"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

karma.jpg

Wanabodi,

Sio mara moja au mbili, umewahi kusikia mtu akitendewa jambo baya, anasema "namwachia Mungu!", au neno "Malipo ni hapa hapa duniani!". likitokea jambo zuri lolote watu hufurahi na kumshukuru Mungu, au likitokea jambo baya lolote, watu hufarijiana kuwa kusema hiyo ni "kazi ya Mungu!'. haina makosa!. Natumaini mmewahi kusikia kuwa kuna watu wenye bahati, familia zenye bahati, wamebarikiwa, wamesoma na wote wana kazi nzuri, na kuna watu/familia wenye mikosi, wamelaaniwa na kuandamwa na majanga, mikosi etc?, au nini huwa kinampata mtu aliyeachiwa kitu kinachoitwa 'laana!"?.

Hakuna kitu chochote ni kipya chini ya jua, hakuna bahati nzuri wala bahati mbaya, hakuna jambo lolote linalotokea kwa kujitokea tuu, au kwamba limetokea ghafla tuu, au kwa bahati mbaya, or just a coincident!, no way!. Kila jambo linalotokea, linatokea kwa sababu na lilikuwa destined kutokea hivyo hivyo lilivyotokea, yaani everything is a premeditated move, caused by cause and effects, by our actions or inactions!.

Jee ni nguvu gani zinafanya watu wengine wafanikiwe, na mambo yao kuwaendea vizuri, huku watu wengine wakikwama, kuandamwa na mikosi, majanga, mabalaa na kuishi kwenye maisha duni na umasikini uliotopea huku wakiandamwa na majanga, visa na mikasa lukuki?!.

Hizi ni powers zinazotumika kwenye 'cause and effects', ndizo zinazoitwa "Powers of Karma" yaani "what goes around, comes around".

Mambo yote haya hufanya kwa kupitia nguvu zinazoitwa Universal Laws, ambazo zinatumia zile kanuni tatu za Newtons Laws of Motion.

Kanuni ya Kwanza ya Karma ni The 1st Newstons Law of Motion
Newton's
first law states that "every object will remain at rest or in uniform motion in a straight line unless compelled to change its state by the action of an external force. ... The third law states that for every action (force) in nature there is an equal and opposite reaction"

Kanuni hii ni kuwa kila kitu kitaendelea kuwa hivyo kilivyo kilivyo hadi nguvu nyingine ije kukibadilisha. Yaani kama kitu kimesimama, kitasimama hivyo hivyo hadi nguvu nyingine ije kukihamisha, au kikiwa kwenye motion, kitaendelea kwenda hadi nguvu nyingine ije kukisimamisha! . Every object in a state of uniform motion tends to remain in that state of motion unless an external force is applied to it.
Kanuni ya Pili ya Karma, The 2nd Newtons Law of Motion
The second law states that the acceleration of an object is dependent upon two variables - the net force acting upon the object and the mass of the objec
t.
Hii ndio kanuni ya mafanikio katika kila jambo unalolitenda hadi mafanikio ya kimaisha, kufundisha kuwa ili kupata mafanikio katika jambo lolote, yatategemea nguvu unayotumia katika kulitekeleza jambo hilo. Ukifanya kazi kwa bidii kwa kutumia nguvu kubwa utapata mafanikio makubwa,

Kanuni ya Tatu ya Karma ni The 3rd Newton's Law of Motion.
Kanuni ya tatu ya kila nguvu itakayotumika kukihamisha hicho kitu, kuna nguvu nyingine ya pili, ambayo pia inatengenezwa ikivuta upande tofauti na hiyo nguvu inayotumika. For every action there is an equal and opposite reaction. This is the law of cause and effects!.

Msingi wa hoja hiyo ndio hizo nguvu zinazotumika kufanya kila kinachotokea duniani kwenye maisha ya kila binadamu! na ulimwenguni kwa ujumla zikiitwa cosmic forces. Yaani binadamu ameumbwa kwa mwili wa nyama, na damu ya kimiminika (Ying na Yang) na sehemu kubwa ya mwili wake ni maji, lakini kitu kikubwa binadamu alichoumbwa nacho ni roho, yaani spirit, uhai, hii roho yenye uhai, imeumbwa kwa powers, ndio hivyo nguvu responsible kwa kila kitu kuanzia uhai hadi kila kitu kinachomtokea binadamu, kinasababishwa na nguvu hizi zilizoko ndani ya kila binadamu, ambazo zinaitwa 'nature!'.

Wafanya Miujiza ya Uponyaji Wanatumia Nguvu Zao Kuamshia Nguvu Zako Ndizo Zinakuponya!
Wachungaji wote na imani za wokovu, walokole, wanaojitapa kuwa wana nguvu za uponyaji, au waganga wa kienyeji au tiba asili na tiba mbadala wanaotibu kwa kutumia tiba ya imani, (faith healing), wanatumia hizi powers zao kuziamsha tuu nguvu hizi zilizoko ndani yako, yaani ndani ya kila mtu kuna hizi nguvu, ambazo zikiamshwa ndizo zinazotenda miujiza ya uponyaji na mtu kujiponya mwenyewe bila kujijua huku akiamini huyo Mchungaji au mganga ndie amemponyesha!.

Kinachoponya ni Imani Yako Ndio Ina Nguvu za Uponyaji na Sio Mganga au Jina Lolote!
Wachungaji hutumia Jina la Yesu kuponyea, kutokana na kuamini, milango ya nguvu za Mungu zilizo ndani yako inafunguka na kuzifanyia muujiza wa uponyaji kwa kuamini ni Jina la Yesu, lakini kiukweli kilicho kuponya sio hizo nguvu za Mchungaji wala sio hilo jina Yesu bali ni nguvu zako zilizo ndani yako ila zimewezeshwa kuamka na kukuponya kwa imani yako kupitia kuamini ni Jina la Yesu, hivyo kinachoponya ni imani yako. Waganga wa kienyeji hutumia tunguli kuziamsha.

Mungu Hayuko Juu Mawinguni, Mungu ni Omnipresent, Yupo Kote Hadi Ndani Yako!
Wengi huwa wanaomba Mungu kwa kutazama juu kwa sababu hivyo ndivyo wengi tuliovyoaminishwa kwa kudanganywa na hizi dini za wazungu na waarabu kuwa Mungu yuko juu mbinguni, peponi, ahera, mawinguni etc, kitu ambacho sii kweli!.

Dunia ni Dunia Mbili, Physical World, Ulimwengu wa Mwili na Spiritual World, Ulimwengu wa Roho
Hii dunia tuliomo, japo inaonekana kama ni dunia moja au ulimwengu mmoja, sio dunia moja wala ulimwengu mmoja, bali ni dunia mbili, dunia hii au ulimwengu huu wa kifizikali, yaani Physical World wenye vitu vya kuonekanika, watu, ardhi, wanyama, mimea, milima, mabonde, bahari, mito, maji, hewa etc, na kuna dunia au ulimwengu mwingine ambao ni Spiritual World, Ulimwengu wa Roho, ambao haionekani kwa macho ya mwili bali kwa macho ya roho, huko sasa ndio mbinguni. Ulimwengu huo ndio mbinguni kwa mungu, huko zinaishi roho, spirits, both good and bad, huko ndiko mbinguni kwa Mungu na motoni kwa shetani.

Hivyo ukweli wa Mungu wa kweli hayuko mbinguni wala mbinguni sio juu mawinguni!, bali mbinguni, motoni na duniani kote ni hapa hapa tulipo, ila kategemea na state ya kiumbe kilivyo, ukiwa kwenye physical state of flesh state, mwili wa nyama kama tulivyo then tunajiona tuko duniani ndani ya physical world na mbinguni tunaelekezwa ni juu, lakini tukichange state into spirit, then ndio tunajiona tuko mbinguni, peponi or motoni, lakini Mungu wa kweli ni omnipresent, yupo popote na kila mahali, na sii mbinguni tuu, na kitu ambacho dini nyingi hazifundishi ni kuwa Mungu wa kweli, yuko ndani yako!.

Binadamu Ameumbwa Kwa Sehemu Mbili, Body, Mwili na Spirit, Roho

Kama ilivyo dunia ina sehemu mbili za ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho, binaadamu nae ana sehemu mbili, ule mwili wa nyama ulioumbwa kwa udongo, mwili huu ndio unaokufa, kuoza na kurudi mavumbini, ila mwili wa roho, ulioumbwa na ile pumzi ya uhai binadamu aliyopuliziwa Mungu na kupata uhai, yaani 'life force', mwili ule haufi, unaishi milele, hivyo huko mbinguni na motoni, mwili unaokwenda kule ni ule mwili wa roho, huu mwili wa nyama ni kasha tuu, ukiisha kufa, zile taratibu nzuzi za mazishi, kwenye jeneza zuri, kaburi zuri, siku hizi hadi makaburi ya marumaru, kwa lengo la kukuhifadhi vizuri, ni kufurahisha tuu nafsi zetu, mwili huu wa nyama ukiisha kufa, ndio kwisha habari yake, unakwenda kugeuka mavumbi, na hapa naomba ili nisikosee heshima maiti za binaadamu, naomba nisiseme kile kinachoutokea huo mwili huko sandukuni baada ya kuzikwa, lati watu wangekuwa wanapata fursa ya kuuona huo mwili huko kabuni nini kinautokea, watu wengi wanfe opt for cremation na sio burial!.

Subject matter ya bandiko hili ni zile powers za Mungu zilizo ndani yetu na ndizo responsible kwa kila kitu kinachotokea kwa kila kiumbe humu duniani wakiwemo binadamu na ndizo zinazoitwa karma!.

Binadamu Ana Powers Ndizo Responsible Kwa Kila Kitu!.
Kupitia nguvu hizi za Mungu zilizo ndani yetu, binadamu amepewa utashi wa kuamua kuchagua au atende matendo mema au atende matendo mabaya au maovu!. Akitenda mema, ile nguvu inategeneza kitu kinachoitwa "positive energy", hivyo kila jema analotenda kwa kulitoa ndani yake, jema hili linatengeneza positive energy, ambayo inatoka ndani yake na kuwafikia wengine, hiyo nguvu ya matendo mema utakayo tenda, inafuata ile kanuni ya Newton kwa kureproduce equal and oposite positive energy ambayo itavurumishwa kutoka kila upande ambao umepeleka wema na kukuzalishia wema kutoka kila upande na kukurudia wewe, hivyo wema huo utakurudia kwa nguvu mara dufu ya ile uliopeleka wewe na hapa sasa ndipo inapotumika kanuni ya tatu ya Newton, ambayo ule wema ulioufanya utalipwa mara dufu na utakurudia wewe na kizazi chako kutegemeana na ukubwa wa wema wenyewe!. The relationship between an object's mass m, its acceleration a, and the applied force F is F = ma. Acceleration and force are vectors. in this law the direction of the force vector is the same as the direction of the acceleration vector.

Kila Mtenda Mema, Hulipwa na Karma, Mema Mara Dufu!.
Hapa ndipo inapokuja hoja ya kila mtenda wema, atalipwa mema na kila mtenda ubaya au maovu atalipwa ubaya au uovu na malipo haya hufanyika hapa hapa duniani, ila malipo huwa ni mara dufu ya wema ulioutenda, au uovu ulioutenda, hii ndio hiyo karma yenyewe, what goes around comes around!.

Mfano wewe sio lazima uwe tajiri, bali umejaaliwa kuwa na kajiuwezo japo kadogo, lakini kwa kutumia uwezo huo huo kidogo ulio nao, ukasaidia masikini. Mfano kuna masikini amelala na njaa kwa muda wa siku 3, ikipita siku ya 4 bila kupata chochote, masikini huyu atakufa njaa!. Wewe ukampa masikini yule Shilingi 500, akanunua mkate wa 100 na kuula na maji ya vichochoroni, akala na kuendelea kuishi kwa siku 5 zaidi!. Ile mia 500 yako hapa imetenda wema mkubwa sana wa kuokoa maisha ya masikini yule, hivyo positive energy itakayo kurudia wewe sio tena ya ile 500 uliotoa bali ni 500 mara 500 sawa na thamani ya ile life uliosave, hivyo wema utakao kurudia ni wema wa mamilioni!.

Vivyo hivyo unaweza kutoa msaada wa bilioni 1.6 kama alivyotoa Rugemalila kwa mama Tibaijuka, japo ametoa bilioni, kumbe net value ya mama Tubaijuka ni bilioni 100!, hivyo hicho alichotoa Rugemalila ni kama punje tuu ya mchele kwenye gunia, ambayo ni asilimia 1% ya net value ya Mama Tibaijuka la labda ni 0.01% ya gross value!, hivyo positive energy toka kwa mama Tibaijuka kwenda kwa Rugemalila ni positive energy kiduchu tuu ya asilimia 1% tuu!, kutegemeana na umuhimu wa hiyo bilioni moja!. Kama lengo halisi la msaada ule lilikuwa ni kumsaidia mama T. "kupanda ghorofani", lakini wakazuga kuwa ni fedha za kusaidia watoto wa shule, lakini ni kweli sehemu ya fedha zile, ili kwenda kusaidia watoto wa shule, then payback ya hiyo bilioni moja itabaki ile ile asilimia 1% ya net value ya mama Tibaijuka, lakini kama kweli fedha zile zote zimepelekwa kwa the needy, kule shuleni kusaidia watoto, hata kila mtoto akipata mlo mmoja tuu wa siku moja kutokana na fedha hizo, then msaada huo una produce multiplied effects ya hiyo bilioni moja kwa watoto 1000, ambayo kwao ni muhimu, itamrudia Rugemalila mara dufu!, ndio maana watu wanashangaa, baada ya wema wa Rugemalila kwenye mgao wa escrow, sasa amepata tenda ya Shilingi Trilioni 54 upanuzi wa bandari ya Mwambani Tanga!.

Muujiza wa Pesa Uitwao Money Mystic!

Kwenye mambo ya pesa hii kitu inaitwa 'money mystic" "the more you spend the more you get!". Ila hiyo spending iwaguse the need ambayo watatoa big and huge positive energy ndio maana from time to time tunashuhudia matajiri wa kihindi na kiarabu, wanaojua the power of karma, wakiwafolenisha watu masikini siku nzima, kisha kuwapa mgao wa 10,000 some specific days siku ya Ijumaa na haswa kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani, au kuwafuturisha watu masikini/yatima etc, wanatengeneza hii positive energy ambayo wema wake hurudi maradufu!. Hii pia inasababisha wale masikini mnaowaona mjini haswa omba omba hawaishi kwa sababu wanapata!. Kanuni hii pia hutumia na matajiri wanaitwa ma philanthropists ku multiply utajiri wao, hivyo msiwashangae kina Manji, Mo, Mengi ku spend bilions za misaada kwa ufadhili wa timu za soka, au kufadhili masikini, huku wafanya kazi wakilipwa kiduchu na wakati mwingine kukosa hata mishahara on time!.

Kila Mtenda Ubaya, Hulipwa na Karma, Ubaya Mara Dufu!.
Vivyo hivyo kama ambavyo wema hurudi kwa kulipwa mema mara dufu, vivyo hivyo ukitenda ubaya, ubaya ule pia nao una tabia ile ile kama ya wema, nao pia huwa unakurudia mara dufu, unaweza kutenda ubaya mdogo tuu mfano mama wa kambo kumtesa mtoto yatima, kwa kumlaza na njaa, pay back ya mapigo yake ni kubwa sana kuliko ubaya unaotendwa!.

Sisi Wakristu Wakatoliki tulifundishwa kuwa siku ya hukumu ya mwisho, matendo yako mema yanachukuliwa na kuwekwa kwenye mizani, na kulinganishwa na matendo yako mabaya/maovu, mema yakizidi, unaingia mbinguni, mabaya yakizidi, unatupwa motoni!. Lengo ni binadamu tutende mema kuliko maovu!.

Maajabu ya Karma, Waovu Kulipwa Mema, Wema Kulipwa Maovu, Mfano wa Bush, Blair na Obama Upande Mmoja Huku Osama, Saadam na Gaddafi Upande Mwingine!.

Kwa kutumia kanuni hii, mfano Osama aliua idadi fulani ya watu ile September 11 kule Marekani lakin Osama huyo amewasaidia Taleban wengi zaidi kuliko idadi ya wale aliowaua kwenye September 11, na Bush kwa hasira ya September 11, ameaua watu wengi zaidi wasio na hatia kule Iraq, kuliko wale Osama aliowaua, siku ya hukumu ya mwisho, mnaweza kushangaa kuwakuta Osama, Saadam na Gaddafi wakaingia peponi!, halafu Bush, Blair na Obama wakatupwa motoni!.

Vivyo hivyo mnaweza msiamini pale mtakaposhuhudia viongozi wa dini tunao waaminia, wakitupwa motoni, huku majambazi na wauaji wakipeta kuingia peponi, kutegemeana na ukumbwa wa wema wao ukilinganisha na ubaya wao, yaani ile 'karma ya mema yao ndio what matters most after all tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo, na ila kuhukumiwa ni kwa matendo mema au mabaya yako.

Karma ina Apply Kwenye Kila Kitu, Kisiasa, Kiuchumi, Kijamii!.
Karma hii ina apply kwenye kila kitu, kifamilia, kisiasa, kiuchumi na kijamii mfano Zitto ametimuliwa Chadema kwa tuhuma za usaliti, kama ni kweli Zitto ni msaliti, then Karma ya usaliti itamshughulikia Zitto na hiki Chama chake cha ACT kitajinyaukia na kujifia kabla hata hakujakuchwa kwa uchaguzi!, na Chadema kitaendelea kung'ara, kuneemeka kuchanua na kushamiri!. Lakini kama Zitto amesingiziwa usaliti na hakuhukumiwa kwa haki bali ameonewa, then Karma ya kuonewa itamlipa Zitto kwa kumuimarisha, ACT itaneemeka, itachanua na kung'ara, Zitto atarejea bungeni kwa kishindo, wakati Chadema, wale walio husika kusingizia uovu, karma itawatandika bakora za Karma, mmoja baada ya mwingine, in two ways, a collective karma kwa Chadema kama chama kitakula bakora zake na kitaishia kupukutika, lakini wana Chadema individual wenye mkono kwenye dhulma hii kwa Zitto, nao karma zao zitawatembelea mmoja mmoja kwa mujibu wa mchango wake hivyo watadhoofika, kudorora na kunyauka!.

Pamoja na Karma Kuwa Hukumu ya Haki, Ina Uzuri na Mazuri Yake, Uzuri wa Karma ni...
Pamoja karma kuwa ndio hukumu pekee ya haki hapa duniani, pia karma nayo ina mazuri yake na mabaya yake. Moja zuri kubwa la karma ni kila unachotenda, lazima utalipwa!, haikopeshi!, ukitenda mema, utalipwa mema na ukitenda ubaya utalipwa ubaya au lazima utalipa, ila pia katika hukumu za karma, kuna wakati unatenda baya dogo, unakuja kulipwa ubaya mkubwa wa ajabu, au una tenda ubaya, haulipwi ubaya na unalipwa wema, vivyo hivyo, kuna wakati unaweza kutenda wema mdogo, ukalipwa wema mkubwa ajabu, au ukatenda wema mkubwa, ukalipwa wema kiduchu au usilipwe na hata ukulipwa ubaya!. This explani kwanini sometimewa watu wabaya ndio wanapeta, halafu watu wema wanasulubiwa!.

Uzuri Mmoja wa Karma, Ukitenda Wema Halafu Ukafa Kabla ya Kulipwa, Familia Yako Inalipwa!.
Kwa haraka haraka na uzuri mmoja wa karma na ubaya mbili. Uzuri ni ukitenda wema halafu ukafa kabla ya karma kukulipa ule wema wako, then familia yako uliyobakia huku nyuma, itaendelea kulipwa pensheni ya wema wewe ulioutenda hivyo kupelekea watu kuona kuna familia fulani fulani zimebarikiwa kila wanafamilia hiyo wanapata mafanikio lukuki!, na hapa ndipo ulipo ule msemo wa "wema hauozi", and tenda wema uende zako, usitarajie shukrani", ikimaanisha ukitenda wewe wowote bila kujionyeshea wala kujitangaza, unapata karma kubwa zaidi, kuliko wale watenda wema huku wakijitangaza!, mfano Bakhressa anasaidia sana ila kamwe hutakaa uone akiita waandishi kujitangaza au kuonyeshea jinsi anavyosaidia!. Hili la kutenda wema, kiofisi linaitwa Corporate Social Resiponsibility (CSR) ambalo makampuni au mashirika yanafanya wema kwa jamii iliyowazunguka, hivyo ku produce positive energy itakayofanya wakubalike na kupendwa katika eneo husika. Huku kukubalika na kupendwa, kuna produce positive energy, ambayo inayanyoosha mambo ya hiyo kampuni, kama ni mgodi, unatema!.

Ubaya Mmoja wa Karma, Ukitenda Ubaya Halafu Ukafa Kabla ya Kulipwa, Familia Yako Inafidia!.
Kama ilivyo kwa wema, na kwa ubaya ni vivyo hivyo!, ukitenda ubaya au uovu, halafu ukafa kabla ya kuchapwa bakora za karma kuulipia ubaya wako, kwa vile malipo ni hapa hapa duniani, then familia yako uliyoiach huku nyuma ndio inaendelea kuubeba ubaya huo, hivyo kuchwapwa hizi bakora za karma bila kosa lolote!, kitu ambacho kwa maoni yangu, this is not right na sio fair kabisa, it is very unfair!.

Sometimes Karma Haitendi Haki ni Unfair na Unjust!
Ubaya wa pili wa karma ni kiwango cha adhabu kinakuwa determined na maumivu ya mtendewa na sio mtenda. Unaweza kutenda dhambi kubwa kama kumuua mtu adhabu yake inapaswa kuwa kubwa lakini ukakuta mtu ni muuaji halafu anapeta tuu, kumbe yule uliyeuliwa alikuwa muovu sana, mchawi, mlozi, mwanga, mfitini, mchonganishi etc kiasi kwamba kifo chake ni blessing kwa wengi, muuaji anabarikiwa badala ya kuhukumiwa. Na ukakuta mtu umetenda ubaya mdogo tuu kama kumuahidi mtu kumuoa halafu humuoi, ikitokea huyo mtu hakuolewa tena, mapigo ya karma yatayokushukia ni usipime.
Yaani unaweza kupata mapigo makubwa kwa kosa ndogo na mapigo madogo kwa kosa kubwa. This is not fair.

Kama Inawahukumu Wasio na Makosa!
Mfano kwa mtoto mdogo malaika wa Mungu kuzaliwa bila dhambi yoyote kisha anakuja kujikuta kumbe mzazi wake alifanya ubaya fulani, hivyo mtoto huyo kujikuta anapaswa kubebeshwa mizigo ya dhambi za wazazi wake bila kosa lolote!.

Karma Hutoa Hukumu Kali Kwa Makosa ya Hisia, Emotions Yanayosababisha Kulia Machozi ya Ndani!
Kati ya malipo makubwa ya 'karma' yenye fidia kali ni pale ubaya au uovu unaofanyika ni uovu wa mambo ya moyoni, emotions kama mapenzi, uongo, kusingizia, fitna, dhulma, etc na hata uongo kwenye mambo ya mapenzi!. Mfano ikitokea binti amekupenda anatamani wewe ndio umuoe, akakuonyesha kila dalili ya kukupenda kumbe wewe hujampenda ila kwa vile kajileta, unaamua kumpitia tuu binti wa watu lakini huna mpango naye wowote wa maana zaidi ya kumtafuna!. Katika kumpitia kule binti akakuuliza utanioa?!, wewe ukajijibia tuu "ndio nitakuoa!", lakini hukumaanisha bali amejibu tuu ili kupata game!, na baada ya kupata ulichokitaka , unaendelea na maisha yako as if nothing happened huku huna mpango tena na huyo binti!. Kama binti atakuwa amejitunza ili kukutunzia kwa ajili ya ahadi yako kuwa utamuoa, na kupoteza chances zake zote za kuolewa kwa sababu yako, utakapo amua kuoa mwanamke mwingine yoyote, kama huyu binti atakuwa anakulilia chozi la ndani, ambalo karma yake ni kali sana, karma ya mtu aliyedhulumiwa!, then wewe utalipia adhabu ya karma kwa mikosi kwenye ndoa yako, hadi kumaliza deni la yule mwanamke wa mwanzo uliyemuahidi kumuoa ukamtosa, hivyo kujikuta huyo mke wako mpya ambaye hana kosa lolote kuingia kwenye ndoa ya mateso na akiadhibiwa kwa raha ya ndoa yako kuwa counter checked kwa matukio ambayo yeye hayamhusu kabisa!.

Kuweni makini sana na kutochezea feelings za watu!, if you don't mean it, don't promise chochote, ukiahidi ahadi, lazima utimize na kuitekeleze ulichoahidi, kwa sababu ahadi ni deni lazima deni hilo lilipwe, na lisipolipwa linafidiwa kwa gharama kubwa maradufu!.

Hitimisho
Kwa kumalizia, hivyo jambo lolote zuri lilikutokea, usidhanie ni kwa bahati nzuri tuu, au limejitokezea tuu!, shukuru Mungu huku ikihesabu hayo ni malipo ya mema yako au ya wazazi wako!, hivyo una obligation ya kutenda mema ili kuendelea kupata mema na kuwawekea pensheni ya mema watoto wako wakati wewe umeishaondoka kwenye dunia hii!.

Kila Majanga ni Ama ni Majaribu ya Mungu, Mipango ya Shetani au Fidia ya Karma.
Ukikutwa na majanga yoyote na mabalaa yoyote, yapokee kwa mikono miwili, kwa hoja kuwa majanga hayo yalikuwa destined kukutokea, namna hiyo hiyo yalivyotokea, yaani premeditated moves, huku ukijihesabu sababu ya hayo majanga ni moja kati ya mambo matatu haya.

Moja: Majanga hayo ni ama ni majaribu au mitihani ya Mwenyezi Mungu kukupa mitihani ni kwa kiasi gani wewe ni mcha Mungu, hivyo kukuletea majaribu ili kujihirisha uwepo wake na uwezo wake kwa kukuwezesha kuyashinda, kama alivyowafanyia wana Israel wakiwa utumwani Misri.

Pili: Majanga mengine ni kazi ya mwovu shetani, amekuletea majanga makubwa zaidi ambayo aliyapanga ikiwemo kukuangamiza kabisa wewe, familia yako na ukoo wako wote mfutike kutoka kwenye uso wa dunia, lakini Mungu ameyazuia hayo makubwa na mabaya ambayo yameelekezwa kwako, na katika vita vya kukukinga na kukuokoa, then hayo yaliyokukuta, ni kiduchu tuu, hivyo ni kushukuru Mungu, ndio nafuu yake ukilinganisha na yale yaliyozuiliwa au kuepushwa yasikufike, kama Mungu alipomuepusha Lutu na ile Sodoma na Gomola, japo Lutu alimpoteza mkewe kwa kugeuka jiwe la chumvi, na aliwalala mabinti zake bikira,na kuwapa ujauzito, yote hayo ni madogo ukilinganisha na kilitokea Sodomana Gomora.

Tatu: Majanga hayo ni mavuno ya karma ya ulichokipanda, au malipo ya fidia ya kufidia ya ulichokifanya au walichokifanya wazazi wako, hivyo una obligation ya kuepuka kufanya matendo maovu, uli usihukumiwe na kuwaachia watoto wako mizigo ya kukulipia madeni ya uovu wako wakati wewe haupo duniani!.

Uzuri wa Karma, Ukiisha Lipa, Deni Linafutwa, .
NB. Kitu kizuri kuhusu hii karma, ukiisha adhibiwa, au kupata mapigo ya karma, deni likiisha, au kuisha fidiwa, adhabu inamalizika, unainuka tena.

Uzuri wa Karma ni Reversible, Ukifanya Ubaya, Unaweza Kuupindua Ubaya Huo Kwa Wema, Ukaepuka Adhabu ya Karma!.
ila pia kwa kujitambua, ukifanya jambo baya, ukaomba msamaha kabla karma haijaanza kukushughulikia, then una weza ku reverse bad karma isikutokee, au hata kuizuia kabisa kwa kufanya mema mengi zaidi kuliko uovu!. Hii inaitwa kuireversi karma, hivyo mtu muuaji, akibaini kosa lake na kujutia, kisha akatembea na fuko la fedha kuwagawia yatima na masikini, adhabu ya karma ya uovu wake inapinduliwa na mema yake, anabarikiwa!.

Shukuru Kwa Yote!
Tukipata mema na mafanikio, tuseme asante, na tukipata balaa na majanga, pia tuseme asante, kwa sababu hata kama ni majanga, majanga mengine ni blessing in disguise, kama ilivyo kwa Yesu, japo ni Yuda ndio alimsaliti Yesu, na Yesu aliteswa kwa usaliti wa Yuda, lakini tukio lote, lilikuwa pre meditated siku nyingi, litokee hivyo hivyo lilivyotokea na kuonekana kama janga, kumbe kwa kuteswa kwake, sisi tuliponywa!.

Nawatakia Jumapili njema!.

Paskali

Kwa ufahamu zaidi kuhusu haya mambo ya powers, tembelea nyuzi hizi,
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo Bila Kujitambua!,

"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani!. Kila Mtu Anazo!.
Andiko refu balaaa!! Anyway ni kawaida yako kwahiyo huu ni kama msahafu mpya niachane na kweli ya Biblia? ( Mi ni mkristo) Maana Biblia inasisitiza Jina la Yesu lina nguvu nikiliamini, haijasema jina la Mandela, Nyerere, Mayala, au Mkapa!!
 
Mkuu Amri kuu ni Upendo, kwa Wakristo, Biblia na Bwana wetu Yesu Kristu, kila alipoponya alisema ni imani yako imekuponya. Hivyo kitu kinachoponya sio jina la mtu yoyote, ndio maana hata kabla ya ujio wa wakoloni, mababu zetu walijitibu kwa imani zao na walipona.

Mungu ni omnipresent, yuko ndani yako. Kinachokuponya sio mtu bali Imani, ukiamini Baba Askofu Mayalla ana nguvu za upako wa kuponya, akikuwekea mkono na kusema "Upone kwa jina la Yesu", ukapona, kilichokuponya sio nguvu ya upako ya Baba Askofu Mayalla, wala sio hilo jina bali ni imani yako, na nguvu zilizoko ndani yako.
Rejea muhimu "Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!

Na Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?
P
 
karma.jpg
Karma ina Apply Kwenye Kila Kitu, Kisiasa, Kiuchumi, Kijamii!.
Karma hii ina apply kwenye kila kitu, kifamilia, kisiasa, kiuchumi na kijamii mfano Zitto ametimuliwa Chadema kwa tuhuma za usaliti, kama ni kweli Zitto ni msaliti, then Karma ya usaliti itamshughulikia Zitto na hiki Chama chake cha ACT kitajinyaukia na kujifia kabla hata hakujakuchwa kwa uchaguzi!, na Chadema kitaendelea kung'ara, kuneemeka kuchanua na kushamiri!. Lakini kama Zitto amesingiziwa usaliti na hakuhukumiwa kwa haki bali ameonewa, then Karma ya kuonewa itamlipa Zitto kwa kumuimarisha, ACT itaneemeka, itachanua na kung'ara, Zitto atarejea bungeni kwa kishindo, wakati Chadema, wale walio husika kusingizia uovu, karma itawatandika bakora za Karma, mmoja baada ya mwingine, in two ways, a collective karma kwa Chadema kama chama kitakula bakora zake na kitaishia kupukutika, lakini wana Chadema individual wenye mkono kwenye dhulma hii kwa Zitto, nao karma zao zitawatembelea mmoja mmoja kwa mujibu wa mchango wake hivyo watadhoofika, kudorora na kunyauka!.

Paskali
Kwa ufahamu zaidi kuhusu haya mambo ya powers, tembelea nyuzi hizi,
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo Bila Kujitambua!,

"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani!. Kila Mtu Anazo!.
Baada ya hukumu ya kina Halima Mdee kutoka, naomba kuwahakikishia hukumu hii ni kama ile hukumu ya Zitto, it's legal technicalities. Sheria na haki ni vitu viwili tofauti. Mahakama imeangalia sheria, lakini sio haki. Naendelea kusisitiza Kina Halima Mdee na kundi lake hawakutendewa haki na Chadema, lakini kwenye Mahakama ya Karma, amini usiamini, watapata haki, kwa kuanzia Chadema itakula bakora za haja, karma ya Zitto ni cha mtoto!. Mimi nimeshauri
Wanabodi.

Sasa kwenye hili la Halima Mdee, Chadema, imejikwaa tena pale pale ilipojikwa kwenye issue ya kumtumua Zitto, safari hii Chadema bado haijaanguka na bakora za karma bado hazijaanza kutembea.

Kwa vile Zitto alikimbilia mahakamani akashindwa, Chadema wakashangilia ushindi huo, nashukuru mimi niliwaeleza humu kuwaelimisha kuhusu karma, na nikawaambia the consequences ya matendo, hivyo kwenye hili la Halima Mdee, nae amekimbilia mahakamani, ikitokea na Halima akashindwa kama alivyoshindwa Zitto, hivyo Chadema wakafanikiwa kuwatimua rasmi hao wanaowaita Covid 19, naomba mimi niwe mtu wa kwanza kuwaambia the consequences will be very devastating, kwenye karma ya Zitto, angalau someone survived miraculously, I'm not sure kwenye hili, if anyone will!. Kwa kuchelea this, nimejitolea kuishauri Chadema the right thing to do na kuepuka adhabu ya karma.

Paskali.
Wanabodi,
Baadhi ya mabandiko yangu sio mabandiko ya average mind ni mabandiko ya deep thinkers, moja ya mabandiko hayo ni Bandiko hili Ushauri wa Bure: Ukijikwaa ukaanguka, usiangalie tu pale ulipoangukia, bali angalia pale ulipojikwaa

Maadam Mahakama Kuu imetupilia mbali kesi ya kina Mdee, hiki nilicho andika kwenye bandiko hili, sasa ndio kinakwenda kutokea!. It will be very devastating and disturbing!.

Wale ambao sio average mind, wana uwezo to connect the dots, baada ya Chadema kumtimua Zitto kwa dhulma, there are bad things that happed to Chadema na wahusika wa kadhia ya Zitto, but no one connected the dots and linked the consequences, hivyo sasa baada ya Chadema kuwatimua hawa Wabunge 19, naombeni sasa watch closely what will happen to Chadema and the main players and connect the dots.

God forbids!.
P.
 
Baada ya hukumu ya kina Halima Mdee kutoka, naomba kuwahakikishia hukumu hii ni kama ile hukumu ya Zitto, it's legal technicalities. Sheria na haki ni vitu viwili tofauti. Mahakama imeangalia sheria, lakini sio haki. Naendelea kusisitiza Kina Halima Mdee na kundi lake hawakutendewa haki na Chadema, lakini kwenye Mahakama ya Karma, amini usiamini, watapata haki, kwa kuanzia Chadema itakula bakora za haja, karma ya Zitto ni cha mtoto!. Mimi nimeshauri

Wanabodi,
Baadhi ya mabandiko yangu sio mabandiko ya average mind ni mabandiko ya deep thinkers, moja ya mabandiko hayo ni Bandiko hili Ushauri wa Bure: Ukijikwaa ukaanguka, usiangalie tu pale ulipoangukia, bali angalia pale ulipojikwaa

Maadam Mahakama Kuu imetupilia mbali kesi ya kina Mdee, hiki nilicho andika kwenye bandiko hili, sasa ndio kinakwenda kutokea!. It will be very devastating and disturbing!.

Wale ambao sio average mind, wana uwezo to connect the dots, baada ya Chadema kumtimua Zitto kwa dhulma, there are bad things that happed to Chadema na wahusika wa kadhia ya Zitto, but no one connected the dots and linked the consequences, hivyo sasa baada ya Chadema kuwatimua hawa Wabunge 19, naombeni sasa watch closely what will happen to Chadema and the main players and connect the dots.

God forbids!.
P.
Wameshupaza shingo hawawezi kukuelewa mkuu

Sent from my SM-J730GM using JamiiForums mobile app
 
CDM ina watu wenye chuki nyeusi kuzidi masizi na hayasafishiki hata utumie 'Bleaching agent' labda umwagie 'concentrated sulphuric acid' ili kuiumua nyama ya INDA. The karma shall whip on both parties in the political arena and the executive government
 
karma.jpg

Uzuri wa Karma, Ukiisha Lipa, Deni Linafutwa, .
NB. Kitu kizuri kuhusu hii karma, ukiisha adhibiwa, au kupata mapigo ya karma, deni likiisha, au kuisha fidiwa, adhabu inamalizika, unainuka tena.

Uzuri wa Karma ni Reversible, Ukifanya Ubaya, Unaweza Kuupindua Ubaya Huo Kwa Wema, Ukaepuka Adhabu ya Karma!.
ila pia kwa kujitambua, ukifanya jambo baya, ukaomba msamaha kabla karma haijaanza kukushughulikia, then una weza ku reverse bad karma isikutokee, au hata kuizuia kabisa kwa kufanya mema mengi zaidi kuliko uovu!. Hii inaitwa kuireversi karma, hivyo mtu muuaji, akibaini kosa lake na kujutia, kisha akatembea na fuko la fedha kuwagawia yatima na masikini, adhabu ya karma ya uovu wake inapinduliwa na mema yake, anabarikiwa!.

Shukuru Kwa Yote!
Tukipata mema na mafanikio, tuseme asante, na tukipata balaa na majanga, pia tuseme asante, kwa sababu hata kama ni majanga, majanga mengine ni blessing in disguise, kama ilivyo kwa Yesu, japo ni Yuda ndio alimsaliti Yesu, na Yesu aliteswa kwa usaliti wa Yuda, lakini tukio lote, lilikuwa pre meditated siku nyingi, litokee hivyo hivyo lilivyotokea na kuonekana kama janga, kumbe kwa kuteswa kwake, sisi tuliponywa!.

Nawatakia Jumapili njema!.

Paskali

Kwa ufahamu zaidi kuhusu haya mambo ya powers, tembelea nyuzi hizi,
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo Bila Kujitambua!,

"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani!. Kila Mtu Anazo!.
Natambua unatambua kwa hakika kwa kipindi cha 2015 mpaka sasa ama kwa kujua au kwa kutojua ulijijengea nguvu hasi kubwa sana...ila kuna hiki kitu kinaitwa KARMA!
Mkuu Mshana Jr, kwanza asante sana kwa yote.
Pili asante sana kwa kuniandaa kisaikolojia ili ikitokea nimeangukia pua ni karma ya 2015.
Kuna nguvu hasi nyingine pia ambayo inaweza kuwa kigingi cha kukwamisha ndoto zako.. Nacho ni chama cha siasa utakachotumia kuombea nafasi firikirika.. Kimejaa tuhuma, ubaya na uchafu wa kila aina... Kimeumiza na kutesa wengi, kimedhulumu na kufanya kila aina ya hila ili kiwepo mahali kipo..! Baraka huwa hazikai mahali kama hapo!
Mimi nilidhani baada ya karma kula kile kichwa, hili deni la chama cha siasa firikirika.. ambacho kimejaa tuhuma, ubaya na uchafu wa kila aina... zikiwemo tuhuma za kuumiza na kutesa wengi, kudhulumu na kufanya kila aina ya hila ili kiwepo mahali kipo, litakuwa limelipwa limelipwa in full!.
Thanks again.
P
 
karma.jpg

Wanabodi,

Sio mara moja au mbili, umewahi kusikia mtu akitendewa jambo baya, anasema "namwachia Mungu!", au neno "Malipo ni hapa hapa duniani!". likitokea jambo zuri lolote watu hufurahi na kumshukuru Mungu, au likitokea jambo baya lolote, watu hufarijiana kuwa kusema hiyo ni "kazi ya Mungu!'. haina makosa!. Natumaini mmewahi kusikia kuwa kuna watu wenye bahati, familia zenye bahati, wamebarikiwa, wamesoma na wote wana kazi nzuri, na kuna watu/familia wenye mikosi, wamelaaniwa na kuandamwa na majanga, mikosi etc?, au nini huwa kinampata mtu aliyeachiwa kitu kinachoitwa 'laana!"?.

Hakuna kitu chochote ni kipya chini ya jua, hakuna bahati nzuri wala bahati mbaya, hakuna jambo lolote linalotokea kwa kujitokea tuu, au kwamba limetokea ghafla tuu, au kwa bahati mbaya, or just a coincident!, no way!. Kila jambo linalotokea, linatokea kwa sababu na lilikuwa destined kutokea hivyo hivyo lilivyotokea, yaani everything is a premeditated move, caused by cause and effects, by our actions or inactions!.

Jee ni nguvu gani zinafanya watu wengine wafanikiwe, na mambo yao kuwaendea vizuri, huku watu wengine wakikwama, kuandamwa na mikosi, majanga, mabalaa na kuishi kwenye maisha duni na umasikini uliotopea huku wakiandamwa na majanga, visa na mikasa lukuki?!.

Hizi ni powers zinazotumika kwenye 'cause and effects', ndizo zinazoitwa "Powers of Karma" yaani "what goes around, comes around".
Sometimes unaweza usiwe mwema lakini kuna vitu vinakuwa havina faida wala umuhimu wa kuvifanya, especially linapokuja swala la utu wa wengine mbele ya maslahi yako binafsi. unaweza usiitwe wema lakini ni normal human empathy and instincts.
Tuseme sawa ungeenda kumuuliza kuhusu uhakika na credibility ya hizo taarifa na kumuomba favors za mambo ya kawaida ya kibinadamu lakini kama angekataa wala usingemlipua sababu bila shaka kulikuwa hakuna ulazima wa kufanya hivyo na leo angekumbuka siku ile basi bila shaka kusingekuwa na tension ya kisasi na labda angekuona mwema zaidi kwamba aliona taarifa fulani na akaniambia lakini akapuuza na hakunilipua.
Mkuu Chris Hemsworth , kwanza asante, na hii ndio faida ya jf, unapata waalimu wa humility humu. Hapa umenifundisha somo moja kubwa sana na zuri sana!. Somo la wema vs empathy, kuna watu wanafanya wema wa kuonekanika na watu, hivyo machoni kuonekana kama watu, lakini mioyoni wana roho mbaya za ajabu!. Ni kweli katika tukio hilo nilifanya makosa, nilikosa kabisa empathy, tena enzi hizo, kijana shababi foleni toka Tegeta mpaka Feri!, sikupaswa kufanya nilio yafanya, acheni tuu karma i take its toll, tunahukumiwa kwa matendo yetu ndio maana sasa going to 60, nawasisitiza sana watu tutende wema, kumbe ni tunatakiwa tuwe na empathy.
Tatizo sio kuwa mtu mwema bali ni kukosa empathy sababu kila mtu anaweza kuwa mwema, na mkuu bila shaka ulikosa empathy.
Ukiwa na empathy automatically unakuwa mwema hata kama hauonekani mbele ya watu na kiwa unafanya mambo ya ajabu ikiwemo blackmailing.
Kiukweli kuna fani na fani, fani nyingine mtu ukikosa kabisa empathy ndio unaonekana shujaa. Mimi nikiwa JKT Makotupora kwenye somo la range, kila mtu anapewa risasi 10 to hit the bull. Dada mmoja ndio aliongoza kwa kuhit 10/10 mimi nikawa wa pilo nili hit 9/10 nadhani hadi 8/10 tulikuwa listed. Baada ya miezi 6 tukahamishiwa MMJKT pale Mlalakuwa kuja kumalizia. Baada tuu ya kumaliza JKT sisi tuliokuwa listed kwa kufanya vizuri range, tukapelekwa moja moja JWTZ, wenzetu wengine wakapelekwa CCP Moshi na wale jamaa zetu wa Mbweni, wakachukua watu wao.

Tukapangwa kufanya upya deppp ya JWTZ kwa miezi 6 pale Air wing Ukonga, kabla ya kwenda Monduli kwenye Officer Cadet. Kwenye Deppo ya JW range nikapiga 10/10!. Instructer wetu Sajini Meja Kahamba, akanisifu kwa kulenga shabaha, jina langu likaondolewa kwa watu wa kwenda Cadet, natakiwa kwenda kwenye kozi ya udunguaji, yaani snipers, nikaelezwa kazi yangu itakuwa ni moja tuu, kulenga kichwa!. Ndipo nikaelezwa kazi ya jeshi la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, wale wa Mbweni ni kulinda usalama wa nchi na wa serikali, kazi ya JWTZ ni kulinda nchi na mipaka yake hivyo kazi ya mwanajeshi anafundishwa ku ...tuu!. Tena kwenye mafunzo hayo ndio mnafundishwa mkiwa front line, amri ya ku "charge" ikitoka ni macho mbele, mbele kwa mbele, atakaye geuka tuu nyuma, wenzake ni 'hapo hapo' mnamalizana nae!. (Yule Jamaa aliyekuwa CinC aliposema "vita ya uchumi ni mbaya sana, afadhali vita ya kawaida, mkiwa front line wasaliti huwa wanafanywa nini!, huwezi kuwasaliti wenzako ukaachwa hivi hivi una survive!", we all know what happened!, (zile pyu pyu!).

Baada ya kujua kumbe mimi kazi yangu jeshini itakuwa ni hiyo!. Dhamira yangu ikanigomea!. Nikaacha jeshi na kujiunga TSJ kusomea uandishi wa habari!.

Huku kwenye uandishi, ukifanya Investigative Stories za uchunguzi na kuwalipua watu ndio unaonekana shujaa kumbe bila kujua una accumulates bad karma ya kutosha due to kukosa empathy na mwisho wa siku zetu waandishi wengi wa IJ wana end up horribly Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...
Wema mtu atafanya ili kuonekana mbele za watu kwa maana hiyo yoyote anaweza kuwa mwema, lakini empathy sio kila mtu anaweza kuwa nayo, wema ni fake na empathy is real.
Namuomba sana Mungu, sio tuu anafundishe kunyamaza, bali pia anijalie empathy kwa hizi siku zangu zilizobakia!.
Asante tena, post yako hii, imekuwa ni darasa kubwa kwangu kwa somo la wema, empathy na karma!. Ubarikiwe sana!.
P
 
Wanabodi,

Sio mara moja au mbili, umewahi kusikia mtu akitendewa jambo baya, anasema "namwachia Mungu!", au neno "Malipo ni hapa hapa duniani!". likitokea jambo zuri lolote watu hufurahi na kumshukuru Mungu, au likitokea jambo baya lolote,
Shukuru Kwa Yote!
Tukipata mema na mafanikio, tuseme asante, na tukipata balaa na majanga, pia tuseme asante, kwa sababu hata kama ni majanga, majanga mengine ni blessing in disguise, kama ilivyo kwa Yesu, japo ni Yuda ndio alimsaliti Yesu, na Yesu aliteswa kwa usaliti wa Yuda, lakini tukio lote, lilikuwa pre meditated siku nyingi, litokee hivyo hivyo lilivyotokea na kuonekana kama janga, kumbe kwa kuteswa kwake, sisi tuliponywa!.

Nawatakia Jumapili njema!.

Paskali
Wajameni, kwa kilichonitokea kwenye EALA, usikute ni malipo ya matendo yangu ya nyuma, hivyo tumefundishwa kushukuru kwa yote!, hivyo kama jina langu lingepitishwa, ningeshukuru kwa kupita, sikupitishwa, ninawajibika pia kushukuru kwa yote, nawashukuru, wote walionichangia michango ya hali na mali.

Pia nawaomba sana, wale wanaonibeza, wanibeze kwa kiasi tuu kama ilivyo kwenye utani wa jadi wa Simba na Yanga!, wasinibeze wakapitiliza, na kunitukana, mimi pia ni binadamu mwenye mwili wa nyama wenye ngozi laini na moyo na roho teke teke, sijajaaliwa ngozi ngumu au moyo wa jiwe au wa chuma, wasinibeze wakapitiliza na kuniumiza!. Sisi wengine tunajijua karma zetu tukiumizwa!. Tubeze tuu kwa kiasi tuu, sasa itoshe na maisha, yaendelee!.
Asante kwa yote!.
P.
 
Hivi hiyo "laana' au "karma" huwapata tu watu kwa kuwa tu fulani wewe Pascal Mayalla umsema, au..?

CHADEMA ni karma gani inayowatandika kwa mfano...?
Mkuu The Palm Beach, karma is the law of cause & effects kwa kuhukumiwa kwa matendo yako, ukitenda mema, unalipwa mema, na ukitenda uovu unaafhibiwa!.

The biggest toll ya karma ni kifo.

Kila binadamu kuna mazuri yake na mabaya yake, akitenda mema anabarikiwa, akitenda maovu analaaniwa. Kila kitu kinachomtokea binadamu hapa duniani ni matokeo ya matendo yake.

Kwa upande wa Chama, pia kuna karma za taasisi na karma za viongozi wa taasisi ambazo ndio watoa maamuzi. Taasisi inapotoa maamuzi ya dhulma, taasisi inaadhibiwa na watoa maamuzi nao wanaadhibiwa individually!, wakati wale wanao dhulumiwa karma ikiwafidia kwa kuwabariki.

Angalia baadhi ya viongozi wa Chedema waliofukuzwa bila kutendewa haki, baada ya kutimuliwa Chadema au kujitoa Chadema, angalia walikuja kuwa wapi?.

Angalia ma sterling wa matukio haya kilikuja kuwakuta nini?.

Angalia hali ya sasa ya Chadema kama Chama kikuu cha upinzani huku bara, amini nakuambia mwisho wa siku, Chadema itafanikiwa kuwatimua hawa makamanda mabinti 19 lakini machozi yao jasho na damu walioigharimikia Chadema, hayatapotea bure!, there is a price to pay and Chadema will pay dearly!.

Kwa vile Chadema inayo katiba yake na imeweka taratibu za haki kabisa kushughilikia nidhamu, zikiwemo mamlaka tofauti tofauti za nidhamu kwa viongozi tofauti tofauti, kwanini hazifuatwi?.

Mfano wakati wa kumtimua Zitto, Zitto alikuwa NKM, kwa mujibu wa katiba ya Chadema, mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu na mamlaka yake ya rufaa ni Mkutano Mkuu, mamlaka ya CC ya Chadema ni kumsimamisha tuu na sio kusikiliza shauri lake!, sasa hiyo CC ya Chadema ilimtumua Zitto kwa mamlaka gani?. Angalia Zitto baada ya kutimuliwa alikuwaje na angalia yule sterling wa kutimuliwa Zitto nini kilikuja kumkuta?.

Angalia Kitila Mkumbo baada ya kutimuliwa Chadema alikuja kuwa nani?.
Angalia Juliana Shonza baada ya kutumiwa Chadema alikuja kuwa nani

Hivyo kiukweli kabisa karma ipo and it acts upon us kwa matendo yetu!.

Muulize mbowe kuhusu brother shadhiry ni nani?
 
...Hii Karma Mbona haifanyi Kazi Kwa wale Waheshimiwa kule Dodoma ambao yote wanayopitisha yanatuumiza Wananchi ? Karma ni Kwa Walalahoi lakini Sio Kwa Wanapokea Mshahara wa MILIONI 14 KWA MWEZI ???

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom