The Richest Man In Africa: Kila Utajiri una Ukafiri nyuma yake

Wa Africa hatujadumazwa kiakili tuko safi na makini sana. labda mtu.mmoja mmoja tu.

Angalia tulipo leo kimaendeleo na pale tulipo achwa na Wakoloni wasomi na matajiri.walitawala miaka 100.lkn hovyo tu .sisi leo miaka nusu ya utawala wao tunajitegemea na tumeongezeka maradufu. Watangulizi walitupa hiyo elimu tunayoona duni ili tuanzie hapo
Hayo yote ni kwa msaada wa hao hao mabeberu na ndiyo maana unakuta bajeti ya serikali lazima kuwepo na beberu aliyekutawala hama kikombe kinaenda kwa beberu yoyote ili ajazie, 😔!!.
 
Some people bwana!!! sasa hapa tuelewe nini? makurasa meeengi nothing! no substance usiweke jina langu huko kwenye list bana.

watu wanasifia wala hakuna kitu, hapo nani tajiri? kabila au hao ID CO of Israel? mbona maskini tu wanahangaika hao!

Kwa maelezo yako kilichofanyika was struggling for the fittest.Sioni kipya cha kusisimua hapo. zaidi ya hadithi za Kabila profiles. hayo yapo hata kwa kuku tu. achilia mbali maisha ya Simba dume porini au ng'ombe wa zizini kwako. chukulia kuku tu km majogoo mawili umeyaweka ndani ya zizi moja lazima lingine litawaliwe.kwa timing au nguvu, ikibidi kifo!

Piga ni kupige ni maisha ya kawaida sana, chukulia makanisani tu, misikitini watu wanashindana kushika zaka. au kuswalisha. angalia hata maisha tu ya maskini wa uswahilini, km hapo manzese, kipawa nk, ukiwa na vijicent utaibiwa hata kukodiwa majambazi bila kujali ni ndg yako anafanya ivo.
Ili uishi sasa utafanyaje? wengine ndo maana wanakuwa wachawi, wababe, wambea.

Hata wewe umepata akili hii ya kuandika ni bibi yako mzaa Baba yako alikuwekea kifua dhidi ya watu wabaya yaani kijicho, bila ivo ungekuwa unavuna mihogo ya kuchemsha huko Musoma vijijini, hawa watu wabaya wasingependa ufike hapo ulipofika. kukaa nyuma ya key board! Sema tu wengine hukosea timing km mzee Kabila

Nothing new here please! ajabu watu wanakupa kichwa eeeh safi hawajayasoma haya yaliyomo,
you've wasted ma time meeen!.
Jf kuna vilaza pia
 
Tayari mr slim ameshafanya yake nini mkuu?
Wakuu, kumradhi sana... kuna masuala yako nje ya uwezo wangu yamejitokeza. Makala hii haitoendelea. Kumradhi sana kwa hili but there is nothing I can do.

Nimeweka makala mpya ambayo ilikuwa exclusive kwa wale walioko kwenye group tu. But nimeona nishee nanyi kupunguza walau udhia wa kukosa makala hii ya "The Richest Man".

Kumradhi sana.
The Bold: Ujasusi Sebuleni Kwetu - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Some people bwana!!! sasa hapa tuelewe nini? makurasa meeengi nothing! no substance usiweke jina langu huko kwenye list bana.

watu wanasifia wala hakuna kitu, hapo nani tajiri? kabila au hao ID CO of Israel? mbona maskini tu wanahangaika hao!

Kwa maelezo yako kilichofanyika was struggling for the fittest.Sioni kipya cha kusisimua hapo. zaidi ya hadithi za Kabila profiles. hayo yapo hata kwa kuku tu. achilia mbali maisha ya Simba dume porini au ng'ombe wa zizini kwako. chukulia kuku tu km majogoo mawili umeyaweka ndani ya zizi moja lazima lingine litawaliwe.kwa timing au nguvu, ikibidi kifo!

Piga ni kupige ni maisha ya kawaida sana, chukulia makanisani tu, misikitini watu wanashindana kushika zaka. au kuswalisha. angalia hata maisha tu ya maskini wa uswahilini, km hapo manzese, kipawa nk, ukiwa na vijicent utaibiwa hata kukodiwa majambazi bila kujali ni ndg yako anafanya ivo.
Ili uishi sasa utafanyaje? wengine ndo maana wanakuwa wachawi, wababe, wambea.

Hata wewe umepata akili hii ya kuandika ni bibi yako mzaa Baba yako alikuwekea kifua dhidi ya watu wabaya yaani kijicho, bila ivo ungekuwa unavuna mihogo ya kuchemsha huko Musoma vijijini, hawa watu wabaya wasingependa ufike hapo ulipofika. kukaa nyuma ya key board! Sema tu wengine hukosea timing km mzee Kabila

Nothing new here please! ajabu watu wanakupa kichwa eeeh safi hawajayasoma haya yaliyomo,
you've wasted ma time meeen!.
Hayo unayoyasema sijui record za matajiri Duniani, wakimuonyesha Putin, hizo tunazijua sana kuwa ni propaganda za kimagharibi, si ndo silaha zao, kwani wewe unafikiri silaha mpaka iwe IBM tu

Hata maneno, habari, maandishi yeyote yale, km ya F/Book ni silaha kubwa na za hatari mno.zinaweza hata kuachanisha ndoa km hamjajipanga.
 
Hayo yote ni kwa msaada wa hao hao mabeberu na ndiyo maana unakuta bajeti ya serikali lazima kuwepo na beberu aliyekutawala hama kikombe kinaenda kwa beberu yoyote ili ajazie, 😔!!.

Wanajipendekeza na kulazimisha hiyo Misaada yao, baadhi tu ya sababu hizo ni kama;

1.ili tusije dai fidia yeyote kama matokeo ya utumwa, na Ukoloni.

2.na ili tujione duni hatuwezi ktk nyanja zote. km wewe unavoamini.

3.tuendelee kuwa na uchumi tegemezi vizazi hadi vizazi.

4.kudumaza ubunifu.

5.Kukuchangia bajeti yako, na misaada siyo kwamba wanakupenda sana, bali ni silaha hatari mno kuliko bomu la Nuclear. ichukulie km bomu linalo lipuliwa chumbani kwako, ni waafrica wachache sana tuliojaliwa kuitambua hatari hii

6.kuendelea kutu kopesha kadri ya mahitaji yetu ya Maendeleo. wakati Dhahabu wanachukua, Almas, Mafuta na tunaambulia kiducuuchu, sasa wewe kama Rais kohoa uone. ma chimbo ya Mwadui tu yanatosha kutoa magari mawili ya Ford Rangers na kula vizuri kwa nusu ya Watanzania, yaani watu million 30

.
wanajua fika kuwa wakituacha tu. na njaa zetu tuta fika mbali ni usipime. ili kutudhibiti wanaweka mapandikizi ya waafrica vibaraka kandamizi, ili tudhoofike waendelee kutunyonya, na kututawala, kwa kushangilia msaada wa bajeti fake.
Watu kama Savimbi, Mobutu, Alfonso Dhlakama nk. walitumika tu kwa maslahi ya Mabepari, mwishowe wakawatupilia mbali ka makapi, tena kwa dharau sana.

Viongozi wa kia frica walio jitokeza hadharani kupinga vitendo vyao kwa nguvu zote, na kukataa suala la bajeti tegemezi na wakainua nchi zao, kwa uaminifu waliuawa kikatili mno, tena bila sababu, au walibanwa mbavu kama Zimbabwe ya leo,
viongozi wa weusi mfano; Marcom x, Martn Luther, p. Lumumba, Samora, Gaddafi, Murtala mohamad, Dr Steve Bikko nk. waliuawa sababu hiyo. nina mengi but.......
 
Nini kifanyike ili mageuzi yafanyike kwa hawa waafrika?
 
  1. Nilikuwa najiuliza,Habibu B.Anga ni nani tena! Mbona anaandika km the bold!?? Kumbe ndo yeye! Naona mzee umetag member wote kasoro mm tu...!! Lkn usijali...nasubiri madini mkuu!!
    Aksante san comrade na nimekufatilia kwa muda sana naomba unitag mkuu
 
Wanajipendekeza na kulazimisha hiyo Misaada yao, baadhi tu ya sababu hizo ni kama;

1.ili tusije dai fidia yeyote kama matokeo ya utumwa, na Ukoloni.

2.na ili tujione duni hatuwezi ktk nyanja zote. km wewe unavoamini.

3.tuendelee kuwa na uchumi tegemezi vizazi hadi vizazi.

4.kudumaza ubunifu.

5.Kukuchangia bajeti yako, na misaada siyo kwamba wanakupenda sana, bali ni silaha hatari mno kuliko bomu la Nuclear. ichukulie km bomu linalo lipuliwa chumbani kwako, ni waafrica wachache sana tuliojaliwa kuitambua hatari hii

6.kuendelea kutu kopesha kadri ya mahitaji yetu ya Maendeleo. wakati Dhahabu wanachukua, Almas, Mafuta na tunaambulia kiducuuchu, sasa wewe kama Rais kohoa uone. ma chimbo ya Mwadui tu yanatosha kutoa magari mawili ya Ford Rangers na kula vizuri kwa nusu ya Watanzania, yaani watu million 30

.
wanajua fika kuwa wakituacha tu. na njaa zetu tuta fika mbali ni usipime. ili kutudhibiti wanaweka mapandikizi ya waafrica vibaraka kandamizi, ili tudhoofike waendelee kutunyonya, na kututawala, kwa kushangilia msaada wa bajeti fake.
Watu kama Savimbi, Mobutu, Alfonso Dhlakama nk. walitumika tu kwa maslahi ya Mabepari, mwishowe wakawatupilia mbali ka makapi, tena kwa dharau sana.

Viongozi wa kia frica walio jitokeza hadharani kupinga vitendo vyao kwa nguvu zote, na kukataa suala la bajeti tegemezi na wakainua nchi zao, kwa uaminifu waliuawa kikatili mno, tena bila sababu, au walibanwa mbavu kama Zimbabwe ya leo,
viongozi wa weusi mfano; Marcom x, Martn Luther, p. Lumumba, Samora, Gaddafi, Murtala mohamad, Dr Steve Bikko nk. waliuawa sababu hiyo. nina mengi but.......
Weee jamaa hebu hiyo comment yako iongezee vitu vichache na baada ya hapo,nakuomba uigeuze ili iwe thread inayojitegemea.
 
View attachment 815633

The Richest Man in Africa: Kila utajiri una ukafiri nyuma yake

PREMIERE

Nimekuwa kimya sana, nimejikita sana katika tafakuri. Tafakuri juu ya masuala yaliyo bayana lakini hayasemwi... masuala yaliyo dhahiri lakini hayaonwi. Pengine kuna sababu kwa nini hayasemwi na pengine kuna juhudi ya kufanya yasionwe.

Nahisi imefika zama kwa wale ambao tumeamua kufanya kalamu kuwa maisha yetu labda tuthubutu kuoneshwa visvyoonwa na kusema yasiyosemwa. Ni hatari, nafahamu. Lakini hatuna fursa nyingine ya kuweka alama juu ya uso wa dunia zaidi ya fursa ya maisha haya tuliyonayo sasa.

Moja kati ya vitu vibaya zaidi na vya kukaraisha kuishi katika nchi za ulimwengu wa tatu si umasikini wake tu bali ni namna ambavyo tumejiwekea mifumo ya kudumaza uthubutu wa kuwaza na kujenga fikra mbadala. Pengine mifumo hii dumavu ndio sababu hasa ya kufanya umasikini usikome katika nchi zetu hizi.
Utete wa kiwango cha kujiamini (fragile egos) cha viongozi wetu wa nchi hizi umefanya watu kuwa na mawazo mbadala liwe ni mwiko kabisa. Na siongei tu kuhusu ukosoaji, la hasha bali najenga hoja pia juu ya utamaduni wa nchi zetu kuijenga jamii yetu kuwa na mawazo ya 'kundi la ng'ombe'. Mawazo mfanano. Utamaduni wa kuona kwamba tukiwaza sawasawa ndiyo inatufanya kuwa jamii bora tukisahau kuwa maendeleo duniani yameletwa na uwepo wa watu waliofikiri kinyume na mawazo yaliyojengeka kwa muda mrefu kwenye jamii. Watu wenye kufikiri nje ya mawanda yaliyozoeleka.

Utete wa viwango vya kujiamini vya viongozi wetu unafanya hofu na woga kutamalaki kwenye jamii yetu kiasi kwamba hata wenye kujua kidogo tu hawakisemi na kuogopa kuifumbua macho jamii juu ya machache wajuayo. Matokeo yetu jamii zetu za kiafrika zinaishi katika ukimya, ukimya wa wanaojua wakiacha jamii ukifungiwa gizani na hata watoto wetu mashuleni kulishwa historia iliyokobolewa na kupembuliwa na kubakia makapi wasijue ukweli halisi.

Ni muda muafaka nadhani kwa viongozi wa kiafriaka kutambua kuwa mawazo mbadala hata yale ambayo wanaweza wasiyafurahie ni mbolea katika ustawi wa jamii. Jamii inakua kwa mawazo yenye kukinzana. Kukinzana kwa dhamira ya kuisukuma mbele jamii.

Mwaka jana nilifurahishwa sana na makala kinzani ambayo ilikuwa imekuja na wazo mbadala lenye kukinzana na jarida la Forbes ambalo hutoa orodha ya watu matajiri zaidi duniani. Makala ile ilimuainisha Vladmir Putin Rais wa Russia kama mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 200. Kwa haraka haraka baadhi ya watu walihisi ni propaganda za magharibi kumjengea picha Putin kama kiongozi mwenye kujilimbikizia mali na mlafi.
Yawezekana ni kwelil lakini watu wanaruka ukweli kwamba ukiwatazama maswahiba wa karibu wa Putin kama vile Roman Abramovich wana utajiri mkubwa kuzidi ule ambao unatajwa na jarida la Forbes. Lakini pia ukitazama kwa mahesabu ya kihasibu kuna kiwango kikubwa sana cha fedha ambacho hauwezi kukisema kilienda wapi katika kipindi cha mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili kipindi ambacho kinatambulika nchini Rusia kama kipindi cha 'alluminium war'.

Lakini pia ni ukweli ulio wazi kuwa jarida la Forbes halivutiwi na kuwaweka kwenye orodha ya utajiri viongozi wa kiserikali na wahalifu. Ndio maana utaona ma-Prince wa nchi za kiarabu licha ya utajiri wa kufuru walionao lakini hawapo kwenye orodha hizo. Vivyo hivyo na wahalifu wa daraha la kwanza kama akina Guzman El Chapo ambaye ana utajiri wa kutupwa lakini bado haorodheshwi kwenye orodha hiyo.

Ndipo hapa ambapo nataka kujadili juu ya mtu tajiri zaidi Afrika ambaye huwezi kumsoma kwenye jarida la Forbes. Lakini utajiri wake ambao nataka kuujadili si utajiri wa fedha pekee bali nataka kujadili namna ambavyo mtu huyu anavyo ratibu matumizi ya rasilimali katika nchi nne za ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, yaani Tanzania, Rwanda, Burundi na Kongo.

Vuta pichani kichwani mwako akitokea mtu mmoja mahiri na kuweka rasilimali za nchi nne tofauti mikononi mwale. Vuta picha ya mtu mwenye uwezo wa kusema neno lolote na likatekelezwa kote ukanda mzima wa Afrika mashariki na nchi za maziwa makuu.

Kwa heshima na taadhima, leo saa kumi jioni nakukaribisha kusoma makala yangu mpya "THE RICHEST MAN IN AFRICA: Kila Utajiri una Ukafiri Nyuma Yake"

SEHEMU YA KWANZA BOFYA HAPA

SEHEMU YA PILI BOFYA HAPA

SEHEMU YA TATU BOFYA HAPA

Stay here and keep your eyes (and your mind) open!

Habibu B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond
napanua "ubongo"...
Asante
 
Hii nyuzi sio ya kusoma nikiwa nayumba yumba. Naipa siku ya leo mchana naiamkia asubuhi mapema. Asante Habibu
 
Nini kifanyike ili mageuzi yafanyike kwa hawa waafrika?
Tujue chanzo cha tatizo letu kwanza! then tuwapuuze, tuwe wamoja Waafrica wote Duniani! kwa kile kidogo tulicho nacho! tupeane na kukiendeleza, tuwaseme sana pale inapobidi km kitendo alichofanyiwa Mmarecan mweusi George Floyd tumekuwa pamoja safari hii na wametikisika.

Wanavochukua Mali zetu, na wanatutengenezea uadui miongoni mwetu, dhiki na shida ili hatimaye kutuletea silaha tupigane, tuuuane, ili tusidhalishe mali, Ukweli ni kuwa tupaze sauti kwa pamoja, tuwalaumu, na kuwalaani kwa matendo yao' tuwazodoe Yaani siraha ya maneno tu zitatuweka sawa.
 
View attachment 815633

The Richest Man in Africa: Kila utajiri una ukafiri nyuma yake

PREMIERE

Nimekuwa kimya sana, nimejikita sana katika tafakuri. Tafakuri juu ya masuala yaliyo bayana lakini hayasemwi... masuala yaliyo dhahiri lakini hayaonwi. Pengine kuna sababu kwa nini hayasemwi na pengine kuna juhudi ya kufanya yasionwe.

Nahisi imefika zama kwa wale ambao tumeamua kufanya kalamu kuwa maisha yetu labda tuthubutu kuoneshwa visvyoonwa na kusema yasiyosemwa. Ni hatari, nafahamu. Lakini hatuna fursa nyingine ya kuweka alama juu ya uso wa dunia zaidi ya fursa ya maisha haya tuliyonayo sasa.

Moja kati ya vitu vibaya zaidi na vya kukaraisha kuishi katika nchi za ulimwengu wa tatu si umasikini wake tu bali ni namna ambavyo tumejiwekea mifumo ya kudumaza uthubutu wa kuwaza na kujenga fikra mbadala. Pengine mifumo hii dumavu ndio sababu hasa ya kufanya umasikini usikome katika nchi zetu hizi.
Utete wa kiwango cha kujiamini (fragile egos) cha viongozi wetu wa nchi hizi umefanya watu kuwa na mawazo mbadala liwe ni mwiko kabisa. Na siongei tu kuhusu ukosoaji, la hasha bali najenga hoja pia juu ya utamaduni wa nchi zetu kuijenga jamii yetu kuwa na mawazo ya 'kundi la ng'ombe'. Mawazo mfanano. Utamaduni wa kuona kwamba tukiwaza sawasawa ndiyo inatufanya kuwa jamii bora tukisahau kuwa maendeleo duniani yameletwa na uwepo wa watu waliofikiri kinyume na mawazo yaliyojengeka kwa muda mrefu kwenye jamii. Watu wenye kufikiri nje ya mawanda yaliyozoeleka.

Utete wa viwango vya kujiamini vya viongozi wetu unafanya hofu na woga kutamalaki kwenye jamii yetu kiasi kwamba hata wenye kujua kidogo tu hawakisemi na kuogopa kuifumbua macho jamii juu ya machache wajuayo. Matokeo yetu jamii zetu za kiafrika zinaishi katika ukimya, ukimya wa wanaojua wakiacha jamii ukifungiwa gizani na hata watoto wetu mashuleni kulishwa historia iliyokobolewa na kupembuliwa na kubakia makapi wasijue ukweli halisi.

Ni muda muafaka nadhani kwa viongozi wa kiafriaka kutambua kuwa mawazo mbadala hata yale ambayo wanaweza wasiyafurahie ni mbolea katika ustawi wa jamii. Jamii inakua kwa mawazo yenye kukinzana. Kukinzana kwa dhamira ya kuisukuma mbele jamii.

Mwaka jana nilifurahishwa sana na makala kinzani ambayo ilikuwa imekuja na wazo mbadala lenye kukinzana na jarida la Forbes ambalo hutoa orodha ya watu matajiri zaidi duniani. Makala ile ilimuainisha Vladmir Putin Rais wa Russia kama mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 200. Kwa haraka haraka baadhi ya watu walihisi ni propaganda za magharibi kumjengea picha Putin kama kiongozi mwenye kujilimbikizia mali na mlafi.
Yawezekana ni kwelil lakini watu wanaruka ukweli kwamba ukiwatazama maswahiba wa karibu wa Putin kama vile Roman Abramovich wana utajiri mkubwa kuzidi ule ambao unatajwa na jarida la Forbes. Lakini pia ukitazama kwa mahesabu ya kihasibu kuna kiwango kikubwa sana cha fedha ambacho hauwezi kukisema kilienda wapi katika kipindi cha mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili kipindi ambacho kinatambulika nchini Rusia kama kipindi cha 'alluminium war'.

