The Tanzanian Paradox: The Background is working fine... so "nini mbaya?" "Tatizo iko nini?"

Tatizo kubwa ni lack of political will to implement these development plans....nafikiri the rulling class' interests ziko against the larger public ones na hapo wanapata taabu sana hawa wakubwa kufanya haya maamuzi ya kitaifa...from BOT, TRA, ministries plan nzuri na wasomi walioenda shule kubwa duniani wapo ila nani atazifanyia kazi wakati unagusa wale wenye nguvu katika nchi...tafuta thread yangu ya nani anamiliki uchumi wa tz na athari zake iko humu
 
Kama kuna sehemu ambapo wakati mwingine wa Kenya wananivuruga ni maswali hayo mawili ambayo kwa kweli yanataka kuuliza "kuna tatizo gani?" Lakini ni maswali ambayo yanahitaji udadisi na majibu yanayotokana na ukweli. Miaka hii michache iliyopita nimepata nafasi ya kipekee ya kuweza kufuatilia yale yanayofanywa kwenye background ya political scene ya Tanzania. Nimepata nafasi ya kuanglaia jinsi policy review inavyofanyika na hata kuandikwa kwa sera mbalimbali mpya ambazo nyingine zimeshaanza kufanya kazi.

Lakini vile vile nimepata nafasi kutokana na udadisi kupitia vyanzo mbalimbali kusoma mambo yale yanayofanywa na wizara, idara, taasisi na vyombo binafsi katika kujaribu kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi. Mipango, utafiti, ushauri n.k Nimegundua kitu kimoja huku nyuma inaonekana vitu vinaenda vizuri kweli. Hakuna kitu ambacho - as far as I can tell - ambacho hakijawahi kufanyiwa utafiti wa kina au kutolewa mapendekezo mazuri sana ya kukabiliana na mambo mbalimbali. Kuanzia elimu, maji, barabara, fedha, n.k There are a lot of materials out there! Kuna nyaraka, makaratasi ( white, brown and green!)

Lakini ukija huku juu au niseme mbeleni something seems to be oddly dysfunctional. Ni kana kwamba watu wanafanya vitu kwa kukisia au making up as they go along! This is what I call "The Tanzanian Paradox". Na utaona inahusiana hata kwenye mambo ya matumizi ya utajiri wetu (tuna ardhi, maji, mbuga, madini, gesi n.k) lakini bado ni maskini!

Is it possible then that we are in a sort of 'caught in a time warp'? Kwamba kwenda hatwendwi lakini twaonekana twaenda? Tunatoka jasho na kutembea kwa nguvu kumbe tuko kwenye treadmill of underdevelopment?
Najisikia kukumbishai tu mawazo ya zamani; ili tusije kudhania kuwa kuna kitu kipya kinaendelea ambacho hakjawahi kujadiliwa humu
 
Back
Top Bottom