The Political Economy of the investment climate in Tanzania

KWA MENTALITY ZA JF hakuna atakeyeisoma hii

watu wanataka CHADEMA vs CCM ligi
 
WAKATI wafadhili wakikabidhiwa ripoti inayoonyesha bado Tanzania kuna ufisadi, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameibuka na kusema hatorudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa kutokana na serikali kuwaogopa wala rushwa na mafisadi wakubwa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Raia Mwema, jana, Jumanne, Dk. Slaa amesema wakati wote ambao yeye na wenzake katika Upinzani wakipigania hatua kuchukuliwa dhidi ya mafisadi na wala rushwa wakubwa, serikali imekuwa na kigugumizi katika kuchukua hatua; huku ikitumia mbinu za kuwafunga midomo.

Akitoa mfano wa kesi mbalimbali zikiwamo za wizi katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA) kupitia kampuni ya Kagoda Agricultural Limited na kashfa ya rushwa katika ununuzi wa rada ya kijeshi, Dk. Slaa amesema serikali inawalinda wahusika wakuu.

"Kampuni kama Kagoda wahusika wanajulikana lakini hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika. Hii si dalili nzuri maana inaashiria kwamba wakubwa wanahusika ama wanawaogopa wahusika. Hatudanganyiki na hatunyamazishwi, tutaendelea kusema na kutaka hatua zichukuliwe," anasema na kuendelea;

"Kashfa ya rada ni aibu kusikia serikali inadai fedha za rada wakati ilikuwa na kigugumizi wakati Uingereza wakichunguza wahusika wa rada na walishindwa kutoa ushirikiano kwa wachunguzi, lakini sasa eti wanasikia kuna fedha ndio wanazitaka. Kwa nini walikataa kushughulikia wahusika kwa sheria zetu za Tanzania na kuachia Waingereza kila kitu?" alihoji Dk. Slaa.

Alitoa mfano wa kashfa ya Meremeta inayohusiana na kampuni iliyohusishwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ); huku kukiwa na wanasiasa nyuma ya kampuni husika akisema fedha zilizopotea katika kashfa hiyo zingeweza kutumika kusomesha walimu 19,000.

Dk. Slaa amesema sasa ana muda zaidi wa kupambana kwa kufanya utafiti wa kina na kwamba atahakikisha wananchi wote wanaelimika na kufahamu haki zao. Amesema amekua akifanya ziara vijijini kukutana na wananchi mara kwa mara na kuzungumza nao juu ya mustakabali wao.

Wazungu wawasilisha ripoti kwa donors

Wakati huo huo ripoti iliyoandaliwa na waandishi wawili wa Kizungu, Brian Cooksey na Tim Kelsall, yenye jina "The political economy of the investment climate in Tanzania", imekabidhiwa kwa wafadhili wakuu wa Tanzania.

Baadhi ya mambo muhimu kuhusu uchumi wa Tanzania yameanishwa katika ripoti hiyo, ambayo Raia Mwema lina nakala yake, ikiwa ni pamoja na mifano hai ya rushwa kubwa kubwa inayogusa wanasiasa.

Waandishi hao waliandaa ripoti hiyo kwa niaba ya taasisi ya kimataifa ya Africa Power and Politics Programme (APPP) ya Uingereza. Uandaaji wa ripoti hiyo umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) na Shirika la Misaada la Ireland (Irish Aid); licha ya kuwa taasisi hizo zimejipembua kwenye utangulizi wa ripoti hiyo kwamba si lazima mawazo ya waandishi hao yafanane na ya kwao.

Katika ripoti hiyo, waandishi hao wameonyesha wazi kwamba bado Tanzania inaathiriwa na mabadiliko ya kisiasa na ufisadi unaowahusisha wanasiasa pamoja na kuwa imekuwa ikipokea wawekezaji wengi kutoka nje katika kipindi cha miaka kumi na tano iliyopita.

Lowassa , Rostam watajwa kwenye ripoti

Ripoti hiyo imewataja kwa majina wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chama hicho kimewataja kuwa chanzo cha kushuka kwa umaarufu wake mbele ya umma kikielezea kuhusishwa kwao na kashfa mbalimbali, baadhi zikiwa zinatajwa hadharani kwa mara ya kwanza.

Wanamtaja Waziri Mkuu, aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wakianzia na wakati akiwa Waziri wa Ardhi na baadaye Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, wakimuelezea kuwa alitumia madaraka kwa maslahi binafsi. Wameorodhesha mifano.

Ripoti hiyo yenye kurasa 96 imemtaja pia Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz, wakimuelezea kuwa mmoja wa wanasiasa walioonyesha umahiri mkubwa katika kutengeneza viongozi na kupewa jina la ‘king-maker' akihusishwa kikamilifu katika kampeni za urais wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete hata kabla ya kuingia rasmi katika Kamati Kuu ya chama hicho akiwa Mweka Hazina nafasi aliyodumu nayo hadi mwaka 2007.

Katika ripoti hiyo, Rostam anatajwa kuhusishwa kwake na sakata la Richmond lililomgharibu marafiki zake, Lowassa, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, ambao kwa pamoja walijiuzulu nafasi zao za uwaziri mkuu (Lowassa) na Wizara za Nishati (Karamagi) na Madini na Afrika Mashariki (Dk.Msabaha).

Ripoti hiyo, ambayo imetolewa Juni 2011, imetolewa katika kipindi ambacho nchi wahisani zimeonyesha kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi pamoja na kuwapo kesi kadhaa za rushwa zilizofikishwa mahakamani na nyingine kuwa katika hatua za upelelezi.

Tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekuwa katika wakati mgumu kukabiliana na changamoto hizo, huku kukiwa na kampeni za kisiasa za kuzima hatua kadhaa zinazofanywa na taasisi hiyo ambayo kwa sasa imepanua matawi yake nchi nzima.

Vyanzo vya habari mjini Dodoma vimeeleza kwamba watuhumiwa wakuu wa ufisadi wamemwaga mamilioni ya fedha kuendesha kampeni za kuzuia uchunguzi dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwatisha watendaji wa TAKUKURU akiwamo Mkurugenzi wake Mkuu, Dk. Edward Hosea, wakitaka ang'olewe katika nafasi yake.

"Baada ya kuona kwamba kuna majalada yameanza kukamilika, baadhi ya watuhumiwa wanaendesha kampeni za kutaka Hosea ang'olewe ili kesi hizo zisimame na wao wapate kujipanga upya. Inabidi wabunge wetu wawe macho na watuhumiwa hao ambao wamekwishafikia Dodoma kuendesha kampeni hizo wakishirikiana na wenzao walioko huko," anaeleza mtendaji mmoja serikalini.
 
Lets walk the talk we cannot deny the rule of law.................Dr.Slaa go! go! go! go ahead you have the legitimate
 
EL.RA na AC msitoke ndani ya ccm. Ng'ang'ania humo, mking'ooka basi ng'ookeni na ccm yote. Deal la Kagoda lilikuwa la ccm woooote! CCM wasishangilie ushindi wao na huku wakitaka kuwatosa mlioufanikisha ushindi huo. MSING'OOKEEE!
 
thanks itanisaidia kiasi chake ila ile yenyewe haipatikani, raia mwema walisema wana copy, cant we get that document kweli mafisadi wameificha haippatikani

Wanasikitisha kweli wanaficha copy wakati original ipo in safe hands? I already told them they will go east west north and south nothing will change the verdict that is passed over them kwamba hakuna fisadi atakaye baki salama nchi hii. Awe popote pale kwenye power ama nje ya power the power hand is changed nilazima wapate portion yao sasa ya uovu walioutenda kwa raia wema wa TZ ambao hawana uwezo wakupata kwa uhakika hata mlo mmoja wa kujaza matumbo yao.


Wanafikiri kwamba itakuwa kama kawaida; this time let them count days for them to see how law of righteousness works and how princes make decree!
 
hivi hii jamii forums haina moderators, edward lowassa ametajwa kwenye report ya africa power and politics iliyokabidhiwa kwa wahisani kuwa ni kinara wa rushwa....riport hiyo ipo kwenye mtandao...kwa nini nyie jamii forums mnaruhusu propaganda za lowassa zipenye humu ndani? Mimi ninavyofahamu presidential aspirant ni lazima awe mtu safi sasa kwa nini nyie jamii forums mnakuwa hivyo?
 
uliambiwa wapi kuwa jf ndiyo inayoruhusu nani awe rais...? acha upopo wewe au na wewe unataka uonekane umeanzisha thread?
 
hivi hii jamii forums haina moderators, edward lowassa ametajwa kwenye report ya africa power and politics iliyokabidhiwa kwa wahisani kuwa ni kinara wa rushwa....riport hiyo ipo kwenye mtandao...kwa nini nyie jamii forums mnaruhusu propaganda za lowassa zipenye humu ndani? Mimi ninavyofahamu presidential aspirant ni lazima awe mtu safi sasa kwa nini nyie jamii forums mnakuwa hivyo?
Hapa sio sehemu ya porojo, weka hiyo link hapa ili members wasome hiyo ripoti.
 
Jike dume asante kunipa cheo cha popo bawa unajua kazi ya popobawa nadhani....link nimekwisha iweka
 
Kila mtu ana maoni yake. If you ask others watakuambia kuwa JK hakuwa msafi wakati anajiandaa kugombea but still he was elected the President of the Republic of Tanzania.
 
Back
Top Bottom