The Relocating dilemma

Shishi

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
1,242
39
Hey good pple,

Ningependa kujua maoni yenu kuhusu the need to relocate mkikubaliana kuonana na kuanzisha familia. If you are a professional woman/man and living in different cities or countries and would like to start a family... who should relocate. my take is that familia za siku hizi mama yuko bongo baba yuko Majuu haziendi vema.. should you really be living together under the same roof to make it work? What should you consider when relocating if you have to? and who should relocate? it seems like its the woman who always has to relocate.
 
Itategemea na makubaliano yenu na mko mbali kiasi gani,
lakini kuishi mbalimbali pia si vizuri kwa sababu wanandoa mnatakiwa muishi wote ili mdumishe ndoa kuishi mbalimbali ndo kunamkaribisha shetani na usaliti ndo unaanzi hapo, pia watoto watakosa mapenzi
mara nyingi huwa wanawake ndo wanahama lakini wakati mwingine hata wanaume wanahama itategemea lakini .mimi binafsi siwezi
 
Inategemea kwanza kama mna mapenzi nikiwa na maana ya mapenzi, pili ni nani ana uchumi mdogo kuliko mwingine, kama mke ana uchumi mkubwa basi mume ahame na kinyume chake.
 
Ndoa kwa mtanzamo wangu ni watu kuishi under one roof and share a life together. Mambo ya kuishi mbalimbali ni choice ya wanandoa lakini haikupaswa iwe hivyo. Nashauri wanandoa waishi pamoja kwa gharama yoyote labda kama wamepatana kuishi separate kwa muda mfupi labda 1 year not more kwa sababu imeshindikana kabisa kuishi pamoja.

Kutokana na mfumo dume, wanawake ndo wamekuwa wanahamia kwa waume lakini sasa mambo yamebadilika. wanaume wamekuwa objective na hoja zinajadiliwa mezani na inayokuwa na mshiko inashinda!!!

Kipato cha mwanandoa mmojawapo, upatikanaji wa shule ya watoto, propspects za kazi bora na mambo mengine ya kuijenga familia yatazamwe objectively kabla ya kuamua nani ahamie!!

Those are my few cents
 
Utandawazi ndani ya mapenzi unatuvuruga akili. Kuna ndoa nyingine zina mbio nyingi huku watu wanaishi pamoja na hawana mpango wa kuhama kwenda popote. Kuna ndoa nyingine wako well organized mmoja yuko Kigali mwingine Dar es salaam.

Ninachokiona hapa ni mipango jenga kati ya wanandoa kukaa chini kuangalia ni vipi wanawezadumisha unyumba wao wakiwa mbali walau kila baada ya miezi kadhaa wakutane. Siyo lazima eti kuishi pamoja ndiyo inazuia watu kutokuplay fyongo.

Kiukweli walioko ndani ya ndoa na wale ambao bado mko ndani ya urafiki, ni vizuri kuweka mikakati ya kukumbushana majukumu na kuweka uwazi fulani kati yenu ili kudumisha familia. Wakati mwingine ubinadamu ni mwingi, inabidi tumuhusishe mungu aweke baraka.

Am sure yote yawezekana.
 
...Ningependa kujua maoni yenu kuhusu the need to relocate mkikubaliana kuonana na kuanzisha familia.

...i dont believe there is a need to, unless the circumstances wants you to be together whatever the consequences... (mfano; mimba/mtoto akizaliwa)

otherwise;

should you really be living together under the same roof to make it work?

...too much hassles za nini kununiwa siku nzima bila sababu, ...kama naweza ku sms, chat kwenye msn messenger, kuonana nae kwenye web cam yatosha.

What should you consider when relocating if you have to?

...location location location! ...living costs, comfortability, na accessibility ya huduma muhimu.

and who should relocate?

...mytake; neither of the us, stay at your place and i stay at mine, tukikutana (at a fixed time) honeymoon inaanza upya!

it seems like its the woman who always has to relocate.

...habibty, 'paukwa pakawa' hizo, hakuna sheria inayolazimisha hivyo.
 
Inataka nyote muwe mnaaminiana sana ili kuishi mbali mbali pamoja na kuwa wana ndoa. Kuna vishawishi vingi sana ambavyo vinaweza kabisa kusababisha kutembea nje ya ndoa. Wapo wana ndoa ambao wanaishi mabara tofauti na ndoa zao zinaendelea bila matatizo lakini bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.

Wengi wamesema hapo juu kwamba yule mwenye kipato kidogo ndiye anayestahili kuhama, na mimi nawaunga mkono. Pia kuna umuhimu wa kuangalia wapi kuna more opportunities, low crime rate, quality of life, mtakuwa mnaonana mara ngapi kwa mwaka, je, gharama za kusafiri kwenu mtaweza kuzimudu bila matatizo?

Kuna unafuu kidogo kama hamna watoto lakini mkishajaliwa watoto maisha yanakuwa magumu. Kila la heri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom