The Radar Scandal: Investigation & Progress

huenda kuna uhusiano wa moja kwa moja na ushindi wake wa kishindo kwenye kuira za nec, that means walioko ccm hasa nec walishinda kwa kuhonga

Bila shaka jamaa alipata kura nyingi sana NEC naona hizi Bil 25 zilitumika pia, kama anapeleka suti zake dry cleaner UK kwa DHL na anakunywa maji kutoka France unafikiri nini?

Ushi
 
Waziri Chenge atua Dar,agoma kujiuzulu,asema ni tuhuma za vijisenti
Na Muhibu Said

WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge, jana alirejea nchini akitokea China na kukataa kujibu tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya shilingi anazodaiwa kuzihifadhi katika akaunti nje ya nchi.

Chenge ambaye aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam jana saa 9:00 alasiri na ndege ya Emirates alisema kwa sasa hawezi kuzungumza lolote kwa vile tuhuma zilizotolewa dhidi yake zinachunguzwa.

"Unapotuhumiwa, uchunguzi unafanyika. Na kwa kanuni na taratibu za uchunguzi, siruhusiwi kuzungumza. Kwa sasa ni mapema mno. Tuvipe nafasi vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake," alisema Chenge na kuongeza:

"Ninaheshimu na nitaendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya uchunguzi".

Hata hivyo, Chenge ambaye alizungumza mbele ya jopo la waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi, huku akitetemeka na kujikanganya katika kauli, alisema tuhuma zilizotolewa dhidi yake, ni nzito kupita kiasi, hivyo, hawezi kuzijibu kwa kukurupuka, badala yake anaviachia vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake.

"Hoja ya msingi hapa, ni kwamba, nimelipwa fedha na kampuni ya BAE System (ya Uingereza) katika ununuzi wa rada. Tuhuma hiyo ni nzito kweli kweli na siyo ya kupopoa," alisema Chenge.

Alisema taarifa za kutuhumiwa kwake, alizipata akiwa na Rais Jakaya Kikwete China na amerejea nchini kwa taratibu za kawaida na si kwa kukatiza ziara kutokana na kuelemewa na tuhuma zilizotolewa dhidi yake.

"Nafurahi kurudi nyumbani. Tulikuwa China na Rais na ametuwakilisha vizuri. Tulipokuwa China, ndio tukasikia hizo tuhuma za vijisenti," alisema Chenge.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu tuhuma zinazomkabili za kujilimbikizia zaidi ya Sh24bilioni katika akaunti nje ya nchi kuziita vijisenti, Chenge alisema: "Kila mtu ana viwango vyake na ana haki ya kusema anavyotaka. Na mtu akikutuhumu, unajua nafsini mwako".

Pia hakuwa tayari kabisa kujibu tuhuma za kusaini mkataba wa kampuni ya kuzalisha umeme ya IPTL alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), badala ya kushauri, na pia kujibu tuhuma kuhusu mabilioni ya fedha anayodaiwa kuyahifadhi nje ya nchi kama aliyaorodhesha kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi, badala yake, alisema: "Yote yaliyosemwa na kuandikwa, mimi siyafahamu".

Alipoulizwa kama yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake ili kwa vile ameshatuhumiwa na ili avipe nafasi vyombo vinavyochunguza tuhuma zinazomkabili kufanya kazi yake kwa uhuru, Chenge alisita kutamka suala hilo, badala yake aliishia kusema: "Myonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni" bila kufafanua.

Awali, alisema atatumia fursa ya kuwapo kwake nchini kutafakari tuhuma zote zilizotolewa dhidi yake kisha atawasiliana na mwanasheria wake ili kuangalia uwezekano wa kuvichukulia hatua za kisheria vyombo vya habari alivyodai kwamba, vilivuka mipaka katika kuandika na kutangaza tuhuma dhidi yake.

Alisema atafanya hivyo kwa kuwa tuhuma zilizotolewa dhidi yake, ni nzito na zimelenga kumchafulia jina.

Tuhuma dhidi ya Chenge za kujilimbikizia fedha hizo, ziliibuliwa na gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza katika toleo lake la Jumamosi wiki iliyopita ambalo lilieleza kuanza kwa uchunguzi dhidi ya waziri huyo, kutokana na akaunti yake kukutwa na zaidi ya dola 1 milioni.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, taasisi ya kuchunguza makosa makubwa ya jinai nchini humo ijulikanayo kwa jina la Serious Fraud Office (SFO), inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28, ambazo ni sawa na Sh70bilioni, mwaka 2002.

Gazeti hilo lilieleza katika kuwa uchunguzi huo wa SFO unatarajia kuanza katika kipindi cha wiki sita zijazo.

Kwa mujibu wa habari hizo, uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, moja ya mambo yanayofuatiliwa ni kujua iwapo fedha hizo zinazoaminika kuwa za Chenge, zilizowekwa katika akaunti moja iliyoko katika Kisiwa cha Jersey zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutoka katika Kampuni ya BAE System, inayotuhumiwa kuinyonya Tanzania kwa kuiuzia rada hiyo kwa bei kubwa kuliko ilivyotakiwa.

The Guardian katika habari yake hiyo iliyowekwa katika mtandao wa intaneti, liliripoti kuwa taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.

Gazeti hilo lilimkariri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni mali yake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa AG katika serikali ya awamu ya tatu.

Siku moja baada ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa taarifa rasmi zikifika serikalini kuhusiana na tuhuma hizo, sheria itachukua mkondo wake na kuonyesha kushangazwa kwake iwapo Chenge alizipata fedha hizo kihalali au la.

Siku moja baadaye, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kumtaka Rais Jakaya Kikwete amsimamishe kazi Waziri Chenge na awekwe chini ya ulinzi, wakati uchunguzi wa kina wa mali zake ndani na nje ya nchi unafanyika.

Profesa Lipumba alisema anamfahamu vema Waziri Chenge na kwa hiyo, mshahara na marupurupu ya serikali anayolipwa, havimuwezeshi kulimbikiza kiasi hicho cha fedha katika akaunti.

Kabla ya gazeti la The Guardian kuibua tuhuma hizo, Septemba 15, mwaka jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, walimtaja Chenge katika orodha ya vigogo 11, wakiwamo viongozi kadhaa wa serikali nchini wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi wa mabilioni ya shilingi za walipakodi.

Baadaye, Septemba 19, Waziri Chenge aliliambia gazeti hili kuwa walioibua hoja ya ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali kama wakipata au kama wana ushahidi, yeye binafsi anatoa ruksa waupeleka katika vyombo husika vya dola ili ufanyiwe kazi.

Hata hivyo, Chenge alithibitisha kwamba yeye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Tangold, ambayo Inamilikiwa na serikali na kwamba hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia kuwa mkurugenzi.

"Nasubiri nipate hizo tuhuma kwa maandishi maana siwezi kuzungumza tu bila kuziona, lakini kama ni ukurugenzi Tangold, mimi siyo kwamba niliwahi kuwa mkurugenzi, ni mmoja wa wakurugenzi hadi sasa. Hii ni kampuni ya serikali, tatizo nini?" alihoji Chenge na kuongeza:

"Lakini kama mtu ana ushahidi wa tuhuma za ufisadi, jamani tunavyo vyombo vyetu, si wapeleke zikafanyiwe kazi," alisema Chenge.

Waziri huyo alisema hapendi malumbano, isipokuwa yote yaliyozungumzwa atahitaji kuyaona kwa maandishi na uonyeshwe ushahidi wa yeye kuhusika moja kwa moja na ufisadi uliotajwa.

Februari 12, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitangaza Baraza jipya la Mawaziri baada ya Februari 7, kulivunja baraza la awali ambapo baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri waliachwa na kumteua Chenge kuendelea na wadhifa wake katika Wizara ya Miundombinu.

Hata hivyo, uteuzi wa Chenge kuendelea na wadhifa aliokuwa nao katika wizara hiyo, ulizua mjadala mkali kutoka kwa wananchi, ambao wakidai kuwa hafai kutokana na kuhusika kwake na mikataba mibovu akiwa Mwanansheria Mkuu katika serikali ya awamu ya pili na ya tatu.

Pia baadhi ya wananchi walisema tangu ashike wadhifa huo mwaka 2005 hakuna mabadiliko katika ujenzi wa barabara zaidi ya mafanikio na ufanisi vilivyoachwa na serikali ya awamu ya tatu, ambayo John Magufuli alikuwa Waziri wa Ujenzi.

Pamoja na malalamiko hayo ya wananchi, Waziri Chenge aliwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kujiuzulu kutokana na maneno ya watu na kwamba suala la yeye kuendelea kukaa katika baraza hilo aulizwe Rais Kikwete ambaye ndiye aliyemteua.

Chenge alisema hayo mara tu baada ya kuapishwa na Rais Kikwete kuendelea kuiongoza wizara hiyo katika sherehe za kuwaapisha mawaziri katika Ikulu ya Chamwino, mjini Dodoma Februari 13, mwaka huu.

Source: gazeti mwananchi
 
I love jamboforums so much!

mwa mwa mwa mwa ncthwa!!!!!!!
 
Hivi huyu Chenge amepata wapi kiburi cha kuita Sh. Bilioni moja visenti ??

Kama kuna mtu anaweza kupata taarifa ya mali zake alizoorodhesha ni vizuri akazimwaga hapa uwanjani ili tuone kama na hivyo visenti viliorozeshwa hapo kabla
 
Haya yote yanafuatiliwa mkuu!
Hapa ndipo mtiifu na mwenzetu hapa JF mwanakijiji huwa anakuwa kwenye top of his game! Pasha moto vitumbua vyako na hiyo chai ya rangi upate the best of JF!
 
Pamoja na malalamiko hayo ya wananchi, Waziri Chenge aliwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kujiuzulu kutokana na maneno ya watu na kwamba suala la yeye kuendelea kukaa katika baraza hilo aulizwe Rais Kikwete ambaye ndiye aliyemteua.

Mimi sitashangaa kama huyu Mheshimiwa akawa na sababu kamili za kueleza namna gani alipata hivyo vijisenti. Na pia sitashangaa kwamba hii akaunti na pesa zake aliorodhesha katika mali alizokuwa nazo kwa hao jamaa wa ethics. Haondoki kwa hili.
 
Shilingi bilioni moja na laki mbili kwa fisadi Chenge ni vijisenti sasa sijui hao waliopata mshiko mnono akina fisadi Mkapa, Mramba na wengineo wana balance kiasi gani katika bank accounts zao za nje.
 
Shilingi bilioni moja na laki mbili kwa fisadi Chenge ni vijisenti sasa sijui hao waliopata mshiko mnono wanabalance kiasi gani katika bank accounts zao za nje.

Anaziita vijisenti kwa sababu hizi ni part ya pesa zote ambazo bado zinafuatiliwa ili zianikwe hadharani. Yote ya Chenge yakiongelewa, Sitashangaa kama mmoja wa watunza amani wetu pale Kurasini akiamua kumpiga risasi kwa hasira!
 
Shilingi bilioni moja na laki mbili kwa fisadi Chenge ni vijisenti sasa sijui hao waliopata mshiko mnono akina fisadi Mkapa, Mramba na wengineo wana balance kiasi gani katika bank accounts zao za nje.

Kama Tanzania ni nchi inayoomba omba mpaka Rais wetu kila Siku yuko kwenye Nchi za watu anaemea inakuwaje kumbe tu matajiri mpaka Milioni za dola ya USA tunayaita vijisenti?

Chenge anataka kutwambia nini hapa? Kumbe ndo alivyo na kiburi
 
East African Business Week (Kampala)
14 April 2008
Posted to the web 14 April 2008
Daniel Said

A fourth senior minister (name withheld) in President Jakaya Kikwete's cabinet is expected to tender his resignation following allegations related to his involvement in the radar scandal, East African Business Week can reveal.
The senior minister was searched recently by five officials from the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), Office of the Inspector General of Police and Attorney General's Chambers and Intelligence and the UK's Serious Fraud Office (SFO). His office and residence was searched following allegations of his involvement in the 28 million British pounds radar scam.
The radar was sold to Tanzania by the UK military manufacturer, BAE Systems.
According to the investigations, kickbacks were paid to a personal Swiss account of fugitive businessman Mr. Shailesh Vithlani who it is said, transferred some of the cash to government officials in former President the Benjamin Mkapa's regime.
Reliable sources told East African Business Week that it is alleged that the minister received bribes from the controversial 2002 military radar and air traffic control system.
The source told this paper that investigators in the UK have established that the minister has stashed about 5 million pounds into one of his UK bank accounts. Some of the money had been transferred to the account of one of the senior officials working with the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco). It was yet to be established why some of the money was transferred to the official's account.
Reports have it that the five-hour search came out with important documents and correspondences that may assist in the on going investigations.
Earlier, the minister had resisted the search, but to his surprise, the Attorney General Chambers in Tanzania issued an instrument to that effect. This, according to lawyers, may raise questions as to the legality of the instrument taking into account that the minister is a senior government official.
Following the ongoing investigations, the minister has been "advised" to resign to pave way for the smooth investigations. "The minister is in President Kikwete's delegation to India, China and later to the UK, but he has been advised to resign when he returns home," a source said.
If he resigns, he will be the fourth minister in Kikwete's government to resign on graft related allegations in two months. In February, 2008 the Prime Minister Edward Lowassa, Energy and Minerals minister, Mr. Nazir Karamagi and the EastAfrican Cooperation minister, Dr. Ibrahim Msabaha resigned following graft related allegations leveled against them by a Parliamentary Probe Committee on a power generating company, Richmond.

Tutege masikio hilooooooooooooooooo linakuja

Gazeti jongo. Limeandika habari za kuotea otea tu. Chenge kasema hasemi lolote, kashaingia katika hali ya kujitetea, sio kujiuzulu. Nchi za watu ukiandika kama hivi gazeti lako ndio mwisho wake.

Vyombo vya habari Tanzania ndio kiungo dhaifu kuliko vyote kwenye mnyororo wa kuvuta gurudumu la maendeleo.
 
Jamani msing'oane meno bure. Habari mpya nilizozipata hapa ni kwamba kumbe hizo hela za Chenge ni dola za Zimbabwe. Du, tuendeleeni na mijadala mingine tuachane na hivi vijisenti vya chenge.
 
Huyu bwana anadharau sana yaani hela ya kujenga shule kibao za sekondari na kuacha kulaza watu misituni anaita vijisenti, kanitukana mimi na baba yangu anayelala polini kumkwepa katibu kata mwenye mgambo wenye virungu tayari kumpiga kwasababu hajalipa sh. 5000. shenzi sana chengele
 
Hivi kada mpinzani ameamua kuingia mitini kweli mimi nilifikiri ni utani tu namiss sana comment zake katika hili. Please kada kama unasoma please comment japo mara moja tu.
 
Jamani msing'oane meno bure. Habari mpya nilizozipata hapa ni kwamba kumbe hizo hela za Chenge ni dola za Zimbabwe. Du, tuendeleeni na mijadala mingine tuachane na hivi vijisenti vya chenge.

Tehe Tehe Tehe... Chenge aipende dola ya Zimbabwe aache ya US..

Wednesday, April 16, 2008

1 US Dollar = 30,633.0 Zimbabwe Dollar
1 Zimbabwe Dollar (ZWD) = 0.00003264 US Dollar (USD)

Median price = 29,369.0 / 30,633.0 (bid/ask)
Minimum price = 29,369.0 / 30,633.0
Maximum price = 29,369.0 / 30,633.0

FXConverter - Currency Converter for 164 Currencies164 Currency Converter © 1997-2008 by OANDA.com.
 
Halafu unaambiwa hilo ni deal moja tu! bado kuna deal kibao ambazo hatujazifahamu! kweli wajinga ndio waliwao! hapo bado hujajua madeal ya Mramba,Mkapa,Sumaye,Karamagi,Rostam Aziz,Lowasa na wengineo!..ndiyo maana hawa watu huwa wanakiburi sana kumbe ni kwa sababu ya mimali waliyojilimbikizia.

Halafu na Rais Kikwete bado hajui ni kwanini nchi yetu ni masikini?

-Wembe
 
Back
Top Bottom