani ya chama na si kwenye vyombo vya habari......
Juzi tu hapa watu walimkalia kooni Zitto kwa kwenda TBC na kuropoka habari za kikao cha ndani cha Chadema na kusema maamuzi yake. Sasa nyie kuja na habari za Mwanachama wenu wa Chadema na kuanza kumpaka matope, mnafikiri mnamkomoa Zitto peke yake? Mnamuabishia hata Rais wetu Dr. Slaa na kuabisha kazi yake nzito aliyoifanya. Yaani mmekosa cha kuandika kuhusu CCM, CUF .... hadi muanze kushambuliana wenyewe kwa wenyewe? Mmekuwa akina Mzindakaya wa kurusha mabomu wakati CCM ikishambuliana wenyewe kwa wenyewe? Acheni hiyo bana.
Ninaimani hili swala litafanywa kitalaamu na akina Tundu Lissu, Slaa, Mbowe na wengineo bila kumwaga Mtama wa Chadema kwenye kuku wengi. Kama kweli mna mapenzi na Chadema na viongozi wake, himizeni hili swala walimalize ndani ya chama na si nyie kuanza kulishughulikia kwa njia mnazofanya. Sidhani kama tumeshafika huko kwa kutaka KUMKATA mkono Zitto nje ya chama. Mwacheni Zitto na viongozi wenzake wayamalize na kama ataendelea kuwa mbishi na kuwa akiingiza sumu ndani ya chama basi Watanzania wataona. Hamuhitaji sasa hivi kuwaambia Watanzania kuwa fulani ni wa ovyo. Mwakyembe alisema "Watanzania si mabwege........."
Zitto si wa kukata ila pia si wa kuacha aendelee na tabia yake. Jana nilimalizia kwa kusema "Zitto Kabwe ni kama glass ya Wine - Handle with care."

Kubenea, Kibanda na Ngurumo wanakiua chadema, wanaaandika habari za Zito wauze magazeti. I am telling you guys! haiwezekani watu mnaowaita wanamapinduzi, wafichua ufisadi issues kama hizi za kuigawa chadema wanaziandika pasi uoga wala detailed info, udaku tu!!!
kwa heri chadema!!