The Return of Mkapa-Sumaye as Lowassa is politically shaken. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Return of Mkapa-Sumaye as Lowassa is politically shaken.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crucifix, Nov 25, 2011.

 1. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa ninawafananisha kama Medvedev na Putin wa Russia ambao wanatawala tangu miaka ileee kwa kupishana urais na uwaziri mkuu. Ni wazi Mkapa hawezi kuwa waziri mkuu wa Tz lakini ujio wao na ushawishi waliionesha katika vikao vya NEC, kuna dalili jamaa wamejipanga kurejea (au pengine wanashiriki) katika medani za siasa kitu kinacheweza kumweka Sumaye katika ukuu wa nchi na Mkapa akiwa mshauri mkuu endapo jitihada za Lowassa kujisafisha zikishindikana. Swali alilouliza Sumaye juu ya kuchafuliwa Lowassa halikuwa na nia ya kumtetea Lowassa bali kuibua mambo zaidi ili kambi ya Lowassa na ile inayompinga zote zipoteze mvuto katika jamii. Na mbinu hii ikifanikiwa, basi CCM hawatahitaji kuendelea na marafiki wa JK bali watarudi nyuma kuanzia pale Mkapa alipoishia na itakuwa ni return ya Mkapa-Sumaye Era.
   
 2. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binafsi nitafurahi kuliko ikiwa kama ninavyoona. maana era ya mkapa - sumaye haikuwa hivi so labda ukombozi utapatikana.
   
 3. r

  raffiki Senior Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niliwahi usemaa humu jamvini kwa CCM wenzangu..!kuwa sio gamba CCM kuoga au kujimaliza 2012..na kuwa desturi zinaonesha rais mstaafu huwa anaushawishi kwa rais hajaye,nikaanza na JKN kwa Mwinyi na mkapa maana ya alitawara zaidi ya miaka 20, akaja Mwinyi akashawishi kwa kikwete..nikasema sasa ushawishi ni wa Mkapa. CCM wenzangu walinishambulia humu mara sieleweki,mara oooh naota ,mara oooh sijui ndoto za mchana. haya ona sasa gaba limesaidia????je Mkapa ajaanza kugeuka nuru kwenye vikao hadi kupendekeza hoja iishe na ikaisha?tafakari kabla hayachangia hoja ya watu wa JF ni balaa balaa.
   
 4. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mie pia niliwadokeza ujio mpya wa Mkapa ktk medani za kisiasa kupitia uchaguzi wa Igunga. Niliwaambia kuwa Yale yalikuwa maandalizi ya kumnadi mteule wake/wao wa Urais muda ukifika. Ambaye aweza kuwa Maghufuli.
   
 5. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Ntakubaliana nawe kwamba Mkapa anaweza akawa muda huu na ushawishi ndani ya CCM lakini siyo kitaifa. Matatizo mengi CCM na Taifa linapitia ni kwasababu ya utawala wa kibabe na usiofuata demokrasia wa Mkapa. Katika utawala wake amehujumu vyama vya siasa na taasisi huru za kiraia kwa kutumia vyombo vya usalama,matokeo tunayaona sasa kuongozwa na wanasiasa wala rushwa,dhaifu na wezi.
   
 6. P

  Pax JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwa lugha rahisi kabisa hatuhitaji chama kinachoitwa CCM kwa miaka hii, structure yake imeoza kuanzia chini mpaka juu. Tunahitaji uongozi usio na network za kimaslahi, CCM inatakiwa ife halafu izaliwe upya.Hakuna jema linaweza kutokea humo hata kama kuna watu wanaweza kuonekana kwa sura ya nje kuwa ni wasafi. Hakuna kiongozi ambaye wananchi wamewahi kuwa na imani naye kama huyu wa sasa, lakini wote tumeona nini kilichotokea. Inahitaji akili za uwendawazimu kabisa kujipa matumaini kuwa Tanzania inaweza kupata kiongozi mzuri kutoka CCM. Enough is enough!

  Chama kinachotaka kutawala hata kwa kutumia mabavu kimepoteza taswira yake kwa jamii. Hapana jamani, tunahitaji kuanza upya sasa. Ningeona CCM bado ni chama cha maana kama wangeruhusu wananchi waunde katiba wanayotaka, tuwe na chaguzi huru, wezi wa mali za umma washitakiwe kwa mujibu wa katiba n.k. Lakini hawataki ili waendelee kutuongoza tu, wabadilishane madaraka na wototo wao miaka nenda rudi kwa njia za hila?

  Naunga mkono kundi la " KATIBA YA WANANCHI", wewe je?
   
 7. k

  king11 JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kuna kitu kimoja wameunganishwa nacho ni kupinga kauli ya UVCCM wa pwani waliosema rais ajaye hawezi kutoka kaskazini na jk ndio anayejua rais ajaye
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  PAX,
  Umenena vema rafiki.
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Nashangazwa na kuhuzunishwa sana na usahaulifu, ubinafsi na upofu tulionao. Mkapa huyu-huyu ni moja ya vyanzo vikuu vya ufisadi Tz....leo hii mtu anadiriki kusema ni zamu yake ku-influence ccm candidacy for 2015. Tuhurumieni wananchi jamani.

  Kama kuna maslahi binafsi ndani ya hizo sarakasi za ccm kwenu sawa, lakini inatosha sasa. Tanganyika kwanza.
   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Ronald Reagan

  ni kweli PAX amemaliza kila kitu
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Kikwete woga utamponza...
  anataka kuua nyani huku anawatazama usoni...
   
 12. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hawatamwasha salama. Ndugu zake JK wanasema "Akuanzaye, mmalize" Namwonea huruma ritz1 maana baada ya ngwe ya Baba yake, mtawala yeyote ajaye lazima ale naye shubiri sahani1
   
 13. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sumaye,Lowasa,Slaa wote from kaskazini.Sijui itakuwaje hapo!
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ndani ya siasa za magamba mnaona hivyo,otherwise walitakiwa wajibu mahakamani wizi.
   
 15. U

  Umsolopogas JF-Expert Member

  #15
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wacha mbwembwe zako. Uafazali unauona wewe. labda enzi zake na wewe ulikuwa mzee wa vijisenti. Maana kwa uhakika Mkapa alilima shamba, akapanda Ufisadi, tena wakati wa kiangazi, akaumwagilia, Ukaota na kukuwa kuwa mti mkubwa, kala matunda yake mpaka akatosheka na kuwagawia wanawe na majirani pia. Kama muachia mwenzie kwa shingo upande manake alitaka hata wajukuu wale kidogo. Mwenzie alichofanya ni kuendeleza na kulipanua hilo shamba. Kama maunvi naye akiingia naye agenda itakuwa hiyo hiyo. Ingawa nasikia yeye itakuwa mbaya zaidi. Manake jamaa akitembea barabarani harafu shillingi ikaanguka chini akisikia mlio husema achaaaa. Yangu Hiyo. Anafikiri kwamba ana haki miliki ya hela yote nchi hii.
   
 16. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Sumay na Mkapa wametuma ujumbe kwa Lowassa. Tufuate sisi tutakusafisha na tutakupa kacheo lakini si uraisi au baki na rafiki yako Kikwete halafu uone utaishia wapi?. Lowassa ingawa alikuwa mpinzani mkubwa wa sumay hana njia bali kujiunga na sumay, Mkapa, kingunge badala ya kubakia na kikwete ambaye inaelekea atammaliza kisiasa. Sumay vilevile ataanzankusifia wapinzani na kuweka vizuri mahusiano yake na balozi hasa Marekani. Kuna uwezekano mkubwa tu kwamba sumay anaweza kuwa rasi wa Tanzania!!
   
 17. N

  Nonda JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mwanzisha mada umetuweka nja panda.
  Hivi miaka 34-40 ya Rais kutoka CCM haijatosha?

  Kwa nini tunakazania kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano baada ya Kikwete atatoka CCM?


  Jee tumefikia hitimisho kuwa hatutapata TUME HURU YA UCHAGUZI?


  Tumefikia hitimisho kuwa hakututapata KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO? Katiba itokanayo na wananchi na sio matakwa ya Kikwete na CCM?

  Je Tunataka kusema kuwa hakutakuwa na muafaka wa kitaifa juu ya KATIBA MPYA kama wanaoupigania CHADEMA?

  Bado inaonekana sisi wadanganyika tuko kwenye "love and hate relationship" na CCM na propaganda zao.

  Badala ya kuwaanikia wananchi mbadala bado tunawachanganya kwa kuwaambia wajitayarishe na miongo mengine ya utawala wa "maisha bora kwa kila mtanzania". Kweli CCM na mfumo wao wa propaganda ni kiboko!!!
   
 18. T

  Tanzania Senior Member

  #18
  Nov 26, 2011
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Samahani, nimejaribu kufuatilia post zako, napata wasiwasi na wewe. Issue ni taifa/watanzania au Kikwete? Unakuwa uko concern sana na Kikwete badala ya taifa/watanzania.
   
 19. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Rais ajaye atatoka CCM kwa sababu CCm ikiteua mgombea, kambi zote zinavunjwa (kinafiki au kwa hiari ya moyo) na wote wanaamriwa kuchagua chama na sio mtu. Makundi hutokea kwa minajili ya uchaguzi unaofuata. Hata mpinzani wa mgombea wa CCM atamuunga mkono ili chama kiwe na nguvu ZAMU yake itakapofika.
   
 20. N

  Nonda JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu Crucifix

  Unasema,"Rais ajaye atatoka CCM". Huu ni utabiri wako au tayari umepata siri ya mkakati wa usalama wa Taifa(usalama wa CCM) na tume ya uchaguzi?

  Wewe utapigia kura yako CCM? Ninasoma kila leo hapa JF kuwa CHADEMA wana nguvu ya umma, huu umma utapigia kura mgombea wa CCM?

  Mkuu kama wewe sio CCM basi umekata tamaa mapema! Au umeshapata "maisha bora" wewe?

  Hivi hakuna mbinu ya kuzuia uchakachuaji wa kura na matokeo ya uchaguzi?

  Kwa maisha yalivyo bora Tanzania hakuna mwenye uzalendo na uchungu na TZ na ambaye hana faida binafsi na CCM atakayeipigia kura ya ndio CCM.
   
Loading...