Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,001
- 112,650
Ni kweli Kalamu mpaka sasa wanaopinga pendekezo hili hawajatoa jina mbadala kwa hiyo kuonyesha dhahiri kwamba Dr. Slaa anakubalika na wengi au hakuna majina mengine yanayoonekana yanafaa kumzidi yeye. Kuna umuhimu mkubwa wa katiba yetu kubadilishwa ili kukidhi haja ya mfumo wa vyama vingi na kuongeza uwazi zaidi katika kuwachunguza au kuwashitaki viongozi mbalimbali ambao watatuhumiwa kuwa mabadhirifu wa mali za umma. Ukiangalia kwa undani zaidi utaona mtu ambaye kwa kiasi kikubwa amechangia katika kuifahamisha jamii ya CCM kuhusiana na Ufisadi unaofanywa na viongozi wa Serikali kutoka CCM ni Dr. Wilbroad Slaa.
Kwa hiyo hii ndiyo sifa pekee inayomfanya aonekane anafaa kwa uraisi 2010? Je, historia ya utendaji wake wa kazi na mafanikio vipi, kuna mtu anayeijua? Pia na historia ya mahusiano yake na watu mbalimbali, kuna yeyote anayeijua?