NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
The power Game, Anaeweza kushika madaraka ndie yupo juu zaidi, Mfano kwa Nigeria kanda ya kaskazini wapo nyuma kielimu na kibiashara lakini linapokuja suala la Power wao ndio wameikamta na kuweza kuitumia kuwa juu ya kanda ya kusini mashariki walioshika biashara za nchi na kanda ya kusini magharibi wanaoongoza kwa elimu.
Power game sio kuangalia kwa sasa anaongoza nani, ni kuangalia katika kipindi kirefu ni nani alieweza ku dominate zaidi, Power game haihusiani na maendeleo ya sehemu wanakotoka wenye power, wanakotoka kunaweza kuwa choka mbaya lakini power imewapa ulinzi, connecions na ukwasi wa kutisha ila wanauficha ikiwa ni moja ya mbinu za power game.
Kwangu mimi kwa hapa kwetu naona ni ukanda wa pwani wanajua sana kuucheza huu mchezo kama bao, kanda hii hujumuisha Tanga, Pwani, na Zanzibar .. nguvu yao kuu ni viongozi kuandaa watoto waje kuwa viongozi hapo baadae (suvcesion plan) tofauuti na sehem nyingine mtoto anakazaniwa zaidi aje kuajiriwa ama apewe mtaji, connection wanazijenga kuhakikisha mambo yapo smooth, wanaishi maisha ya kawaida wanayoyapenda watu ilhali wana ukwasi na power kubwa, n.k