"The theory of Everything" Travelling to Infinity My Life with Stephen.

puker

JF-Expert Member
Nov 22, 2018
940
1,847
Habari za muda huu wanajamvi. Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.

Mnamo tarehe 07 September 2014, ilizinduliwa filamu kali kabisa kuwahi kushika hisia za watu wengi duniani iliyokwenda kwa jina la "The theory of Everything".
Humo ndani utakutana muigizaji mahiri kabisa ajulikanae kwa jina la " Eddie Redmayn, ambaye kwenye filamu hii alitambulika kwa jina la "Stephen Hawking".
Pia yupo mwanadada mahiri kabisa ajulikanae kwa jina la "Feliety Jones" kwenye filamu hii alitambulika kama "Jane Wilde"


**********. ***********. ********
Unaweza kujiuliza kwa nini nimeleta filamu hii kwako? vizuri. Ni hivi filamu hii imejaa mkasa mzito na wa kusisimua sana. Naamini kwa aliyeitizama filamu hii kwa jicho la tatu atakuwa amejifunza vingi pengine hata kubadilisha mtazamo wa maisha yake juu ya masuala mbali mbali kama vile mapenzi, kupambania ndoto yako, uaminifu pia Nafasi ya Mungu katika maisha yako.

Binafsi hii ni moja filamu zangu bora kabisa zilizoacha alama katika maisha yangu. Nikaona si vibaya nikushirikishe wewe mdau ambae inawezekana hujabahatika kukutana na filamu hii.
Ndani ya hii film Inazungumzia safari ya mapenzi ya wanachuo wawili bwana Stephen Hawking na mpenziwe Jane Wild waliokuwa wakisoma katika chuo Cha "Cambridge University". Huyu bwana Stephen alikuwa akichukua PHD ya physics Yani ( Physicist) huku mpenziwe akisomea science.
Wawili hawa walijikuta kwenye mapenzi mazito..wakiwa chuoni hapo ni mara baada ya kukutana kwenye sherehe za kufunga mwaka zilizofanyika nje kidogo ya mji. Wakiwa mapenzini ghafla Stephen aliaza kupata tatizo la strock (kupooza) kwa baadhi ya viungo vyake, hii hali ilimpelekea kuwa mnyonge na kukosa furaha, lkn mpenz wake Jane alikuwa nae bega kwa bega akimtia moyo, kwamba matatizo aliyoyapata, hayawezi mbadilisha kuwa mtu tofauti na awali wala kufanya asiweze kufikia ndoto zake, (Yani kuhitimu masomo).
Kadri siku zilivokuwa zikienda, hali ya Stephen iliendelea kuwa mbaya, pamoja na juhudi za madaktari kila siku mwili wake ulizidi kupoteza nguvu na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi. Lakini hali ilikuwa tofauti kwa msichana huyu(Jane )...ndio kwanza mapenzi yaliongezeka mpk kufikia hatua ya kufunga ndoa na kuwa mke na mume.( Hapa tunaona mapenzi ya kweli) Tuliowengi tunampenda mtu kwa mwonekano/maumbile hatumaanishi kutoka moyoni pindi tu vile vilivyotuvutia vikipotea na mapenzi huisha.

Lakini pia, tatizo hili la kupooza (strock) halikumfanya Stephen kuacha kupigania ndoto zake, aliendelea na masomo yake kama kawaida Japo kwa shida kwani mwili wake haukuwa kama awali. Aliendelea kusoma kwa bidii akiamini kwamba ipo siku atafanikisha anachokipigania. (Hapa tunajivunza namna ya kupigana kufa na kupona juu ya ndoto zetu).

Familia yao ilibarikiwa kupata watoto wenye afya nzuri ya mwili na akili. Ingawaje kila kukicha hali ya baba yao iliendelea kuwa mbaya hadi kufikia hatua ya kushindwa kabisa kuongea, lakini walikuwa wakicheza nae nakumpa furaha ili hali kuwa mwili wake haukuweza kufanya chochote kwa wakati huo...alikuwa akitembezwa na wheelchair.( Hapa tunaona jinsi gani watoto huleta furaha na faraja katika familia hata ukiwa na hali gani, watoto ni zaidi ya zawadi.

Jane Wild alikuwa ni mama bora katika familia yake, licha ya kuwa alikuwa na majukumu mazito ya kuilea familia, lakini hakuwah kuchoka alifanya vyote kwa upendo akiamini kwamba bila yeye familia ile haiwezi kuwa. Hapa tunaona thamani ya upendo kwa familia. Misukosuko, Vita, fedheha, manyanyaso n.k nisehemu tu ya maisha, ukiwa kama mzazi ni jukumu lako kuhakikisha familia inastawi vyema.

Filamu hii ina mambo mengi ya kujifunza, hayo ni machache tu, kwa asie ona filamu hii namshauri akaitizame hakika hatotoka mtupu, ina mafunzo lukuki yatakayo kujenga na kukuimarisha.

The_Theory_of_Everything_(2014).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom