The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Halo Mr.president kikwete, kama upo humu JF, hivi wewe mwenzetu, kwa hili hii tuliyonayo leo, kwa kukata tamaa kwa watz kimaisha huku, kwa kutokuwa na imani na selikali kiasi hiki,kwa kushindwa kuwakamata mafisadi wanaorudisha pesa kinyemela na wewe unawaacha waende kiulaini kiasi hiki, kwa kuwalinda kina lowasa na vijisenti na wengine wote kiasi hicho hata hujawasagia meno hata kwa kubip tu tuone kama uko serious, kwa maisha magumu kiasi hiki? utakuwa mgeni wa nani mwaka 2010 mwenzangu?

Mimi sikukupigia kura,hilo sifichi, sasa naona sijui utawakomvinsi kinamna gani watz ambao leo hii wameamka kiasi hiki.

yaani, vile wanavyobip watu wa Tarime, ndo itakuwa Tz nzima, si kichwa chako ndo kitapasuka? nikupe ushauri?, OK, fanya hivi, at least, washughulikie mafisadi kiuhalali hadi watz waridhike ili wapinzani tuje tukose cha kukushitaki kwa wapiga kura, acha kutapanya mihela kwa misafari ya kitalii ulaya,matokeo yake unatuletea tu The sullivan wanaoleta kashule kamoja na wewe umetumia hala za nauli za shule 50. tafadhali rafiki yangu, sijui utakuwa mgeni wa nani. watz wa mwaka keshokutwa, sio wale wa enzi za nyerere. think about it.
 
Am counting down, bado wiki tatu ile siku ya mwisho alowapata wezi waungwana wa EPA, sijui huyu mkwere atakuja na story ipi tena...21 days to go!!
 
His approach is "to cross the river when he gets there". No clear strategy for now.
 
sipati picha, hilo litakuwa kama picha la gavana wa california.

Manake, CUF wataanzia zanzibar hadi pwani yote,mwanza yote,Tabora na kigoma karibia yote, Dar es salaam ndo usiseme. Utakuja Chadema wataanzia TArime,knjaro,iringa,na bara kote vijana lazima waipige chini CCM.

Ukija kwahabari ya Mbeya, Watu wa Mbeya na kyela yote, na tukuyu, wanasema wataipigia kura chadema au chama chochote kile cha upinzani, kwasababu, KIKWETE HAJAMPA ULINZI AU PROTECTION YA AINA YOYOTE Mwakyembe alipojilipua na wenzake kule bungeni. mtoto wa kyela hadi anadondoka ovyo kwa mawazo kwasababu mafisadi wanamfuatilia wanataka kumtoa roho, hadi anatamani bora asingalijilipua hivyo. kwasababu asingekuwa target ya mafisadi kiasi hicho na baba mwenye nyumba yaani Kikwete hajakuwa na fadhila zozote kwake, ndo amemtelekeza.

kusema ukweli, CCM watapata shida sana. umebaki mwaka mmoja tu, there is nothing wanaweza wakafanya kwa maandalizi au kufanya chochote cha kuweka kama geresha ili watu wawaamini tena. wanasubiria kung'oka tu.
 
Don`t rush to judge Kubenea, govt told

2008-10-11 10:30:47
By Rose Mwalongo

The Editors Forum has called on the government to give chance to MwanaHalisi editor Saed Kubenea to give proof of his story regarding an alleged to plot to remove the president before judging him the way it is doing now.

Forum`s chairperson Sakina Datoo made the remarks in Dar es Salaam yesterday when giving her reaction to a statement made from the State House.

On Wednesday, MwanaHALISI tabloid carried a story on its front page, saying there was a plot to oust the President by barring him to run for another term, a move said to be spearheaded by some senior leaders in the ruling party and his own son.

The tabloid reported that schemers were working to bar the president from vying for presidency in 2010.

In response, the State House, through its Director of Communications Salva Rweyemamu, was quoted as saying that the story was a total fabrication and a tale of a century and that it was run to gain popularity among readers.

Rweyemamu said it was ironical that the newspaper was running such a faltering story at a time when the personal performance of the President and his government were being well spoken inside and outside the country.

In a quick rejoinder yesterday, the Editors Forum through its chairperson Datoo said: We feel the government is overreacting by threatening closure of the paper. The time frame given to Kubenea to defend himself was too short. The ministry of Information has already given its judgment, something which is not right.

Datoo stressed that the era of closing down newspapers was long gone, adding: We are now in a democratic era. We will not accept any threats.

The government should present the issue to the ethics committee of the Media Council before reaching a verdict, said Datoo.

Saed Kubenea is both an editor and owner of MwanaHALISI weekly tabloid.

SOURCE: Guardian

Habari hiyo hapo juu inakuwaje?

Mwenye data na 'uhakika' wa hiyo atupashe
 
yangu macho tu,huo uchaguzi wa Tarime ulikuwa wa kubip tu, kuna siku watz wote watampigia hadi ccm haitaamini majicho yake.
 
you can fool some people sometime but you cannot fool all the people all the time. Bob Marley the great
 
JAMANI WAULIZENI VIZURI CCM; SHILINGI BILIONI MOJA (1,000,000,000) KWA JIMBO LA TARIME TU--WANAZITOA WAPI HIZO PESA?? JAMANI CHONDE PESA ZETU tz ZINALIWAA!!! HEBU PIGA HESABU KATIKA UCHAGUZI MKUU BILIONI MOJA MARA MAJIMBO YOTE YA UCHAGUZI ITAKUWA MABILIONI MANGAPI?? SI CHINI YA BILIONI 100, JE HIYO HAIONYESHI DALILI YA KUWA 'EPA' NA UCHAFU MWINGINE NDIO MRIJA WA HAO JAMAA KUPATA PESA?????? WAULIZENI VIZURI

NA WAKATOKA KAPA NA MAHELIKOPTER YAO
 
JAMANI WAULIZENI VIZURI CCM; SHILINGI BILIONI MOJA (1,000,000,000) KWA JIMBO LA TARIME TU--WANAZITOA WAPI HIZO PESA?? JAMANI CHONDE PESA ZETU tz ZINALIWAA!!! HEBU PIGA HESABU KATIKA UCHAGUZI MKUU BILIONI MOJA MARA MAJIMBO YOTE YA UCHAGUZI ITAKUWA MABILIONI MANGAPI?? SI CHINI YA BILIONI 100, JE HIYO HAIONYESHI DALILI YA KUWA 'EPA' NA UCHAFU MWINGINE NDIO MRIJA WA HAO JAMAA KUPATA PESA?????? WAULIZENI VIZURI

NA WAKATOKA KAPA NA MAHELIKOPTER YAO

Watu wa Tarime bwana wanapendeza na kufurahisha, pesa wanachukua, kanga na kofia wanapokea, pombe na fulana zinachukuliwa lakini kura wanapiga kwa yule wanayemuona anawafaa bila kujali vitisho vya polisi na Makamba aliyewaita kuwa wao ni walevi na wahuni.
 
Source pls

Nakula likizo yangu kwenye Mlima Mmoja Mkubwa tuu sasa mmoja wa vijana wa kazi nikasikia anasema kuhusu hili jamba la CCM kutumia bil 2 nilibisha sana sasa nikaona nipite humu JF niulize lakini nikakuta kuna mjanja kashalidaka.Sasa swali la kujiuliza yaani hawa CCM hizi fedha ni za kwao kweli?Siyo za walipa kodi jamani?Kweli hizo fedha zitawatokea puani kama wanatubia!

Vilevile kama jimbo moja tuu wametumia hivyo sasa nchi nzima itakuwaje?ama kuna sehemu maalumu za kumwaga fedha nyingi kiasi hicho kwa sababu ni maeneo ya upinzania ya kujidai?

Vitu vingine vinaweza vikakufanya ulie hayo machozi ya samaki!
 
Kwanza kabisa hizo fedha wanatumiaje kwenye kampeni? Wanahonga watu au wanafanya nini! maana kama ni posho za viongozi na dizel za magari sidhani kama pesa hizo zote zingetumika. Hata kama walikodi helicopter 2 na kuchapa tishet na kanga 200,000 bado haziwezi kufika kiasi hicho.

Wanatakiwa walete breakdown ya matumizi yao. Kweli mafisadi balaa, yaani hata wanakiibia chama chao wenyewe?

Hizo fedha bil 2 au hata 1 kama wangekuwa wameiwekeza kwenye barabara, zahanati na mashule huko tarime si wangepta kura zote?

Tatizo lao badala ya kutumia strategy ya kuwaletea maendeleo wananchi ili waendelee kubaki kwenye utawala, wao wanatumia strategy za kifisadi wakati wa uchaguzi. Shame on them.
 
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, ambacho jina lake linahifadhiwa, bifu la wawili hao limefikia mahala ambapo watu hao hawasalimiani wala kutazamana usoni.

Habari zinasema kuwa waheshimiwa hao mwishoni mwa wiki iliyopita, walipanda ndege moja wakitokea Mwanza hadi Dar es Salaam huku wakiwa wamenuniana.

“Tangu walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kila mmoja alionekana kumkwepa mwenzake,” alisema mtoa habari huyo ambaye alisafiri ndege moja na waheshimiwa hao.

Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa wakiwa ndani ya ndege hiyo kila mmoja alionekana ‘bize’ na simu yake ya kiganjani, jambo lililozua maswali kwa watu waliowafahamu wabunge hao ndani ya ndege hiyo.

Mara baada ya kupata taarifa hiyo, mwandishi wetu alimpigia simu Shibuda, alipomuuliza kuhusu madai ya kutozungumza na mbunge mwenzake, kabla ya kutoa jibu alicheka.

Baada ya muda, alisema kuwa Chenge ni ndugu yake na alimfahamisha mwandishi wetu kuwa, akiona ndugu wanagombana, yeye achukue jembe akalime.

“Unasikia bwana mwandishi, ndugu wanapogombana, wewe chukua jembe ukalime,” alisema Mheshimiwa Shibuda.
Alipoulizwa sababu hasa ya yeye na mbunge mwenzake kununiana, wakati wanatoka katika mkoa mmoja wa Shinyanga, Shibuda alisema kuwa hajui na kwamba hadi sasa anafanya utafiti ili kujua sababu.

“Hadi sasa nafanya utafiti, nikipata jibu la utafiti wangu nitazungumza, kwani yeye Chenge kasemaje?” Aliuliza Shibuda huku akicheka.

Naye Chenge ambaye siku za hivi karibuni alipachikwa jina la Mzee wa Vijisenti, alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Simu hiyo, ilipigwa mara kwa mara na hadi tukwenda mitamboni ilikuwa haina majibu.
Kama ilivyokuwa kauli ya Shibuda kuwa anafanya utafiti, nasi tunafanya uchunguzi ili kujua sababu hasa ya waheshimiwa hao kununiana, tukibaini ukweli tutaweka mambo hadharani - Mhariri.
 
Date::10/25/2008
Wasomi kusaidia wapinzani kuing'oa CCM 2010
Na Boniface Meena
Mwananchi

Wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa nchini wamevitaka vyama vya upinzani kuandaa wagombea wazuri ili wavisaidie kuking'oa Chama Cha Mapindi (CCM) madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Vijana hao walisema hayo wakati wakijadili mada "Mfumo wa elimu Tanzania unavyomuumiza na kumuharibia maisha mtoto wa kimasikini," iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar ), Juma Duni Haji kwenye kongamano lililoandaliwa na Sekretarieti ya Vijana ya Chama cha Wananchi(CUF) na kuwashirikisha wasomi wa wataasisi za elimu ya juu nchini.

Katika kongamano hilo waliazimia kuunda mtandao wa "2010 is tomorrow" kwa ajili ya kuingoa CCM, baada ya kuchoshwa na matatizo yanayoikabili sekta ya elimu ya juu hapa nchini.

Akichangia katika mada hiyo, mwakilishi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) aliyejitambulisha kwa jina moja la Justine alisema serikali inawafanya wanafunzi wajenge chuki dhidi yake hasa kwa kuweka matabaka katika suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

"Wanafikiria tunatania, lakini itawagharimu mwaka 2010 na tutahakikisha inakuwa hivyo, hivyo vyama vya siasa viweke wagombea wanaoeleweka ili tuweze kuleta mabadiliko," alisema Justine.

Wanafunzi hao walisema sera ya mikopo kwa wanafunzi ipigwe marufuku kwasababu inawaathiri zaidi kuliko kusaidia familia masikinii.

Naye Michael Dalali ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu cha Dar es Salaam na pia Katibu Mkuu wa Taasisi ya Vijana nchini (TYVA) alisema mfumo wa elimu unaelekea kubaya na kwamba viongozi wanaichimbia kaburi.

"Ni vizuri kufanya makongamano kama haya lakini ni lazima kuhakikisha kuwa yanafanyiwa kazi lasivyo tunaweza kuyafanya sisi wenyewe," alisema Dalali.

Alisema utaratibu wa kila chuo kudai jambo lake kipekee haufai badala yake waunganishe nguvu ili kuyapa umuhimu.

Alisema kupigwa mawe msafara wa rais ni ishara kwamba wananchi wamechoshwa na tabia ya viongozi kutosikiliza matatizo yao.

"Msishangae hao viongozi wakifanya ziara zao vyuoni wakipopolewa mawe, ndipo watakapotusikia," alisema Dalali.

Mohammed Seif ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini Dar es Salaam alisema haoni sababu ya wanafunzi kurudisha mikopo hiyo wakati wakubwa serikalini wanaponda raha.

"Mimi nafikiri sasa tumechoka na cha kufanya ni bora tusilipe hiyo mikopo kwani ni haki yetu kusoma bure," alisema Mohammed.

Akiwasilisha mada hiyo Duni alisema ni wazi kuwa viongozi walioko serikalini ambao ni vijana wa hayati Mwalimu Nyerere wameshindwa kazi na wamepoteza mwelekeo wake.
 
Kwanza wapinzani waache fitina,umimi,umamluki,mizengwe ya wao kwa wao,WAUNGANE.Kisha ndipo hayo mengine yafuate.
 
Kwanza wapinzani waache fitina,umimi,umamluki,mizengwe ya wao kwa wao,WAUNGANE.Kisha ndipo hayo mengine yafuate.

Vyama vyote vilianzishwa na watu tofauti wenye sera na itikadi mbalimbali ambazo wanafahamu wao. Hatakama wataunganishwa bado matokeo yake yatakuwa kama ilivyokuwa aliance kati ya ATC na South african airways.

Mimi imani yangu ni kuwa kila chama kisimamie kile kinachoamini, vyama ambavyo ni mamluki vitashindwa na vile amabavyo ni vyama kwa ajili ya mabadiliko ya Tanzania vitasimama na ndivyo vitakavyoibadilisha Tanzania. Mbona safari inakolea tu!!!

Muungano ungewezekana, kama nyoyo za watu zingekuwa transparent!
 
Ndio matatizo yetu haya badala kwa hiyo wanachukia CCM kwa sababu ya matabaka kwenye mikopo! Well matabaka yakiondolewa CCM mwendo mdundo! kazi kweli kweli....
 
Vyama vyote vilianzishwa na watu tofauti wenye sera na itikadi mbalimbali ambazo wanafahamu wao. Hatakama wataunganishwa bado matokeo yake yatakuwa kama ilivyokuwa aliance kati ya ATC na South african airways.

Mimi imani yangu ni kuwa kila chama kisimamie kile kinachoamini, vyama ambavyo ni mamluki vitashindwa na vile amabavyo ni vyama kwa ajili ya mabadiliko ya Tanzania vitasimama na ndivyo vitakavyoibadilisha Tanzania. Mbona safari inakolea tu!!!

Muungano ungewezekana, kama nyoyo za watu zingekuwa transparent!

Mkuu hapo yanapigwa mahesabu ya kukiondoa CCM madarakani 2010.Upinzani unaunganishwa na itikadi moja-kukiondoa madarakani chama kinachotawala.Hayo mengine yanajadilika.

Ukisema usubiri mpaka mamluki washindwe,utasubiri sana na mwisho haitatokea. Njia rahisi ya kukiondoa CCM madarakani kwa sasa ni wapinzani kuungana na kusimamisha mgombea mmoja katika kila nafasi ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom