masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,173
- 13,776
Hali ya kisiasa Zanzibar kwa miaka mingi sasa ni ya mivutano isiyoisha.
Mivutano hii ni ya kihistoria na pengine naweza kusema hata mapinduzi ya mwaka 1964 ni sehemu tu ya mivutano hiyo.
mivutano hii inatokana na polarisation, au kuwepo kwa makundi tofauti katika jamii, makundi ambayo kwa miaka sasa hayakubaliani kwa jambo lolote ikihusiana na mustakabali wa wazanzibari wenyewe.
Muungano wa Zanzibar na Tanganyika umepunguza kidogo tu hizi polarisation katika jamii ya kizanzibari.
Mwalimu Nyerere alijaribu sana kuondoa tofauti kati ya makundi tofauti ya kisiasa Zanzibar, lakini hakufanikiwa kuyamaliza.
Mwinyi na Mkapa hivyo hivyo, makundi hayo yapo, yanadumu na inaelekea kama wazanzibari wenyewe hawatayamaliza, ni ndoto ya mchana kutegemea Magufuli kuyamaliza.
Tofauti zilizomo ndani ya jamii ya wazanzibari ndiyo ilipelekea mapinduzi ya mwaka 1964.
Leo mwaka 2016, ni miaka 52 imepita na bado ukiikuna tu jamii ya kizanzibari kisiasa, damu kumwagika linakuwa jambo la dhahiri.
Tunaweza kusema pengine somo la 1964, wazanzibari wa sasa hawakulipenda au wamelisahau?
Au tuseme mapinduzi yenyewe hayakuleta mafanikio yaliyotarajiwa?
Mambo yote hayo ni maswala yanayowahusu wazanzibari wenyewe, na si watanganyika.
Hivyo basi mchawi wa uchaguzi huko Zanzibar ni wazanzibari wenyewe, na wasipokuwa na muafaka kati yao wenyewe maalif Seif na Dr Shein wasitegemee sanawatu wasio wazanzibari kuwaonyesha njia.
Zanzibar ni Nchi ati.