The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

 • Edward Lowassa

  Votes: 0 0.0%
 • Dr. Slaa

  Votes: 7 38.9%
 • Prof. Lipumba

  Votes: 0 0.0%
 • Mizengo Pinda

  Votes: 5 27.8%
 • Samwel Sitta

  Votes: 0 0.0%
 • Jakaya Kikwete

  Votes: 2 11.1%
 • Mark Mwandosya

  Votes: 2 11.1%
 • Harisson Mwakyembe

  Votes: 2 11.1%
 • None of The above

  Votes: 0 0.0%

 • Total voters
  18
 • Poll closed .

KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
1,225
Yah, sipingi mada, napinga Dr Slaa kugombea urais 2010. Nimekupata kabisa

Ukiwa unapinga ni vizuri ukatoa kwa nini unakataa. Pia ukikubali unatakiwa kuona kwa nini unakubali.

Mimi siwezi kusema fulani agombee suala ni je anakubalika kwa wananchi wa vijijini? Anauzika? Lakini pia ana aseti nyingi sana.

Mkandara amehoji udini, mimi ninachojua ni kwamba kiongozi yeyote anayefikiria katika kundi fulani, mara nyingi ni kushindwa kuongoza. Ukiona kiongozi ni mdini ujue uwezo wake ni mdogo anatafuta support.
 
Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,848
0

Nilikwisha eleza mwazoni kabisa kwa nini sisupport Slaa kuwa rais
 
TAIKUBWA

Senior Member
Jan 20, 2008
115
0
kaka tunaitaji watu wa kuwasha mabomu na kukubali kujilipua kama wapalestina hivyo huyu mtu mwacheni tena aitaji anasa kama hiyo jamani
 
Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
1,500
To be a president on undeveloped country like Tanzania need more than handsome face. We need someone with strong education background( not necessary PhD), strong leadership techniques, rule of law mentality and working ethics.

I don't know much about Dr. Slaa, but i see the leadership and rule of law mentality, however i wouldn't take a risk to endorse him.

My president is inside CCM, but he has fear of his credibility and network. I will definitely vote CCM if he will become the nominee.
 
Nsaji Mpoki

JF-Expert Member
Nov 5, 2007
396
195
Nadhani wengi wetu mnalijua jina la Dr. Wilbroad Slaa Mbunge wa Karatu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Mimi ni Mtanzania ambaye sifungamani na chama chochote lakini mwenye kuamini kabisa ya kwamba, miongoni mwetu kuna Watanzania ambao wanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika njanja mbalimbali kama za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nchi yetu iko kwenye wakati mgumu sana hivi sasa na tunahijati kiongozi bora na sio bora kiongozi ambaye ataweza kuleta mabadiliko makubwa na ya kweli katika kuiendeleza nchi yetu kiuchumi.

Kama mjuavyo tatizo la ufisadi na rushwa limekithiri sana na imeshajionyesha wazi ya kwamba, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameshindwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza majukumu yake aliyopewa na watanzania kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naamini huu ni muda thabiti kabisa kumtafuta mtu atakayefaa kukichukua kiti chake itakapofika wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2010. Binafsi ningependa Kikwete aondoke hata leo hii na arudi kijijini kwao Bagamoyo akalime Mananasi yake na huku akiendelea kujichekesha mbele ya ndugu zake. Naamini kabisa Dr. Slaa ndio mtu anaefaa kuwa Rais wa nchi yetu na mwenye uwezo mkubwa wa kulianzisha gurudumu la maendeleo nchini. Mimi niko tayari kulipia gharama zote za kutengeneza tovuti ya Dr. Slaa na kulipia hosting charges kutoka hivi sasa mpaka wakati wa uchaguzi mwaka 2010. Kwa hiyo ningeomba watanzania wenzangu tumhamasishe Dr. Slaa agombee hiki kiti cha Urais mwaka 2010. Tumebakisha miaka miwili na nadhani huu ni muda muafaka kuanza kujiandaa ili kuhakikisha Kikwete na CCM hawarudi tena kwenye uongozi.

Ahsanteni.

(Haya ni maoni yangu binafsi hayaingiliani kabisa na maamuzi ya CHADEMA) www.drwilbroadslaa2010.com

Na upande wa ccm wamweke Dr Mahiga,ili pawepo na uwiano wa hoja mzuri.Huyo ashawishowe kugombea ana uwezo mzuri kuliko mtu yeyote aliyekuwemo kwenye serikali za awamu zilizoanzia awamu ya pili.
 
Mtu wa Kwao

JF-Expert Member
Jan 15, 2008
258
0
Nimeguna kwanza Geeque,,,

Muda bado baba... By 2009 February issues kama hizi zitakuwa ndio nyakati muafaka. Utakuwa ushawajua vema wanasiasa wetu na kujua nani ni nani na kwanini! Kuna mengine yatarajiwayo kujiri kabla ya Julai, unaweza kuwachukia hata uliowaamini. Kuna vichwa vichache vijavyo utajikuta mwenyewe unavikubali. Kimoja toka humu humu JF!

Note the date I gave you buddy...

Hii ndio Bongo...!
jamani si mbali san kama tunavyodhani.Kama mtakumbuka rail alianza kampeni siku nyingi toka wakati wa world cup.Na alito wesite yake pale kw hto mwenzetu aliyeamua kumkampenia DR SLAA hajakosea
 
Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
1,250
Naona hadi sasa ingawa mwanzisha mada alitaja jina la mtu mmoja,yameisha tajwa majina zaidi ya kumi kadiri tunavyochangia mada. Labda twende hatua nyingine zaidi. kati ya waliotajwa ni nani anatimiza vigezo vya rais tunayemhitaji kwa sasa.Hapo hapana budi hata vigezo tuvitaje. Pengine tutumie hata perspective ya mwalimu aliyoitumia mwaka 1995 aliposema tunazo nyufa,na rais wetu aoneshe si tu kuziona hizo nyufa bali pia awe na uwezo na nia ya kuziziba.
ufa wa kwanza...
ufa wa pili...
wa tatu...
n.k.
Tena nyufa nyingine alizozibainisha mwalimu ndio kwanza zinapanuka na nyumba inakaribia kubomoka.
 
Geeque

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
936
500
Na upande wa ccm wamweke Dr Mahiga,ili pawepo na uwiano wa hoja mzuri.Huyo ashawishowe kugombea ana uwezo mzuri kuliko mtu yeyote aliyekuwemo kwenye serikali za awamu zilizoanzia awamu ya pili.

Najua CCM kuna baadhi ya watu wazuri lakini kutokana na CCM kuwa na mfumo wa kulindana na kufichiana maovu sidhani kama wanafaa kurudi kwenye uongozi nchini mwetu. CCM ni wachafu, wananuka na uongozi wao ni mbovu. Kitu kingine ni kwamba asilimia kubwa ya wana CCM ni kama bendera ifuatayo upepo, wao kazi yao kushabikia kila jambao ambalo viongozi wao wanalowaambia, hawatumii akili zao kuchanganua mambo na ku-scrutinize maovu mbalimbali yanayoendelea nchini ambayo yanafanywa na watu wao. CCM has to go.Dr. Slaa ndio jibu katika uongozi Tanzania.
 
Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,065
1,195
Mimi nitajitosa kwenye hiyo patashika ya Ubunge hapo 2010.
Jimbo kwangu kuna mchovu mmoja ambaye namfahamu tangu enzi za kucheza cha ndimu, ni mtu kutoka kijiji cha jirani.
Maandalizi yamekwisha anza, kampeni za chini kwa chini zimefunguliwa tangu January,2008. Zaidi ni kukusanya Data na weakness za opponent wangu.
Timu ya kutafuta Fungu la kusaidia kufinance uchaguzi itaundwa rasmi hapa UESIEI January 2009. Watu 3 mashuhuri katika timu hiyo wamekwisha arifiwa nawasubiri watoe tamko lao la mwisho wakati wowote kabla ya 2009.

Kuna uwezekano mkubwa wa kushinda endapo tu mipango mingi ilo pangwa itasukumwa mpaka kwenye ukingo wake na kampeni kufanyika kama ilivyo pangwa.
 
KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
1,225
Kama ni kutoka CCM hata kama mtu atakuwa Mzuri namna gani ni vigumu kurekebisha mifumo waliyonayo. Watu wa CCM waliowengi ni Wazembe wakati huo huo wakitaka kupata maslahi makubwa na huo ndo mwanzo wa mzizi wa UFISADI. UFISADI umekidhiri chi nzima viongozi wengi mafisadi(wakiwemo mashirika yote ya kiserikali) wamejikinga ndani ya mgongo wa CCM. Sheria Zipo lakini hakuna wa kuzifuata. Kila Sehemu Tanzania imeoza na inanuka rushwa.

Kuondokana na janga hili hakuna mtu yeyote ndani ya chama cha mapinduzi mwenye uwezo wa kuondoa maovu tanzania.Labda akiingia na kuwafukuza viongozi na watendaji wote wa juu serikalini, kitu ambacho hakiwezekani.CCM imeisha kuwa ya matajiri, hili linajulikana kwa kila mtanzania na pia wafadhiri wake wakubwa wanaonekana wana kila dalili za UFISADI(Ni MAFISADI):

Kinachowezekana ni pale CCM wazuri (kama wapo kweli!) watakapo amua kuunganisha nguvu zao na kuunda CCM B kama ilivyo Kenya ODM ya Kalonzo na ODM ya ODinga. Huwezi kuwa mzuri ukamkaa kwenye uchafu usiitwe mchafu. Kwa hiyo kwa Kwa tanzania tunahitaji CCM ya Wazuri na CCM ya MAFISADI vinginevyo utakuwa ni utapeli

Lakini CCM ikija kama CCM ya sasa hata walete mtu anayefananaje hakuna maendeleo yatakayo patikana tanzania. Hataweza kuwageuka wenzake(wakiwemo wazuri na wabaya).

Watu waliowengi(viongozi/wakuu wa mashirika mbali mbali na makada) wameisha zoea kura bila kufanya kazi.Mpaka sasa ninachoona ni suluhisho ni kuimalisha upinzani na kumtoa mgombea makini sana atakaye weza kutuletea mabadiliko ya kweli Tanzania. Haya mambo ya majina ambayo baadhi yetu tumezaliwa tukayakuta yanaongoza mpaka sasa yanatakiwa yatafutiwe pa kwenda. Tunahitaji sura nyingine mpya.Tunahitaji watendaji makini.

Kwa hiyo hii inanikumbusha msemo wa mgombea urais wa chama cha kimojawapo, aliyoyasema kwamba watanzania wakimchagua mgombea mmoja wapo wasitegemee maendeleo hila mchiriku. Labda kwa kuwa alikuwa professor, make wakati mwingine wanmaweza kutabili.

Mwisho mpaka ninapoandika ujumbe huu nakubaliana na mtoa hoja kwamba anayeonekana ni Slaa.
 
Nakubaliana nawe kabisa Mazee kakindomaster. CCM imeshashindwa kufanya chochote kuliletea Taifa maendeleo na kadri siku zinavyozidi imekuwa kama ugonjwa kwa watanzania kujaribu kuwapa muda zaidi. CCM hawana jipya ni wale wale MAFISADI ambao hawatobadilika milele. Wako pale kulisha matumbo yao na ya mabwana zao. CCM has to go, Dr. Slaa for President.
 
Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,330

CCM kunaitajika mabadiliko makubwa sana kama yaliyotekea kwenye chama tawara (wakati huo) malawi, wanaitaji mtu wa kuwambia lazima watoane kafara au ajitoe kwenye chama maana wengi wameoza, otherwise tutaendelea kuona hii ya kulindana kwa kutumia taasisi za umma.
 
KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
1,225
Nakubaliana nawe kabisa Mazee kakindomaster. CCM imeshashindwa kufanya chochote kuliletea Taifa maendeleo na kadri siku zinavyozidi imekuwa kama ugonjwa kwa watanzania kujaribu kuwapa muda zaidi. CCM hawana jipya ni wale wale MAFISADI ambao hawatobadilika milele. Wako pale kulisha matumbo yao na ya mabwana zao. CCM has to go, Dr. Slaa for President.

Hiyo ndo solution

Kama yale yale ya Mkapa na JK, watanzania walikuwa wamekata tamaa akaja JK, hatukujiuliza maswali ya kwa nini mgombea amekaa kwenye matope halafu mnasema ni mzuri?.

Tukafikiri tumepata kumbe tumepatika. Kumbe nilicho ona ndani ya CCM mtu akiona ameharibu CV yake kwa UFISADI, hizo hizo alizowafisadi watanzania anampasia mwenzake.

Watanzania wanafikiri sasa hii ni nguvu mpya, kumbe ni yule yule karudi hila sasa amejiwekea marashi mazuri. Baada ya kupata ndipo unagundua kumbe yule FISADI hajatoka hila kilichobadirka ni sura tu.
 
suleimani

Member
Dec 9, 2006
43
0
Slaa for the Presidewncy? My foot what a silly joke!!Hivi nyie mnajua vizuri huyo mtu alieshindwa kuweka kiapo cha kanisa katoliki? Ndiye aje kuapa kuwatumikia Watanzania? Huyo ni fisadi mkubwa. Kwenye kesi ya jimbop la Karatu imedhihirika hivi karibuni yeye na chama chake waliiba kura. Hafai hafai hafai.
 
Geeque

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
936
500
Slaa for the Presidewncy? My foot what a silly joke!!Hivi nyie mnajua vizuri huyo mtu alieshindwa kuweka kiapo cha kanisa katoliki? Ndiye aje kuapa kuwatumikia Watanzania? Huyo ni fisadi mkubwa. Kwenye kesi ya jimbop la Karatu imedhihirika hivi karibuni yeye na chama chake waliiba kura. Hafai hafai hafai.

Yes Slaa for Presidency na anafaa kabisa kwenye hilo. Slaa ni kiongozi ambaye kwa uzalendo wake ameweza kufichua maovu mbalimbali yanayofanywa na Majambazi wa CCM.Nilishasema huko nyuma CCM ni chama kinachonuka uvundo wa RUSHWA. Hell NO to CCM, CHAMA CHA MAJAMBAZI.
 
Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
873

Katika wakati huu Dr. Slaa ndiye aliyependekezwa hapa, na sijaona aliye bora kuliko yeye. Kama yupo mwingine tumpendekeze hapa ili naye tumjadili na kumpima uwezo wake katika kuwatumikia wananchi. Upadre tu sio sababu ya kumzuia Dr. Slaa kuwa kiongozi wa Tanzania. Kama yeye ni mzalendo anayejali maslahi ya wananchi; anayo 'vision' ya kuielekeza Tanzania katika maendeleo ya watu wake inatosha. Afterall, utumishi wa Dr. Slaa akiwa mbunge umeonekana dhahiri- anayo rekodi tunayoweza kuiangalia ukilinganisha na rekodi ambayo haikuwepo kabisa wakati tunamchagua Kikwete kuwa Rais.

Walio karibu na huyu Slaa, inafaa waanze kumtia msukumo, wakati wa kujiandaa ndio huu sasa hivi, kama atataka kugombea 2010.
 
Ni kweli Kalamu mpaka sasa wanaopinga pendekezo hili hawajatoa jina mbadala kwa hiyo kuonyesha dhahiri kwamba Dr. Slaa anakubalika na wengi au hakuna majina mengine yanayoonekana yanafaa kumzidi yeye. Kuna umuhimu mkubwa wa katiba yetu kubadilishwa ili kukidhi haja ya mfumo wa vyama vingi na kuongeza uwazi zaidi katika kuwachunguza au kuwashitaki viongozi mbalimbali ambao watatuhumiwa kuwa mabadhirifu wa mali za umma. Ukiangalia kwa undani zaidi utaona mtu ambaye kwa kiasi kikubwa amechangia katika kuifahamisha jamii ya CCM kuhusiana na Ufisadi unaofanywa na viongozi wa Serikali kutoka CCM ni Dr. Wilbroad Slaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom