The Switch ya Lil' Ommy

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,576
18,894
Binafsi ninakuwaga sisikilizi Mara kwa mara kipindi tofauti na habari za michezo kwenye redio,Jana nilibahatika kuona video fupi hiv akisambaa mitandaoni ikimuonesha lil ommy akifanya mahojiano na Mama Kanumba, Jennifer na Patrick kwenye kipindi kipya Cha "the switch" cha Wasafi FM kama sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya marehemu Kanumba kwenye Bongo Movie kipindi hiko kinaundwa na Lil Ommy a.k.a The King of Interview or The Real M.V.P akiwa na mwanadada Ammy Gal pamoja na Ray Mshana

Tokea iki kipindi kianzishwe nilikuwa bado sijakitazama kupis hiyo video fupi niliyoona mtandaoni nikashawishia kwenya kukicheki hiko kipindi kwenye YouTube ya wasafi media honest,Nimekipenda kwa angle hiz

1. Kina arrangement nzuri Hakuna muinguliano wa presenters kuuliza maswali
2. Presenters wana uliza maswali vizuri kwenye angle zote bila kubase kwenye udaku kama mapresenters wengi wa kibongo wanavyofanya.Una ona Kuna ubunifu kwenye kuuliza maswali.
3. Ubunifu (setting up nzima ya kipindi kuna segment mpya kabisa ambapo lil ommy amefanya tofauti na kipindi yupo Times FM segments hizo kama Kaa Kijanja n.k

Mwisho kabisa nimalizie kwenye kipindi ambacho kipindi cha Block 89 kimesimamishwa kinatakiwa kijifunze kupitia Lil' Ommy anachofanya kupitia kwenye kipindi chake chake cha "The Switch" Kuna mengi wanatakiwa kujifunza especially kwa watu kama mtu imara na Calypso.

Calypso anatakiwa ajifunze kwa Ammy Gal; awe serious aache utoto na mtu imara ajifunze kwa Ray Mshana ambaye role yake inafanana na mtu imara mwenzake ana vikorombwezo zinazovutia listeners hata kama hayupo serious muda mwingi.

Nimalizie kwa kutoa hongera kwa lil ommy pamoja na crew yako kwa kutuletea kipindi kizuri.

Lil Ommy.jpg

Lil' Ommy
 
Hicho kipindi chakawaida sana kwanza radio yenyewe inasikika maeneo machache ndani ya dar
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom