The University of DODOMA-UDOM

Povu wapi man kawaida au sio, kwahyo ulisema nani watulize makalio vile? au we kiswahili alokusomesha hilo alikufunza ni jambo la kawaida ukiongea na wakubwa?
Ni yule yule aliyenifunza kuwa kusem "Nyani halioni kundu lake " mbele ya wakubwa ni sahihi
 
Hahahahahaaa nadhani Novemba ile nimeingia zangu Dom nikafikia lodge palipokucha kulikuwa na mdau wangu nikaacha mizigo yangu nikadandia boda nikapandisha chuo.... The very first day naenda kuregister,sasa baada ya kutoka utawala mkuu nikapanda boda nikaingia utawala social, sasa nikajikuta natakiwa nirudi tena utawala mkuu, nilivyoona daladala zinatoka humanities nikadandia chap kusevu hela maana nilipaona ni karibu mno kipindi naletwa na bodaboda mara paap naona tunapita geti kuu pale mara hamad tunaishusha ile down baada ya chimwaga pale, nikamtonya konda oya nishushe kituo kinachofuata, akaniuliza MAKULU? wakati sikijui nikamwambia ndio, kufika nikashuka nikazuga naingia shop kuchukua vocha then nikavuka upande wa pili wa kituo kurudi chuo nikadandia za education/ng'ong'ona bila kuuliza ila uzuri ilikuwa inapitia njia ya utawala mkuu haikunyoosha pale njia panda benki.. nikashuka naona lile libarabara lireefu jengo lipo mbali jua la Dodoma limeshachanganya nikanyakua hatua pale..

kumbukumbu nyingi sana nzuri UDOM nakihusudu sana kile chuo, ingawa kuna lecturer mmoja muhindi ***## yule popote pale alipo na pia walikuwa wanakera kwenye mazingira ya kutegeana ili tupigane mafine ya kukomoana kwenye time extension ya tafiti..
#Embracing Knowledge
ah ah dah mwannagu nmecheka kama chizi./...nakumbuka mgomo mmoja prof mlacha alisema nyie kitu pekee mlichonizidi ni urefu na ujinga sasa endelleeni kugoma muone 2008-2011 dah maisha matamu sana..Big up mende bar wazee wa block 2 room 246 tulifanya bapa party kiingilio konyagi kubwa hadi asubuh tulipata chupa za konyagi kubwa kama 50..maisha matamu..ila usnitch mwingi hivi philip mwakibinga bado tu anassoma chuma. ACT Wazalendo wamvua uanachama Philipo Mwakibinga baada ya kutoa tamko lake dhidi ya maaskofu wa KKKT
 
Kwa wale wa COED na tiba msisahau kutembelea Elly Outfit mjipatie codes kali za kichuochuo.
Tupo UJASI opposite na makut kwa Bonge.
 
Wakati mwingine nafikiria kuhusu aina ya wasomi tulio nao wanabishana kuhusu vyuo ,Mimi nimesoma UDOM 2009 -2012 Elimu niliyopata imenisaidia sana (PPM&CD) ,Wadogo zangu mliopata nafasi UDOM nendeni mkapige shule msiwasikilize wanaosema chuo ni Cha kata huenda hata kidato Cha nne hawajamaliza ,Tanzania hatujafikia kuwa na chuo kikuu Cha kata tukifikia huko itakuwa ni maendeleo ya hali ya juu kila kata kuwa na chuo kikuu
 
Wakati mwingine nafikiria kuhusu aina ya wasomi tulio nao wanabishana kuhusu vyuo ,Mimi nimesoma UDOM 2009 -2012 Elimu niliyopata imenisaidia sana (PPM&CD) ,Wadogo zangu mliopata nafasi UDOM nendeni mkapige shule msiwasikilize wanaosema chuo ni Cha kata huenda hata kidato Cha nne hawajamaliza ,Tanzania hatujafikia kuwa na chuo kikuu Cha kata tukifikia huko itakuwa ni maendeleo ya hali ya juu kila kata kuwa na chuo kikuu
Mkuú hii kozi inahusiana na nn
 
Ni yule yule aliyenifunza kuwa kusem "Nyani halioni kundu lake " mbele ya wakubwa ni sahihi
Asee maisha magumu.Mjipange sisi vijana tunatokaje?Tusaidiane tuachane na ujuaha huu.Tupeane connection tu.Umesomea wapi sio issues tuache utoto.Nawapenda jamaa wa UDOM ni jamaa zangu.Wamenitoa kutoka kudharaulika mpaka kuwa mtu.Yaani unatengwa jamaa wanakuokota daah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom