The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Was very intelligent person Kwanza alikuwa na idea ya kuunganisha bara la Afrika iwe na rais mmoja na bank ya Afrika
Ma dikteta wote huwa wana akili sana hapa nazungumzia “dikteta” sio Dikteta uchwara
ukimsikiliza Idd amin sahivi utagundua alikuwa na upeo wa kutizama mbali mno hata Saddam Hussein aliwahi mpaka kutengeneza silaha kama bunduki na vifaru na kuinua maisha ya wananchi wake,marekani kuona vile akastuka
 
1. Hakukuwa na bili ya umeme nchini Libya; umeme ulikuwa bure kwa wananchi wake wote.

2. Hakukuwa na riba ya mikopo, benki za Libya zilimilikiwa na serikali na mikopo ilitolewa kwa raia wake wote kwa riba ya asilimia sifuri kisheria.

3. Kuwa na nyumba kulizingatiwa kuwa ni haki ya binadamu nchini Libya.

4. Wanandoa wapya nchini Libya walikuwa wakipokea dinari 60,000 (464,503,937 TZS) na serikali ili kununua nyumba na kusaidia kuanzisha familia.

5. Elimu na matibabu yalikuwa bure nchini Libya. Kabla ya Gaddafi ni 25% tu ya Walibya walikuwa wanajua kusoma na kuandika. Leo, takwimu ni 83%.

6. Kama Walibya wangetaka kuanza kazi ya ukulima, wangepokea ardhi ya kilimo, nyumba ya kilimo, vifaa, mbegu na mifugo ili kuanzisha mashamba yao... yote haya bure.

7. Ikiwa Walibya hawakuweza kupata elimu au vifaa vya matibabu walivyohitaji, serikali iliwafadhili kwenda nje ya nchi. Maana haikulipwa tu, bali walipata £1585 (4,057,553 TZS) kwa mwezi kwa ajili ya malazi na posho ya usafiri.

8. Raia wa Libya akinunua gari, serikali ilikuwa inatoa ruzuku kwa 50% ya bei.

9. Bei ya petroli nchini Libya ilikuwa £0.09 (230 TZS) kwa lita!

10. Libya haikuwa na deni la nje na akiba yake ilifikia pauni bilioni 103 - ambazo sasa zimegandishwa duniani kote.

11. Ikiwa Mlibya hakuweza kupata ajira baada ya kuhitimu, serikali ingelipa wastani wa mshahara wa taaluma hiyo, kana kwamba ameajiriwa, hadi ajira ipatikane.

12. Sehemu ya kila mauzo ya mafuta ya Libya iliwekwa moja kwa moja kwenye akaunti za benki za raia wote wa Libya.

13. Mama aliyejifungua mtoto alipokea £3447 (8,824,218 TZS)

14. Mikate 40 nchini Libya iligharimu pauni 0.10 (298 TZS)

15. 25% ya Walibya sasa wana shahada ya chuo kikuu.

16. Gaddafi alianzisha mradi mkubwa zaidi wa umwagiliaji duniani, unaojulikana kama ''The Great Manmade River Project", ili kufanya maji yapatikane kwa urahisi katika nchi nzima ya jangwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom