The Richest Man In Africa: Kila Utajiri una Ukafiri nyuma yake

View attachment 815633


The Richest Man in Africa: Kila utajiri una ukafiri nyuma yake



PREMIERE


Nimekuwa kimya sana, nimejikita sana katika tafakuri. Tafakuri juu ya masuala yaliyo bayana lakini hayasemwi... masuala yaliyo dhahiri lakini hayaonwi. Pengine kuna sababu kwa nini hayasemwi na pengine kuna juhudi ya kufanya yasionwe.

Nahisi imefika zama kwa wale ambao tumeamua kufanya kalamu kuwa maisha yetu labda tuthubutu kuoneshwa visvyoonwa na kusema yasiyosemwa. Ni hatari, nafahamu. Lakini hatuna fursa nyingine ya kuweka alama juu ya uso wa dunia zaidi ya fursa ya maisha haya tuliyonayo sasa.


Moja kati ya vitu vibaya zaidi na vya kukaraisha kuishi katika nchi za ulimwengu wa tatu si umasikini wake tu bali ni namna ambavyo tumejiwekea mifumo ya kudumaza uthubutu wa kuwaza na kujenga fikra mbadala. Pengine mifumo hii dumavu ndio sababu hasa ya kufanya umasikini usikome katika nchi zetu hizi.
Utete wa kiwango cha kujiamini (fragile egos) cha viongozi wetu wa nchi hizi umefanya watu kuwa na mawazo mbadala liwe ni mwiko kabisa. Na siongei tu kuhusu ukosoaji, la hasha bali najenga hoja pia juu ya utamaduni wa nchi zetu kuijenga jamii yetu kuwa na mawazo ya 'kundi la ng'ombe'. Mawazo mfanano. Utamaduni wa kuona kwamba tukiwaza sawasawa ndiyo inatufanya kuwa jamii bora tukisahau kuwa maendeleo duniani yameletwa na uwepo wa watu waliofikiri kinyume na mawazo yaliyojengeka kwa muda mrefu kwenye jamii. Watu wenye kufikiri nje ya mawanda yaliyozoeleka.

Utete wa viwango vya kujiamini vya viongozi wetu unafanya hofu na woga kutamalaki kwenye jamii yetu kiasi kwamba hata wenye kujua kidogo tu hawakisemi na kuogopa kuifumbua macho jamii juu ya machache wajuayo. Matokeo yetu jamii zetu za kiafrika zinaishi katika ukimya, ukimya wa wanaojua wakiacha jamii ukifungiwa gizani na hata watoto wetu mashuleni kulishwa historia iliyokobolewa na kupembuliwa na kubakia makapi wasijue ukweli halisi.

Ni muda muafaka nadhani kwa viongozi wa kiafriaka kutambua kuwa mawazo mbadala hata yale ambayo wanaweza wasiyafurahie ni mbolea katika ustawi wa jamii. Jamii inakua kwa mawazo yenye kukinzana. Kukinzana kwa dhamira ya kuisukuma mbele jamii.

Mwaka jana nilifurahishwa sana na makala kinzani ambayo ilikuwa imekuja na wazo mbadala lenye kukinzana na jarida la Forbes ambalo hutoa orodha ya watu matajiri zaidi duniani. Makala ile ilimuainisha Vladmir Putin Rais wa Russia kama mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 200. Kwa haraka haraka baadhi ya watu walihisi ni propaganda za magharibi kumjengea picha Putin kama kiongozi mwenye kujilimbikizia mali na mlafi.
Yawezekana ni kwelil lakini watu wanaruka ukweli kwamba ukiwatazama maswahiba wa karibu wa Putin kama vile Roman Abramovich wana utajiri mkubwa kuzidi ule ambao unatajwa na jarida la Forbes. Lakini pia ukitazama kwa mahesabu ya kihasibu kuna kiwango kikubwa sana cha fedha ambacho hauwezi kukisema kilienda wapi katika kipindi cha mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili kipindi ambacho kinatambulika nchini Rusia kama kipindi cha 'alluminium war'.

Lakini pia ni ukweli ulio wazi kuwa jarida la Forbes halivutiwi na kuwaweka kwenye orodha ya utajiri viongozi wa kiserikali na wahalifu. Ndio maana utaona ma-Prince wa nchi za kiarabu licha ya utajiri wa kufuru walionao lakini hawapo kwenye orodha hizo. Vivyo hivyo na wahalifu wa daraha la kwanza kama akina Guzman El Chapo ambaye ana utajiri wa kutupwa lakini bado haorodheshwi kwenye orodha hiyo.

Ndipo hapa ambapo nataka kujadili juu ya mtu tajiri zaidi Afrika ambaye huwezi kumsoma kwenye jarida la Forbes. Lakini utajiri wake ambao nataka kuujadili si utajiri wa fedha pekee bali nataka kujadili namna ambavyo mtu huyu anavyo ratibu matumizi ya rasilimali katika nchi nne za ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, yaani Tanzania, Rwanda, Burundi na Kongo.

Vuta pichani kichwani mwako akitokea mtu mmoja mahiri na kuweka rasilimali za nchi nne tofauti mikononi mwale. Vuta picha ya mtu mwenye uwezo wa kusema neno lolote na likatekelezwa kote ukanda mzima wa Afrika mashariki na nchi za maziwa makuu.

Kwa heshima na taadhima, leo saa kumi jioni nakukaribisha kusoma makala yangu mpya "THE RICHEST MAN IN AFRICA: Kila Utajiri una Ukafiri Nyuma Yake"


SEHEMU YA KWANZA BOFYA HAPA

SEHEMU YA PILI BOFYA HAPA


SEHEMU YA TATU BOFYA HAPA



Stay here and keep your eyes (and your mind) open!



Habibu B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond
Muendelezo wa sehemu ya nne naomba usisahau kunitag
 
Hii thread ingekua imeanzishwa na member asiye na jina kubwa humu muda huu thread ingeshajaa matusi sababu anaboa kutoiendeleza hadi abembelezwe km mtoto wa kike


Ila kwavile imeandikwa na sekretarumi wa komando kipensi naona watu wamefunika kombe na kujifanya vipofu na wavumilivu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hiki ulichoandika unaona sio matusi?!
 
Mkuu hiki ulichoandika unaona sio matusi?!
Naona nilichoandika kimeanza kuonesha ujalisia.....hamtaki mtu wenu akosolewe mnaona km ni matusi........Hujui km huyu demu wake wa hapa Jf alikuwa sekretari wa komando kopensi pale Jangid Plaza kisha akaandika thread ya kupigia upatu utapeli wa komando kiprnsi skijitapa hana maslahi kwenye hiyo ofisi
 
Wakuu, kumradhi sana... kuna masuala yako nje ya uwezo wangu yamejitokeza. Makala hii haitoendelea. Kumradhi sana kwa hili but there is nothing I can do.

Nimeweka makala mpya ambayo ilikuwa exclusive kwa wale walioko kwenye group tu. But nimeona nishee nanyi kupunguza walau udhia wa kukosa makala hii ya "The Richest Man".

Kumradhi sana.
The Bold: Ujasusi Sebuleni Kwetu - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii thread ingekua imeanzishwa na member asiye na jina kubwa humu muda huu thread ingeshajaa matusi sababu anaboa kutoiendeleza hadi abembelezwe km mtoto wa kike


Ila kwavile imeandikwa na sekretarumi wa komando kipensi naona watu wamefunika kombe na kujifanya vipofu na wavumilivu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo ya Pwani.. Mpiga ngoma akigoma atapewa hata kama anataka nini.. Mpeni anacho taka aendeleze story
 
Wakuu, kumradhi sana... kuna masuala yako nje ya uwezo wangu yamejitokeza. Makala hii haitoendelea. Kumradhi sana kwa hili but there is nothing I can do.

Nimeweka makala mpya ambayo ilikuwa exclusive kwa wale walioko kwenye group tu. But nimeona nishee nanyi kupunguza walau udhia wa kukosa makala hii ya "The Richest Man".

Kumradhi sana.
The Bold: Ujasusi Sebuleni Kwetu - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilijua haitafika mbali, nilishaacha kufuatilia story za miendelezo JF uishaji wake unasumbua sana
 
single people will be online the whole day jus commenting, tweeting, Rtin, and liking until their phones become hot
 
Sasa naogopa kusoma tena maana mauhondo huwa yanaishia mapema njiani. Kuanzia sasa nitakuwa nasoma mwisho kwanza, nikiona kitu itaendelea, sijui subiri part two.....!! Baasi sijihusishi na hiyo habari
 
Wakuu, kumradhi sana... kuna masuala yako nje ya uwezo wangu yamejitokeza. Makala hii haitoendelea. Kumradhi sana kwa hili but there is nothing I can do.

Nimeweka makala mpya ambayo ilikuwa exclusive kwa wale walioko kwenye group tu. But nimeona nishee nanyi kupunguza walau udhia wa kukosa makala hii ya "The Richest Man".

Kumradhi sana.
The Bold: Ujasusi Sebuleni Kwetu - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
Group nilikupa number uniweke! Ukanitosa live
 
The bold yaani Habibu B. Anga Kama soft copy hapa JF is banned, natumai hard copy a k a kitabu unaweza kuchapisha na kila muhitajia akanunua. I believe ni haki yako kama Muandishi kuandika kile ukijuacho baada ya utafiti ulioufanya, then kama kuna critics wataonyesha mapungufu au uongo wa hoja husika badala ya kuzuiana hata ile fundamental right ya Kupashana habari zilizotafitiwa na kutoka kwenye undisputed sources.
 
112 Reactions
Reply
Back
Top Bottom