The Tomorrow War ni Time Travelling theory?

Acha kutumia neno "mzungu"
Halafu hizo ni Sci-fi movies
Tunachanganya concept kadhaa za sayansi pamoja na fiction(kufikirika)

So sci-fi movies ni uongo ulio tiwa nakshi na concepts kadhaa za sayansi

Time travel ni jambo halisi kulingana na sayansi, lakini aina pekee ya time travel iliyoruhusiwa au inayowezekana ni Forward Time travel, tunaweza kinadharia na wala sio kivitendo (kwa sasa) kwenda mbele ya mda na sio nyuma ya mda


Kwenda mbele ya mda inawezekana, ila kurudi haiwezekani kwa sababu inatupa paradox nyingi...

Mfano hii, Grandfather paradox

Unarudi nyuma ya mda na kwa bahati mbaya una muua babu yako kabla hajamzaa baba yako,

Hivyo mama yako hawezi kutana na baba yako ambaye hajazaliwa baada ya wewe kumuua babu yako

Hivyo wewe hutozaliwa,

Kama huto zaliwa huwezi kurudi nyuma ya mda kumuua babu yako kwa sababu hujazaliwa

Kwa sababu huwezi rudi nyuma ya mda kumuua babu yako, hivyo babu yako ana mzaa baba yako ambaye anakutana na mama yako na kukuzaa wewe

Kisha unarudi nyuma ya mda na kumuua babu yako

Hio loop...

So sayansi na logic zina kataa

Kwa hio nikutoe hofu hicho kitu hakipo kwa sababu hakiwezekani

Ni kitu cha kifikirika kutoka Hollywood

Time travelling movie inayo ingia akilini ni Tenet tu
Sijajupata,hata kama ni mfano,
Kwanini uende kwenye past ukamuue babu Yako?
To me huu mfano hauendani na sedmr
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom