The Radar Scandal: Investigation & Progress

Jamani Kuna Akinachenge Wangapi Huko Katika Serikali Ya Msanii
Ah Masikini Wadanganyika Chamoto Tunakiona Na Kufa Tuna Kufa
 
Hivi mwanasheria mkuu wa serikali,DCI si ndio wanatakiwa sasa kujump in wakisikia kashfa kama hizi au wanasubiri muungwana aunde tume? kweli culture ya ufanyaji kazi wetu ndio inatuponza maana hao jamaa sijui kazi yao ni nini kama hawawezi kusadia vitu kama hivi.
 
Hivi mwanasheria mkuu wa serikali,DCI si ndio wanatakiwa sasa kujump in wakisikia kashfa kama hizi au wanasubiri muungwana aunde tume? kweli culture ya ufanyaji kazi wetu ndio inatuponza maana hao jamaa sijui kazi yao ni nini kama hawawezi kusadia vitu kama hivi.

Wao wenyewe wana skendo zao zinasubiri zinatafuta jinsi ya kutoka halkafu wajamp kwenye skendo ya mtu mwingine. Hii issue kama ingekuwa ya mtu mdogo wangekuwa wameshamkamata. Sijui Prof. Mahalu anajisikiaje sasa baada ya kupata mwenzie.
 
chenge sauti ya watu ni sauti ya mungu...hapa maji yalipokufikia hata ukitumia milungula haitafua dafu....tafadhali achia ngazi mzee ule hivyo vijisenti na watu watakusahau taratibu maana ndio zetu waTZ.....Duh yule binti yako alivyo mzuri natamani ningekuja wakati huu kumchumbia najua ungenipunguzia bei
 
Nahisi alikosa courage tu ya kumalizia statement yake pale aliposema kuwa hizo hela zake ni 'vijisent tu'.....I believe deep down in his heart alitaka kumalizia kwa kusema 'ukilinganisha na wenzangu'

...duh, ebwana weeeeh, hii without a doubt ni kali ya mwezi huu, chonde chonde spin doctors wasijebadilisha hili skendeli na kusema 'mheshimiwa' alishinda jackpot kwenye lottery huko, au accumulation of consultancy fees alizokuwa analipwa kwenye legal practices!

hawashindwi hawa kutuacha midomo wazi!
 
Kitu kimojawapo kibaya cha ufisadi ni kwamba pesa zinapelekwa nje ya nchi na zinasaidia nchi tajiri.Kama pesa zote za uizi zingebaki Tanzania zingesaidia sana kiuchumi. Kitu kingine ambacho watu wengi hawakiongelei ni kwamba ufisadi umekuwa culture na kwa wakati mwingine hakuna sababu muhimu ya kuiba zaidi ya culture ya kufikiria ukiweza kuiba iba bila kuwa na sababu ya msingi. Mafisadi wengi watakufa bila kutumia hizo fedha na ndugu na watoto wanaoachiwa pesa za wizi hawaendi mbali na pesa za laana. Kama watoto wako huwapi discipline na elimu na watafanikiwa kwenye hali yeyote. Pesa zitaisha kwenye kizazi kimoja tu!!
 
yesuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu Naaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Maaaaaaaaaaaaaaaaariaaaaaaaaaaaaa Uwiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mmesikia Jamaa Kadai Miaka Kumi Ya Uanasheria Mkuu Inamtosha Kuwa Na Hela Haya Mzee Mwanyika Kazi Kwako Kumi Ujafikisha Uko Kwenye Epa Ukifikisha Kumi Si Utakuwa Na Trillion....mi Bado Nakuhesabia Miak Inaonekana Hiko Cheo Kizuri Sana Jamani Kwa Mwaka Mmoja Inaamana Anapokea Million Miamoja Yaani 100,000,000 Uwiiiiii Kama Hivyo Ana Haki Ya Kuwa Na Billion Kwenye Acc Jamani Tena Hizo Ni Vijiisent Mlivyovijua Msivyovijua Na Nyie Wakubenea Hamwachi Kitu Si Mtamuuuaa Mzee Wa Watu Maana Alivyoondoka Na Jk Tofauti Na Alivyorudi Inaoonekana Afya Imeshaanza Kuchoka Na Kashfa Za Acc Zaker Jinsi Watu Walivyozishugulikia....jf Tusiache Kitu
 
Richard Kasema Hata Na Wala Hafikiriim Kujiuzulu Kwa Hiyo Swala La Kujiuzulu Na Imani Liko Kwa M,uungwaaana Na Wananchi Kazi Kwenu
 
Asijiuzulu maana akijiuzulu ataitwa "ajali ya kisiasa" halafu case closed kama Lowassa na wenzake waliohusika na Richmond. Mwacheni abaki hapohapo mengi yazidi kutoka
 
Ukweli wa kauli ya vijisenti kwa alivyoitoa ni kuwa wako ambao wamemshinda au hicho kiasi cha fezwa aliyokuwa nayo yeye si lolote si chochote ukilinganisha na wengine ...hapa napata picha kuwa huyu jamaa huenda amekamata guruneti alilokwisha lifungua just ametuliza kidole kwenye ufuniko , sasa sijui nani aliepigwa dongo lile ,hivi ikiwa huyu Chenge anamiliki kiasi ambacho mwenyewe amekiita " vijisenti" Je Mkapa atakuwa anamiliki kiasi gani maana Nkapa yeye ndie alikuwa amefungua genge kabisa pale Ikulu wateja wakiingia kuuza na kununua....huyu nae aanze kuweka maji kwenye kichwa !!! Kikwete na Pinda mnayo kazi !
 
Chenge hawezi kujiuzuru kwani sio tamaduni ya viongozi wa dunia yetu ya tatu. Chenge ataendelea kuwakejeli walipa kodi( waajiri wake) kwa kufahamu kwamba hakuna atakae mtisha.

Jakaya nae hawezi kumfanya kitu kwani nae analinda heshima ya CCM, Makamba nae amabe ameshindwa kumnyang'anya kadi ya chama sababu anatunza heshima ya CCM. Sasa ukiangalia haya yote utagundua kwamba kuna kitu kinaitwa status quo ndio inawafanya hawa viongozi wasimdenounce huyu Chenge.

Poor Tanzania
 
Naona picha kama la French revolution vile,

Watu wanakula msoto, watawala wanakula raha, mara watu wanalalamika hawana mkate, malkia anaripotiwa kuwaambia wale keki, next thing chinja chinja linaanza.

Hivi Chenge ana akili timamu kweli kuziita hizo hela "vijisenti"?

Arrogance nyingine ni ujinga mtupu.

Kwa kweli Chenge kwa lugha yake hiyo ametutukana sana watanzania wenzake tunaoishi maisha ya chini ya dola moja ya kimarekani kwa siku. Pia ametupa clue kwamba ana matrilioni somewhere,wanaofanya uchunguzi wakitumia hilo neno alilotamka mwenyewe watagundua mengi.Ni wale wale, yule mwingine alituambia tuna kasungura kadogo!!
 
AC afukuzwe/afutwe kazi na si kujiuzulu.
Mkuu wa kaya ulimteua kwa hiyo waweza kumtema pia. Tafadhali JK chukua hatua!
 
Anaviita vijisenti kwa vile alijua pesa inayozungumziwa ni kidogo nyingine hamjaigundua au hamtaigundua .... pia kiburi cha chenge kinatokana ukweli kuwa yeye ndo ameshikila mafaili ya mafisadi wenzie kwa maana ya kushiriki kuidhinisha mikataba mbalimabli toka enzi za BM hivyo anajua atalindwa na JK mwenyewe, BM, mawaziri na makatibu mafisadi wote, TSAKUKURU, Polisi, mahakama na bunge!!!! Hivyo confo ALILONALO SIO LA KAWAIDA!!!

Tukiangalia historia ya matukio ya kufunuliwa kwa mafisadi toka wanaanza kumtaja Balali, Richmond, TICTS, KIWIRA, IPTL, nani kawajibishwa??? Hivyo JK nae anajipa moyo kuwa kelele ya chura haimzuii ... lunywa maji!!!!
 
chenge vile kaviita vijisenti kwa vile ana mara nyingi ya pesa zile kwenye accounts nyengine tele.
 
Jakaya Kikwete ameziba masikio ... kilio cha wananchi kinamfanya yeye azidi kutabasamu tu!!!! Why dont you say something??? Ile kasi mpya tuliyoiunga mkono kumbe ndo mwelekeo wake??? Je, 2010 utatueleza mafanikio ya viongozi wako kujaza mifuko yao kwa mabilioni wakati watu wakitembea kwa miguu kwa kukosa nauli ya daladala na kulala gizani kwa kushindwa gharama za umeme, na kushindwa kupata mahitaji la lazima kutokakana kila bidhaa kupanda kwa ajili ya bei ya mafuta???

Wewe ni rais kwa ajili ya wenye pesa na viongozi wako tu ... sisi wananchi umetuacha siku nyingi
 
Jakaya Kikwete ameziba masikio .....Ile kasi mpya tuliyoiunga mkono kumbe ndo mwelekeo wake??? ......

Did you believe katika ari, nguvu & kasi mpya? Just hopes and dreams .......
Chenge will definetly go, but how? Resign? Be sacked? Lets wait and see.


 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom