The Vitruvian man: Ufahamu mchoro wenye utata kuhusu mwili wa mwanadamu uliochorwa na Da Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,622
106,556
1594153305325.png

Parental Advasory: 18+

MATES
Hapo zamani dunia ilipitia kipindi butu/kibaya cha maisha ambapo dunia ilikua imesimama katika kila Nyanja ya maendeleo ya maisha ya mwanadamu kiliathiri zaidi bara la Ulaya. Kipindi hicho kiliitwa Zama za Kati/Middle Age (sio zama za mawe). Kipindi hiki kilianza baada ya anguko la utawala wa Rumi/Roma mwaka 476 AD. Kipindi hicho kiligubikwa na vita, uchawi, ujinga, njaa, magonjwa nk. Karne ya 14 kipindi hiki cha giza kwa binaadamu kilikoma, karne hiyo ndipo kulitokea kipindi muhimu zaidi katika maendeleo ya maisha ya mwanadamu.. kipindi cha Renaissance

Renaissance kwa Kiswahili ni kuzaliwa upya (Rebirth) katika hiki ndipo walitokea watu mashuhuli, wenye akili nyingi waliotumia akili zao kutengeneza maisha haya tunayoishi leo hii kwa kutumia misingi ya wazee wa zamani (Giants kama vile Plato, Socrate, Archimedes, Aristotle, Jesus, Paulo nk). Ikumbukwe kwamba katika kipindi cha middle age wazungu walaikua hawakuzipa kipaumbele falsafa za Ugiriki na Rumi ya zamani (falsafa ndio imebeba kila ustarabu wa mwanadamu. Kipindi cha Renaissance kilianzia kwenye mji uitwao Frolance katika nchi ya Italy kisha kusambaa ulaya nzima. Hapa sasa ndio wakatokea watu wenye akili nyiingi, wanasayansi walianza kujali kazi zao kwa kuwea saini, kujali tamaduni na sanaa. Baadhi ya watu maarufu ambao ni zao la kipindi hiki ni..
  • Leonardo da Vinci
Huyu jamaa ndio baba wa Renaissance maana ilianzia kwenye jiji lake, hakuna binaadamu anaweza mzidi akili huyu jamaa
  • Desiderius Erasmus
Ndio alitafsiri agano jipya kwenda lugha ya kigiriki
  • Rene Descartes
Huyu ndio baba wa falsafa ya kisasa pia alikua mwanahisabati
  • Galileo
Huyu twamjua sana na nadharia zake za jua na sayari
  • Nicolaus Copernicus
  • Thomas Hobbes
  • Niccolo Machiavelli
  • Titian
  • William Tyndale
Huyu alikua ni mtafsiri wa lugha alikufa kwa kuchomwa moto akiwa hai baada ya kutafsiri biblia kwenda kingereza
  • William Shakespeare
  • Donatello
  • Sandro Botticelli
  • Raphael
Alikua mwanafunzi wa Da’ Vinci na Michelangelo ni mchoraji
  • Michelangelo

The Vitruvian Man

Jina Leonardo da Vinci sio ngeni masikioni mwa wengi waliopita pita shule, moja ya kazi zilizomfanya kua maarufu ni michoro ya MonaLisa, Last supper. Diamond anaweza kua maarufu na pesa nyingi lakini anashindwa uwezo wa kuimba na utunzi na Ruby, ndivyo ilivyo kwenye michoro ya Da Vinci. MonaLisa na Last Supper ni michoro maarufu lakini inashindwa mbali sana na mchoro wake usiofahamika na wegi uitwao The Vitruvian man, huu ndio mchoro wenye siri na mafumbo mengi kuliko mchoro wowote ule uliowahi kuchorwa na Da Vinci.

Huko juu nimesema kua kipindi cha Middle age wazungu walikua hawakuzipa kipaumbele sana tamaduni na falsafa za Rumi na ugiriki ya zamani mpaka kipindi cha Renaissance. Sasa basi kati ya mwaka 30BC kulikua kuna mkandarasi wa majengo aitwae Marcus Vitruvius Pollio almaarufu kama Vitruvius, aliaandika kitabu kimoja kinachohusu maswala ya ujenzi kiitwacho De Architectura taafsiri yake ikiwa ni On Architecture. Ndani ya kitabu hicho alieleza kwamba kitovu ndio sehemu ya katikati katika mwili wa mwanadamu hivyo ukichukua compass (bikali) ukaiweka kwenye kitovu unaweza kuchora duara kamili linalozunguka mwili wa binaadamu. Pia akasema kwamba urefu kutoka kichwani mpaka miguuni ni sawa na urefu wa kutoka mkono mmoja mpaka mkono mwingine mtu akitanua mikono yake, pia kupitia katika mikono hiyo unaweza ukachora umbo la pembe nne mraba…Kupitia hapo akapata kitu kinachofahamika kama proportion of human body.

Kupitia statement hiyo wachoraji mbalimbali walijitahidi kuchora mchoro wa mtu kwa kutumia maalezo hayo lakini walishindwa. Kuchora duara ilikua rahisi kazi kubwa ilikua ni vipi utaliweka duara katika umbo la mraba/ Squaring the circle likiwa na area sawa?. Hapo sasa ndio mwamba Leonardo alikuja kujichukulia point za bure kabisa maana alichora vilevile kama inavyotakiwa ila kama tunavyofahamu Da Vinci kila kazi yake aliyokua anafanya aliifanya katika ukamilifu wa 99.9% na hua anaiweka katika mfumo wa mafumbo. Lakini cha kufurahisha zaidi katika mchoro wake Vinci alitumia idea tu ya Vitruvius lakini aliweka mambo mengine magumu kwa namna yake anayojua mwenyewe.
vitruvian.jpg

Picha ya the Vitruvius man ikimuonyesha mtu yupo katikati ya duara na maraba.

Da vinci siku zote maandiko yake hua anaandika kinyumenyume ili usome maandishi yake lazima utumie kioo, hivyo kwenye maelezo yaliyo kwenye picha maelezo ya kipanche kwanza yanasema…
vidole vinne sawa na kiganja kimoja, viganja vinne ni sawa na mguu mmoja, viganja sita ni sawa cubit 1 (cubit ni kipimo chenye urefu sawa na inchi 18) cubit 4 ni sawa na futi 6 ambazo ni urefu wa mtu pia alisema kwamba viganja 24 ni sawa na urefu wa mtu mmoja.
Maelezo ya kipande cha pili cha mchoro yanasema kwamba
-Kutoka kwenye shina la nywele mpaka chini ya kidevu ni sawa na sehemu ya kumi ya urefu wa mwanadamu
-kutoka kwenye kidevu hadi juu ya kichwa ni moja ya nane ya urefu wa mwanadamu
-kutoka kwenye usawa wa matiti mpaka juu ya kichwa ni sawa na moja ya sita ya urefu wa mtu
-Kutoka juu ya kifua hadi kwenye shina la nywele ni sawa na sehemu ya saba ya mtu mzima.
-Kuanzia kwenye chuchu hadi juu ya kichwa ni sawa na sehemu ya nne ya mtu
-Upana mkubwa wa mabega ni sawa na sehemu ya nne ya mtu.
-Kutoka kwenye kiwiko hadi ncha ya mkono ni sawa na sehemu ya tano ya mtu
-Kutoka kwenye kiwiko hadi kwenye kwapa nisawa na sehemu ya nane ya mtu.
-Mkono mzima ni sawa na sehemu ya kumi ya mtu
-Sehemu za siri zinapoanzia ndio katikati ya mtu
-Mguu ni sawa na sehemu ya saba ya mtu
-kutoka kwenye unayo hadi kwenye goti ni sawa na sehemu ya nne ya mtu
-Kutoka chini ya goti hadi mwanzo wa sehemu za siri nisawa na sehemu ya nne ya mtu
-Umbali kutoka chini ya kidevu hadi puani na kutoka shina ya nywele hadi kwenye nyusi ni sawa na theluthi ya uso. Yaani uliugawa uso kutoka kwenye kidevu hadi kwenye nywele katika visehemu sawa vyenye ukubwa wa theluthi.

Hayo ni maelezo tu aliyoyaweka wazi yeye mwenyewe, ila sasa kuna mambo mengine mengi ambayo kayaficha ndani ya huo mchoro inatakiwa uwe mchunguzi kuyagundua.

Kwanza kabisa huu mchoro haukua maalumu kwa Da Vinci kama michoro mengine, alichoro akauweka ndani tu hakudhani kama unaweza kua maarufu. Alikamilisha kuuchora mwaka 1490 alichanganya sayansi na sanaa katika sehemu moja, hesabu kali sana za geometry zilitumika kuchora huo mchoro. Kinachovutia zaidi kwenye mchoro huu ni kwamba sisi si tunaona tu ni mtu mmoja kakaa mapozi mawili tofauti ila kiuhalisia huyo mtu kakaa mapozi 16 hivyo alivyo nimeweza kuona mapozi 12 tu mengine bado natafuta.. Mchoro wa Vitruvian man Da Vinci aliukata katika vipande 14 ambavyo nimeelezea huko juu, 14 ukiigawa kwa 2 unapata 7 ambayo ni namnba ya utimilifu kwa Mungu ambapo baada ya kumaliza kumuumba mwanadamu alipumzika.

Uhusiano wa Vitruvian man na Pyramid

…ukiangalia kutoka kwenye kitofu mpaka kona ya upanede wa pembe ya kulia inafanana na mteremko wa kona ya pyramid,pyramid imejumuisha uwiano kipenyo (radius) ya mwezi na Dunia vipenyo hivyo ukiviweka pamoja (mwezi na Dunia) halafu ukachukua mchoro wa Vitruvian man kile kitovu kinafit kabisa kwenye radius hizo ambapo unapata pyramid 6. Katika vile vipande 14 alivyokata da vinci kwenye mchoro ni sawa na vipande 14 ambavyo Seth alikata mwili wa Horus –ni Eagyptian myths (kwa ambao mmetizama muvi ya Gods of Eagypt) lakini pia kwenye mchoro huo huo kaonyesha muundo wa vyumba vyathe great pyramid of giza zilivyo ila chumba kimoja cha Malkia ndio hakionekani

The vitruvian nimchoro wenye mambo mengii sana yaliyofichwa tukiyaeleza yote hatutamaliza,hata hapa nimeeleza just basic meaning za mchoro.. ila ni mchoro umebeba kila kitu kinachomuhusu mwanadamu na ulimwengu. Watu wa ujenzi wanautumia mchoro huu,watu wa anatomy wanautumia,wanajimu,watu wa masuala ya giza wanautumia, budha wanautumia kufanya meditation, watu wa programming pia wanasema kwamba sura iliyopo kwenye mchoro imefichwa na alogarithms zilizowekwa na Vinchii nk. In rarely way ile sura ya huyo mwanaume yuko hapo ni ya da vinci mwenyewe alijichora

Plato, plotonus, proclus na Aristotle wanafalsafa wa zamani wa kigiriki walitoa oncept inaitwa The Great Chain of Bein ambapo ilikuja kuelezewa zaidi baadae kwenye Neoplatonism . walisema kwamba maisha yapo kwenye ngazi Fulani ambazo juu kabisa anaanza Mungu,wanafuta malaika, kisha mwandamu, wanafuta wanyama,wanafuata mimea halafu mwisho kabisa yupo shetani. Davinci alichukua idea hii kisha pale katikati alipo mwanadamu akauweka mchoro wake wa The Vitruvian man. Aliuweka pale akiamini kwamba mchoro wake unamuonyesha mwanadamu kamili aliyeumbwa na jinsi mazingira yake yanayomzunguka anavyoweza kuyamudu, pia kigezo cha mwandamu kuwekwa katikati kwenye the great chain of being wanafalsafa hao wanaamini kwamba mwanadamu ni kiumbe kamili na mwenye hadhi kubwa kuliko viumbe wote.

Mwanadamu kwaumba na roho ambayo ni immortal na Mwili ambao ni mortal hivyo inamuwezesha mwanadamu kuweza kuishi sehemu yoyote ile, duniani au mbinguni ambacho ni kitu malaika,shetani au wanyama na mimea wamenyimwa. Mwanadamu kwakua ana roho yenye uungu na mwili wa kibanaadamu amepewa chaguzi la yeye kuweza kuishi uungu kwa kutenda mema maishani mwake au uushetani kwa kutenda ubaya maishani mwake. Hicho kitendo cha kuchagua ndio kinaufanya tuwe viumbe tuliopendelewa zaidi kuliko kiumbe chochote.

Watu wenye akili zaidi waliowahi kuishi duniani wanatambua mungu yupo ndio maana wakatoa concept hiyo ya the great chain of being, ila wewe una kadigrii kamoja huna ulichokifanya kwenye jamii kutokana na digrii yako hiyo ila kwa frustration za maisha yalivyokudunda unasema hakuna Mungu..pole sana…Chaguo ni lako kama unataka upande ile ngazi ya juu kwa kuiishi uungu au uishi ngazi ya chini uuishi ushetani. Huyo ndio mwamba Leonardo Da Vinci polymath genius.

~Davinci
 
"Marcus Vitruvius Pollio Ndani ya kitabu hicho alieleza kwamba kitovu ndio sehemu ya katikati katika mwili wa mwanadamu"

Na Da Vinci katika mchoro wake anasema
"Sehemu za siri zinapoanzia ndio katikati ya mtu"

Kama Da Vinci alichora mchoro kutokana na kitabu cha Vitruvius,Je unadhani ni nani alikuwa sahihi juu ya mwili wa binadamu, maana naona wanapishana maelezo?
 
Uzi mzuri lkn kwangu sijui kwanini inakuwa ngumu kuamini kama hiyo picha inamafumbo mengi kama inavyoainishwa!!, mengine kama vile yanakuzwa tu nawatu na kuitafsiri waonavyo!!.

Ila nahisi na mweka mada unamaana yako kutuwekea picha hiyo!,nahisi kabisa kuna kaujumbe unataka kukafikisha ila lazima ukafikishe kwa siri!.. hata hivyo usitilie maanani ni kuhisi kwangu tu!..

Elezea hayo mapozi 12 uliyoyaona nje na hayo yanayoonekana!.
 
Mkuu Da'Vinci mara nyingi umekuwa ukitumia msemo fulani hivi “mwenzenu katumia nguvu kidogo ili asieleweke nyie mnatumia nguvu kubwa kumuelewa” nami leo naazima huu msemo wako kuwakilisha mtazamo wangu juu ya hii picha ya Da'Vinci.

Huu ni mtazamo, ila naamini siyo kweli, unawapima katika nyanja zipi linganifu? Maana kuna wataalamu na wagunduzi wenye hekima katika nyanja sisizofanana/ wiana mfano mtaalamu wa hisabati huwezi mpambanisha na mtaaalamu katika nyanja za sanaa au kilimo au afya.
Kumbe umejichimbia hukuuuu....vinci ni something else kwenye mafumbo ya picha. Ngoja niweke baadhi ya mochoro yake
 
Mkuu Da'Vinci mara nyingi umekuwa ukitumia msemo fulani hivi “mwenzenu katumia nguvu kidogo ili asieleweke nyie mnatumia nguvu kubwa kumuelewa” nami leo naazima huu msemo wako kuwakilisha mtazamo wangu juu ya hii picha ya Da'Vinci.

Huu ni mtazamo, ila naamini siyo kweli, unawapima katika nyanja zipi linganifu? Maana kuna wataalamu na wagunduzi wenye hekima katika nyanja zisizofanana/ wiana mfano mtaalamu wa hisabati huwezi mpambanisha na mtaaalamu katika nyanja za sanaa au kilimo au afya.
Kinachofanya nione huyu mtu ndio mwenye akili kuliko wote ni kwamba hakuna angle ya maisha ambayo hakuigusa. Wengi walijaliwa uwezo wa kitu kimoja au viwili..kama Newtown yeye alikua ni mwanasayansi tu. Mozart alikua mwanamuziki tu, Plato slikua mwanafalsafa tu,Carpenicus alikua mwana anga tu..ila Vinchii katenda yote hayo kwa utimilifu mkubwa..
 
Uzi mzuri lkn kwangu sijui kwanini inakuwa ngumu kuamini kama hiyo picha inamafumbo mengi kama inavyoainishwa!!, mengine kama vile yanakuzwa tu nawatu na kuitafsiri waonavyo!!.

Ila nahisi na mweka mada unamaana yako kutuwekea picha hiyo!,nahisi kabisa kuna kaujumbe unataka kukafikisha ila lazima ukafikishe kwa siri!.. hata hivyo usitilie maanani ni kuhisi kwangu tu!..

Elezea hayo mapozi 12 uliyoyaona nje na hayo yanayoonekana!.
Ngoja nitaje baadhi ya mapozi niliyoyaona
1. Mwanaume katanua mikono juu na kutanua miguu
2. Mwanaume nyoosha mikono juu na kukusanya miguu
Haya ndio ambayo tunayaona wote..
Mengine ni...
3.Mwanaume kanyoosha mkonoo juu kushoto mwingine kulia kaushusha chini ila miguu kaikusanya
4.mwanaume kanyosha mkono juu kulia mwingine kaushusha kushoto ila minguu kaitawanya
5. Mwanaume mguu mmoja upo kati kati ya duara mwingine upo kulia mwisho kautanua kidogo ila mikono kaitanua..
........itaendelea
 
Umeona sasa! Mimi namuona mama akimshikilia vizuri mtoto asianguke anapousogelea aushike msalaba.
Wewe unahisi kwanini michoro yake ni maarufu na inathamani kuuubwa sana.? Huo mchoro wa vitruvian unalindwa hatari na ni mara chache kua displayed public
 
"Marcus Vitruvius Pollio Ndani ya kitabu hicho alieleza kwamba kitovu ndio sehemu ya katikati katika mwili wa mwanadamu"

Na Da Vinci katika mchoro wake anasema
"Sehemu za siri zinapoanzia ndio katikati ya mtu"

Kama Da Vinci alichora mchoro kutokana na kitabu cha Vitruvius,Je unadhani ni nani alikuwa sahihi juu ya mwili wa binadamu,maana naona wanapishana maelezo?
Ni kama marcus aliacha gogo ila vinci akachonga kinyango. Vinci alichukua concept tu ya marcus na kuufanya more advanced hata yeye marcus hakuwahi kuchora mtu akiwa hivo kwenye duara na boksi.
 
Hapa kwenye kuamini Mungu pia kuna utata, wengi huamini Mungu kama Concept katika uumbaji(mwanzo wa uhai)
, siyo kama vile tuaminivyo katika Ukristo Mungu baba, Mwana na Roho Mtakatifu, Mungu YAHWEH wa kwenye Biblia.

Wasome tena kwa jicho la tatu utawaelewa.
Ila ni kweli ndio wanavyoamini ila wanabaki palepale kua waligundua Mungu ndio chanzo cha maisha yote
 
Wa nini sasa wanahangaika nao wakati niko hapa chumbani kwangu nina access nao kupitia bandiko lako 😀😀
Exegrations mkuu, ni kama propaganda zingine tu, kukipa kitu umuhimu mkuuubwa for personal interests, ni kama vile tunaaminishwa nyeupe( wazungu) ni bora kuliko nyeusi( weusi/waafrika) na sababu zinatolewa nzuri tu, ukikaa bila kutafakari hilo then utaona hivyo na utaishi ukijua na kuamini hivyo.
Kama ni hivo mkuu watalii wasingekuja serengeti au mlima kilimanjaro maana wanaweza kuAccess kupitia Tv Documentaries
 
Picha is an art...Kilimanjaro na Serengeti ni nature, kwangu mimi(namaanisha me myself and I) ni vitu viwili tofauti havifananishwi.
Sawa lakini ukienda museum una explore mengi ambayo huwezi kuyapata kwenye uzi au kwenye net.
Hafu wazungu wanapenda vitu original ndio maana yupo tayari anunue wimbo kuliko kuupakua bure
 
Hata mimi naona hivyo, labda anataka kutueleza juu ya siri iliyopo kati ya viungo vya siri na mambo mengine ya maisha.
Mkuu funguka tu
Sio mimi vinci ndio picha zake nyingi alikua anazichora in nudity form. Sio yeye tu si unaona ile picha juu kabisa ya creation of Adam inechorwa na michalengello..adam yupo uchi.
Watu wa Rome/Itally ilikua jadi yao naona kuwa uchi uchi sana
 
Back
Top Bottom