Lakini pia ni ukweli ulio wazi kuwa jarida la Forbes halivutiwi na kuwaweka kwenye orodha ya utajiri viongozi wa kiserikali na wahalifu. Ndio maana utaona ma-Prince wa nchi za kiarabu licha ya utajiri wa kufuru walionao lakini hawapo kwenye orodha hizo. Vivyo hivyo na wahalifu wa daraha la kwanza kama akina Guzman El Chapo ambaye ana utajiri wa kutupwa lakini bado haorodheshwi kwenye orodha hiyo.

Ndipo hapa ambapo nataka kujadili juu ya mtu tajiri zaidi Afrika ambaye huwezi kumsoma kwenye jarida la Forbes. Lakini utajiri wake ambao nataka kuujadili si utajiri wa fedha pekee bali nataka kujadili namna ambavyo mtu huyu anavyo ratibu matumizi ya rasilimali katika nchi nne za ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, yaani Tanzania, Rwanda, Burundi na Kongo.

Vuta pichani kichwani mwako akitokea mtu mmoja mahiri na kuweka rasilimali za nchi nne tofauti mikononi mwale. Vuta picha ya mtu mwenye uwezo wa kusema neno lolote na likatekelezwa kote ukanda mzima wa Afrika mashariki na nchi za maziwa makuu.

Kwa heshima na taadhima, leo saa kumi jioni nakukaribisha kusoma makala yangu mpya "THE RICHEST MAN IN AFRICA: Kila Utajiri una Ukafiri Nyuma Yake"

SEHEMU YA KWANZA BOFYA HAPA

SEHEMU YA PILI BOFYA HAPA

SEHEMU YA TATU BOFYA HAPA

Stay here and keep your eyes (and your mind) open!

Habibu B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond
Habibu B. Anga
Samahani naomba nitoke nje ya mada kidogo!
Nawezaje kutengeneza hypertext links hapa JF, kama hizo za kwako hapo juu zenye maandiko "sehemu ya kwanza bofya hapa"?
 
ni zaidi ya mwaka Sasa, ni Nini kilitokea huu Uzi haukumaliziwa? Mkuu Habib
 
Some people bwana!!! sasa hapa tuelewe nini? makurasa meeengi nothing! no substance usiweke jina langu huko kwenye list bana.

watu wanasifia wala hakuna kitu, hapo nani tajiri? kabila au hao ID CO of Israel? mbona maskini tu wanahangaika hao!

Kwa maelezo yako kilichofanyika was struggling for the fittest.Sioni kipya cha kusisimua hapo. zaidi ya hadithi za Kabila profiles. hayo yapo hata kwa kuku tu. achilia mbali maisha ya Simba dume porini au ng'ombe wa zizini kwako. chukulia kuku tu km majogoo mawili umeyaweka ndani ya zizi moja lazima lingine litawaliwe.kwa timing au nguvu, ikibidi kifo!

Piga ni kupige ni maisha ya kawaida sana, chukulia makanisani tu, misikitini watu wanashindana kushika zaka. au kuswalisha. angalia hata maisha tu ya maskini wa uswahilini, km hapo manzese, kipawa nk, ukiwa na vijicent utaibiwa hata kukodiwa majambazi bila kujali ni ndg yako anafanya ivo.
Ili uishi sasa utafanyaje? wengine ndo maana wanakuwa wachawi, wababe, wambea.

Hata wewe umepata akili hii ya kuandika ni bibi yako mzaa Baba yako alikuwekea kifua dhidi ya watu wabaya yaani kijicho, bila ivo ungekuwa unavuna mihogo ya kuchemsha huko Musoma vijijini, hawa watu wabaya wasingependa ufike hapo ulipofika. kukaa nyuma ya key board! Sema tu wengine hukosea timing km mzee Kabila

Nothing new here please! ajabu watu wanakupa kichwa eeeh safi hawajayasoma haya yaliyomo,
you've wasted ma time meeen!.
Wewe ya kwako yenye substance ni yapi?? Haya uliyobwabwsja?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom