The top six best politicians from opposition

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289


  • UTANGULIZI
Kwanza naomba nianze kwa kukiri kwamba haya ni maoni yangu kutokana na ufuatiliaji wa siasa za upinzani kuanzia mwaka 2010-2012. Yawezekana kabisa wapo wenye maoni tofauti na haya, itakuwa jambo zuri kama watayawasilisha.

Lakini vilevile ieleweke kuwa dhana nzima ya maoni haya haijaegemea kwenye ubaguzi wa kiitikadi bali umezingatia vigezo nilivyotumia hapo chini kwani natambua wapo wanasiasa vijana kutoka upinzani ambao ni wazuri kwenye siasa za majukwani,uhamasishaji n.k. Hivyo sina maaana kwamba wanasiasa hao si chochote wala lolote katika makuzi ya siasa za upinzani, La Hasha.


  • VIGEZO
Kwa mujibu wa maoni yangu wanasiasa vijana ni wale ambao hawakufufikisha miaka hamsini(50) na kwa namna moja au nyingine wamepata coverage kubwa ya media. Baadhi ya vigezo vya msingi vilivyotumika ni:


  1. Uwezo wa kifikra katika kuchanganua masuala mbalimbali na kushirikisha jamii katika kuibua fikra na mitazamo mbadala.
  2. Ufuatiliaji na utafiti wa masuala mbalimbali yanayogusa maslahi ya Taifa kwa ujumla.
  3. Uwezo wa kujenga na kusimamia hoja mbalimbali.
  4. Utulivu na umakini katika kufanya maamuzi mbalimbali.
  5. Uvumilivu wa kisiasa katika kukabiliana na changamoto (critics) mbalimbali.
  6. Ujasiri wa kuibua masuala mbalimbali yanayodhoofisha ukuaji wa maendeleo na ustawi wa jamii kwa ujumla.
  7. Uelewa wa masula mbalimbali katika jamii nje ya taaluma hisika(kwa mhusika)

SITA BORA

1. Zitto Zuberi Kabwe (Mb)
Kwa kuzingatia vigezo nilivyotumia hapo juu Zitto is the best politician and well-contented among the five hasa kwa kuzingatia kigezo namba 1, 2, 6 na 7. Ujasiri wake umekuwa kielelezo cha mafanikio yake kisiasa.

Bungeni: Ameuliza maswali 9, maswali ya ziada 33, Michango 89.

2. Dr.Kitila Mkumbo
Japokuwa huyu si Mwanasiasa per se bali Mwanataaluma (Academician) ni muhimili mkubwa wa siasa za upinzani (hasa CDM) kwa kuzingatia kigezo namba 1,2,4, na 7. Utulivu na umakini wake katika kuwasilisha na kufafanua masuala mbalimbali katika jamii ni kielelezo na ushahidi tosha wa mchango wake kwa siasa za upinzani (hasa CDM).

3. Tundu Antipus Lissu(Mb)
Huyu ni Mwanasiasa na Mwanasheria anayejua kuitumia taaluma yake vizuri katika kukabiliana na hoja mbalimbali zinazolenga kuua mijadala mbalimbali katika jamii na anakidhi kigezo namba 2,3, na 5.

Bungeni:
Ameuliza maswali 8, maswali ya ziada 20, Michango 120.

4. John J. Mnyika(Mb)
Utulivu, ujasiri na uvumilivu wake katika kujenga na kukabiliana na hoja mbalibali ni kielelezo cha kukubalika kwa siasa za upinzani (hasa CDM) na hasa anakidhi kigezo 2,3,4 na 7.

Bungeni: Ameuliza maswali 8, maswali ya ziada 33, Michango 229.

5. Halima James Mdee(Mb)
Huyu naweza kumuita Mwanamke Jasiri na sauti kubwa ya wanasiasa (wanawake) vijana ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anakidhi kigezo namba 2,3,6 na 7.

Bungeni: Ameuliza maswali 7, maswali ya ziada 17, Michango 71.

6. Joseph Moses Machali (Mb)
Ufuatialiji na utafiti wa mambo mbalimbali yanayoigusa jamii ni moja ya mambo yanayomtambulisha Maachali kama mwanasiasa mahiri kijana kutoka upinzani na kukidhi kigezo 1,2 na 6.

Bungeni: Ameuliza maswali 9, maswali ya ziada 33, Michango 89.

ZINGATIA: Baadhi ya majina yameweza kuwa na vigezo zaidi au pungufu hii haiakisi mtitiririko wa ufafanuzi kwa mhusika.

Nawakilisha.
 
Mmmmmh,Napita.Unautani nakina Ritz,STK nawengine?Ngoja waje usikie.........!
 
Ingawa kichwwa cha habari kinapingana na maelezo yako muhimu,

Ingekuwa maelezo yanaendana na kichwa cha somo, namba moja mpaka tatu ingekuwa ni Dr Slaa!


Kwamantiki hii ulioyokusudia, Mimi nampandisha Tundu Lissu hadi nafasi ya Kwanza,

Nafasi ya pili ashuke Zitto, ya tatu Mnyika, wa nne Dr.Kitila Mkumbo,

Wa tano ni Halima Mdee, wa sita ni Wenje!


Mtazamo wangu
 
Tafiti ni nzuri ila hao Makamanda Sita Vijana uliowataja hapo Wasibweteke na Kusifiwa, wakaze Buti, kuwafikia Wananchi walala hoi. Tunataka Heshima ya Nchi irudi.
 
Aliye mponza kafulila sijui nani Kijana huyu bila tamaa za usaama wa taifa angefika mbali
 
Back
Top Bottom