The Secret: IPTL kuwasha mitambo miezi 3 ijayo!?

Mkataba wa IPTL ulisainiwa na Mheshimiwa wakati akiwa Waziri, sasa anaagiza iwashwe akiwa Rais, lakini wataalam wanasema haiwezi kuwashwa ndani ya kipindi kifupi lakini mafuta ya kuendesha mitambo yameletwa/yameweza kuagizwa ndani ya muda mfupi sana (2-3 wks), kama ikishindikana nani atabebeshwa mzigo wa hizo gharama?
 
hivi rais huwa haumizi kichwa kuchunguza yeye anapelekewa tu report???
ni aibu
 
Invisible,

Mosi, kuna dosari kwenye takwimu zako! Labour charges za hao Wartsila si ni dola mia na hamsini elfu? Umeiandika tofauti kidogo. Jumla ya gharama (kama ulivyoposti) ni dola milioni 23 na nusu ($23,490,000). Ni lundo la fedha.

Pili, asilimia 92 ya gharama ni kwa ajli ya mafuta. Ya nini wakati tuna gesi nyingi? Umeme wa gesi ni cheaper na cleaner. Nchi yenye gesi ya kutosha haihitaji kununua mafuta ya kutengenezea umeme. Ujinga ni umasikini mkubwa sana.
Mwalimu,

Ume-download doc na kuisoma? Haijaandikwa na Invisible, ni nyaraka ya ndani kabisa ya kikao baina 'yao' ambapo huu ndio ukweli usiofahamika kwa 'wananchi' wakati 'walanchi' wakiendelea kufanya mavitu yao!
 
Invisible

Wewe ni Kiboko........Hongera sana kwani unatufungua Macho sana huku JF.

May almighty God bless you na uendelee na Moyo huo huo
 
Yaani kama hao wapinzani wetu Bongo wangekuwa na japo sense ya umoja 2010 is their year.

Yani kila siku najiuliza hasnt CCM given Tanzanians enough reasons within the last 4yrs kuwamwaga? Upinzani hapa kazi ni kucopy and paste kwenye majukwaaa...kazi kwenu...Mkishindwa kuongeza viti 2010 hamta ongeza ever!
 
Wartsila wana contract ya maintenance kwenye hii plant ya IPTL.Hawajalipwa kwa miaka yote hiyo miwili tangu isimamishwe.Wawekezaji walivyo, that is an opportunity to return their money.

But as well kuna plant nyingine pembeni ya IPTL inayomilikiwa na Tanesco yenye capacity ya 45MW.Itawashwa lini?

Kwanini tusijenge power plant zetu wenyewe badala ya kuwatumia watu kama IPTL? Mbona ile ya 100MW ya ubungo na 40 MW ya mwanza ambazo zilikuwa kwenye plan hazisemwi zimeishia wapi?
 
Mkuu taratibu hapo wasije kukusikia maana tangu mgao umeanza hawajawahi kuiwasha yote!
 
Tangu Dkt Idris Rashidi adai kwamba kama nchi ingeingia gizani asilaumiwe, kwa kweli kauli yake ilibeba ujumbe mzito sana.

Japokuwa wengi walimlaumu kwa kutoa kauli hiyo kwa maana kwamba kama yeye alikuwa kiongozi wakati nchi inaingia gizani angewezaje kukwepa lawama! Hata hivyo hali ya mambo inavyoonyesha masuala yahusuyo umeme na matatizo yake yalianza tangu enzi za kuingia kwa Richmond mwaka 2006!

Kumbuka kwamba kampuni hewa ya Richmond haikuanza kuzalisha umeme hadi mvua za masika zilipoanza kunyesha na ule udharura wa kuzalisha umeme kupitia Richmond haukusaidia lolote! Hivi karibuni nako tumeona mwendelezo wa siasa kwenye uzalishaji wa umeme! Kama serikali ingekuwa serious ingejifunza kwenye sakata la Richmond na isingekubali kurudia matapishi yake! Ingejifunza kutotegemea umeme wa maji na kutafuta njia ya mbadala!

Badala yake imekaa kimya ili kusubiri mwanya wa kufisadi kwa kutumia "UDHARURA" ambao ulipingwa vikali kwenye Ripoti ya Kamati ya Mwakyembe! Ingeweza hata kuchukua tahadhari wakati Dkt Idris Rashidi alipoanza kukwepa liability!

Kitu cha ajabu ambacho kimetokea ni kwamba IPTL wameshikishwa hela zao na wanadai mitambo itakuwa tayari baada ya miezi 3! Wenye akili tumeshaanza kunusa harufu ya ufisadi, tulishaumwa na nyoka aitwaye Richmond ndio mana tunapoona unyasi wa IPTL tunarusha mguu! Baada ya miezi 3 mvua itakuwa imenyesha na hatutahitaji umeme wa IPTL! Sasa watarudisha fedha zetu walizolipwa?

Sio ufisadi mwingine huo? Kaazi kweli kweli!
 
Nimesikia kuwa Wartisla wanawadai IPTL USD million 7, na IPTL kwa sasa hawana pesa hawajalipwa na serikali (Tanesco). Pia kuna kesi kati ya wawekezaji IPTL wa hapa TZ na wawekezaji wa nje wa IPTL hawa wana kesi yao, laikini pia kuna kesi kati IPTL na Serikali. Nadhani wamekubaliana waweke pembeni kesi wawashe umeme, then marumbano yaendelee baadae.

Ila kila kitu hapo kinaendeshwa kisiasa siasa tu bla, bla, bla, kibaoo. Nadhani RAISI Kikwete haambiwi ukweli, na kama anaambiwa ukweli hajui aanziye wapi kwani mambo ni mengi sana na yako very complicated. Wahusika ni washikaji wake. Hana ubavu wa kuwagusa.

Serikali inawalipa mahela kibao IPTL, Songas etc. etc. Umeme utakuja ila tutaendelea kusota sota kwani pia migodi ya madini imekuja mipya inahitaji umeme, umeme tulio nao kwa sasa hautoshi ni mdogo sanaaaa, TANESCO wameingia ubia na migodi hiyo.

Cha kujiuliza ni je Tanesco hawakuona kama hiyo migodi inakuja?? wakaanza kujiandaa mapema??

Wizi mtupuuuuu...

We have a long way to go my friends.

Bunge la Dodoma livunjwe warudi majimboni wakafanye kazi, wanakula pesa bure huko waliko. Wizi mtupuuu...
 
Invisible,

Mosi, kuna dosari kwenye takwimu zako! Labour charges za hao Wartsila si ni dola mia na hamsini elfu? Umeiandika tofauti kidogo. Jumla ya gharama (kama ulivyoposti) ni dola milioni 23 na nusu ($23,490,000). Ni lundo la fedha.

Pili, asilimia 92 ya gharama ni kwa ajli ya mafuta. Ya nini wakati tuna gesi nyingi? Umeme wa gesi ni cheaper na cleaner. Nchi yenye gesi ya kutosha haihitaji kununua mafuta ya kutengenezea umeme. Ujinga ni umasikini mkubwa sana.

Mwalimu Moshi,

Kama jinsi Lowassa alivyofanya upuuzi na Richmond, ndivyo ngwe hii inafanya upuuzi na IPTL.

Kama hizo ni pesa za kutumika kwa mwezi mmoja tuu, kwa nini tusinunue mitambo yetu wenyewe tukawapa Tanesco?
 
Tunaweza kuongea mpaka tukapasuka vichwa lakini utashangaa akina ngeleja na JK wapo tu wana furahia maisha. Nadhani imefikia wakati wa kuchukua sheria mkononi kwa sbabu CCM wanankera. Hebu fikiria Sofia punda anasimama na kusema chenge hana makosa?? wakati hili limama linajua chenge ndo ka sign mkataba wa TRL??

Sofia paka anasimama anasema Edward Lowasa hana makosa kuhusu richmond?? wakati ushahidi upo wa jinsi alivyo ingilia mchakato wa kuletwa richmond?? hivi kikwete huwa unafikiria nini kuwa na mawaziri wapumbafu kama hili li mama?? au ni hawara zako??? ah........inakera
 
duh hii kali 34,185,000,000 kwa mwezi? 34bil? hapana huu ni ufisadi mwingine na tuambiw hiyo hela imetoka wapi?why isitumike kujenga vyanzo vyetu wenyewe? its lot lot of money per month!
 
duh hii kali 34,185,000,000 kwa mwezi? 34bil? hapana huu ni ufisadi mwingine na tuambiw hiyo hela imetoka wapi?why isitumike kujenga vyanzo vyetu wenyewe? its lot lot of money per month!

Wakuu gharama ya kununua mitambo mipya ya angalau 100MW ni kiasi gani, tuanzie hapa
 
Mwalimu Moshi,

Kama jinsi Lowassa alivyofanya upuuzi na Richmond, ndivyo ngwe hii inafanya upuuzi na IPTL.

Kama hizo ni pesa za kutumika kwa mwezi mmoja tuu, kwa nini tusinunue mitambo yetu wenyewe tukawapa Tanesco?

Wanasema hayo ni makisio ya gharama kwa miezi sita.

Ila hizo Wartsila O&M costs mbona wamezikosea makusudi. Ili baadaye walete usanii na wakwibe Dollar 1,498,500?
 
Wakuu gharama ya kununua mitambo mipya ya angalau 100MW ni kiasi gani, tuanzie hapa

Hili ndilo swali langu kila siku, nashkuru siko mwenyewe

kwanini tunakuwa reactive instead of being pro-active??????????

%^$(^*&%^($^%(*) AAaaaaaaghhhhhhhh
 
siku ngapi vile zishapita tokea kauli ya JK? .............na abanwe na wananchi wamuulize kuwa 'iwashwe mara moja' alikusudia wananchi waendelee kula dhiki kwa angalau miezi mitatu mengine au aliropokwa tu?
 
Yaani kama hao wapinzani wetu Bongo wangekuwa na japo sense ya umoja 2010 is their year.

Wapinzani wameweka ubinafsi mbele zaidi kuliko maslahi ya nchi. Kwa jinsi Serikali ya Kikwete ilivyoshindwa kazi katika miaka hii mitano uchaguzi wa 2010 ungekuwa wa kukifuta Chama Cha Mafisadi katika anga za siasa za nchi yetu, lakini WAPI! Kichwa cha Mwendawazimu ni kichwa cha mwendawazimu tu miaka nenda miaka rudi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom