Think Global RC
Member
- Mar 5, 2008
- 23
- 1
huyu jamaa ni mweupe mazee,chungulia hapa mkuu
http://www.afdevinfo.com/htmlreports/peo/peo_378.html
http://www.afdevinfo.com/htmlreports/peo/peo_378.html
Namjua sana huyu jamaa yaani ni ombaomba anamshinda hata Matonya!Niliwahi kukutana nae wakati fulani mitaa ya Salamander nilikuwa nimesimama namsalimia ndugu Ahmed Saggaf wa Salamender akajibalaguzabalanguza akamganda Ahmed wakaingia Salamander. Siku mbili zilizofuatia nikakutana nae mitaa ile ile akaniomba nimnunulie chai ( ilikuwa mida ya asubuhi ) niliona haya nikampa vijisent ( sio vya chenge ) akanywe hiyo chai.
Siku ya pili akaniona mchana akaniganda anataka nimnunulie chakula cha mchana! nilimuuliza jamaa mmoja hivi huyu mtu vipi?akaniambia huyo ni mwandishi wa habari wakati ule alikuwa Habari Cooparation sijui ss yupo wapi.
Hayo malipo yalikuwa kwa kazi maalum. Usikute katika hayo majina la Shy lipo pia! hehehehe namiss sana rafiki yangu kada mpinzani.
sitaacha kulia na hii namba mpaka kieleweke
GRAY S. MGONJA
Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.
Nilivyomuelewa mwandishi hiyo ya kumalizana ni uelewa wake ya yale aliyoyasema Pinda. Quotation ya Pinda ni hiyo niliyoibold kwa rangi nyekundu. Bado ni vitu viwili tofauti. Mwandishi amemwekea maneno Pinda kinywani. Na zaidi ya hayo maneno aliyoyasema Pinda sijui wenzangu mlitaka aseme nini? Tukitilia maanani yeye akiwa ni waziri mkuu katika serikali hii! Sidhani kama ushauri wa kumng'oa au kutokumng'oa Chenge anaweza kuutoa hadharani kabla ya bosi wake kutoa tamko. Anafuata utaratibu wa kufanya kazi na si kumkingia mtu kifua. Hawezi kuamka mbele ya kadamnasi na kusema kuwa nimemshauri Rais amtimue kazi mara moja hata kama alifanya hivyo. Ni lazima uamuzi kama huu uonekane umetoka kwa aliyemteua na si mwingineyo katika uongozi.Ndivyo ilivyo.
1.Vyanzo hivyo vya habari vilidai kuwa mkataba huo ulisainiwa na mawaziri hao wawili kutokana na jinsi ulivyokuwa umeendaliwa licha ya ukweli kwamba ulikuwa ukihusu zaidi wizara moja.
Walidai kuwa mkataba huo uliokuwa ukihusisha masuala ya wizara ya miundombinu, katika mazingira yasiyoeleweka ulianza kusainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na kisha kusainiwa na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge.
.
licha ya ukweli kwamba ulikuwa ukihusu zaidi wizara moja.
kama tukitaka kila mmoja awajibike nani atabaki,read between the lines what is posted kabla ya kutoa quote yoyote.na hatachukua hatua zozote za uwajibishaji