"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Pasco
"...Kwa kutumia kanuni hii, mfano Osama
aliua wale aliowaua ile Septembe 11,
lakini amewasaidia Taleban wengi zaidi
kuliko wale aliowaua kwenye September
11, na Bush kwa hasira ya September
11, ameaua watu wengi zaidi wasio na
hatia
kuliko wale Osama aliowaua, siku
ya hukumu, mnaweza kushangaa
Osama, Saadam na Gaddafi wakaingia
peponi, halafu Bush, Blair na Obama
wakatupwa motoni!.

Kwa maelezo yako ni kwamba osama aliowaua septemba 11 walikua na hatia ila aliowaua Bush hawakua na hatia,unaona ulivyojichanganya hapo juu?
 
Hii thread ilipaswa kuwa mbaali saana.

Ila maandishi murua saana haya muhimu watu wayasome na kuyatafakari ili kukua kiroho.

Maana roho nayo hupigishwa nondo za kiroho ili ikue na iwe imara kama mwili, ndio maana kuna watu sio rahisi kukabwa na majini maana wako imara rohoni. " Destruction of ur soul is your vanity!" Usiiache roho yako wazi mwanadamu..train ur spirit to be strong and aggresive.
 
Kuna kitu kuhusu karma ambacho Pasco hujagusia
karma ya mwenza inavyo muathiri mtu

Nimeona majambazi wengi walio oa wanawake wachamungu wakisalimika vifo.....
Au kuoa mtu mwenye destiny ya kitu kitu fulani kinavyoweza kumpa mtu mwingine 'bahati' ya kufika huko
 
Last edited by a moderator:
Karma katika falsafa ya wahindu na wabudhist maana yake utavuna ulichopanda. Kumbuka hawa watu wanaamini katika reincarnation,kufa na kuzaliwa tena duniani. Kwa hiyo malipo yanaweza kuwa utakapozaliwa tena baadaye. Kwa kawaida mtu akifanya kosa kubwa sana analipwa mradi wake katika maisha haya . Lakini karma ni kama bank account. Mtu anaweza kutumia sh milioni moja kila wiki asifilisike,kama rafiki yetu mmoja anayegombea urais. Inategemea alikuwa na feaha ngapi benki.
 
Katika lugha ya sanskrit inaitwa karma. Katika lugha ya pali,lugha aliyokuwa anaongea Budha,inaitwa kamma. Kiswahili inaitwa kama. Sasa unaweza kuona dhahiri kwamba karma,kamma na kama ni neno moja. Kwamba ukifanya jambo sasa,itakutokea baadaye kama ulivyofanya sasa. Wanasema, Budha anasema,karma ya mkatili,muuaji,ni kuwa na maisha mafupi. Nakumbuka siku ile alipokufa ditopile mzuzuri,ilikuwa takriban mwaka mmoja baada ya ile tafrani. Nilikuwa ndani ya daladala ilipokuwa inatangazwa,watu wakawa wanaelezana earnestly kwamba hiyo ni karma. Kwa hiyo kuua,kufanya ukatili karma yake ni kuwa na maisha mafupi. Kuwa mwizi karma yake ni kuwa maskini. Kuwa fuska karma yake ni kuchukiwa. Kuwa mwongo karma yake ni watu kukudanganya na kukuletea unafiki mkubwa. Ukifanya wema unalipwa wema ukifanya ubaya unalipwa ubaya. Ukifanya uhalifu ukipelekwa mahakamani na baadaye gerezani hiyo pia ni karma. Lakini kama ukimgonga mtu na gari,halafu baadaye ukaenda marekani ukagongwa na gari,basi labda atakuwepo mtu atakayesema hiyo ni karma. Haya mambo unaweza kuyasoma katika buddhasutra.com
 
Karma katika falsafa ya wahindu na wabudhist maana yake utavuna ulichopanda. Kumbuka hawa watu wanaamini katika reincarnation,kufa na kuzaliwa tena duniani. Kwa hiyo malipo yanaweza kuwa utakapozaliwa tena baadaye. Kwa kawaida mtu akifanya kosa kubwa sana analipwa mradi wake katika maisha haya . Lakini karma ni kama bank account. Mtu anaweza kutumia sh milioni moja kila wiki asifilisike,kama rafiki yetu mmoja anayegombea urais. Inategemea alikuwa na feaha ngapi benki.
 
Maada ni nzuri ,comments pia nzuri
Lakin bado kuna critics katika hili ambalo ni kwa wale wanaotumia akili wanaweza kuzitambua
Labda nimuombe mwandishi ai iandike tena katika. Critics point of views with vivid itakuwa vizuri mno

Pia atumie mifano ya kisayansi na aiandike kama makala yaani views zake au itikadi yake asiidhihirishe

Good.
 
Kuna watu walisababisha mauti ya jamaa yangu mmoja na baada ya kifo walifanya sherehe na kufurahia kuwa wametoa kikwazo maana alikuwa hapendi mambo ya 10%. Nataman sn kuona hii kitu inawatokea japo moyo wangu upate kupoa kidogo.
 
karma.jpg
Pasco

Mkuu Pasco kuelekea kesho na yaliyotokea Zanzibar leo kunasoma tunaweza unganisha na hii hoja?

Najaribu tu kuwaza!
 
Last edited by a moderator:
Karma katika falsafa ya wahindu na wabudhist maana yake utavuna ulichopanda. Kumbuka hawa watu wanaamini katika reincarnation,kufa na kuzaliwa tena duniani. Kwa hiyo malipo yanaweza kuwa utakapozaliwa tena baadaye. Kwa kawaida mtu akifanya kosa kubwa sana analipwa mradi wake katika maisha haya . Lakini karma ni kama bank account. Mtu anaweza kutumia sh milioni moja kila wiki asifilisike,kama rafiki yetu mmoja anayegombea urais. Inategemea alikuwa na feaha ngapi benki.
Aisee...
 
Kuna ndugu yangu. WA damu kabisa alinishitakia mengi mabaya kwa mtu ambaye alikuwa msaada mkubwa kwangu, na alifanya hivo ili yule mtu amsaidie yeye na amsilkilize yeye. Badala ya Mimi, na kweli yule mtu akawa Hana Habari na Mimi tena wakati huo nilikuwa mjamzito WA miezi 8, hakika iliniuma kuliko chochote maishani mwangu,nilikunywa pombe wakat wote ili nitoe mawazo lakin wapi?, had najifungua ilipita miez kadhaa bila ya maumivu Yale kunitoka, hata mwaka haukuisha yule ndugu yangu balaa zikamuandama, biashara zake zikafilisika, na kuishi maisha magumu na ya kukopa, na ya kuomba kwa ndugu ili watoto wake waweze ishi, ILA hakika allichonifanyia maumivu yake hadi Leo sijawahi sahau.
 
Uliyosema ni SADKTA...malipo yote papahapa duniani.Dhana,Dhulma ni miongoni mwa dhambi na tunahadharishwa kuepukana navyo.Mimi na wewe tukifuata tuliyoamrishwa na kuacha tuliyokatazwa hakuna shaka tutafanikiwa hapa duniani na huko kwenye maisha ya milele.
Kumbuka.....Dua ya mwenye kudhulumiwa huwa haina pazia inapokelewa haraka saana.

usipo jua kuwa mtu flani kakudhurumu,na uakaendelea kucheka nae na kumuona kawaida tu bila kujua uovu wake,je atapata madhara???????
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom