The Richest Man In Africa: Kila Utajiri una Ukafiri nyuma yake

View attachment 815633


The Richest Man in Africa: Kila utajiri una ukafiri nyuma yake



PREMIERE


Nimekuwa kimya sana, nimejikita sana katika tafakuri. Tafakuri juu ya masuala yaliyo bayana lakini hayasemwi... masuala yaliyo dhahiri lakini hayaonwi. Pengine kuna sababu kwa nini hayasemwi na pengine kuna juhudi ya kufanya yasionwe.

Nahisi imefika zama kwa wale ambao tumeamua kufanya kalamu kuwa maisha yetu labda tuthubutu kuoneshwa visvyoonwa na kusema yasiyosemwa. Ni hatari, nafahamu. Lakini hatuna fursa nyingine ya kuweka alama juu ya uso wa dunia zaidi ya fursa ya maisha haya tuliyonayo sasa.


Moja kati ya vitu vibaya zaidi na vya kukaraisha kuishi katika nchi za ulimwengu wa tatu si umasikini wake tu bali ni namna ambavyo tumejiwekea mifumo ya kudumaza uthubutu wa kuwaza na kujenga fikra mbadala. Pengine mifumo hii dumavu ndio sababu hasa ya kufanya umasikini usikome katika nchi zetu hizi.
Utete wa kiwango cha kujiamini (fragile egos) cha viongozi wetu wa nchi hizi umefanya watu kuwa na mawazo mbadala liwe ni mwiko kabisa. Na siongei tu kuhusu ukosoaji, la hasha bali najenga hoja pia juu ya utamaduni wa nchi zetu kuijenga jamii yetu kuwa na mawazo ya 'kundi la ng'ombe'. Mawazo mfanano. Utamaduni wa kuona kwamba tukiwaza sawasawa ndiyo inatufanya kuwa jamii bora tukisahau kuwa maendeleo duniani yameletwa na uwepo wa watu waliofikiri kinyume na mawazo yaliyojengeka kwa muda mrefu kwenye jamii. Watu wenye kufikiri nje ya mawanda yaliyozoeleka.

Utete wa viwango vya kujiamini vya viongozi wetu unafanya hofu na woga kutamalaki kwenye jamii yetu kiasi kwamba hata wenye kujua kidogo tu hawakisemi na kuogopa kuifumbua macho jamii juu ya machache wajuayo. Matokeo yetu jamii zetu za kiafrika zinaishi katika ukimya, ukimya wa wanaojua wakiacha jamii ukifungiwa gizani na hata watoto wetu mashuleni kulishwa historia iliyokobolewa na kupembuliwa na kubakia makapi wasijue ukweli halisi.

Ni muda muafaka nadhani kwa viongozi wa kiafriaka kutambua kuwa mawazo mbadala hata yale ambayo wanaweza wasiyafurahie ni mbolea katika ustawi wa jamii. Jamii inakua kwa mawazo yenye kukinzana. Kukinzana kwa dhamira ya kuisukuma mbele jamii.

Mwaka jana nilifurahishwa sana na makala kinzani ambayo ilikuwa imekuja na wazo mbadala lenye kukinzana na jarida la Forbes ambalo hutoa orodha ya watu matajiri zaidi duniani. Makala ile ilimuainisha Vladmir Putin Rais wa Russia kama mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 200. Kwa haraka haraka baadhi ya watu walihisi ni propaganda za magharibi kumjengea picha Putin kama kiongozi mwenye kujilimbikizia mali na mlafi.
Yawezekana ni kwelil lakini watu wanaruka ukweli kwamba ukiwatazama maswahiba wa karibu wa Putin kama vile Roman Abramovich wana utajiri mkubwa kuzidi ule ambao unatajwa na jarida la Forbes. Lakini pia ukitazama kwa mahesabu ya kihasibu kuna kiwango kikubwa sana cha fedha ambacho hauwezi kukisema kilienda wapi katika kipindi cha mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili kipindi ambacho kinatambulika nchini Rusia kama kipindi cha 'alluminium war'.

Lakini pia ni ukweli ulio wazi kuwa jarida la Forbes halivutiwi na kuwaweka kwenye orodha ya utajiri viongozi wa kiserikali na wahalifu. Ndio maana utaona ma-Prince wa nchi za kiarabu licha ya utajiri wa kufuru walionao lakini hawapo kwenye orodha hizo. Vivyo hivyo na wahalifu wa daraha la kwanza kama akina Guzman El Chapo ambaye ana utajiri wa kutupwa lakini bado haorodheshwi kwenye orodha hiyo.

Ndipo hapa ambapo nataka kujadili juu ya mtu tajiri zaidi Afrika ambaye huwezi kumsoma kwenye jarida la Forbes. Lakini utajiri wake ambao nataka kuujadili si utajiri wa fedha pekee bali nataka kujadili namna ambavyo mtu huyu anavyo ratibu matumizi ya rasilimali katika nchi nne za ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, yaani Tanzania, Rwanda, Burundi na Kongo.

Vuta pichani kichwani mwako akitokea mtu mmoja mahiri na kuweka rasilimali za nchi nne tofauti mikononi mwale. Vuta picha ya mtu mwenye uwezo wa kusema neno lolote na likatekelezwa kote ukanda mzima wa Afrika mashariki na nchi za maziwa makuu.

Kwa heshima na taadhima, leo saa kumi jioni nakukaribisha kusoma makala yangu mpya "THE RICHEST MAN IN AFRICA: Kila Utajiri una Ukafiri Nyuma Yake"



Stay here and keep your eyes (and your mind) open!


Habibu B. Anga "The Bold"
Xcuz me!!! etii?!!? Putin tajiri zaidi duniani!!? Aaahh umebugg mjomba

Sikia mjomba maisha yako yote mwanasiasa tajiri hawezi mzidi mfanyabiashara tajiri hata aibe vipi, achana na kitu inaitwa biashara, acha mchezo kabisa na iyo kitu, tena usilete utani ata kidogo

Cheki apa Bill gates anaingiza dolla za kimarekani 23,148 kwa dakika1 sawa na Tzsh Milioni 53, 240,400 hiyo ni kwa dakika mjomba lakini kwa siku anaingiza dolla za kimarekani Millioni 1,380,000 sawa na Tzshs Tillion 3,174,000,000 bajeti ya wizara hiyo mjomba

Dangote anaingiza Tzsh Million 11,600,000 kwa siku sawa na Million 350,000,000 kwa mwezi sasa unapokuja kutuletea porojo za watu kama akina kagame eti ni matajiri hahahahaa umekula maharage ya wapi mjomba

Achana na iyo mambo, kama unawaingiza chaka watu, waingize lakini kaa ukijua hapa Jf ni jukwaa la watu smart sana, usije ukaleta porojo zako ukadhani umewalisha matango yako, no way

Eti kagame tajiri africa,
Umebugg meeeen
 
Mualiko
IMG-20180614-WA0002.jpg
 
Xcuz me!!! etii?!!? Putin tajiri zaidi duniani!!? Aaahh umebugg mjomba

Sikia mjomba maisha yako yote mwanasiasa tajiri hawezi mzidi mfanyabiashara tajiri hata aibe vipi, achana na kitu inaitwa biashara, acha mchezo kabisa na iyo kitu, tena usilete utani ata kidogo

Cheki apa Bill gates anaingiza dolla za kimarekani 23,148 kwa dakika1 sawa na Tzsh Milioni 53, 240,400 hiyo ni kwa dakika mjomba lakini kwa siku anaingiza dolla za kimarekani Millioni 1,380,000 sawa na Tzshs Tillion 3,174,000,000 bajeti ya wizara hiyo mjomba

Dangote anaingiza Tzsh Million 11,600,000 kwa siku sawa na Million 350,000,000 kwa mwezi sasa unapokuja kutuletea porojo za watu kama akina kagame eti ni matajiri hahahahaa umekula maharage ya wapi mjomba

Achana na iyo mambo, kama unawaingiza chaka watu, waingize lakini kaa ukijua hapa Jf ni jukwaa la watu smart sana, usije ukaleta porojo zako ukadhani umewalisha matango yako, no way

Eti kagame tajiri africa,
Umebugg meeeen
Karibu sana... nafurahi kukuona hapa. Naheshimu mawazo yako.


Asante.
 
112 Reactions
Reply
Back
Top Bottom