The Silent Mutiny

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Amani, Utulivu na Mshikamano.
Maisha bora kwa kila Mtanzania.
Kasi, Ari na Nguvu Mpya.

Hizi tenzi tatu zimekuwa zikiimbwa majukwaani kwa miaka nenda rudi kuonyesha Tanzania kuwa nchi yenye amani na watu wake wanafuraha ya hali ya juu.

Lakini, Jumapili iliyopita ya Oktoba 31 2010 siku ya uchaguzi, kauli hizi zimedhihirika kuwa si kweli. Wala sizungumzii wale waliowapigia kur wagombea wa vyama vya upinzani, bali ni wale ambao waliamua kwa amani, utulivu na mshikamano kufanya mapinduzi baridi ya kuacha kupiga kura.

40% ya waliojiandikisha hawakupiga kura.

Je kama Taifa, tunalionaje jambo hili?

Je kama upinzani , tunalipimaje jambo hili?

Je kama CCM wanafikiria nini kuhusu jambo hili?

WaliesmaGA mapinduzi hayatatangazwa kwenye Luninga, taratibu mapinduzi baridi yameanza.
 
% of eligible voters who voted in 2008 USA presidential election was 61.7%
Source
Answers.com - What percent of eligible voters voted in the 2008 presidential election

% of eligible voters who voted in kwenye uchaguzi ulioisha wa UK nadhani haizidi 65% .

Kwa hiyo nafikiri kwa kiasi tatizo hili si la chama chochote research na wenzeutu wana baadhi ya majibu tayari

Ukisoma Voter turnout - Wikipedia, the free encyclopedia tunaweza kujifunza vitu
Different countries have very different average voter turnouts. For example, in the United States 2008 presidential election turnout was 63%[2] and 68% among African Americans. In Australia, which has compulsory voting, and Malta, participation reaches 95%. These differences are caused by a mix of cultural and institutional factors.
In summary sababu ya turn out ndogo ndio hizo.Nimeipenda hii approach ya Australia ambayo inaonekana kutatua tatizo

Compulsory voting

One of the strongest factors affecting voter turnout is whether voting is compulsory. In Australia, voter registration and attendance at a polling booth have been mandatory since the 1920s. These rules are strictly enforced, and the country has one of the world's highest voter turnouts. Several other countries have similar laws, generally with somewhat reduced levels of enforcement. If a Bolivian voter fails to participate in an election, the citizen may be denied withdrawal of their salary from the bank for three months.[35] In Mexico and Brazil, existing sanctions for non-voting are minimal or are rarely enforced. When enforced, compulsion has a dramatic effect on turnout. In Venezuela and the Netherlands compulsory voting has been rescinded, resulting in substantial decreases in turnout. In Greece voting is compulsory, however there are practically no sanctions for those who do not vote.
 
The NEC had considerable contribution to the low number of voters. All those people who did not see their names although they had registered!
 
Kwa sisi tunaoishi uswahilini tunajua wazi kuwa moja ya sababu ya watu wengi kutopiga ni matokeo ya kupoteza matumaini ya uongozi wa nchi. Wengine wanaamini kuwa hata wakipiga kura yule wanayemataka ataibiwa na wataanguka, rafiki yangu mwingine pale Arusha siku moja kabla ya kura aliniambia kuwa anaona maaskari wengi sana mitaani kwa hiyo hatatoka nyumbani siku ya uchaguzi, ingawa amejiandikisha hataenda kupiga kura wachakachuaji wasjiempiga mabomu bureeeeeee! naamini zipo na sababu nyingine nyingi tu.
 
Hivi wale walioohofia kuwa wangepiga kura bado kura zao zingeibwa au kungechezwa mchezo fulani wana sababu ya kuona kuwa hofu yao ilikuwa haina msingi?
 
Companero,

Let just say unpreciously kuwa it was 40% that abstain for the sake of gumzo!

Mzee Mwanakijiji,

Someone got to pay and shme on those who were part of mchezo mchafu. Unajua quest nyingine zinatiaGA aibu. Kama isingekuwa hili la kung'ang'ania high percentage win, bado aliyeshinda angeshinda japo kwa idadi ndogo.
 
Hizo for the sake of gumzo ndio zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi hii, takwimu halisi umepewa ila unaona vyema kuchakachua for the sake of gumzo - yaani ni sawa na kusema hela za EPA zilizochotwa ni Tsh 400,000 for the sake of gumzo! Acha uvivu angalia takwimu and be precise!
 
Hivi wale walioohofia kuwa wangepiga kura bado kura zao zingeibwa au kungechezwa mchezo fulani wana sababu ya kuona kuwa hofu yao ilikuwa haina msingi?

Waziri katika Ofisi ya Mkuu mwenyewe anadai za kwake zimechezewa huko A-Town sembuse mwananchi wa kawaida?

Aisee tafadhali jibu barue pepe niliyokuandikia kuhusu makala ya wanasiasa vijana au nikutumia kwa anuani nyingine?
 
... bali ni wale ambao waliamua kwa amani, utulivu na mshikamano kufanya mapinduzi baridi ya kuacha kupiga kura.

Ndio!

Hawa; 2005 walipiga kura..kwani walikwenda kumuingiza kiongozi wakitegemea atakuwa na 100% ya maamuzi ya uongozi wake..kwa miaka 5 baadaye, wamegundua uongozi waliopigia kura..una ubia na mafisadi.. hauna maamuzi ya dhati!!

Kama ni Uongozi wa kuchangia tungepewa idadi na wasifu...wa wote watakao changia.. ili nao wawe sehemu ya kupigiwa kura...

Kama mafisadi kumi watahusika kuyumbisha na kumzidi maamuzi niliyempigia kura... nao wangekuwa kweye kampeni na mchakato wote...nk na picha zao ziwe zinamzunguka mgombea mkuu ili zote tuzidubukize kwenye kibox cha kura.

Sasa katika hao kumi na moja nani ni Kiogozi halisi wa Taifa...!?

Leo wabia wa uongozi wamechagia kumrudisha Kiongozi mkuu kwenye madaraka ...bila hata kuhesabu kura niliyopiga...au wameongeza kura ambazo wanafanya ya kwangu isiwe hata na maana..

Kwa hiyo bora aliyejua mapema ...akaachana na huo usanii na usumbufu wa vijimstari na mahesabu ya kitoto

Wabia wa Uongozi ndio wanaoamua ...Kiongozi na sio Kibox cha kura....

Niulize kama waliopiga kura wangekuwa woooooteeeee..100%...nani kakuabia ingebalidisha matokeo ya hiyo 40%? .... sasa kwanini tusumbuaneeeeeh!!

Tunachotaka ni kupiga kura au ni kumpata kiogozi...? Tutafakari swala hili bila kubabaisha...
 
Hizo for the sake of gumzo ndio zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi hii, takwimu halisi umepewa ila unaona vyema kuchakachua for the sake of gumzo - yaani ni sawa na kusema hela za EPA zilizochotwa ni Tsh 400,000 for the sake of gumzo! Acha uvivu angalia takwimu and be precise!

Niko msibani...nihurumie
 
Comrade Companero.

Between 50-55 percent of registered voters abstain from casting their votes, the big question is WHY?

Je is it possible kuwa Wananchi hawa are no longer engaged with Siasa za Tanzania na hasa Serikali yake?
Je hawaitegemei Serikali na hawaoni manufaa ya kupiga kura?
Je wamechoshwa na CCM na Sera zake na hawaoni sababu kukipa kura?
Je Upinzani bado haujaweza kujitangaza ipaswavyo kwa kundi hili lililozira na kuaminika kuwa wanaweza kuleta mabadiliko kuliko CCM?
Je Watanzania wameridhika na hali waliyonayo na mfumo wa kidemokrasia tulio nao?

Na hayo maswali manne, tuyachukulie kuwa hapakuwa na uchakachuaji wa namna yeyote ile, na tuhitimishe na Swali kubwa, je ni vipi kundi hili linaweza kusisimuliwa ili washiriki uchaguzi mkuu wa 2014 (Tamisemi) na 2015 (wabunge na rais)?

Tukiangalia kusita kwa hawa wapiga kura kwa mazingira ya Uchakachuaji tujiulize:

Je idadi hii ilivyo kubwa ina maana somo la uraia na haki za kikatiba bado havieleweki kwa Mtanzania?
Je imani na trust kwa Serikali kusimamia haki na kujiendesha kwa haki na kisheria imepotea kabisa?
Je kundi hili lilirubunika kirahisi kwa vile vitisho vya vurugu au umwagaji damu na kuogopa kupiga kura?
Je madai yao ya kuwa hata iweje CCM itashinda tuu, yanaashiria nini ukizingatia mwenendo mzima wa uchaguzi ambapo NEC, Polisi, JWTZ na TISS waliingilia mchakato mzima wa uchaguzi?

Kwangu mimi, 55% ya watu kutopiga kura ni jambo la hatari sana na kama ningekuwa Serikali, nisingejivunia kitu wala kushangilia Ushindi wowote. Hii kwangu ina maana Wananchi wa nchi yangu wamekataa na kufanya mapinduzi baridi kwa kususia kutumia haki yao ya kikatiba na kuchagua Serikali wanayotoaka ukizingatia kuwa Serikali ni watu.

Hii ni alama ya watu kuwa actively disengaged na ningekuwa Serikali, jambo la kwanza ni kuanza kuhamasisha Watanzania wote waelewe elimu ya Uraia na kuwafanya wawe washiriki na wabia kamili katika kuliendesha Taifa na si kuwafanya wao Watumwa wa kuchagua na kutoa dhamana ya kuongoza nchi kwa kundi fulani na kisha kusahauliwa.

Changamoto kwa Upinzani ni hii, ni vipi wanaweza kuliamsha hili kundi na kulifanya lipigie kura Upinzani kwenye Uchaguzi unaokuja?
 
Kuna kupoteza imani kwa kiasi fulani kwa serekali hasa pale inaposhindwa kuwatatulia wananchi wake matatizo yanayowakabili,ambapo mwananchi anaweza kuubadili uongozi kwa kutumia kura yake.Lakini pale serekali inaposhindwa kuleta maendeleo huku ikiendesha ubadhirifu mkubwa na kuzidi kudidimiza ndoto za wananchi za maisha bora,kuwalinda na kuwakumbatia mafisadi inakuwa wazi kwamba hata ile haki ya raia ya kuchagua viongozi haipo kwani ni wazi kura zitaibiwa na hao madhalimu hivyo kumfanya mtu kukataa tamaa asijue la kufanya kwani kura yake haina thamani tena.Hiyo inadiscourage kupiga kura,ukiangalia yaliyotokea hapa kwetu mwaka huu mimi naamini waliopiga kura walikuwa wengi zaidi ya waliotajwa kwani mwamko ulikuwa mkubwa sana ila kilichoripotiwa ni matokeo ya uchakachuaji hivyo haitoi picha halisi ya wapiga kura.mfano kura ziliharibika nyingi sana ila wao katika analysis wanasema turnout ilikuwa 42% bila kujumuisha ziliharibika achilia mbali walionyimwa haki yao.Lakini kwa hali hiyo sasa ndio inaweza kuwavunja watu kupiga kura kipindi kijacho kutokana na mapungufu makubwa ya kipindi hiki huku mengi yakionekana wai kuwa ni makusudi.
 
Rev. Kishoka,
Mkuu wangu, habari tulopewa ni kwamba - Waliopiga kura ndio 40%..(millioni 8 kati ya millioni 20)
 
Nitasamehew kwa kuwa sina ushahidi wa kutosha kutoa kauli hii.. lakini ninahofu kuwa kulikuwa na mkono unaotaka watu wasipige kura kwa idadi ile ile iliyojiandikisha...mustakabali mzima wa watu wale walioshindwa kupigwa kura kwa kisingizio cha majina yao au picha zao kutokuwepo katika daftari lakudumu + Mashart magumu kwa wale waliojikuta mbali na vituo vyao walivyojiandikishia + Wanafunzi wengi wa vyuo kushindwa kupata nafasi ya kupiga kur kutokana na vyuo kutofunguliwa kabla ya uchaguzi....

Sidhani kama kulikuwa na uamsho kwa mamlaka husika kuwasukuma wananchi wakapige kura...kwa nini hilo halikufanyika?????
Hilo ni swali jingine all together
 
40% ya waliojiandikisha hawakupiga kura.

Je kama Taifa, tunalionaje jambo hili?

Je kama upinzani , tunalipimaje jambo hili?

Je kama CCM wanafikiria nini kuhusu jambo hili?

WaliesmaGA mapinduzi hayatatangazwa kwenye Luninga, taratibu mapinduzi baridi yameanza.

Ukweli ni kuwa waliopiga kura ni zaidi ya milioni 13 na NEC hawapo tayari kusema ukweli kwa sababu kura nyingi wameziharibu ili kuhitimisha malengo yao..............................
 
Lakini tusilipuuzie hili jambo na kudai ni uchakachuaji pekee, kama ni kuchakachua, nani awajibishwe ,maana tulitumia pesa nyingi kujianda kwa huu uchaguzi, na hivyo nusu ya fedha zilizopangwa kutumika siku ya uchaguzi zimepotea na ni hasara.
 
Lakini tusilipuuzie hili jambo na kudai ni uchakachuaji pekee, kama ni kuchakachua, nani awajibishwe ,maana tulitumia pesa nyingi kujianda kwa huu uchaguzi, na hivyo nusu ya fedha zilizopangwa kutumika siku ya uchaguzi zimepotea na ni hasara.

The last thing you need to worry about ni the so called uchakachuaji, upinzani hawa ogopi juhudi zote za campaign bado kuna low turnout. Ukizingatia na hiyo hiyo percentage ndogo iliyojitokeza bado CCM inashinda kwa ushindi wa asilimia sitini na kitu.

What does this say about the nation ina maana bado watanzania wengi sana kuchoshwa na CCM wala kutaka kudai mabadiliko. Hii si hasara kwa CCM kwao wao ni kwamba bado wanakubalika its more of a problem to the opposition kwa kuwa bado wengi hawako tayari kwa mabadiliko na kujitokeza kupiga kura za kuleta hayo mabadiliko.
 
Je mwaka huu na zoezi la BVR kuwa la mashaka mashaka tutegemee nini kwenye voters turnout?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom