The Radar Scandal: Investigation & Progress

Wakukabwa koo na masikio ni hao waliokubali kulipa kodi yetu huko BAE...ohha nimekumbuka pengine hawakuwa na UTAALAMU wa kutosha.[/B]
Ni kina nani hao?Tukiwafahamu,tujiulize je waliopo madarakani sasa hawakuhusika?Na kama walihusika kwa njia moja au nyingine watajiepusha vipi na hilo au watajiingiza vipi katika saga hiloWakati hukumu yeyote itakayotolewa huenda ikawagusa?
 
Na Amri Lugungulo, PST Kisarawe


Rais mstaafu, Bw. Benjamin Mkapa, amesema hababaishwi na watu wanaosema sema.

Bw. Mkapa amesema hababaishwi na watu hao kwani tangu alipoingia madarakani mwaka 1995, CCM ilipata kura nyingi, vivyo hivyo mwaka 2000, na hatimaye mwaka 2005 baada ya aliyemuachia madaraka, Rais Jakaya Kikwete, kuwabwaga vibaya wapinzani kwa kujizolea zaidi ya asilimia 80 ya kura zote zilizopigwa.

Aliyasema hayo mjini hapa juzi alipokuwa akizungumza na viongozi, wanachama, wakereketwa, wapenzi wa CCM pamoja na wananchi, muda mfupi baada ya kurejea kutoka Shule ya Sekondari Marumbo iliyopo wilayani humu.

Bw. Mkapa ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM, alikwenda katika shule hiyo kwa mwaliko maalum na kuombwa kuwa mlezi.

Alisema ameanza kuwa na wasiwasi dhidi ya watu wa namna hiyo kwani kushindwa kwao katika uchaguzi, hakuathiri chochote na taifa limezidi kubaki na mshikimano, utulivu na amani huku wananchi wakizidi kupata maendeleo.

Alisema ameshangazwa na kelele za wapinzani hao kwani wanajua kabisa wananchi hawawezi kuwapa ridhaa ya kushika madaraka ya nchi kwa kuwa wamewaona hawana uwezo huo.

Aliongeza kwamba hivi karibuni wapinzani walibwagwa kwenye uchaguzi mdogo wa jumla ya kata 14 na kuambulia kiti kimoja cha udiwani.

Hata hivyo, alisema hata hcho kiti kimoja cha Udiwani, CCM ilikikosa baada ya mgombea wake kufanya makosa katika kujaza fomu ya kuwania nafasi hiyo.

Bw. Mkapa aliwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Kikwete azidi kuleta maendeleo nchini.

`Mkiendelea kumuunga mkono kwa namna hii, mtanipa raha kweli kweli,` alisisitiza.

Aidha, aliahidi kuendelea kuitetea CCM na kuhakikisha kwamba inadumu daima, licha ya kustaafu nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

`Muda wa miaka kumi wa kuwa Rais nimemaliza salama. Naona raha kubwa lakini suala la CCM, sipumziki ng�o. Sasa nani kama CCM. Mimi sipumziki, nataka CCM idumu milele, izidi kuwarejesha wapinzani kwani CCM ni mkombozi na wa kuleta maendeleo,` alisisitiza.

Kabla ya kuzungumza katika mkutano huo, Mkoa wa Pwani ulimkabidhi zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ng�ombe wa maziwa, mpunga magunia matatu, kilo 50 za unga wa muhogo, debe moja la korosho za kukaangwa na seti moja ya makochi.

Katika siku za karibuni, baadhi ya watu, hususan wa kambi ya upinzani, wamekuwa wakimsakama Rais huyo mstaafu, Bw. Mkapa kuhusu sakata la ununuzi wa rada huku baadhi yao wakimtaka atoe maelezo namna ilivyokuwa.

Lakini Rais Kikwete akiwa nchini Ubelgiji, aliwataka Watanzania, wamuache Rais mstaafu Bw. Mkapa, apumzike.

Hata hivyo, katika mkutano huo wa mjini Kisarawe, Bw. Mkapa, hakugusia suala la rada.

Source: http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/03/08/85875.html
 
Ama kweli haya yapo Tanzania peke yake. Wakati rais wa Jamhuri hii akiwaomba wananchi wamwache mzee wa watu APUMZIKE, huyu Mkapa anakuja na majivuno kuwa HABABAISHWI na mtu...
 
Ama kweli haya yapo Tanzania peke yake. Wakati rais wa Jamhuri hii akiwaomba wananchi wamwache mzee wa watu APUMZIKE, huyu Mkapa anakuja na majivuno kuwa HABABAISHWI na mtu...

He was right, kwasababu kama kuna ambao wangekuwa na uwezo huo ni wale walioshika mpini wa Nchi Lakini hao ndiyo wanamkingia ngao sasa tulitaka aseme nini na Anafurahia matunda ya kumpitisha JK ngazi ya Chama!
 
Katika sakata la kununua Rada Tanzania ilipewa mkopo wa US Dollar 40 milioni. Milioni $12 zimeingia mfukoni kwa mdosi mbongo ambaye inasemekana alikuwa kama wakala wa mkataba huo kati ya Tanzania na BAE. Mkopo wowote ule huwa ni lazima utozwe riba (interest). Swali langu ni kama hili lifuatalo, je Tanzania bado inalipa riba ya mkopo wote wa milioni $40 au milioni $28?
 
Kwa hili swali usiulize kwenye topic husika?

Jamani mderators mbona topics zinajirudiarudia sana; au nyie hamuoni. Topic moja inafunguliwa thread 2, 3 !!
 
Katika sakata la kununua Rada Tanzania ilipewa mkopo wa US Dollar 40 milioni. Milioni $12 zimeingia mfukoni kwa mdosi mbongo ambaye inasemekana alikuwa kama wakala wa mkataba huo kati ya Tanzania na BAE. Mkopo wowote ule huwa ni lazima utozwe riba (interest). Swali langu ni kama hili lifuatalo, je Tanzania bado inalipa riba ya mkopo wote wa milioni $40 au milioni $28?

kwani kwa uelewa wako walikopa ngapi?
 
Katika sakata la kununua Rada Tanzania ilipewa mkopo wa US Dollar 40 milioni. Milioni $12 zimeingia mfukoni kwa mdosi mbongo ambaye inasemekana alikuwa kama wakala wa mkataba huo kati ya Tanzania na BAE. Mkopo wowote ule huwa ni lazima utozwe riba (interest). Swali langu ni kama hili lifuatalo, je Tanzania bado inalipa riba ya mkopo wote wa milioni $40 au milioni $28?


we unauona mkia halafu unaulizia nanihii....ushasema ilipewa mkopo...na si...walipewa mkopo!
 
Mzee Bubu,

Heshima mbele mkuu, uliposema kuwa "...Tanzania tulipewa mkopo wa dola millioni 40...." ina maana kwamba tutaulipa mkopo mzima yaani dola millioni 40,

Hizo za mdosi ni tatizo letu kama Tanzania sio la waliotukopesha!
 
Mzee Bubu,

Heshima mbele mkuu, uliposema kuwa "...Tanzania tulipewa mkopo wa dola millioni 40...." ina maana kwamba tutaulipa mkopo mzima yaani dola millioni 40,

Hizo za mdosi ni tatizo letu kama Tanzania sio la waliotukopesha!
Afadhali umechukua muda kidogo Kumjibu kwa undani Lakini Yeye anafahamu walikopa ngapi na anafahamu wanahitajiwa kulipa riba Lakini ktk swali lake inaonesha anataka walipe million $28 tu na riba yake,Lakini wasilipe Mil$12 na riba yake.sasa sijui benki walihusika kuwaambia wampe dalali mil.12 na hawazihitaji wazirudishe na wala hawatazitolea riba.
 
Tumekopeshwa $40 milioni lakini kuna ushahidi wa kutosha kwamba kati ya hizo $12 millioni zimeingia mifukoni kwa mdosi mbongo ambaye amewagawia wale waliompa uwakala wa ununuzi wa Rada hiyo. Sijui riba hiyo ni kiasi gani, lakini tuchukulie tu riba hiyo ni 5% basi tunalipa $600,000 kwa mwaka kwa hizo milioni $12 ambazo zimetafunwa na mdosi mbongo na wale waliopma uwakala.

Awamu ya nne kama ingekuwa inajali maslahi ya nchi yetu basi ingeanzisha ufuatiliaji wa hali ya juu ili kurecover pesa zote alizolipwa mdosi mbongo na rafiki zake. Pesa hizi zimelipwa katika bank moja pale Switzerland, hata kama kuna transactions nyingine zimefanyika zote zingeweza kuwa tracked down ili kuhakikisha Tanzania ina recover kila senti ya hizo milioni $12. Tanzania inaweza hata kuomba msaada wa mashirika mbali mbali ya kimataifa kama WB na IMF ili kuibana bank hiyo iweke wazi transactions zote tangu lilipoingia bulungutu na zile zilizofuata.

Lakini awamu ya nne haijali sijui kwa kuwalinda wale waliohusika na scandal hili au haioni umuhimu wa kurecover pesa hizo. Inasikitisha kuona nci maskini ya Tanzania inabebeshwa mzigo mkubwa wa deni ambalo limewanufaisha wajanja wachache na kuendelea kulipa riba kubwa. Nilikuwa na matumaini makubwa uongozi wa awamu ya nne, lakini jinsi walivyobweteka katika kushughulikia sakata hili na makosa mengi yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka mmoja na ushee. Basi matumaini yangu yametiwa dosari kubwa.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Jamani hii scandal ni nzito kuliko tunavyoifikiria, maana kama serikali ya awamu ya nne iseme ianike kila kitu kwenye uwazi basi, nadhani JK naye yumo kwenye kundi.Nadhani linafumbiwa macho kulinda majina ya wahusika wakuu.
 
Naona kama sisi WaTanzania ni wagonjwa wa akili.We are able to talk alot but can do nothing .Tunajadili nini hapa mwaka mzima.Kesho tutasikia Scandal nyingine and then start a new thread.Toothless Bulldogs. Long live CCM and the Crooks whom we cannot live without.
 
70mairoad: "Long live CCM and the Crooks whom we cannot live without".

Kaka maneno yako yanakuna....ingawa inauma. Tupo wengi katika mkumbo huu ama mnasemaje ndugu wana JF?

Watanzania hatuna uthubutu na manyang'au wa ndani na wa nje wanalijua hilo na wanalitumia vizuri sana.....

Ndugu Issa Shivji alisema "thubutu kufikiri, fikiria kuthubutu". hilo ni somo gumu kwa watanzania wa leo sijui labda wa kesho kama tutakuwa nayo hiyo kesho.....

Tanzanianjema
 
Serikali yajivunia rada
*Yatamba imeingiza faida ya mabilioni


HATIMAYE Serikali imetoa kauli kwamba suala la ubadhirifu wa fedha unaodaiwa kufanywa wakati wa ununuzi wa rada, litajadiliwa na Bunge baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi kutoka serikali ya Uingereza.

Sambamba na hilo, serikali imesema kuwa, zaidi ya sh bilioni 17 ya mapato ya ziada, zimepatikana tangu rada hiyo inayolalamikiwa kunununuliwa kwa ulanguzi, ianze kutumika nchini.

Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk. Maua Daftari alitoa kauli hiyo bungeni jana, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kigoma Vijijini, Zitto Kabwe (CHADEMA), aliyetaka kujua endapo serikali ina mpango wa kuleta hoja ya rada ijadiliwe bungeni.

Akijibu swali hilo, naibu waziri huyo alisema kwa vile Serikali ya Uingereza bado inaendelea na uchunguzi wa kashfa hiyo, serikali kwa sasa haiwezi kuleta hoja hiyo bungeni.

Kuhusu mapato ya ziada yaliyopatikana tangu rada hiyo ianze kutumika, Dk. Maua alisema takwimu za mapato katika kipindi cha miaka miwili kabla ya rada na baada ya kununuliwa zinaonyesha zimeongezeka.

Alisema kabla ya rada hiyo kuanza kutumika, hasa katika shughuli za kuongoza ndege, mwaka 2000/2001, mapato yalikuwa sh bilioni 2.3 na mwaka 2001/2002, yalikuwa sh bilioni 2.8.

Alisema baada ya rada kununuliwa na kuanza kutumika, mwaka 2002/2003, mapato yalikuwa sh bilioni 3.4, mwaka 2003/2004 yalikuwa sh bilioni 3.9, mwaka 2004/2005, sh bilioni 4.1 na mwaka 2005/2006, yalikuwa sh bilioni sita na hivyo kufanya kiasi cha pesa kilichokwishapatikana kutokana na huduma ya rada, kufikia sh bilioni 17.5.

Rada hiyo ilinunuliwa kwa zaidi ya sh bilioni 40 na muuzaji kudaiwa kupata kamisheni ya sh bilioni 12, jambo ambalo Serikali ya Uingereza inafanya uchunguzi kubaini waliohusika katika ulanguzi huo.

"Kwa hiyo, kumekuwapo na ongezeko la mapato kwa asilimia 113.7 kutoka mwaka 2002 kabla ya rada haijaanza kutumika hadi mwaka 2006. Ni dhahiri kuwa ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa ndege zinazotumia anga na viwanja vyetu kwa jinsi huduma zilivyoboreshwa," alisema Dk. Maua.

Alisema kuwapo kwa rada, kumesaidia pia ongezeko hilo kwani wateja wamekuwa na uhakika wa usalama zaidi wa ndege na abiria wakati wanapitia kwenye anga na viwanja vya Tanzania.

Mbali ya kuongeza pato, Dk. Maua pia alisema wastani wa gharama za uendeshaji wa rada kwa mwaka ni sh milioni 234.7.

Alitaja gharama hizo kuwa na kiasi cha pesa kinachotumika kwenye mabano kuwa ni mishahara ya waongoza ndege na wahandisi (sh 145,597,121.30), mafunzo ya waongoza ndege na wahandisi (sh 50,000,000), matengenezo madogo madogo (sh 6,704,330,00), matumizi ya umeme (sh 28,002,443,00) na usafiri wa wafanyakazi na matumizi mengine, sh 4,419,147,00.

"Tangu rada hii inunuliwe, haijafanyiwa matengenezo makubwa. Hata hivyo, kulikuwa na utengenezaji wa Uninterruption Power Supply - UPS (ununuzi wa betri), mwaka 2006 na matengenezo ya Motor ya Antenna. Jumla ya gharama ya vipuri na matengenezo hayo ilikuwa sh 47,861,632," alisema.

Waziri Daftari alitoa ufafanuzi huo kutokana na swali la Msingi la Mbunge wa Ole, Bakari Shamis Faki (CUF), aliyetaka kujua mapato za ziada yaliyotokana na huduma ya rada, gharama za uendeshaji wa rada hiyo kwa mwaka na kwamba imefanyiwa matengenezo mara ngapi.

Mbali ya kutumika kuongoza ndege, rada pia husaidia kupunguza ucheleweshaji wa safari za ndege, huwezesha kuelekezwa kwa ndege ili kukwepa maeneo yenye hali mbaya ya hewa na husaidia marubani kuona uwanja wa kutua.
 
Ohooo, sasa kazi ipo. Hapa mjadala utakuwa namna rada ilivozalisha mamilioni ya fedha na wala sio namna hiyo rada ilivyopatikana. Na jinsi mambo yalivyo, upatikanaji wake ukizungumziwa tu, spika atasema "..mjadala huo UMEFUNGWA!"
Kazi kweli kweli!
 
Back
Top Bottom