The SGR War: MagufuliKagame vs MuseveniKenyatta ni Vita Kubwa!. Who Will Win, Loose or Its Win Win Situation?.

Na hapo ndipo mnapokosea kwa maoni yangu, ni kama vile mnageuza lengo la sisi kujenga Reli yetu kutumiwa na nchi nyingine, hilo siyo lengo kuu au niseme halipaswi kuwa lengo kuu, lengo kuu linapaswa kuwa kwa ajili ya matumizi yetu ya ndani na hizo nchi za nje iwe secondary tu.

Na ndiyo maana naisifu Serikali yetu kwa kutaka kuishirikisha Rwanda kwenye kuchangia gharama kama wanataka kuitumia Reli pia lkn hakuna nchi Dunia hii ambayo hujenga Reli eti ili itumiwe na nchi nyingine kwangu kama hauna mizigo ya ndani ya kusafirisha ni bora uache kujenga.

Na mizigo ya kuendesha Reli yetu ipo ni swala la sisi kujipanga tu, Migodi yetu yote inaweza kutumia Reli yetu kwa Exports na Imports hata tunaweza kumfikishia Dangote Makaa ya Mawe kwa Reli yetu, hivyo tukijipanga tunaweza kuiendesha Reli yetu wenyewe na hao wa nje ya mipaka yetu wanaweza kuja kama nyongeza tu ya mapato lkn siyo wawe ndiyo chanzo kikuu cha mapato yetu ya kuendesha Reli yetu au Bandari yetu kama ukiniuliza mimi!!
Aisee we jamaa... lazima utakuwa una taaluma ya unesi...

Kachome wagonjwa sindano wapate tiba we jamaa...

Mambo ya uchumi waachie wenye taaluma zao...
 
Sisi tutamaliza Kigali tutaunga na hiyo ya Uganda kutoka Kigali mgoma itakija gharama za usafirishaji route yetu fupi na running cost zetu ni chini WAo wanatumia diesel sisi umeme pia wakenya ni wezi sana kwenye mizigo ya wateja
 
Nadhani tuna tatizo mahali, iko master plan ya railway ya east Africa sijui kama bado iko kwenye mipango ya utekelezaji
 
P.Kagame ndiye Raisi wa Afrika, either with Kagame or against Kagame, isitoshe Kagame na Museveni ni kama mtungi na kata!
Nadhani ubongo wako umeanza kuathirika na sumu.Tangu lini Kagame kapewa urais wa Afrika kwanza hicho cheo sijawahi kukisikia.

Mada kama hizi ni vyema ukaziacha kando subiria zile mada za kumtukuza bwana yuleee.
 
Mkuu mwaga majibu ya kisiasa tu kwa sasa kwani ndio yenye msaada. Nikashajua toka mradi ulivyoanza mwaka jana mwezi wa 4 mpaka sasa, wangalau ningeweza kukadiria ikifika 2020 mradi wa hicho kipande kidogo utakuwa umekamilika kwa kiasi gani. Sasa kama mradi huo mmoja tu ndio kujivuta kote huko, hizo mbwembwe za mkuu kusema kwamba atafanya mradi wa umeme wa stiegler gorge anazipata wapi? Kibaya zaidi anasema ikifika 2020 hiyo miradi itakuwa imekamilika!!

Waberoya ni ukweli uliodhahiri kwamba uchumi uko pabaya, hasa ukizingatia hizi porojo zenu nyie watetezi wa awamu hii wenye uelewa wa mambo. Halafu tukienda kwenye ajira huko ndio naona wala hamuongelei. Sasa hivi sehemu nawashauri mjikite ni hii ya kununua wapinzani, na kutaja wasaliti, ila huku kwenye mambo mazito ngoja tuwaangalie waKenya wangalau wanajua nini kinaendelea kwenye hii dunia, wacha sisi tuendelee na hizi siasa chafu hapa nchini.

sijawahi kuwa mtetezi, naeleza ninachokijua

una hiyari ya kulaumu tu, siku ikifika yanaonekana mazuri utalaumu, ndio uko hivyo sio kwa JPM watu wa aina yako wanalaumu kila kitu mpaka mkeo, watoto na mpaka viungo vyako vya mwili!!...mguu ukijikwaa utaulaumu na kuuambia "kimbelembele chako hicho"
 
sijawahi kuwa mtetezi, naeleza ninachokijua

una hiyari ya kulaumu tu, siku ikifika yanaonekana mazuri utalaumu, ndio uko hivyo sio kwa JPM watu wa aina yako wanalaumu kila kitu mpaka mkeo, watoto na mpaka viungo vyako vya mwili!!...mguu ukijikwaa utaulaumu na kuuambia "kimbelembele chako hicho"

Kuna mazuri nayaona, hayo silaumu japo sisifii kwani kusifia sio lazima bali ni utashi. Ila pale ninapoona siridhishwi nakosoa bila kuuma maneno. Na kwakufanya hivi sifanyi kosa lolote. Sisi watu tunaolaumu ni muhimu sana kwani tunawafanya waliopewa dhamana kuwajibika ili kutuziba midomo na hatimaye kuwa faida kwa taifa.
 
Thread yako ina maana, inapasa tuweze kufanya hesabu ya Return on Investment (ROI). Nijuavyo mimi, Isaka -Kigali spur is shared 50/50. Wakati wa ukoloni reli zilijengwa kusafirisha bidhaa kupeleka sokoni, purely extractive purposes. Dunia sasa imehama, reli zilijengwa alongside with Fibre optics, express highways, petroleum pipeline, gas pipeline na water pipeline. Kila inapopita reli panajengwa corridor anchor town, huu ndio uchumi wa viwanda
 
Baada ya Rais Kagame na Rais Magufuli, kukubalia kujenga reli ya SGR kutoka Isaka kwenda Kigali, ili mizigo ya Rwanda, ipitie bandari ya Dar es Salaam, Isaka hadi Rwanda, kitu ambacho kingepunguza kuitegemea bandari ya Mombasa, huku rais Museveni na na rais Kenyatta, nao wamekutana na kukubaliana kukamilisha SGR ya Mombasa kupokea shehena ya Uganda.

Shehena ikifanikiwa kufika Uganda, kupeleka mzigo huo Rwanda na Burundi, ni karibu Zaidi, kuliko Kutoka Isaka kupeleka Rwanda na Burundi!.

Hii ni vita kubwa ya kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya, mshindi wa vita hii ni yule ambaye atafanikiwa kuifikisha hiyo SGR mapema. Sisi SGR yetu ujenzi umeanza kwa kipande cha DAR-Moro tuu, na Kutoka Moro-Dodoma jiwe la msingi litawekwa mwezi February, 2018....
...
Paskali, biashara kushamiri na kukua ina mambo mengi ya kuzingatia zaidi ya kuwa na majengo, miundo mbinu nk.

Biashara ni ushindani, niombe ukumbuke hilo. ATC vs Kenya Airways, kwa mfano tu. Kwa mantiki yako hapo juu unashauri ATC isiimarishwe kwa kuwa Kenya Airways inafanya vizuri. Nitakuwa nimekosea nikihoji una maana gani kama siyo kubeza mikakati ya Serikali kukuza uchumi wa nchi hii![/I]
 
Unaongelea vitu tofauti mkuu; Idd Amin na JPM wapi na wapi?? Inawezekana uelewa wako sio level ya hii thread. Kwa taarifa yako wanaopiga hizi tararila za kumpinga rais wetu ni asilimia ndogo sana like 0.0001 ya wananchi wote wa Tz. Ukitaka proven evidence hizo chaguzi chama tawala kinavyoshinda au unafikiri hawa walioko JF ndio wananchi wapiga kura??? Kwahio hilo la SGR wala usiwe na wasi wasi time will tell na huyo UK mnaemuaminia atapigwa za uso mchana kweupe au mnazani Museveni ni mtu wa sport sport. Kingine SGR yetu ni kwa maendeleo yetu sio ya nchi jirani hawa Rwanda wamekuja na kuomba wenyewe wala TZ haikua na huo mpango. Wabongo mnachonga sana.
wewe kweli mdumange! Huelewi kuwa ukiwagawa watu wako unatengeneza maadui wa ndani? Na hiyo asilimia umeitoa wapi? Kwenye lile gulio la viongozi labda!! Suala zima ni kwamba busara na hekima inatakiwa kwa viongozi ili kuunganisha wananchi wote! Idd Amin alipigwa na wananchi 30milion wa wakati huo kwa ajili ya hekima ya uongozi uliokuwepo!. Inatia uchungu kuona kuwa Nchi imefikia kusifu marais wa nchi nyingine! Kosa siyo la wananchi ila VIONGOZI tafakari chukua hatua
 
37% ya mizigo inayopita bandari ya dar ni ya Zambia 35%ni ya Drc lubumbashi njia moja na zambia kwa hiyo njia ya Tazara inahudumia 72% ya mizigo yote inayopitia Dar achaneni na 17% hailipi zaidi ya kumnufaisha Pk tu
Hiyo 17% ni by road,mingine inapitia mombasa so tukipeleka reli tutaichukua 100% ya kizigo yote ya rwanda na burundi plus eastern congo
 
