The Radar Scandal: Investigation & Progress

Mtu Ukiwa Na Hela Zako Tatizo Usipokuwa Nazo Tatizo Kweli Waswahili Noma Sasa Wanaandamana Ili Iweje ? Kwa Faida Ya Nani Mkoa Wa Dodoma Upo Nyuma Sana Kimaendeleo Na Kielimu Wafikirie Mambo Hayo Kwanza Kabla Ya Mengine Yote Waache Longo Longo
 
YAPO mambo mengi aliyozushiwa Andrew Chenge, Waziri wa Miundombinu ambayo mengi watu waliyaona kama mambo ya mtaani tu. Kwa mfano, niliwahi kusikia Chenge alikuwa akisafirisha suti zake kwa DHL kwenda London, Uingereza kufuliwa.

Hii ilikuwa wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiamini Tanzania kulikuwa hakuna kampuni ya kueleweka ya ufuaji nguo.

Lakini pia lipo jingine la kilimbukeni alihusishwa nalo; kila alipokuwa akisalimiana na watu alitafuta upenyo na kwenda kunawa mikono yake na kupaka mafuta laini.

Chenge alipata kuhusishwa na ukiukaji wa misingi ya utendaji, alipokuwa kiongozi wa Salander Bridge Club. Inadaiwa baada ya kushindwa kwa muda mrefu kuitisha mkutano wa wanachama, baadhi ya wanachama waliamua kujiorodhesha ili kushinikiza mkutano uitishwe.

Wakati orodha hiyo ikiwa ukutani na watu wengine wakihamasishwa kujiandikisha ili kumlazimisha bwana mkubwa kuitisha mkutano, Rais Ali Hassan Mwinyi alimteua Chenge kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Habari zinasema kutokana na unafiki wa Kitanzania, orodha ile ilipotea kitatanishi. Hakukuwa tena na shinikizo la kumtaka aitishe mkutano kwa sababu si tu kwamba ujasiri wa wanachama ulikuwa umeyeyushwa na madaraka mapya aliyopewa, bali sasa wengine walianza kukaa mkao wa kupata lolote kutoka kwake.

Hayo ni simulizi. Haya yanayofuatia, nina uhakika nayo maana niliyashuhudia. Kwamba Chenge amejaa kiburi si jambo la kuuliza! Ni kiburi kikubwa kwani aliwahi kukionyesha kwa wabunge kati ya 1995-2005 akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Nitaeleza machache.

Baada ya Bunge kupitisha sheria ya kuvunjwa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na kuundwa NBC 1997 Limited na National Microfinance Bank (NMB) mwaka 1997, pamoja na kuanzishwa kwa kampuni tanzu ya NBC Hodings Limited ili kusimamia mali za iliokuwa NBC ambazo hazikugawiwa kwa NBC 1997 wala NMB, ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilicheza faulo.

Faulo hiyo ni kutunga sheria kinyemela kwa kuiondoa iliyokuwa National Bureau De Change kutoka NBC Holdings ili ionekane kama ni taasisi inayojitegemea.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilijipa jukumu la kupora Bureau kinyemela bila shaka, ili kujinufaisha katika harakati za kupora mali za umma zilizopamba moto wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa. Wabunge makini akiwamo Philip Magani, wakati huo akiwa ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, na Arcardo Ntagazwa, walishtukia suala hilo na kuwasha moto mkali bungeni.

Baada ya Bunge kuchunguza suala hilo, ilithibitika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliingilia kazi za Bunge kwa kurekebisha sheria bila ya kuifikisha bungeni, ikilenga kupora Bureau hiyo iliyokuja baadaye kuwa Twiga Bankcorp. Wabunge walichachamaa wakitaka maelezo ya serikali.

Nakumbuka Waziri Mkuu wakati huo, Frederick Sumaye, alisimama na kuomba radhi kwa niaba ya serikali kuhusu ukiukwaji mkubwa wa taratibu uliotokea na kuahidi kurekebisha kasoro hiyo. Sumaye alikuwa muungwana ambaye kwa mara ya kwanza katika kipindi cha utawala wake nilimuona akiwa mkweli kwa alilokuwa akilisema.

Lakini pamoja na hatua ya Sumaye, Chenge aliibuka. Akasema, "kiti cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kimejaa!" Kebehi iliyoje dhidi ya wabunge pamoja na Waziri Mkuu aliyekuwa ameshasawazisha kasoro.

Kiburi cha Chenge kilijidhihirisha jinsi asivyoheshimu Bunge, wabunge na hata Waziri Mkuu amabye ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.

Katika hali ya kawaida, Sumaye alikuwa na kazi moja tu, kumwomba Rais amuondoe Chenge kwenye wadhifa kwa kuwa alikuwa anafanya kazi yake kuwa ngumu. Hili halikufanyika, Chenge akaendelea kutesa hadi bwana mkubwa Mkapa alipomaliza kipindi chake Novemba 2005.

Baada ya kusikia hivi karibuni Chenge anachunguzwa kwa ukwasi aliojiwekea kwenye kisiwa cha Jersey, Uingereza akiwa na zaidi ya dola milioni moja za Marekani, kwenye akaunti yake, nimeanza kujua kiburi cha ofisa huyu kinakotoka!

Ni kiburi cha mtu aliyeshiba na kuvimbiwa, na unajua ukivimbiwa kuna uwezekano mkubwa wa kuharibu hali ya hewa. Chenge hakumtii Sumaye wala wabunge wa chama chake. Hakuwa na sababu za kuwatii maana yeye na bwana mkubwa walikuwa wanaruka mruko mmoja wa ndege wenye mabawa (manyoya) ya kufanana.

Bwana mkubwa Mkapa naye ukwasi wake haramu umekuwa ni mapambo kwenye magazeti ya Tanzania kwa zaidi ya mwaka sasa. Yeye (Mkapa) ameamua kukaa kimya. Kiburi kile kile cha swahiba wake. Kiburi cha ukwasi, cha kupumua, cha shibe, shibe iliyomlevya kiasi cha kushindwa kujua yeye ni Mtanzania na kwamba kujilimbizia fedha nyingi kiasi hicho ughaibuni ni usaliti kwa nchi masikini kama Tanzania.

Chenge alipochaguliwa kuwa waziri na Rais Jakaya Kikwete Januari 2006, watu walijiumauma na kuuliza, inakuwaje Kikwete ampe uwaziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Chenge wakati zikiwapo tuhuma nyingi mitaani za uchafu unaomgusa.

Mikataba kama ya IPTL, uuzaji wa NBC iliyotolewa kwa Makaburu wa ABSA sawa na bure! Watu waliguna lakini Rais Kikwete naye si tu alipuuza miguno yao, aliwazaba kibao wananchi mwaka jana alipofanya marekebisho madogo katika baraza lake la mawaziri kutokana na kuchemka kwa sakata la Richmond. Chenge aliondolewa Afrika Mashariki na kupelekwa Miundombinu, wizara nyeti na yenye kazi kubwa ya kujenga barabara ambazo ni kilio cha kudumu kwa wananchi na wawekezaji.

Hakuishia hapo tu. Alipolazimika kuvunja baraza la mawaziri ya Edward Lowassa na mawaziri wawili wengine kujiuzulu, kutokana na sakata lilelile la Richmond, Rais Kikwete alimrejesha Chenge pale pale miundombinu katika baraza jipya! Miguno mipya ikaendelea kuzizima.

Sasa Waingereza wametusaidia kumweka hadharani Chenge kuhusu namna alivyopata ukwasi mkubwa. Shaka iliopo si ya kwamba amepataje ukwasi huo, bali pia kwa kuwapo uwezekano wa kuhusiana na mabilioni ya rada iliyouziwa Tanzania kwa bei ya juu na Waingereza haohao wa kampuni ya BAE Systems.

Chenge yuleyule wa kusafirisha suti kwa DHL kwenda kufuliwa Uingereza, hadi kuogopa kuchafuliwa mikono kwa sababu ya kusalimiana mpaka kwa Chenge wa kiburi kwa Waziri Mkuu na wabunge, ni Chenge huyohuyo wa kumiliki ukwasi wa kutosha kula hadi aingie kaburini.

Haya yote yakitokea, Chenge anawajibika kueleza umma alivyopata ukwasi huu. Ni vema akatambua kuwa wakati umefika wa kuwa muungwana na kutambua kuwa ulevi wa ukwasi unaompa kiburi hautamsaidia kitu. Angeamua tu kuachia ofisi ya umma akaendelea na yake. Chenga na kiburi, safari hii havitamponya!

Source: Mwanahalisi
 
Jamani, kwa wenye kujua mambo hebu tuambieni hawa waliopata faraja ya mshiko toka kwa paymaster general ni kina nani hawa, kwa nini wao, je kulikoni?


Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.

Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.

Namjua sana huyu jamaa yaani ni ombaomba anamshinda hata Matonya!Niliwahi kukutana nae wakati fulani mitaa ya Salamander nilikuwa nimesimama namsalimia ndugu Ahmed Saggaf wa Salamender akajibalaguzabalanguza akamganda Ahmed wakaingia Salamander. Siku mbili zilizofuatia nikakutana nae mitaa ile ile akaniomba nimnunulie chai ( ilikuwa mida ya asubuhi ) niliona haya nikampa vijisent ( sio vya chenge ) akanywe hiyo chai.

Siku ya pili akaniona mchana akaniganda anataka nimnunulie chakula cha mchana! nilimuuliza jamaa mmoja hivi huyu mtu vipi?akaniambia huyo ni mwandishi wa habari wakati ule alikuwa Habari Cooparation sijui ss yupo wapi.

Hayo malipo yalikuwa kwa kazi maalum. Usikute katika hayo majina la Shy lipo pia! hehehehe namiss sana rafiki yangu kada mpinzani.
 
Jamani chenge tayari ametajwa na wanashughulikia sasa hawa waliopewa tuwatafute ili tuwamalize serikali wakose pakufichia uovu hebu wanaowajua watoe wasifu wao ili tuwamulike waliko watueleze walilipiwa nini na kwa kazi gani.

huyo wa salamander ndiko chenge alikoiba kwahiyo aliwapa hakika hiyo pesa maana link imetoka huko huko.
tupeni mengi kuhusu majina hayo.
 
Kuna mtu mwenye Ratiba ya Bunge..Mie nadhani Mhe. Chenge anaweza asiende Bungenei coz hakuna mjadala wa kujibu ,na kwa sababu alishajua hili atabakli tu hapa.

Mie nataka waaandamane pindi rais akiawa anatua leo au kesho kama sikosei,apate ujumbe
 
Jamani chenge tayari ametajwa na wanashughulikia sasa hawa waliopewa tuwatafute ili tuwamalize serikali wakose pakufichia uovu hebu wanaowajua watoe wasifu wao ili tuwamulike waliko watueleze walilipiwa nini na kwa kazi gani.

huyo wa salamander ndiko chenge alikoiba kwahiyo aliwapa hakika hiyo pesa maana link imetoka huko huko.
tupeni mengi kuhusu majina hayo.

WENYE KUWAJUA HAO WENGINE KAMA MARY CHITANDA WATULETEE DATA ZAO NASIE TUWAJUE ILI TUKIWAONA TUWASANIFU.

MIE NINAMJUA HUYO LIVINGSTONE NA NIMETOA HINTS ZAKE SASA WANAJF MNAOWAJUA HAO WENGINE TUPENI WASIFU...
 
NDIO AMESHTAKI,KESI HIKO MAHAKAMA KUU NA IMEPANGIWA JAJI SHAHIDI,INAANZA KUSIKILIZWA MWEZI WA SITA.BRAVO NCHIMBI DAI HAKI YAKO KWA MANYANGAU,HUNA CHA KUPOTEZA.


Jamani, unawashangilia mafisadi, mi nakuogopa mwee.
 
Heshima Mbele,

KWa takribani wiki moja nimekuwa nikitafakari mwenendo mzima wa siasa ya chama cha mapinduzi hasa kundi linaloitwa mtandao,toka wakati RA anataka kuwasilisha hoja yake Bungeni na kukataliwa.Kuibuka kwa kashfa ya Chenge na majibu aliyoyatoa chenge wakati akiongea ana waandishi wa habari wakati akitokea china.

majibu aliyayatoa chenge ya kuchafuana na kutolea kashfa yanafanana kabisa kimaana amajibu aliyoyatoa lowassa wakati akitangaza bungeni kauchia ngazi

ukiangalia kwa undani utaona chenge alieegemea sana upande wa Lowassa wakati wa scandal ya RDC,na yeye alipinga wazi wazi kwamba Lowassa ameonewa.

ukijumulisha mambo yote hasa,Kung'oa kwa Lowassa ,then Chenge naye anashinikizwa kujiuzuru unaweza kuona utabiri wa Mwalimu umetimia.CCM inaanza kuyumba sababu watu wote wenye nguvu katika Chama wanahusishwa na Rushwa isiyosemeka.Je Jk ameamua kuwatosa rafiki zake.Hii inaashiria nini?

sikatai kwamba Chenge ameonesha dharau ya khali ya juu,na kiburi ambacho sijui anakitoa wapi,yawezekana pesa zikawa za kwakwe kutokana na biashara anazofanya,kama kweli sheria ya maadili ya uongzoi wa umma inaruhusu kiongozi kufanya biashara.ila kuna jambao hapa na ianweza ikawa mtaji mkubwa sana kwa wenzangu wenye itikadi tofauti.Mie nasubiri uchunguzi ukamilike ili kuweza kubaini kama ni kweli chenge anamiliki kiasi hicho cha pesa.

ila kuchafuana huku kwa wana CCM ambapo nidhamu ya Chama imepungua,kumetoka wapi.Je CCM inataka kugawanyika vipande viwili??

Mie nadhani anguko la tatu la Lowassa ni hili hapa na kwa hakika kuna kundi fulani linataka kuingia.

naomba kutoa hoja.
 
Ila wenye system nimeongea nao wanasema bilion moja ni pesa kidogo kwa mtu mwenye wadhifa kama wa chenge.

Nilikuwa naongea jana na mtu wa ofisi ya raisi utawala bora akasema Chenge amekuwa kwenye uongozi wa juu kwa miaka 30, akaniuliza unajua posho ya mwanasheria mkuu kwa siku akiwa safarini nje ya nchi?.
Nikasema sijui akaniambia thatha mbona unapiga kelele tu, kwa wadhifa wa chenge anaweza kuzipata hizo pesa kihalali kabisa.
Akasisitiza kuwa watanzania tunapenda kudakia mambo bila kufanya utafiti wa kina.
Tulibishana sana, mwisho nikamwambia ukweli daima hujitenga.
 
Nahisi alikosa courage tu ya kumalizia statement yake pale aliposema kuwa hizo hela zake ni 'vijisent tu'.....I believe deep down in his heart alitaka kumalizia kwa kusema 'ukilinganisha na wenzangu'

Nakubaliana na wewe mkuu kwa kweli ukilinganisha na za wenzake anaowajua chenge hasa akiwa AG, vya kwake ni jijisenti tu, ndio maana anaona kama tunamuonea bure mbona mafisadi wenyewe wapo.

Mi nadhani twende nae taratibu atatuambia mengi, maana kama ex- AG anajua siri nyingi za nchi hii, na mafisadi anawajua sana kuliko sisi tunavyohisi.
 
Wakati umefika sasa kwa viongozi kujua wao ni watumishi wa wananchi na wala sio watawala wa wananchi. Wajue kwamba wanawajibika kwa wananchi na sio kinyume cha hapo. Katika demokrasia nyingi pevul, viongozi huwa wanaogopa sana hasira ya wananchi, na hufanya bidii kwenda na maadili ya kazi. Tofauti na nchi yetu, wananchi ndio wanawaogopa viongozi kana kwamba wadhifa waliopewa nao wamepewa na Mungu!
 
Mtu Ukiwa Na Hela Zako Tatizo Usipokuwa Nazo Tatizo Kweli Waswahili Noma Sasa Wanaandamana Ili Iweje ? Kwa Faida Ya Nani Mkoa Wa Dodoma Upo Nyuma Sana Kimaendeleo Na Kielimu Wafikirie Mambo Hayo Kwanza Kabla Ya Mengine Yote Waache Longo Longo


Hizo pesa alizozikomba huyo Chenge zisaidia katika kuuinua kiuchumi mkoa wa Dodoma. Hawa mafisadi ndio wanasababisha hali duni ya maisha ya wananchi wa Tanzania. Ana raha gani na hizo pesa wakati wajomba zake kule Bariadi hata umeme, shule na huduma bora za afya ni ni duni achia mbali upatikanaji wa maji safi ya kunywa.
 
Kwani Kuna Ushahidi Wowote Au Kuna Mtu Wowote Aje Mbele Na Akiri Kweli Pesa Na Mali Za Chenge Sio Halali

Hata Mengi Akiingia Katika Siasa Nae Ataitwa Fisadi
 
Kwani Kuna Ushahidi Wowote Au Kuna Mtu Wowote Aje Mbele Na Akiri Kweli Pesa Na Mali Za Chenge Sio Halali

Hata Mengi Akiingia Katika Siasa Nae Ataitwa Fisadi

Unachanganya mambo. Mengi na Chenge ni vitu viwili tofauti. Tunajua Mengi anauza magazeti, soda, maji ana TV na radio stations. Hujasikia Chenge anamiliki biashara gani. Kama wazijua hizo biashara ziweke hadharani, tumsafishe.
 
mi ningekuwa ni mwanamuziki ningewatungiwa wimbo hawa mafisadi...then ningetengeneza video safi tu.Halafu kwenye video yangu,pale Chenge alipoita bilioni ni vijisenti,pia ningechomeka video ya wanafunzi wanasomea chini ya mti,au wakina mama wanakwenda kuchota maji au kukata kuni...then ningeuliza kama hizo bilioni ni vijisenti,kwa nini kilio cha serikali kila siku ni kuwa haina pesa kuwaondolea kero,ni vijisenti vingapi hivo wanaongelea?
 
Ukiambiwa Ana Hisa Celtel Na Voda Com Utakataa ? Ukiambiwa Yeye Ni Kati Ya Wenye Uwekezaji Mkubwa Katika Banki Ya Akiba Commercial Utakataa ??
 
Napenda tujikumbushe maana upo uwezekano wa wana-CCM kubweteka. Kwa vile tunajua chama chetu kina nguvu na mvuto, hatuweki mkazo mkubwa kwenye kujinoa binafsi. Badala yake tunapigana vikumbo kutafuta kuteuliwa, kwa kuamini ukishateuliwa ndio “umeula”. Na tukishaelekea huko, hakutakuwa na kingine kinachotusukuma ila ubinafsi—ubinafsi wa kusema mimi lazima niendelee, na anayenisogelea ni adui; au ubinafsi wa kusema wewe sasa imetosha, sasa ni zamu yangu.
Benjamin Mkapa, 2004
Nasema ninyi ndio Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi. Hatma ya CCM na Taifa letu imo mikononi mwenu. Jiulizeni: Kama kweli hiyo minong’ono ni ya kweli, hivyo ndivyo mnavyotaka iwe? Ndio mustakabali wa Chama chetu mnaoutaka—kwamba maslahi binafsi yawe na nguvu kuliko maslahi ya CCM na Taifa?
Benjamin Mkapa, 2004

Mkapa aliuliza hayo maswali wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu mwaka 2004.

Hebu tuangalie maono ya Mzee mkapa while we make other thing of Mr. Clean Constant.
Nasema sisi katika Halmashauri Kuu ya Taifa, wenye jukumu la kusimamia maadili, lazima tuwe mfano wa kufuata maadili, mfano wa kuheshimu Katiba; mfano wa kuheshimu haki za kila mwanachama. Agombeaye nafasi si adui. Na tusisahau kuwa sifa moja ya kiongozi iliyo ndani ya Katiba ni kuwa, “Awe ni mtu aliyetosheka, na asiwe mtu aliyetawaliwa na tamaa.” (Katiba ya CCM, (17(1)). Aliyetawaliwa na tamaa yuko radhi kuhujumu haki za wengine kugombea, yuko radhi kuwazulia kashfa anaowaona ni washindani wake, na yuko radhi hata kuhujumu maslahi ya Chama, ili mradi tu apate anachokitamani.
Benjamin Mkapa, 2004
 
Ukiambiwa Ana Hisa Celtel Na Voda Com Utakataa ? Ukiambiwa Yeye Ni Kati Ya Wenye Uwekezaji Mkubwa Katika Banki Ya Akiba Commercial Utakataa ??
Akiba Commercial ???

Pesa Za kuwekeza huko alizitoa wapi? alikopa??
 
Back
Top Bottom