The Richest Man In Africa: Kila Utajiri una Ukafiri nyuma yake

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined
May 7, 2013
Messages
6,446
Points
2,000

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined May 7, 2013
6,446 2,000
Cl9jz-XWIAASy_N.jpgThe Richest Man in Africa: Kila utajiri una ukafiri nyuma yakePREMIERE


Nimekuwa kimya sana, nimejikita sana katika tafakuri. Tafakuri juu ya masuala yaliyo bayana lakini hayasemwi... masuala yaliyo dhahiri lakini hayaonwi. Pengine kuna sababu kwa nini hayasemwi na pengine kuna juhudi ya kufanya yasionwe.

Nahisi imefika zama kwa wale ambao tumeamua kufanya kalamu kuwa maisha yetu labda tuthubutu kuoneshwa visvyoonwa na kusema yasiyosemwa. Ni hatari, nafahamu. Lakini hatuna fursa nyingine ya kuweka alama juu ya uso wa dunia zaidi ya fursa ya maisha haya tuliyonayo sasa.


Moja kati ya vitu vibaya zaidi na vya kukaraisha kuishi katika nchi za ulimwengu wa tatu si umasikini wake tu bali ni namna ambavyo tumejiwekea mifumo ya kudumaza uthubutu wa kuwaza na kujenga fikra mbadala. Pengine mifumo hii dumavu ndio sababu hasa ya kufanya umasikini usikome katika nchi zetu hizi.
Utete wa kiwango cha kujiamini (fragile egos) cha viongozi wetu wa nchi hizi umefanya watu kuwa na mawazo mbadala liwe ni mwiko kabisa. Na siongei tu kuhusu ukosoaji, la hasha bali najenga hoja pia juu ya utamaduni wa nchi zetu kuijenga jamii yetu kuwa na mawazo ya 'kundi la ng'ombe'. Mawazo mfanano. Utamaduni wa kuona kwamba tukiwaza sawasawa ndiyo inatufanya kuwa jamii bora tukisahau kuwa maendeleo duniani yameletwa na uwepo wa watu waliofikiri kinyume na mawazo yaliyojengeka kwa muda mrefu kwenye jamii. Watu wenye kufikiri nje ya mawanda yaliyozoeleka.

Utete wa viwango vya kujiamini vya viongozi wetu unafanya hofu na woga kutamalaki kwenye jamii yetu kiasi kwamba hata wenye kujua kidogo tu hawakisemi na kuogopa kuifumbua macho jamii juu ya machache wajuayo. Matokeo yetu jamii zetu za kiafrika zinaishi katika ukimya, ukimya wa wanaojua wakiacha jamii ukifungiwa gizani na hata watoto wetu mashuleni kulishwa historia iliyokobolewa na kupembuliwa na kubakia makapi wasijue ukweli halisi.

Ni muda muafaka nadhani kwa viongozi wa kiafriaka kutambua kuwa mawazo mbadala hata yale ambayo wanaweza wasiyafurahie ni mbolea katika ustawi wa jamii. Jamii inakua kwa mawazo yenye kukinzana. Kukinzana kwa dhamira ya kuisukuma mbele jamii.

Mwaka jana nilifurahishwa sana na makala kinzani ambayo ilikuwa imekuja na wazo mbadala lenye kukinzana na jarida la Forbes ambalo hutoa orodha ya watu matajiri zaidi duniani. Makala ile ilimuainisha Vladmir Putin Rais wa Russia kama mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 200. Kwa haraka haraka baadhi ya watu walihisi ni propaganda za magharibi kumjengea picha Putin kama kiongozi mwenye kujilimbikizia mali na mlafi.
Yawezekana ni kwelil lakini watu wanaruka ukweli kwamba ukiwatazama maswahiba wa karibu wa Putin kama vile Roman Abramovich wana utajiri mkubwa kuzidi ule ambao unatajwa na jarida la Forbes. Lakini pia ukitazama kwa mahesabu ya kihasibu kuna kiwango kikubwa sana cha fedha ambacho hauwezi kukisema kilienda wapi katika kipindi cha mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili kipindi ambacho kinatambulika nchini Rusia kama kipindi cha 'alluminium war'.

Lakini pia ni ukweli ulio wazi kuwa jarida la Forbes halivutiwi na kuwaweka kwenye orodha ya utajiri viongozi wa kiserikali na wahalifu. Ndio maana utaona ma-Prince wa nchi za kiarabu licha ya utajiri wa kufuru walionao lakini hawapo kwenye orodha hizo. Vivyo hivyo na wahalifu wa daraha la kwanza kama akina Guzman El Chapo ambaye ana utajiri wa kutupwa lakini bado haorodheshwi kwenye orodha hiyo.

Ndipo hapa ambapo nataka kujadili juu ya mtu tajiri zaidi Afrika ambaye huwezi kumsoma kwenye jarida la Forbes. Lakini utajiri wake ambao nataka kuujadili si utajiri wa fedha pekee bali nataka kujadili namna ambavyo mtu huyu anavyo ratibu matumizi ya rasilimali katika nchi nne za ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, yaani Tanzania, Rwanda, Burundi na Kongo.

Vuta pichani kichwani mwako akitokea mtu mmoja mahiri na kuweka rasilimali za nchi nne tofauti mikononi mwale. Vuta picha ya mtu mwenye uwezo wa kusema neno lolote na likatekelezwa kote ukanda mzima wa Afrika mashariki na nchi za maziwa makuu.

Kwa heshima na taadhima, leo saa kumi jioni nakukaribisha kusoma makala yangu mpya "THE RICHEST MAN IN AFRICA: Kila Utajiri una Ukafiri Nyuma Yake"


SEHEMU YA KWANZA BOFYA HAPA

SEHEMU YA PILI BOFYA HAPA


SEHEMU YA TATU BOFYA HAPAStay here and keep your eyes (and your mind) open!Habibu B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond
 

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2013
Messages
3,781
Points
2,000

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2013
3,781 2,000
Pole sana the bold

Nilijua tu watakutisha. Baada ya kusomaga ule uzi wako wa kilio cha machozi kikielekea ethiopia. Mimi kwa kuwa mzazi wangu mmoja ni mtutsi kutoka Rwanda. Nilipotoka likizo nilikaa nyumbani nikamuuliza baada ya kuona argument za zitto jr nilienda kumuuliza japokuwa mengi alinificha nikaja kugundua kwamba hawa watutsi sio wa mchezo mchezo japokuwa ni mzazi wangu ila naonaga ukatili wake.

Anyway bold embu shusha vitu nijue nilipotoka maana sielewagi but nilikuja kumjua mzee wangu ni mbaguzi sana na mkatili kweli kweli ila bado napingana naye na nimemuelewa kwa nini alinifichaga maisha yangu yote asitufundishe ubaguzi wa kule Rwanda
 

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined
May 7, 2013
Messages
6,446
Points
2,000

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined May 7, 2013
6,446 2,000
IMG-20180610-WA0040.jpgThe Richest Man In Africa: Kila Utajiri Una ukafiri nyuma yakeSEHEMU YA TATU


Kwa wasomaji wa makala zangu naamini watakuwa si wageni kwa mtindo wangu wa uandishi ninaopendelea mara kadhaa kwa kuianza simulizi kuanzia mwishoni au katikati na kisha kuchambua mwanzo wa sakata zima na hiki ndicho nakusudia hasa kukifanya katika makala hii.

Katika sehemu zilizopita nilieleza namna ya mazingira ambayo Mzee Kabila aliuwawa na pia nimegusia kiduchu kuhusu washirika wa mauaji hayo.
Lakini pasipo kutoka nje ya mstari na kusahau lengo, makala hii si mahususi hasa kuchambua historia au mgogoro wa Congo bali ni utetezi wangu juu ya hoja ambayo najaribu kuijenga kuhusu mtu ambaye ni tajiri zaidi barani afrika lakini kamwe huwezi kukuona akitajwa katika majarida ya kuorodhesha matajiri kama Forbes na Forbes Africa. Kama ambavyo nilianza kujenga hoja yangu juu ya ushawishi alionao katika ukanda huu wa nchi za maziwa makuu na namna ambavyo ana uwezo wa kuratibu matumizi ya rasilimali katika nchi hizi ndivyo hivi ambavyo nitaendelea na makala hii kwa kuangalia ushaiwhi huo na chimbuko lake.

Sasa basi katika sehemu hii nataka nichambue kwa kina mno (mno hasa) chimbuko la uhusika wa "Paul" kwa kile ambacho kilitokea Congo kuanzia mauaji ya Patrice Lumumba, Kung'olewa kwa Mobutu, kuuwawa kwa Mzee Kabila na hiki ambacho kinaendelea sasa nchini Congo. Naomba ufuatane nami kwa makini sana nikichambua uhusika wake kule Congo na itakuwa rahisi zaidi tukianza kuchambua alionao kwenye nchi nyingine za Afrika mashariki na namna ambavyo anaratibu matumizi ya rasilimali.


Sasa basi….


Kuelewa kinachoendelea hivi sasa Congo pamoja na mfululizo wa vifo vya viongozi wa juu mara tu baada ya baada ya kupata uhuru, karata nzuri ya kuelewa namna ambavyo Paul alifanikiwa kwa umahiri kujipenyeza na kuimarisha ushawishi wake nchini humo.

Ni kwamba, baada ya kupata uhuru na kisha muda mchache baadae nchi ya Congo kuingia kwenye machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na mparaganyiko kwenye jeshi kufuatia kuuwawa kwa Patrice Lumumba kuliibuka vikundi kadhaa vya wapiganaji nchini Congo. Kipindi hiki ninachokiongelea hasa ni mwanzoni mwa mwaka 1964 kipindi ambacho Cyrille Adoula alikuwa ndiye anaongoza nchi ya Congo. Cyrille Adoula alikuwa ni kiongozi dhaifu mno ambaye hakukubalika kwa ukubwa ndani ya Congo kwa wananchi na hata kwa wanasiasa wenzake. Huko mbeleni nitafanya rejea na kugusia hili kwa undani pamoja na kifo cha Lumumba na kuibuka kwa Mobutu.

Mparaganyiko wa kijeshi ulisababisha kuibuka kwa vikundi karibia vinne vya wapiganaji msituni lakini vyote vikiongozwa na umoja uliojiuta NLC (National Liberation Council). Kuna bwana aitwa Gaston Sumaliot alikuwa anaongoza vuguvugu hili kutokea kaslazini mashariki mwa Congo huku moja ya Maluteni wake Bw. Laurent Kabila akiongoza vuguvugu hili kutokea mashariki mwa Congo. Wakati huo huo moja ya maswahiba wakubwa wa Lumumba aliyeitwa Christopher Gbenye na kikundi chake cha wapiganaji walikuwa wanashikilia eneo kubwa pia la Congo kwa msaada mkubwa wa Urusi na Uchina.

Mwezi July mwaka huo 1994 Moise Thsombe alifanikiwa kuingia madarakani kwa kumuondoa Cyrille Adoula na baada tu ya kushika madaraka alianza kutafuta msaada wa kijeshi kwa Marekani, Ubelgiji na kwa makaburu wa Afrika Kusini kitendo ambacho hakikuwafurahisha wazalendo wengi wa Kiafrika.

IMG-20180529-WA0032.jpgIkumbukwe kwamba Marekani wana maslahi makubwa mno nchini Congo kabla hata ya Uhuru wa Congo hasa kutokana na ulukuki wa rasilimali zilizopi nchini humo. Kama ambavyo tutaona hapo baadae kinagaubaga kabisa shirika la ujasusi la Marekani, CIA walihusika moja kwa moja katika mauaju wa Patrice Lumumba kwa mikono ya kina Sese seko Mobuttu.

Kwa hiyo kitendo cha Moise Tshombe kuomba msaada wa kijeshi kwa jumuiya ya kimataifa yalikuwa ni mazingira sawia kabisa ambayo Marekani yaliwavutia.
Rais wa Marekani wa kipindi kile Bw. Lyndon Johnson alimtuma Bw. Averell Harriman ambaye alikuwa ni waziri wa biashara kipindi hicho kwenda nchini Congo katikati ya mwaka 1964. Ilitumiwa 'cover' ya waziri huyo kutembelea nchi ya Congo akiwa na msafara wa 'Wafanyabiashara' wa Kimarekani kana kwamba wameenda kuangalia fursa za uwekezaji nchini humo. Lajini ajabu ni kwamba katika msafara ule alikuwemo moja ya sura ambazo watu wengi hawakuifahamu sana kipindi kile, Bw. Cyrus Vance ambaye alikuwa ni naibu Waziri wa ulinzi wa Marekani (baadae alikuja kuwa Waziri wa Mambo ya Nje).

Dhumuni hasa la safari ile ilikiwa ni kufanya tathimini ya hali halisi ya Congo ili kujua hatua stahiki za kijeshi ambazo Marekani wanaweza kuzifanya.


Safari ile ilizaa matunda mzuri kwani mwezi September mwaka huo 1964 Ubelgiji ilituma kikosi chake kusaidia jeshi la serikali ya Moise Tshombe. Pia makaburu wa Afrika Kusini pamoja na wapiganaji kutoka Rhodesia waliwasili ndani ya Congo katika kipindi hicho hicho. Mwezi November mshirika wa Karibu wa Marekani, Uingereza naye alituma wanajeshi wake nchini Congo. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba vikosi vyote hivi viliingizwa Congo kwa ndege za jeshi la Marekani. Lengo kuu la wanajeshi hawa na vikosi hivi vilivyoingia Congo ilikuwa ni kudhibiti nakutokomeza vikundi vya 'waasi' walioko msituni.
Ni dhahiri kabisa kwamba Marekani alikuwa anajaribu kuficha mkono wake juu ya uhusika wa uingizaji wanajeshi nchini Congo hasa kutokana na aibu kubwa ambaye walikuwa wametoka kuipata nchini Cuba kwenye mapambano ya 'Bay of Pigs' ambayo Marekani na vibaraka wake aliowapandikiza walitandikwa kwa aibu na kuzua mzozo wa kimataifa kati ya nchi za kibepari na zile za mlengo wa kijamaa zikiongozwa na Urusi na Cuba.


Ikumbukwe kwamba katika miaka ile ya sitini vuguvugu la nchi za Afrika kupata Uhuru lilikuwa limeshika kasi, kwa hiyo kitendo cha nchi za Ulaya kuingiza vikosi vya kijeshi Congo kilionekana kana kwamba Wakoloni waliotimuliwa walikuwa wanarejea upya. Viongozi wote wa Afrika walipinga kitendo hicho lakini kiongozi mwenyewe wa Congo kipindi hicho Moise Tshombe aliwakumbatia mabeberu.

Mwaka huo huo 1964 mwezi Desemba kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa, mwanamapinduzi Che Guevara alitoa hotuba kali akilaani juu ya hujuma na uzandiki unaofanywa na mataifa ya magharibi kwenye nchi za Ulimwengu wa tatu na akatoa mfano hai nchi ya Congo. Hotuba ile ni moja ya hotuba za kukumbukwa zaidi mpaka leo hii. Guevara alipinga vikali kitendo hicho ambacho alikiita cha uvamizi wa ardhi huru. Moja ya kauli yake ya kukumbukwa zaidi kwenye hotuba yake ni ile ambayo alisema kuingizwa kwa wanajeshi wa kimagharibi nchini Congo ni njama (conspiracy) ya mataifa yenye nguvu ya kimagharibi kujitwalia tena afrika akitoa mfano wa taarifa ya intelijensia akidai kwamba kwa mfano wapiganaji wa kibelgiji walipakiwa kwenye ndege za jeshi la marekani ambazo ziliruka kutoka kwenye viwanja vya ndege vya kijeshi vya Uingereza (Belgian paratroopers, carried by US planes, took off from British Bases).

Kama tujuavyo kwamba Guevara hakuwa mtu wa utani wala maneno matupu. Guevara ni moja ya wanamapinduzi mahiri zaidi kuwahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Baada ya mkutano ule wa Umoja wa Mataifa Che Guevara kwa kushauriana na Fidel Castro alianza Ziara Barani Afrika kwa nia ya kuratibu mbinu za namna ya kukomboa mataifa hayo ya Afrika. Ziara ya Guevara ilianzia Algeria, kisha akaenda Mali, kisha Congo-Brazaville, kisha Senegali, kisha Ghana, kisha Misri na ziara hii alihitimisha moja ya sehemu ambayo alikusudia zaidi, TANZANIA… naam sio Congo bali Tanzania japo dhumuni lake lilikuwa ni Congo. Alikuja Tanzania kwa sababy moja kubwa, Rais wa Tanzania kipindi hicho, Mwalimu Julius K. Nyerere alikuwa amekusudia kumkutanisha Guevara na kijana wa kikongo mwenye kikundi chake cha msituni na mwenye nia hasa ya kuikomboa Congo. Mwalimu Nyerere alikuwa anataka kumkutanisha Guevara na Laurent Kabila.Itaendelea…


Habib - 0718 096 811
To Infinity and Beyond
 

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined
May 7, 2013
Messages
6,446
Points
2,000

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined May 7, 2013
6,446 2,000
Sehemu ya Tatu...

Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij addenbwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90 Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero agprogrammer JoJiPoJi Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga ABB SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe salaniatz Natasha Ismail jiwe jeusi chibalangunamchezo
John Mloy conjuget Van Pauser great G Mtoto wa nzi Zeus1 hindustan Sci-Fi MAN OF PEACE kashata emnly danny baraka bb MTOTELA kbosho TEMLO DA VINCA
 

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined
May 7, 2013
Messages
6,446
Points
2,000

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined May 7, 2013
6,446 2,000
Binafsi niliwahi kukushauri hili mkuu. Habibu B. Anga anapaswa kuwa mkubwa kuliko The Bold. Jina lako halisi ndilo linalopaswa kubeba heshima inayotokana na kazi zako,na ndilo linalopaswa kuingia katika vitabu vya historia kwa ajili ya kizazi kijacho. Wewe ni mwandishi wa kiwango cha juu mkuu,natamani sana kalamu yako ikufikishe katika levo za juu kabisa za mafanikio katika ukwasi na utukufu!
Nakumbuka chief ulikuwa moja ya watu wa mwanzo kabisa kunishauri nianze kulijenga jina langu halisi badala ya 'alias'.

Nashukuru sana kwa ushauri mzuri siku zote na kuniunga mkono
 

Forum statistics

Threads 1,344,331
Members 515,405
Posts 32,816,070
Top