Propaganda at its highest stage
Kwanza hakuna mkataba wa makubaliano na wachina kujenga reli kutoka Mombasa hadi Kampala, bali ni Mombasa hadi Naivasha. Phase two kwa Kenya bado najuapia kuwa Uganda wanataka electrified SGR ambayo wakenya wameikataa. Mchina machale yanamcheza baada yakuona kuwa tunaenda Kwanzaa speed Uganda, Rwanda name Burundi Anajiuliza kama pesa yake itarudi. Pia Exim tuliwakataa kutokana name conditions walizotaka kutuwekea. Haiwezekani tukope alafu wao waiendeshe reli. Pesa zipo natutafika kabla ya wakenya
Screenshot_20180127-084927.png
Baada ya Rais Kagame na Rais Magufuli, kukubalia kujenga reli ya SGR kutoka Isaka kwenda Kigali, ili mizigo ya Rwanda, ipitie bandari ya Dar es Salaam, Isaka hadi Rwanda, kitu ambacho kingepunguza kuitegemea bandari ya Mombasa, huku rais Museveni na na rais Kenyatta, nao wamekutana na kukubaliana kukamilisha SGR ya Mombasa kupokea shehena ya Uganda.

Shehena ikifanikiwa kufika Uganda, kupeleka mzigo huo Rwanda na Burundi, ni karibu Zaidi, kuliko Kutoka Isaka kupeleka Rwanda na Burundi!.

Hii ni vita kubwa ya kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya, mshindi wa vita hii ni yule ambaye atafanikiwa kuifikisha hiyo SGR mapema. Sisi SGR yetu ujenzi umeanza kwa kipande cha DAR-Moro tuu, na Kutoka Moro-Dodoma jiwe la msingi litawekwa mwezi February, 2018.

Mtihani kwa SGR yetu ni funding, so far hakuna any guarantee ya Fedha za kipande cha Dodoma hadi Isaka, kisha kipande cha Isaka hadi mpakani na Rwanda, lakini kwa wenzetu Kenya na Uganda, Exim Bank ya China, imekubali kutoa mkopo kugharimia kila kitu!.

Wachina hawa wa Exim Bank, ndio mwanzo walikubali kuigharimia, reli yote ya SGR ya Tanzania, ila tenda ilipotangazwa, Waturuki wakashinda, China wakajitoa, sasa wana fund SGR ya Kenya-Uganda. Hii maana yake SGR ya Kenya itatangulia kukamilika kabla ya SGR yetu, kwa Rwanda ni ka nchi kadogo, ili SGR ilete Rwanda, ni kama SGR hiyo itakuwa na outlet. Target ya SGR kwa Uganda ni kupeleka mzigo Juba ambayo ndio the shortest route.

What does this mean to SGR yetu?.
Paskali
Rwanda, Kenya & Uganda Kujenga Reli ya Mombasa-Kampala-Kigali kwa $13bn/-!
https://www.jamiiforums.com/threads...do.561519/da-inakuja-kivingine.1378756/page-6
Mapinduzi makubwa yaja kwenye reli nchini
Uganda seeks joint Exim Bank talks with Kenya on SGR funding

SGRPIC.jpg

President Uhuru Kenyatta (right) welcomes his Ugandan counterpart Yoweri Museveni at State House on December 19, 2017. The two Heads of State agreed to fast-track the remaining sections of the standard gauge railway (SGR) by synchronising the financing.. PHOTO | SAMUEL MIRING'U | PSCU

In Summary
  • Officials in Kampala are banking on Kenya agreeing to the proposal of joint negotiations so that the teams can travel to Beijing to conclude financing details.
  • In December, the two Heads of State agreed to fast-track the remaining sections by synchronising the financing.
By JULIUS BARIGABA
More by this Author
Ugandan and Kenyan authorities are pushing for joint negotiations for the funding of the standard gauge railway, The EastAfrican has learnt.

Kampala, whose application to China’s Export and Import (EXIM) Bank is highly dependent on the treatment of Kenya’s application for funding of the different sections of the railway, has now asked Kenya for a joint mission to Beijing to meet officials of the bank to expedite the financial closure for the two countries’ multibillion-dollar projects.

The projects relate to the remaining sections: Naivasha-Kisumu-Malaba on the Kenyan side and Uganda’s 273km long Malaba-Kampala line that will cost $2.3 billion.

Officials in Kampala are banking on Kenya agreeing to the proposal of joint negotiations so that the teams can travel to Beijing to conclude financing details.

“We hope to go this month,” said Uganda SGR project co-ordinator Kasingye Kyamugambi.

The EastAfrican has seen a letter to Uganda’s High Commissioner to Kenya, dated January 5, 2018, proposing that the High Commissioner requests Nairobi for a “joint Uganda-Kenya engagement of the Chinese authorities and Exim Bank on the Standard Gauge Railway.”

Related Content
The tone of the letter — signed by John L. Mugerwa on behalf of the Permanent Secretary of Uganda’s Ministry of Foreign Affairs — is in line with the meeting of presidents Yoweri Museveni and Uhuru Kenyatta on December 19, 2017 at State House, Nairobi, that proposed the Naivasha-Kisumu-Malaba and Malaba-Kampala legs of the SGR should be done concurrently.

During that meeting, the two heads of state also agreed to fast-track these sections by synchronising the financing and construction, and the two countries’ ministries of Transport followed this up by signing an agreement to this effect.

READ: Kenya and Uganda to collaborate on SGR

Construction of the $1.5 billion Nairobi-Naivasha leg is ongoing, leaving the sub phases of Naivasha-Kisumu and Kisumu-Malaba in Kenya and Malaba-Kampala on the Ugandan side for fast-tracking.

In the letter, also copied to Uganda’s ambassador to Beijing, Mr Mugerwa says Kampala wants to meet with the SGR financiers to “reiterate the commitment of both countries” as it is hoped that this visit would thrash out financing details and pave way for “timely implementation of the remaining sections and resolve any outstanding technical issues.”

READ: China Exim sets terms for financing Uganda’s SGR

ALSO READ: China plan raises hope for East African SGR project

Mr Mugerwa’s docket is to co-ordinate with ministries, departments and agencies to ensure timely implementation of the Northern Corridor Integration Projects (NCIP), which includes infrastructure like the SGR and energy interconnection.

By the time we went to press, the Kenyan High Commission had not responded to our questions on whether Nairobi had agreed to the proposed joint mission to Beijing.

However, in a previous interview, Kenya Railways managing director Atanas Maina said Kenya was yet to submit funding proposals for the Kisumu-Malaba section of its SGR as the government felt it needed to first finish the Naivasha-Kisumu phase.

Kampala is desperate to get the deal over the line so that construction of the Malaba-Kampala SGR phase can start, even as officials say that depending on other requirements that the Chinese might demand, the planned joint visit to Beijing may not guarantee financial closure.
 
Acha mzaha wewe, nani kakwambia Rais anafuatilia shilawadu? Mambo menine tusimsingizie Rais. Hata mtu wa kawaida hanamda huo sembuse Rais?
Sasa mkuu pascal kama mkulu kajifungia magogoni akifwatilia kipindi cha shilawadu na kufwatilia uchaguzi wa siha wakati wenzake wameenda kwenye world economic forum huku wakitumia nafasi hizo kutafuta wawekezaji unatarajia nini??

Nnavyoona kenya na uganda wakifanikisha na kagame akiona mkulu analeta siasa kwenye sgr basi ataungana na akina kenyatta...[/QUOTE
 
Acha mzaha wewe, nani kakwambia Rais anafuatilia shilawadu? Mambo menine tusimsingizie Rais. Hata mtu wa kawaida hanamda huo sembuse Rais?
Sasa mkuu pascal kama mkulu kajifungia magogoni akifwatilia kipindi cha shilawadu na kufwatilia uchaguzi wa siha wakati wenzake wameenda kwenye world economic forum huku wakitumia nafasi hizo kutafuta wawekezaji unatarajia nini??

Nnavyoona kenya na uganda wakifanikisha na kagame akiona mkulu analeta siasa kwenye sgr basi ataungana na akina kenyatta...[/QUOTE
 
Acha mzaha wewe, nani kakwambia Rais anafuatilia shilawadu? Mambo menine tusimsingizie Rais. Hata mtu wa kawaida hanamda huo sembuse Rais?
Wewe ndiye hufwatilii mambo, rais juzi alisema alisikia ugonjwa wa wastara kwenye kipindi cha shilawadu, mwaka jana tena alipiga simu live kwenye kipindi cja shilawadu na kusema anasikilizaga!!

Sasa wewe unabisha nini? Au una hangover?
 
Kuna mazuri nayaona, hayo silaumu japo sisifii kwani kusifia sio lazima bali ni utashi. Ila pale ninapoona siridhishwi nakosoa bila kuuma maneno. Na kwakufanya hivi sifanyi kosa lolote. Sisi watu tunaolaumu ni muhimu sana kwani tunawafanya waliopewa dhamana kuwajibika ili kutuziba midomo na hatimaye kuwa faida kwa taifa.

Katika maisha huo ni udhaifu mkubwa sana. kama macho yako yanaona negative side tu na kukosoa tu. revisit your thinking.
 
Back
Top Bottom